Monday, 6 February 2017
Sunday, 5 February 2017
Tunda Man adai amepokea simu nyingi baada ya jina Tunda kutajwa kwenye list mpya ya Mtandao wa Madawa ya Kulevya
Msanii
wa muziki Tunda Man amedai jana alipokea simu nyingi baada ya Mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kutangaza list mpya ya majina ya watu
wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya ilikiwemo
jina la Tunda ambaye ni video queen.
Baadhi
ya waandishi kwenye mitandao ya kijamii waliandika jina Tunda bila
kutolea ufafanuzi ni Tunda gani, hali ambayo iliwafanya wasiohusika
kupigiwa simu nyingi akiwemo msanii wa muziki Tunda Man.
Tunda Man amedai wengi ambao ulikuwa wanampigia simu walitaka kujua kama kweli ni yeye ndiye aliyetajwa au ni Tunda mwingine.
“Jaman
Tunda alietajwa na Mh Paul Makonda ni huyu sio mie maaana simu zimekuwa
nyingi @soudybrown na wewe hujui au umeamua tu kunipigia,” aliandika Tunda Man Instagram huku akiwa amempost dada huyo.
Pia kwenye list hiyo mpya alitajwa mwanadada Vanessa Mdee ambaye pia anatakiwa kuripoti makao makuu polisi Jumatatu.
Friday, 3 February 2017
Wednesday, 1 February 2017
NECTA:CSEE RESLUTS/ MATOKEO KIDATO CHA NNE/FORM 4 2016
NECTA yaachia matokeo ya wanafunzi ambaowamemaliza kidato cha nne 2016 ,Kama kawaida yetu MASWAYETU BLOG tunaendelea kutoa huduma ya kuangalizia majina endapo unahitaji kujua matokeo yako;
ILI KUANGALIZIWA FANYA YAFUATAYO;
TAFADHALI FANYA YAFUTAYO KAMA UNATAKA KUANGALIZIWA;
KWA MPESA KWENDA NAMBA 0742289379
AU TIGO PESA KWENDA NAMBA 0652740927
UTAJIBIWA BAADA YA DK 1 TU.
TUMA PESA KWANZA NDIO UJIBIWE.
Matokeo yote yapo hapa > BONYEZA HAPA
TANGAZO KWA UMMA: NAFASI ZA KAZI KWA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA ZA SHULE (SCHOOL LABORATORY TECHNICIANS)
Serikali inatarajia kuajiri Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule
Daraja la II. Ajira hii ni kwa Fundi Sanifu wa Maabara ya Shule
waliohitimu kati ya mwaka 2013 - 2015.
Hivyo, wenye sifa stahiki na wanaotaka kuajiriwa Serikalini, wanatangaziwa kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya:
- Elimu ya Sekondari (Kidato cha nne na / au Sita);
Tuesday, 31 January 2017
BREAKING NEWS:HAYA HAPA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016
NECTA yaachia matokeo ya wanafunzi ambaowamemaliza kidato cha nne 2016 ,Kama kawaida yetu MASWAYETU BLOG tunaendelea kutoa huduma ya kuangalizia majina endapo unahitaji kujua matokeo yako;
ILI KUANGALIZIWA FANYA YAFUATAYO;
TAFADHALI FANYA YAFUTAYO KAMA UNATAKA KUANGALIZIWA;
KWA MPESA KWENDA NAMBA 0742289379
AU TIGO PESA KWENDA NAMBA 0652740927
UTAJIBIWA BAADA YA DK 1 TU.
TUMA PESA KWANZA NDIO UJIBIWE.
Matokeo yote yapo hapa > BONYEZA HAPA
Tathmini ya Matokeo ya Kidato cha nne 2016 -Tazama matokeo Hapa
Baraza
la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne
mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53%
mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.
Katibu
Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi
408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu,
wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424
sawa na asilimia 73.26.
Kwa
upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na
asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na
wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.
Kwa
upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu
mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60
Shule 10 Bora na 10 za Mwisho katika Matokeo Kidato cha Nne 2016
Monday, 30 January 2017
TANGAZO JIPYA LA KAZI MASWAYETU BLOG
Habari zenu,
Maswayetu blog inatafuta vijana 10 ambao watafanya kazi na blog hii kwa kupost habari mbalimbali kila zinapotokea na kushare sehemu mbalimbali.
Maswayetu blog inatafuta vijana 10 ambao watafanya kazi na blog hii kwa kupost habari mbalimbali kila zinapotokea na kushare sehemu mbalimbali.
MAALIM SEIF:NITAKUWA RAIS WA ZANZBAR
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema mgogoro wa Zanzibarna anaamkni atakuwa Rais Zanzibar.
Amesema, mgogoro visiwani humo utamalizika endapo viongozi wa vyama vyote va siasa watakaa chini kufanya mazungumzo.
Akizungumza katika mahojiano katika kipindi cha Funguka kinachorushwa
na Kituo cha Televisheni cha Azam, Maalim Seif alisema jambo la muhimu
ni viongozi kukubali Zanzibar kuna tatizo.
Alisema anaamini kama kuna nia njema, maridhiano yanaweza kupatikana Zanzibar na migogoro yote ya kisiasa kumalizika.
“Hii naamini kabisa, kama kuna nia njema, kila upande ukubali
Zanzibar kuna tatizo, ukubali kuna haja ya viongozi kupata ufumbuzi wa
tatizo na watapata vipi, ni kwa kushirikiana pamoja,” alisema Maalim
Seif aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Umoja wa
Kitaifa Zanzibar.
Alisema Serikali iliyopita ya Umoja wa Kitaifa, ilikuwa na mafanikio
makubwa na kwamba anavyoona hakuna kitakachorudisha hali ile, kama si
kwa vyama kushirikiana.
“Kila upande ukiona unawakilishwa itasaidia kuleta Wazanzibari pamoja,” aliongeza Maalim Seif.
Aidha, Maalim Seif alisema anajua kuna majaribio makubwa yanafanywa
kutafuta ufumbuzi, hivyo ufumbuzi ni vema upatikane ili kuridhisha pande
zote, na kwamba kuna njia nyingi ya kupata muafaka na hiyo ni pamoja na
kufanyika mazungumzo, lakini ni baada ya kila upande kukubali kuwa
Zanzibar kuna tatizo.
Akizungumzia kugombea tena nafasi ya urais mwaka 2020, Maalim Seif
alisema ni vema kusubiri ili kuona hali ya kisiasa itakapofika wakati
huo.
“Tusubiri kwanza wakati wake tuone kama tunafanikiwa au hatufanikiwi
kwenye hili, halafu tutafanya maamuzi,” alisema Maalim Seif ingawa
baadaye alisema kuwa karibuni anatarajia atakuwa Rais wa Zanzibar.
“Natarajia muda mfupi ujao, Inshaallah nitakuwa Rais wa Zanzibar,”
alisema bila kufafanua anawezaje kuwa rais wakati hakushiriki uchaguzi
mkuu wa Machi, 2016.
Akizungumzia mgogoro ndani ya CUF, Hamad alisema Msajili wa Vyama vya
Siasa aliruhusu upande wa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim
Lipumba kuchukua Sh milioni 369 ambazo ni fedha za ruzuku na kwamba
baadaye chama kitashindwa kuzijibia matumizi yake.
Kuhusu hilo, alisema wamemwandikia Msajili, Gavana wa Benki Kuu (BoT)
na pia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), waangalie
hatua ya kuchukua.
Akizungumzia afya yake, alisema anamshukuru Mungu kwamba afya yake ni
njema. Hata hivyo alisema tangu aondoke madarakani, amekuwa
akijihudumia mwenyewe katika matibabu na si fedha za serikali ikiwa ni
pamoja na matibabu nchini India.