WATOTO watatu wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 12 wamekufa maji
baada ya kuzama katika bwawa lililopo eneo la Ziwamboga, Mombasa wilaya
ya Magharibi B, mjini Unguja.
Taarifa ya vifo hivyo imetolewa na daktari wa uchunguzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Msafiri Marijani.