Tuesday, 16 August 2016

Vijana wazuia gari la Jeshi kubeba jeneza la Rais Mstaafu wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi

Maziko ya Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi (96) aliyefariki dunia juzi jijini Dar es Salaam yalifanyika jana nyumbani kwake Migombani, Zanzibar huku vijana wakikataa gari la Jeshi kubeba jeneza lenye mwili wake. 

Mwili wa hayati Jumbe uliswaliwa katika Msikiti wa Mushawwar, Mwembeshauri mjini Zanzibar  na wakati wanatoka msikitini vijana walimuomba mtoto wa marehemu Mustafa Jumbe kwamba jeneza lisiingizwe kwenye gari badala yake wao watalibeba hadi nyumbani, umbali wa wastani wa kilomita tatu. 
Hata hivyo, walipofika eneo la Kilimani walikuta gari la Jeshi aina ya Land Rover likiwa limeegeshwa kwa ajili ya kubeba jeneza lakini vijana walikataa kulipandisha badala yake waliendelea kubeba kwa kupokezana hadi nyumbani kwa marehemu Migombani ambako alizikwa. 
Haikuweza kufahamika mara moja kwanini vijana hao walikataa gari la Jeshi kubeba jeneza lakini huenda ilikuwa kutekeleza wosia alioutoa Mzee Jumbe wakati wa uhai wake kwamba akifariki dunia jeneza lake lisifunikwe bendera yoyote kama ishara ya maziko ya kiserikali. 
“Sitaki katika maziko yangu kutumbuizwa chochote kiendacho hata kidogo kinyume na mafundisho ya Uislamu,” aliandika katika wasia. 
“Sitaki beni (bendi), sitaki mizinga, sitaki maombolezo wala lolote jingine lenye hata chembe ya kufuru. Sitaki hivyo nikiwa hai, nitakapoondoka katika dunia. Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi wangu, duniani na akhera.” 
Aidha, wakati wa kuweka mwili kaburini yalitajwa majina ya watoto wanne wa marehemu; Ismail, Amari, Rashid na Mustafa pamoja na Sheikh Zubeir ambao ndiyo marehemu aliwaandika kwenye wasia wake kwamba watakuwa na haki ya kuuhifadhi mwili wake kaburini. 
Kabla ya kuupeleka mwili wa marehemu Jumbe katika makaburi ya nyumbani kwake Migombani kwa ajili ya mazishi, Mufti Mkuu pamoja na Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi na Sheikh Khamis Haji Khamis waliongoza dua na swala maalumu iliyofanyika saa 6:45 mchana katika Msikiti wa Mushawwar. 
Viongozi mbalimbali wa Serikali, wastaafu, vyama vya siasa na mabalozi walikuwapo kwenye mazishi hayo. Miongoni mwao ni Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu Othman Mohamed Chande, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, marais wastaafu wa Jamhuri, Benjamin Mkapa na Ali Hassan Mwinyi, makamu wa Rais mstaafu Dk Mohamed Ghalib Bilali, Rais mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa na aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad. 
Jumbe, aliyechaguliwa kuongoza Zanzibar kuchukua nafasi ya Rais wa kwanza, Abeid Amani Karume aliyeuawa mwaka 1972, aliongoza kwa miaka 12 hadi mwaka 1984 alipovuliwa nyadhifa zote serikalini na ndani ya chama tawala, CCM kutokana na kutofautiana kuhusu muundo wa Muungano. 
Tangu alipovuliwa nyadhifa zake amekuwa akiishi nyumbani kwake Mjimwema, Kigamboni na hakuwa anaonekana kwenye shughuli za kiserikali tofauti na viongozi wengine wastaafu. Mara nyingi wakati akiwa bado ana nguvu alijishughulisha na masuala ya kumcha Mungu.
 Walivyomkumbuka 
Katika mazishi hayo, viongozi mbalimbali wa serikali, wanasiasa na wananchi waliohudhuria walimuelezea kuwa alikuwa jasiri, mnyenyekevu na aliyeishi maisha ya kumcha Mungu. 
“Aliishi maisha ya ucha Mungu, ucha Mungu hauna siasa, hauna chama na hata baada ya kustaafu alichagua kukaa kimya, alishauri kuhusu maendeleo ya nchi bila kuita waandishi wa habari. Ni jambo tunalopaswa kujifunza viongozi tunapostaafu,” alisema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, January Makamba.
Makamba alisema Jumbe ni kiongozi aliyeweka historia ya Zanzibar kwa kuanzisha Katiba ya Zanzibar na Baraza la Wawakilishi na kwamba kuna haja ya kuenzi mchango wake. 
Lowassa alimzungumzia Jumbe kama mtu jasiri aliyesimamia kile alichokiamini na kwamba alikuwa mwaminifu na mwenye kufuata utaratibu. 
Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, alimzungumzia Jumbe kama mtu mwenye msimamo, hasa alipotaka Muungano wa Serikali tatu msimamo aliosema hata yeye anauunga mkono. 
Pia, alisisitiza kwamba Jumbe alikusudia kulinda kikamilifu heshima ya watu wa Unguja na Pemba.
“Nadhani wananchi watakumbuka Jumbe alivyoweza kusimama na kujenga hoja juu ya haja ya kuwa na muundo wa Muungano usiokinzana, yaani wa Shirikisho au kama alivyotaja mwenyewe ‘The partnership’ katika azma ya kuheshimu nchi mbili huru zilizoungana, Tanganyika na Zanzibar”, alisema Maalim Seif. 
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhani Dau alisema, “Marehemu namtamka kwa neno moja tu: Unyenyekevu.” 
Dk Dau alisema maisha ya marehemu Jumbe yalikuwa ya ucha Mungu, alipenda watu na hakuwa mtu wa kujitutumua kutokana na wadhifa wa urais aliokuwa nao. 
Alisema Jumbe aliishi maisha ya kawaida toka nyumba yake ya Mjimwema, Dar es Salaam na Unguja kwenye nyumba yake ya Migombani. 
“Angekuwa kiongozi mwingine hapa ungeona mbwembwe nyingi, lakini huyu mambo yamekwenda kawaida, alijitolea kwenye misikiti na shughuli zote za kidini,” alisema Dk Dau. 
Watoto wa marehemu Jumbe, Suleiman na Ismail walisema kuwa bila shaka baba yao alithamini hatma ya maisha yake ya baadaye, duniani na akhera na hapakuwa na budi wao pamoja na Serikali zote mbili kuheshimu kile alichokiamini yeye kama wasia. 
Maombolezo siku saba 
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza siku saba za maombelezo zitakazohusisha kupandishwa bendera nusu mlingoti, lakini shughuli zingine zitaendelea kama kawaida.
Familia ya Mzee Jumbe ilitangaza kuwa viongozi mbalimbali wa dini na Serikali watajumuika pamoja kesho katika Msikiti wa Mushawwar kwa ajili ya dua ya ziada na khitma ya marehemu. 
Share:

Idris Sultan na Wema Sepetu wazinguana tena

Idris Sultan na Wema Sepetu wamezinguana kwa mara nyingine tena.

Kisa na mkasa ni Wema kuisusia show ya Idris, Funny Fellas kwa mara nyingine tena huku mshindi huyo wa Big Brother akihudhuria za mpenziwe, ikiwemo Black and Tie iliyofanyika mwezi uliopita.

Baada ya kuchoshwa na tabia ya mpenzi wake kutompa support kwenye show zake, Idris naye aliamua kuipotezea show ya Usiku wa Vigoma iliyoandaliwa na Sepetunga mwishoni mwa wiki – na hapo ndipo mambo yalipoharibika. 

Mashabiki wa Wema wamekasirika baada ya shemeji yao kuikwepa show hiyo na wanamshambulia Instagram.

 Kutokana na kuandamwa, Idris amelazimika kuongea:

"Sipendi kuona watu wakiingia na kuongea kama wanajua maisha yangu na watu wangu wa karibu, makosa wakifanya wengine mnakuja kwangu mnaanza “Ndio asingefanya vile kama sio wewe kufanya hivi” mnakazana kusema eti naposti wanawake mara ooo porojo kibao. Sina freedom ya kumpost dada angu ? Kweli ? Au rafiki yangu kazindua brand mpya siwezi mpost nikampongeza?

"Mnauliza kwanini sijaenda vigoma nimesema because show yangu hakuja hata moja na nimeenda show zake zote na yeye halalamiki because anajua nimesema siendi fair enough mbona hamjaongelea hilo? I repeat nikikaa kimya is for a pure reason that it’s not anyones business this is my personal life kama mnaongeleaga fair basi mngefanya kuuliza kwanini mpaka am selling out hajaja.

“Give me a break sina maisha ya kuigiza lets have respect for each other bana. Na nimesema msiniite shemeji for one big good reason, imekua too much i am a brand na jina idris linamezwa na shem, ningejua this from the beginning nisingeruhusu mniite tangu mwanzo so msiwe kila kitu mnafikiria negative tu. Na sikuwa na haja ya kuandika yote haya pia TusichukulianePoa."

Hata hivyo Wema naye alimpigilia msumari wa moto Idris kwa kupost picha ya wanaume anaowapenda #MCM (Man Crush Monday) na mmoja wao ni Diamond.
Wengine ni Alikiba, Korede Bello, Jamal wa Empire, Cyrill, Trey Songz, Van Vicker na wengine.
Share:

Rais Dkt. Magufuli Amjulia Hali Spika Wa Bunge Job Ndugai Pamoja Na Waziri Mkuu Mstaafu John Samuel Malecela Jijini Dar Es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Agosti, 2016 amewatembelea na kuwajulia hali Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samuel Malecela Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kuwajulia hali, Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amewaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone na kupata nguvu haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kawaida katika ujenzi wa Taifa.Akizungumza na Rais Magufuli nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amemshukuru Rais Magufuli kwa kumtembelea, kumjulia hali na kufuatilia kwa ukaribu wakati wote alipokuwa akipata matibabu nchini India hadi aliporejea hapa nchini.

"Kwa kweli nimefarijika sana, kwanza naomba nimshukuru sana Mhe. Rais kwa sababu nilipopata matatizo haya ya maradhi alikuwa karibu sana na mimi nikiwa hapa nchini na hata nilipopelekwa nchini India alinipigia simu mara kwa mara na kunifariji sana, na hapa amekuja kuniona kwa niaba ya watanzania kwa kweli namshukuru sana na namuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kumpa moyo huu wa kuwajulia hali wale wenye matatizo mbalimbali"Lakini niwahakikishie Watanzania, kwamba kwa sasa nina nafuu kubwa sana, naweza kufanya kazi nyingi tu sasa lakini tuendelee kuombeana" Ameeleza Mhe. Ndugai alipokuwa akizungumzia hali yake kwa sasa.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samuel Malecela pamoja na kumshukuru Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli kwa kumtembelea amesema afya yake inazidi kuimarika na pia amewashukuru Madaktari wanaompatia matibabu.

"Mheshimiwa Rais nakushukuru sana, namshukuru pia Mama Janeth Magufuli kwa kunitembelea na kunifariji, naendelea vizuri na matibabu na afya yangu imeimarika kwa kiasi kikubwa" Ameeleza Mhe. Malecela.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam

16 Agosti, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam alipokwenda kumjulia hali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli kushoto akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam walipokwenda kumjulia hali. Kulia ni mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Spika Sala sala jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsalimia Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Sala ya kumuombea Waziri Mkuu mstaafu John Samwel Malecela pamoja na mkewe Anne Kilango Malecela.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na Mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai wakati alipokwenda na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai huku Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Share:

Kundi la Original Comedy Matatani Kwa Kuvaa Sare za Jeshi la Polisi Kwenye Sherehe ya Masanja Mkandamizaji

katika  siku za hivi karibuni, kumejitokeza  tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao za kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za Nchi.

Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za makosa ya Jinai, sura ya 16 na  marejeo yake ya mwaka 2002,  kifungu cha 178 (1) na  (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama,  kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo  bila kibali kutoka kwa  Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia  kitendo kilichofanywa na kundi la kisanii la “ Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linachukua  hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.

Aidha Jeshi la Polisi nchini, linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia  mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na  majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama  kuzisalimisha mara moja katika vituo vya Polisi vilivyokaribu nao.

 Imetolewa na:
Advera John  Bulimba – Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Makao Makuu ya Polisi.     
Share:

New AUDIO | Darassa - Kill Me | Download

Share:

TCU:Call of Application for Applicants with NTA6/Diploma Teachers/FTC/Equivalent Qualifications 2016/2017

Share:

Magazeti Ya Leo Jumanne ya Agosti 16, 2016

Share:

Monday, 15 August 2016

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger