Thursday, 11 August 2016

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AUGUST 11 2016


Share:

Wednesday, 10 August 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Agosti 10

Share:

Tuesday, 9 August 2016

MPYA: Majina ya wanafunzi wasio na sifa vyuo vikuu hadharani

SERIKALI imesema majina ya wanafunzi waliojiunga na vyuo vikuu bila kuwa na sifa yatatangazwa mwezi ujao na kuondolewa masomoni, baada ya uhakiki wake kukaribia kukamilika.
Katika mahojiano maalum na Nipashe jana, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema ameshawaagiza watendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kufanyia kazi suala hilo.
Ili kuwabaini wanafunzi wote wasio na sifa, waziri huyo alisema tayari tume hiyo imeanza uhakiki vyeti vya wanafunzi wote waliopo vyuoni.
Profesa Ndalichako alisema uhakiki huo unafanywa kwa kuangalia vyeti vya wanafunzi walioingia katika vyuo hivyo pamoja na kuhakiki kwa njia ya mtandao.
"TCU ndiyo wanafanya kazi hiyo na wana 'data' (takwimu) zaidi, unaweza kuwauliza, lakini ninachofahamu kuna hatua ambazo wameanza kuzifanya, kuangalia vyeti na pia kupitia usajili wao kwa njia ya mtandao," alisema Prof. Ndalichako.
Kuhusu uhakiki wa wanafunzi hewa, kiongozi huyo wa serikali alisema "mchakato huo bado unaendelea".
Ingawa hakutaka kulizungumzia kwa undani suala hilo kwa maelezo kuwa si msemaji wa TCU, Kaimu Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka wa tume hiyo, Dk. Kokubelwa Mollel, alisema majina ya 'vihiyo' waliopo vyuo vikuu yataanza kuanikwa mwezi ujao baada ya kumalizika kwa udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo wa 2016-17 unaofanyika sasa.
"Tulitakiwa tuanze mapema mwezi huu kuwafichua wanafunzi walio kwenye vyuo bila sifa zinazotakiwa, lakini likaja suala la kudali wanafunzi kwanza na ndiyo kazi ambayo tunaifanya sasa," alisema.
"Tukimaliza kazi hii Agosti 31, tutaanza kazi hiyo ya kuhakiki wanafunzi walioingia vyuoni bila sifa," alisema.
Uhakiki wa wanafunzi walipo vyuoni nchini, unafanyika ikiwa ni wiki chache tangu Prof. Ndalichako atangaze serikali imebaini kuwapo kwa wanafunzi 'hewa' na 'vihiyo' ambao wanapatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Prof. Ndalichako pia alifuta udahili wa wanafunzi 7,423 waliokuwa wamedahiliwa kusoma stashahada ya ualimu wa sayansi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) pasi na sifa.
Akitangaza uamuzi huo wa kuwaondoa Udom wanafunzi hao katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma Mei 25, Prof. Ndalichako alisema serikali itafanya msako kwenye vyuo vyote nchini kuwabaini wanafunzi wasio na sifa za kusoma elimu ya juu.
Prof. Ndalichako alisema msako huo hautaishia kwa wanafunzi waliopo vyuoni, bali utawagusa hata wahitimu walioko kazini ikiwa walipata vyeti vyao baada ya kujiunga na elimu ya juu kwa njia za udanganyifu.
"Sifa zote za wanafunzi walioko vyuo vikuu ninazo kwenye kompyuta yangu," Prof. Ndalichako alisema "Kama kuna watu wanafahamu waliingia vyuoni kwa ujanja ujanja, ni bora wasipoteze muda wao na rasilimali zao kuendelea kujigharimia wakati wanajua wameingia na sifa zisizo sahihi maana tunaenda kuwanyofoa."
Share:

SOMA HAPA GAZETI LA JAMBO LEO TAREHE 9.8.2016 KURASA ZOTE
























Share:

MPYA:HII HAPA LIST MPYA YA WANAFUNZI WA WALIOFAULU KUFANYA RPL EXAMINATIONS 2016

Share:

New AUDIO | FEY - KAJA WENYEWE | Download

Share:

Vyuo Vya Udereva Visivyo Na Sifa Mbioni Kufungwa


JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema litavifungia vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya udereva nchini bila ya kuwa na  sifa.

Kauli hiyo ameitoa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP) Mohamed Mpinga wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (Chashubuta) uliofanyika Dar es Salaam jana.

"Kuanzia sasa Jeshi la Polisi halitasita kukifungia chuo chochote cha udereva kitakachokosa sifa kwani kwa kulea shule mbovu tutaendelea kupata ajali na hivyo kuongeza vifo na majeruhi" alisema Mpinga.

Mpinga alisema kwa mujibu wa sheria ya shule za udereva sura 163 ya 1965 (R.E 2002) mpaka sasa jeshi la polisi limesajili shule za udereva 260 ambazo zitategemewa kutoa madereva bora wenye ueledi wa kutosha kutokana na kuwa chanzo kikubwa cha ajali ni makosa ya kibinadamu ambayo yanafanywa na madereva.

Alisema jeshi hilo litafanya msako nchi nzima kuvibaini vyuo ambavyo havina sifa na wamiliki wake kuchukuliwa hatua na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria.

Mwenyekiti wa Chashubuta Taifa, Robert Mkolla wakati akisoma risala yao mbele ya Mpinga ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, alisema moja ya changamoto waliyonayo ni baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri na usafirishaji kutoona mchango mkubwa unaofanywa na shule za udereva za watu binafsi wakiamini kuwa vyuo vinavyotoa elimu nzuri ni vile vya serikali pekee.

Mkolla alimuomba Kamanda Mpinga uboreshwaji wa mitaala mara kwa mara ili kwenda na mahitaji ya barabara, vyombo na wakati na shule hizo ziwe zinashirikishwa katika kutoa michango ya uboreshaji wa mitaala hiyo.

Share:

Godbless Lema Amtumia Waraka Mzito Rais Magufuli


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amemuandikia waraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akimsihi kuruhusu kufanyika kwa mikutano ya kisiasa nchini bila kujali mipaka ya majimbo.

Lema amepaza sauti yake kupitia waraka wake kwa Rais Magufuli, uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, waraka ambao alithibitisha kuwa ni wake.

Katika waraka huo, Lema ambaye pia na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alimsihi Rais Magufuli kuviruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano hiyo kwani ni sehemu ya matakwa ya katiba.

Alitahadharisha kuwa endapo mambo yaliyoruhusiwa kikatiba hayataruhusiwa, ipo siku amri za utekelezaji wa masuala muhimu kikatiba hazitachukuliwa kwani hakutakuwa na sababu ya kuheshimu katiba na utawala wa sheria.

“Kama hatuwezi kufanya tunayoruhusiwa na Katiba, na anayetuzuia mamlaka yake yametokana na Katiba, hakika mbegu inayopandwa ni hatari kwa ustawi wa Taifa, ipo siku amri ya utekelezaji juu ya masuala muhimu haitachukuliwa kwa sababu umuhimu wa kuheshimu katiba na utawala wa Sheria hautakuwepo,” aliandika.

Lema alimueleza Rais Magufuli kuwa Siasa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na kwamba mfumo huo ndiyo chanzo cha madaraka waliyonayo hapa nchini.

“Mheshimiwa Rais, siasa ni kazi na ndiyo maana wewe ni rais kwa sababu ya siasa, na mimi ni mbunge kwa sababu ya siasa, tena ni kazi muhimu sana tu kwani ndio mfumo pekee unaotafuta utawala wa ngazi mbalimbali na wa juu kabisa katika nchi,”

Aidha, Lema alimsemea kwa Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekitiwa CCM, Msemaji wa chama hicho, Christopher Ole Sendeka kwa kukiuka amri aliyoitoa Rais kwa kufanya mkutano Longido ambako sio jimbo lake.

“Mheshimiwa Rais, jambo hili litaleta mpasuko katika taifa letu, ni kauli inayopaswa kurekebishwa haraka. Hivi karibuni, msemaji wa CCM, Ole Sendeka alifanya mkutano Longido. Je, Ole Sendeka ni Mbunge wa Longido? Au polisi wa Mkoa wa Arusha hawakusikia tamko lake? " Alihoji.

Mbunge huyo alisisitiza kuwa Chadema itafanya maandamano Septemba Mosi mwaka huu, huku akihoji madhara yanayoweza kujitokeza siku hiyo, hivyo akamuomba Rais kutengua amri yake ya kuzuia mikutano ya hadhara
Share:

Nay wa Mitego kuachia video ya wimbo ‘Pale Kati’ Jumatano hii


Rapper Nay wa Mitego amedai ametimiza matakwa aliyopewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) baada ya kufungiwa kwa wimbo wake wa ‘Pale Kati’, ambapo Jumatano hii taachia version ya kwanza ya video ya wimbo huo.

Nay amewataka mashabiki wake wa muziki wa kimataifa kukaa mkao wa kula.

“Mimi na BASATA tulishamalizana, wao walinipa maazimio na mimi nimeshayatekeleza, kwa hiyo na mimi naendelea na issue zingine,” alisema Nay.  
“Jumatano hii mashabiki wangu Wakimataifa pamoja na wa kwenye mitandao ya kijamii wakae mkao wa kula, naachia video,”

Rapper huyo alisema wimbo wa ‘Pale Kati’ una nguvu kubwa sana na unafanya vizuri katika baadhi ya nchi kama Kenya, Uganda pamoja na Ghana, na ndio maana ameamua kuanza kutoa video kwa ajili ya kimataifa kwanza.

Pia amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kusubiria mambo mazuri kwani wimbo huo una video nne.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger