Viongozi wa Tume ya Utumishi wa Walimu waripoti Tamisemi
Viongozi wakuu wa Tume ya Utumishi wa Walimu ambao waliteuliwa hivi
karibuni na kuapishwa leo na Rais Dkt John Pombe Magufuli
wamekwisharipoti katika Ofisi zao zilizopo mjini Dodoma.
Aidha Viongozi hao walipata fursa ya kukutana na Naibu Waziri Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo ofisini
kwake mjini Dodoma.
Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu bwana Oliver Mhaiki na Katibu wa Tume hiyo Bibi Winifrida Rutaindurwa.
Pia viongozi hao walipata fursa ya kutembelea ofisi zao na kuongozwa na
aliyekuwa akikaimu nafasi ya Katibu wa Tume Bibi Christina Hape ambaye
sasa anakuwa Naibu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu.
Kuapishwa kwa Mwenyekiti na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu
kunafungua ukurasa kwa taasisi hiyo kuanza rasmi jukumu la kuwahudumia
walimu katika masuala mbalimbali huku muundo wa utumishi wa tume hiyo
ukihusisha ngazi za chini na juu.