Sunday, 24 July 2016
Saturday, 23 July 2016
TANGAZO LA AJIRA YA MUDA - AFISA MAWASILIANO (Lindi, Mtama & Nzega)
1. UTANGULIZI
Jamii Media ni Kampuni gwiji inayojishughulisha na taarifa na habari kwa kupitia Mitandao ya Kijamii. Kampuni hii inachochea Uhuru wa Kujieleza, Uwazi katika Utawala, na Uwajibikaji kupitia Mtandao wao maarufu uitwao JammiForums.com.
Jamii Media pia inamiliki na kuendesha jarida-mtandao liitwalo FikraPevu.com na kusimamia kurasa zenye wasomaji wengi kwenye mitandao ya Kijamii kama Twitter, Facebook na Instagram.
2. CHIMBUKO
Jamii Media inatarajia kuanza utekelezaji wa Mradi utakaofahamika kama “TUSHIRIKISHANE PROJECT” Lengo la Mradi huu ni kuwawezesha wananchi na kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi, wawakilishi wa kuchaguliwa (hususani Wabunge) na Uongozi wa Wilaya.
Tushirikishane utakuwa Mradi wa miezi kumi na miwili utaotekelezwa kwenye Majimbo tisa (9), ya Uchaguzi na utashirikisha Wabunge tisa (9), Madiwani wa kata katika Majimbo husika, watumishi wa Halmashauri katika majimbo husika na wananchi wa maeneo utakapotekelezwa mradi huu.
Lengo mahsusi la kuhamasisha ushirikiano kati ya wadau wakuu wa mradi huu ni kuharakisha/kurahisisha utekelezwaji wa ahadi za viongozi wa kuchaguliwa, kuchochea ufanisi wa Serikali Wilayani katika kutoa huduma za jamii hususani kwenye Sekta za afya, maji, elimu na mioundombinu. Na mwisho, kuweka mfumo wa kuongeza msukumo wa uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi.
Ili kufikia azma hii, ni muhimu wananchi kuwa na uelewa juu ya rasilimali zilizopangwa kwa ajili ya maeneo yao, lazima wajue mipango ya Serikali kwenye ngazi ya Wilaya zao. Uelewa huu unapatikana kwa wananchi kuwa na fursa ya kupata taarifa tena zikiwa katika mfumo ambao ni rahisi kueleweka.
Kwa bahati mbaya kwa sasa taarifa nyingi zinazowagusa wananchi hazipatikani kirahisi na haziko katika mfumo rahisi wa kueleweka na wengi. Jambo hili linalotoa nafasi kwa baadhi ya watu kutumia taarifa kwa manuaa binafsi ikiwemo kuwahada wananchi wakati wa kuomba uongozi. Mradi wa Tushirikishane ungependa kuziba mwanya huu kwa kuhakikisha wakati wote wananchi wanapata taarifa kwa wakati na katika jinsi ambayo zinaeleweka kwa urahisi.
Ili kutekeleza mradi huu kwa ufanisi, Jamii Media imetengeneza nafasi za AFISA MAWASILIANO kwa kila Jimbo litakaloshiriki kwenye Mradi. Maombi yanakaribishwa kutoka kwa watu wenye vigezo wanaoishi kwenye majimbo yafuatayo:
1. Mtama (Lindi)
2. Kigoma Mjini
3. Nzega
2. Kigoma Mjini
3. Nzega
3. VIGEZO VYA MUOMBAJI
- Awe mkazi aliyeshiriki kupiga kura kwenye Jimbo analoomba kuwakilisha na maskani yake ya sasa iwe Jimboni.
- Awe na taarifa za kina kuhusu ahadi za wagombea wa nafasi za ubunge kutoka uchaguzi uliopita na asiwe na upendeleo
- Awe na uwezo wa kuchambua mambo na taarifa pasipo kuathiriwa na itikadi, mapenzi binafsi au upendeleo wa aina yoyote
- Awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea na ajue kukusanya habari, kuandika taarifa na kufuatilia majibu ya malalamiko au maoni ya wananchi kwa viongozi wa umma.
- Awe mtumiaji mzuri wa mawasiliano ya kisasa hasa mitandao ya kijamii. Na awe mshiriki hai wa mijadala mbalimbali inayogusa jamii.
- Muombaji aliyejisajili na kuchangia mijadala mbalimbali ya JF kwa muda zaidi ya miezi sita ana nafasi pekee
4. JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Watu wote wanaohisi wanakidhi vigezo vilivyorodheshwa hapo juu watume maombi yao kwa njia ya barua-pepe wakijibu maswali yafuatayo:
· Jina lako kamili, anwani yako na
· Ahadi gani zilitolewa na Mbunge wako wa sasa? Taja walau tatu
· Hali ya huduma za kijamii ikoje katika Jimbo unalotaka kuwakilisha?
· Vipaumbele vya Serikali katika Wilaya yako ni vipi?
Majibu yatumwe kwenda vacancies@jamiiforums.com na kwenye kichwa cha habari andika JINA LA JIMBO unalotaka kuwakilisha likifuatiwa na neno AFISA MAWASILIANO. Mfano: UBUNGO—AFISA MAWASILIANO.
Kazi hii itakuwa ya mkataba wa miezi minane (8) kuanzia Julai, 2016 na itamhitaji mhusika kuzunguka katika kata mbaimbali za Jimbo kukusanya taarifa na matukio.
Mwisho wa kutuma maombi na Julai 28, 2016.
ANGALIA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWAPAMOJA NA APPLICATIONS FOR ADMISSION INTO NON DEGREE (DIPLOMA AND CERTIFICATE) PROGRAMMES FOR ACADEMIC YEAR 2016/2017-NACTE
Nacte wametoa majina ya wanafunzi waliofanikiwa kuchaguliwa
katika vyuo mbalimbali
afya,ualimu ,kilimo na mifugo kwa level ya cheti na diploma.
Pia inakaribisha maombi mapya kwa wanafunzi wapya.
Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Udahili wa
Pamoja (CAS) umefunguliwa
tena kuanzia tarehe 22 Julai 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizo
wazi baada ya Baraza kuchagua waombaji udahili waliowasilisha
maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016.
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 5 Agosti 2016 saa sita usiku.
Waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kukamilisha
maombi yao kupitia
mtandao ilipofika tarehe 3
Juni 2016, wanaarifiwa kuanza
kuwasilisha maombi ya udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa
Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji wanahimizwa
kutumia muda huu wa nyongeza ili kuwasilisha maombi.
Baraza linapenda pia kuwaarifu waombaji udahili na umma kwa
ujumla kuwa vikao vya Kamati za kuidhinisha majina ya waombaji
udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) vilipitisha
orodha ya majina ya wenye sifa za udahili kulingana na nafasi za
udahili kwa kila kozi zitolewazo na vyuo husika kati ya tarehe 18
Julai 2016 na 21 Julai 2016. Majina ya waombaji waliochaguliwa
kwa kila kozi itolewayo na chuo husika yamekabidhiwa vyuoni
kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS). Waombaji
waliochaguliwa nao wamearifiwa kupitia kurasa (profile) zao
binafsi au kwa
Waombaji ambao hawakuchaguliwa wamejulishwa sababu
zilizowafanya wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao pia.
Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza waliowasilisha maombi yao
kupitia NACTE, Baraza linapenda kuwaarifu kuwa, mashauriano
kati ya NACTE na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
yanaendelea kufanyika ili kufanikisha udahili wa waombaji wa kozi
za Shahada ya Kwanza kama Serikali ilivyoagiza.
kuwasilisha maombi ya udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa
Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji wanahimizwa
kutumia muda huu wa nyongeza ili kuwasilisha maombi.
Baraza linapenda pia kuwaarifu waombaji udahili na umma kwa
ujumla kuwa vikao vya Kamati za kuidhinisha majina ya waombaji
udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) vilipitisha
orodha ya majina ya wenye sifa za udahili kulingana na nafasi za
udahili kwa kila kozi zitolewazo na vyuo husika kati ya tarehe 18
Julai 2016 na 21 Julai 2016. Majina ya waombaji waliochaguliwa
kwa kila kozi itolewayo na chuo husika yamekabidhiwa vyuoni
kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS). Waombaji
waliochaguliwa nao wamearifiwa kupitia kurasa (profile) zao
binafsi au kwa
Waombaji ambao hawakuchaguliwa wamejulishwa sababu
zilizowafanya wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao pia.
Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza waliowasilisha maombi yao
kupitia NACTE, Baraza linapenda kuwaarifu kuwa, mashauriano
kati ya NACTE na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
yanaendelea kufanyika ili kufanikisha udahili wa waombaji wa kozi
za Shahada ya Kwanza kama Serikali ilivyoagiza.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mte
ndaji
ndaji
NACTE
Tarehe: 22 Julai, 2016
AU
>>>>>BONYEZA HAPA KUSEARCH MAJINA HAYO<<<<
** We wish to inform all
applicants that the online application will be active from Monday, 24 July 2016
Issued by: The Office of Deputy Vice
Chancellor (Academic, Research and
Consultancy)
Kutoka Dodoma: Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi kumthibitisha Dk. Magufuli kuwa Mwenyekiti
Habari wakuu,
Leo Jumamosi, July 23, 2016 ni mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi(CCM) kumthibitisha Rais John Magufuli ili awe mwenyekiti mpya wa chama cha mapinduzi kumpokea kijiti mwenyekiti anayeng'atuka, Rais mstaafu, Dokta Jakaya Kikwete.
Wajumbe wengi wako ukumbini tayari kusubiri mkutano uanze rasmi, tuwe sote pamoja kujuzana yanayojiri kutoka Dodoma.
Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na Rais Magufuli pamoja na wake zao wameshaingia ukumbini, wamo pia Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na marais wastaafu wa serikali ya muungano.
Mkutano umeanza kwa kuimba wimbo wa taifa na kinachoendelea kwa sasa ni wimbo wa chama cha mapinduzi kumuaga mwenyekiti anayeng'atuka, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
nitakujuza................
Uamuzi wa Bodi ya Mikopo kuhusu Wanafunzi ambao hawajarejesha mikopo yao hadi leo
Mnamo mwezi Machi, 2016, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
ilitoa notisi ya siku 60 ikiwataka wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa
elimu ya juu kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.
Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato ya marejesho. Baada ya kipindi hicho kumalizika, kipindi cha notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia kimekwisha.
Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya wale wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.
Zoezi hili litajumuisha pia waajiri ambao hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao. Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa kifungu cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.
Hivyo basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa kuanza kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa au kufika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao kabla ya zoezi la kutangaza majina halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika kupitia Akaunti:
A/C No. 2011100205 – NMB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.
Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato ya marejesho. Baada ya kipindi hicho kumalizika, kipindi cha notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia kimekwisha.
Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya wale wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.
Zoezi hili litajumuisha pia waajiri ambao hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao. Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa kifungu cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.
Hivyo basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa kuanza kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa au kufika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao kabla ya zoezi la kutangaza majina halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika kupitia Akaunti:
A/C No. 2011100205 – NMB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.
Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
JINSI YA KULIPIA TSHS.50000 TCU,ILI UFANYE APPLICATION KWA TIGO PESA AU MAX MALIPO
lengo kubwa la MASWAYETU BLOG ni kukufanya wewe hpo mdau wangu namba moja unaesoma taarifa hii,upate kuelimika na kuwaelimisha watu wengine.
kutokana na wengi kuulizia kuhusu utaratibu wa kulipia pesa TCU ,utaratibu ni kama ufatao;
JK AONGOZA KIKAO CHA NEC LEO MJINI DODOMA, NI KIKAO CHAKE CHA MWISHO, WAJUMBE WAPITISHA KWA KISHONDO JINA LA RAIS DK. MAGUFULI
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimuongoza Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kuingia ukumbini, kwa ajili ya kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) leo katika ukumbi wa Sekretarieti uliopo katika Jengola White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo. Wanaofuata ni Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa , Rais Dk. John Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa ,Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein. Kikao hicho kilikuwa na ajenda moja, ya kupokea jina la Rais Dk. Magufuli ili kuliafiki au kulikataa kuwa Mwenyekiti wa CCM wa awamu ya tano kufuatia Mwenyekiti wa sasa atakapostaafu na kumwachia kijiti cha uongozi huo wa Chama katika mkutano mkuu maalum wa CCM utakaofanyika kesho katika Ukumbi wa Dodoma Convetion.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan (kuashoto) akiingia ukumbini kushiriki katika kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akiongoza shamra shamra baada ya yeye na viongozi wenzake kuwasili ukumbini kwa ajili ya kikao hicho
Wajume wakiwa wamesimama kumlaki Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete baada yeye na viongozi wenzake kuwasili ukumbini kwa ajili ya kikao hicho cha NEC
Mwenyekiti
wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wakiwa tayari
meza kuu kuendesha kikao hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, mtarajiwa
Rais Dk John Magufuli, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk.
Ali Mohammed Shein na kulia niMakamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip
Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika leo. Kulis ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mweyekiti wa CCM mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein wakati wa kikao hicho cha NEC kilichofanyika leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein akijadili jambo na Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa, Rais Dk. John Magufuli wakati wa kikao hicho cha NEC kilichofanyika leo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akitoa taarifa ya maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa CCM utakaofanyika kesho, Julai 23, 2016, wakati wa kikao hicho cha NEC.
Wajumbe wa NEC na Wajume waalikwa wa NEC, wakiwa kwenye kikao hicho. Kutoka kulia ni Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Raijab Luhwavi, Katibu wa NEC Oganaizesheni Mohammed Seif Khatib na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Hamdan Meghji
Katibu wa NEC Itikasi na Uenezi na Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka wakijadiliana jambo wakati wa kikao hicho cha NEC
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati wakijadili jambo wakati wa kikao hicho cha NEC kilichofayika leo
Kiti alichokuwa amekalia Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli (kushoto), kikiwa wazi baada ya Dk. Magufuli kutoka ukumbi kutoa nafasi ya jina lake kutajwa na Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Kikwete (wapili kushoto), kwa wajumbe wa NEC leo, Kama lilivyopendekezwa na Kikao Cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika jana kwa kumpendekeza Dk. Magufuli kuwa Mweneyekiti wa CCM wa awamu ya tano. Kulia ni Makamu Kwenyekiti wa CCM Bara na Katibu Mkuu wa CCM Abduulrahman Kinana
Wajumbe wa NEC wakiwa wamenyoosha mikono kushirikia kulipitisha jina la Rais Dk. Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM, kufuatia kulipitisha, jina hilo kesho litapelekwa kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ili kupigiwa kura ya ndiyo au hapana.
Wajumbe wa NEC wakiwa wamenyoosha mikono kushirikia kulipitisha jina la Rais Dk. Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM, kufuatia kulipitisha, jina hilo kesho litapelekwa kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ili kupigiwa kura ya ndiyo au hapana.
Viongozi wa Meza Kuu wakiwa wamesimama kuwaunga mkono wajumbe waliosimama na kuamsha shamrashamra baada ya jina la Rais Dk John Magufuli kupitishwa na wajumbe katika kikao hicho cha NEC
Wajumbe wakiwa wamesimama kwa shamrashamra hizo
Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli akitoa neno la shukurani baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe wa NEC wakati wa kikao hicho cha NEC
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akimpongeza, Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli baada ya maelezo yake mazuri wakati akitoa neno la shukurani baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe wa NEC
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein,akimpongeza, Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli baada ya maelezo yake mazuri wakati akitoa neno la shukurani baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe wa NEC
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akionyesha katarasi itakayotumiwa na wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM kupiga kura
Juma Borafya kutoka Zanzibar akisimama baada ya kuteuliwa kukubali au kukataa jina la Dk. Magufuli litakapowasilishwa kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM
Mjumbe wa NEC, Waziri Kiongozi Mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha akitoa neno la shukrani mwishoni mwa kikao hicho.
Makatibu wa NEC wakiwa kazini kuhakikisha kila jambo la muhimu la kwenye kikao hicho linanukuliwa vema.
Wajumbe wakiwa amejaa ukumbini
Mweneyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akimpongeza Nahodha kwa neno lake la shukurani
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akionyesha furaha yake kabla ya kufunga kikao hicho baada ya ajenda kumalizika hatua kwa hatua.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akikifunga kikao hicho cha NEC ambacho ni cha mwisho kwake kama Mwenyekiti