Sunday, 12 June 2016
Saturday, 11 June 2016
KISESA DEVELOPMENT AGENCY
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mwanafunzi wa chuo kikKIDEA a Dar es salaamu (UDSM) ambaye pia ni mkazi Wa mkoa Wa simiyu bw. KONDELA NZUNGU, anawaomba wadau wote ambao ni wapenda maendeleo kuisaidia asasi wanayoianzisha ambayo ni KIDEA (KISESA BEVELOPMENT AGENCY) kwa lengo la kupambana na umasikini ikiwemo utoaji Wa elimu hususani katika sekta muhimu katika jamii kwani kumekuwepo na wimbi kubwa la vijana tegemezi "
tumeamua kuanzisha asasi hii kwa lengo na kuisadia jamii kiujumla hivyo basi kama malengo yetu yatakugusa tunaomba sana ushirikiano wako na support yako ili tuweze kufanikisha hayo malengo tumejaribu kadri tuwezavyo lakini imetuwia vigumu
\
kwani ni kazi kubwa inahitajika kufanyika" bw KONDELA pia anaomba pia viongozi kutoka simu kutambua umuhimu Wa asasi hii ili kuisadia serikali katika kutatua changamoto kwani wanasiasa wengi wameshindwa kutambua mchango wa vijana walio na malengo ya kupambana na majanga mbalimabali katika jamii. Yafuatayo ni malengo ya KIDEA;
1. elimu kwa jamii kuhusu kilimo cha kisasa ili kuongeza mapato ya mwaka ya wanajamii ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa chakula na kuisaidia jamii kupata mazao ya biashara ili kujikwamua kiuchumi.
2.KIDEA tutahakikisha kila mtu katika jamii anashiriki katika suala la kilimo na shughuli nyingine za kibiashara .
3.KIDEA kwa kushirikiana na mashirika, makampuni na serikali na wapenzi mbalimbali wa maendeleo tutaboresha huduma za elimu ilikuongeza upatikanaji na matumizi ya elimu bora ya awali, msingi na sekondari na kukuza machaguo kwa ajili ya elimu ya ufundi na elimu ya watu wazima kwa kuhakikisha yafuatayo;
Kuhakikisha shule za msingi na sekondari zina vyumba vya madarasa vya kutosha,
Madawati ya kutosha,
Vifaa vya kufundishia vya kutosha na
Nyumba za walimu za kutosha
(4) Kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira ili kupunguza milipuko ya magonjwa na kupinga mabadiliko ya hali ya hewa
(5)Kutoa elimu kwa jamii kuhusu umhimu wa kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu wa aina yoyote.
(6)Kuielimisha jamii juu ya umhimu wa elimu kwa vijana wa kike na kuzuia mila potofu ya kuwaozesha wakati wakiwa bado wanaendelea na masomo yao
(7).Kuielimisha jamii athari ya mimba za utotoni ( chini ya miaka 18
(8). Kutoa elimu ya kupunguza maambukizo mapya ya virusi vya ukimwi (HIV/AIDS)
(9) Kupambana na imani potofu juu ya watu wenye ulemavu (albino ) na vikongwe ambayo inapekea vifo vya watu wa aina hiyo.
(10). KIDEA kwa kushirikiana na mashirika, makampuni na serikali na jamii tutasadia kupunguza tatizo la maji katika jimbo la kisesa
(11).KIDEA kwa kushirikiana na mashirika, makampuni na serikali na wapenzi mbalimbali wa maendeleo tutaboresha huduma za afya
(12) Kutoa misaada mbalimbali kwa wajasiliamali wadogowadogo ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi
(13)Kutoa elimu ya athari ya matumizi ya madawaya kulevya kwa vijana wanaojihusisha
(14) Kuhamasisha na kuwashauri serekali kuweka mazingira mazuri naSalama ya wanafunzi ya kujifunzia
Kushirikiana na mashirika
(15) mengine ambayo yana malengo kama haya
Kuwasaidia watu ambao wameumizwa na wazazi wao kuendelea na masomo na kuwachukulia hatua wazazi wa namna hiyo kwa kushirikiana na serikali.
TUNAOMBA SANA MJITOKEZE KATIKA KUTOA SUPPORT ILI KUFANIKISHA MALENGO TAJWA HAPO JUU;
BY KONDELA NZUNGU m/kiti KIDEA 0768509696

Ajali Mbaya Yaua 6 na Kujeruhi 8, Same kilimanjaro
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Daktari aliyezungumza na chanzo cha habari hii katika Hospital ya Wilaya ya Same, Dkt Mlay, amesema wamepokea maiti sita ambazo amebainisha kuwa wanaume ni watano na mwanamke ni mmoja.
WATU
sita wamefariki dunia na wengine nane wamejeruhiwa vibaya katika ajali
iliyohusisha basi dogo la abiria aina ya Hiace lililokuwa likitokea
Mjini Same kuelekea Njoro wilayani Same, ambapo liligongana na gari ya
mizigo aina ya Fuso muda mfupi baada ya kuondoka katika kituo cha abiria
cha Same Mjini.
Daktari aliyezungumza na chanzo cha habari hii katika Hospital ya Wilaya ya Same, Dkt Mlay, amesema wamepokea maiti sita ambazo amebainisha kuwa wanaume ni watano na mwanamke ni mmoja.
Aidha,
ameongeza kuwa Majeruhi nane walipatikana kufuatia ajali hiyo, ambapo
katika Majeruhi hao nane wanawake ni wawili na wanaume sita na kati yao
waliopewa rufaa kuelekea Hospitali ya KCMC -Moshi ni watatu, wanaume
wawili na mwanamke mmoja.
Majeruhi
Noel Bakari Kanumba, aliyekuwa anatokea Mjini Same kwenda Kavambughu,
akizungumza na Mwandishi katika wodi ya Wanaume katika Hospitali ya
Same, amesema alikuwa amekaa kwenye kiti cha mbele na dereva ambapo
aligundua kuwa dereva yule alikuwa amelewa akamwonya asikimbize gari
lakini hakutaka kumwelewa, ndipo gari lilimshinda na kuhama upande wake
na kuelekea upande wa pili na kugonga Fuso upande wa dereva la Fuso hali
iliyosababisha ajali ambapo dereva na abiria wake waliokuwa wamekaa
kiti cha mbele walifariki dunia papo hapo.
Majeruhi
wengine ni Musa Chikira (35), alikuwa anatokea Mjini Same kwenda Njoro
na Mariam Omary Mbaga aliyekuwa katika wodi ya wanawake.
Majerhi wa ajali hiyo, Noel Bakari Kanumba (36), alikuwa anatokea Same Mjini akienda Kavambughu.
Majeruhi wa ajali hiyo, Musa Chikira (35), akiwa amelazwa katika wodi ya wanaume, hospital ya Wilaya ya Same.

Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Tizeba apelekwa Kilimo na Mifugo
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Rais John Pombe Magufuli leo tarehe 11 June 2016, amemteua Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi. Mhe. Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Wakati huo huo rais amemteua mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na uvuvi, nafasi iliyokua ikishikiliwa na Mhe. Nchemba.
Wateuliwa wataapishwa siku ya Juma tatu majira ya saa 3:00 asubuhi Ikulu.

Wabunge wa Kambi ya Upinzani Wajitoa Kamati ya Bunge ya Ukimwi Baada ya IKULU Kuwanyiima Kibali cha Kwenda Marekani
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Ofisi ya Rais Ikulu imewanyima vibali vya kusafiri kwenda Marekani wabunge wawili wa Kambi ya Upinzani, bungeni na kumruhusu mbunge wa Geita Mjini (CCM), John Kanyasu.
Wabunge hao wa kambi ya upinzani waliochaguliwa kwenda Marekani ni Savelina Mwijage (CUF) na Mwita Mwaikabwe (Chadema)

Wabunge
hao watatu ni wajumbe wa Kamati ya Masuala ya Ukimwi, lakini baada ya
kunyimwa vibali hivyo wamejitoa kwenye kamati hiyo wakipinga kitendo
hicho.
Akizungumza
na waandishi wa habari bungeni mjini Dodoma, mbunge wa Ukonga
(Chadema), Mwita Mwikwabe alisema walipata barua ya kuteuliwa kushiriki
safari hiyo kutoka Ofisi ya Bunge Mei 24.
“Tunapenda
kukufahamisha kuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amekuteua
kushiriki mkutano wa ngazi ya juu ya maamuzi kuhusu Ukimwi duniani
utakaofanyika 08-10 New York, Marekani,” alinukuu barua hiyo iliyosainiwa na Patson Sobha kwa niaba ya Katibu wa Bunge.
Katika barua hiyo wametajwa wabunge wengine kwenye safari hiyo kuwa ni mbunge wa viti maalum (CUF), Savelina Mwijage.
“Nikiwa
Tarime nilipata simu kutoka kwa Patson kwamba, Naibu Spika alipokea
simu kutoka Ikulu kuwa imezuia vibali vyetu vya kwenda Marekani na
badala yake Kanyasu ameteuliwa,” alisema Mwikabe.
“Tunashangaa, kuteuliwa tuliambiwa kwa barua, lakini kukataliwa tuliambiwa kwa simu,” alisema Mwita.
Alisema kutokana na kutopewa kibali, wajumbe wote wa kambi hiyo wamejitoa kwenye Kamati ya Bunge ya Ukimwi.
“Hayo yote yanafanyika kwa sababu Naibu Spika hatupendi kabisa wabunge wa upinzani ndiyo maana wametufanyia haya,” alisema.
Kwa
upande wake, mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia alisema
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaambia katika mkutano wa wabunge wote
kuwa hawahusiki katika uombaji wa vibali kutoka Ikulu.
“Mimi mwenyewe nimeshawahi kusafiri zaidi ya mara tatu mbona sijawahi kuomba kibali kutoka Ikulu?” alihoji Mbatia.
Katibu
wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alihoji kama wabunge hao ndiyo wenye
haki ya kusafiri. Pia alihoji haraka waliyonayo wabunge hao wakati
walishapeleka malalamiko yao kwa maandishi dhidi ya Naibu Spika, Dk
Tulia Ackson.
“Kwani
wanaharaka gani wao? Si walishapeleka malalamiko hayo na yapo kwenye
kamati. Wasubiri uamuzi ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya
Bunge),” alisema.