Saturday, 11 June 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya June 11

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Friday, 10 June 2016

MPYA:KANUSHO KUHUSU KUSAMBAA KWA TAARIFA KUSITISHWA KWA AJIRA ZA WALIMU 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

VIDEO:NUH MZIWANDA FT ALIKIBA-JIKE SHUPA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Nuh Mziwanda Ft. Ali Kiba (Official Video) - Jike Shupa | Download Mp4


Share:

Mpya:hizi ndio kozi vipaumbele kwa wanafunzi wanaoomba mkopo 2016/2017.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

habari yako,

MASWAYETU BLOG kwa upendo mkubwa tumeamua kukuletea hapa vipaumbele vya wanafunzi watakaopata mkopo serikali ya zanzbar mwaka wa masomo 2016/2017.

Kwa kuwa mkopo unatolewa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,sio vibaya ukajaribu kuona ni kozi zipi zinazotakiwa na serikali ya zanzbar ili kujihakikishia mkopo na ajira.

ANGALIA HAPO CHINI

>>>>>>>VIPAUMBELE VYA WATAALAMU<<<<<<
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Juni, 2016 amemuapisha Mhe. Jaji Shaaban Ali Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Juni, 2016 amemuapisha Mhe. Jaji Shaaban Ali Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu Jijini Dar es salaam.
Kabla ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Jaji Shaaban Ali Lila alikuwa Jaji Kiongozi.
Wakati huohuo, Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi.
Kabla ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Jaji Kiongozi, Mhe. Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mkoani Tanga.
Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Leons Katipwa Wambali amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Shaaban Ali Lila ambaye amekua Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Katika hatua nyingine, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameagana na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Saoud Ali Mohamed al Ruqaishi ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.
Akizungumza na Balozi huyo, Ikulu Jijini Dar es salaam Rais Magufuli ameishukuru Oman kwa kuendeleza ushirikiano na uhusiano wa kihistoria na kidugu na Tanzania, na ameahidi kuwa serikali yake ya awamu ya tano ipo tayari kuongeza ushirikiano huo.
Mhe. Rais Magufuli pia amemuomba Balozi Saoud Ali Mohamed al Ruqaishi kufikisha salamu zake kwa Sultani wa Oman Mtukufu Qaboos bin Said al Said na kumueleza kuwa Tanzania inawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Oman na inatarajia kuona miradi ya ushirikiano katika uwekezaji ukiwemo mradi wa Bagamoyo inaanza kutekelezwa haraka.
"Naomba umfikishie salamu zangu za dhati Mtukufu Qaboos bin Said al Said, Sultan wa Oman na umwambie tunamkaribisha Tanzania na nitafurahi kuona mradi wa uwekezaji wa Bagamoyo unakuwa kielezo cha undugu na urafiki wetu uliodumu kwa miaka mingi" Amesema Rais Magufuli.
Tanzania kwa kushirikiana na nchi za Oman na China zimekubaliana kutekeleza mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
10 Juni, 2016
Share:

Best Nasso - Ukweli Uko Wapi? | Mp3 Download [New Song]

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
https://my.notjustok.com/track/download/id/99705/by/s9mCIK28YA
Share:

New AUDIO | Chemical Ft. Msaga Sumu - KAMA IPO IPO TU | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
DOWNLOAD via MKITO
http://mkito.com/song/11924?referrer=083dd3e411d7220a456da5c5be830337f71f6ee9
Share:

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI, DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) UNAORATIBIWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI,
DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) UNAORATIBIWA NA
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)


Tarehe 3 Juni 2016 ilikuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya udahili wa kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada ya Kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) unaoratibiwa na NACTE.

Baraza linapenda kuwaarifu waombaji udahili wa kozi tajwa hapo juu na umma kwa ujumla kuwa, kwa sasa maombi yote yaliyowasilishwa mpaka tarehe 3 Juni 2016 saa sita usiku yameanza kuchambuliwa kwa ajili ya kuchagua waombaji wenye sifa stahiki. Zoezi la kuchambua waombaji udahili na hatimaye kuchagua waombaji wenye sifa stahiki na waombaji hao kuidhinishwa na mamlaka husika na kutangazwa litachukua muda wa wiki nne (4) kuanzia tarehe 3 Juni, 2016.

Baraza linatambua uwepo wa waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kuwasilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016. Waombaji wa namna hii na wengine wanaopanga kuwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) wanaombwa kuwa na subira mpaka hapo majina ya waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya kufungwa kwa mfumo watakapotangazwa.

Baada ya kutangazwa majina ya waombaji waliochaguliwa, Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) utafunguliwa tena kwa ajili ya kujaza nafasi za udahili ambazo zitakuwa hazijajazwa na waombaji waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi, 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016.

Baraza linatarajia kufungua tena Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kwa ajili ya kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada ya Kwanza wiki ya mwishoni mwa mwezi wa Sita, 2016.

Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 9 Juni, 2016
Share:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 10.6.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

IMG_20160610_044730
IMG_20160610_044755
IMG_20160610_044807
IMG_20160610_044819
IMG_20160610_044843
IMG_20160610_044857
IMG_20160610_044911
IMG_20160610_044928
IMG_20160610_044943
IMG_20160610_044957
IMG_20160610_045033
IMG_20160610_045059
IMG_20160610_045110
IMG_20160610_045129
IMG_20160610_045148
IMG_20160610_045209
IMG_20160610_045222
IMG_20160610_045238
IMG_20160610_045259
IMG_20160610_045312
IMG_20160610_045330
IMG_20160610_045518
IMG_20160610_045411
IMG_20160610_045432
IMG_20160610_045457
IMG_20160610_044515
IMG_20160610_044528
IMG_20160610_044542
IMG_20160610_044558
IMG_20160610_044614
IMG_20160610_044629
IMG_20160610_044642
IMG_20160610_044656
IMG_20160610_044717
IMG_20160610_044730
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger