Monday, 18 April 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI TAREHE 18.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Sunday, 17 April 2016

ANGALIA HAPA MATOKEO YA UE 2016 CHUO CHA SUA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Je,umeangalia matokeo yako na umeshindwa kuyaona kwa sababu mtandao unasumbua?Pata kuangalia hapa matokeo yako ya UE kwa wanafunzi wa SUA kwa link ya uhakika bila kukwama.


<<<<<<PLEASE CLICK HERE>>>> 

Please share na wenzako
its innocent the blogger boy!
Share:

TUNDAMAN APATA AJALI YA GARI IRINGA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Muimbaji wa Tip Top Connection, Tundaman, amepata ajali mbaya ya gari Jumapili hii. Ajali hiyo imetokea katika eneo liitwalo Idetelo, Nyololo katika mji wa Makambako wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Aurion

Aliyekuwa dereva wa gari hilo amepoteza maisha na mwili wake umehifadhiwa kwenye hospitali ya wilaya ya Mufindi.


Meneja wa kundi hilo, Babutale amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

“Nimepokea simu nyingi za kuulizwa hali ya msanii wangu @tundamantz mungu mkubwa ametoka salama ingawa wamepata mtihani mkubwa wa kumpoteza dereva aliyekua anaendesha gari yao amefariki Hapo Hapo. Kazi yake mola aina makosa,” ameandika Tale kwenye Instagram.
Share:

Tangazo la Usaili 20 Aprili 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Image result for serikali ya tanzania 
PropertyValue
Name:Tangazo la Usaili 20 Aprili 2016
Description:TANGAZO LA KUITWA KAZINI 16 MACHI, 2016 Wasailiwa wote wanakumbushwa kufika na vyeti halisi (Orijinal Cerificates)
Filename:TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI 20 Aprili 2016.pdf
Filesize: 629.41 kB
Filetype:pdf (Mime Type: application/pdf)
Creator:psrsweb
Created On: 04/14/2016 19:11
Viewers:Everybody
Maintained by:Editor
Hits:25492 Hits
Last updated on: 04/14/2016 19:17
Homepage:
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRIL TAREHE 17.4.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
20160417_042648
20160417_042704
20160417_042728
20160417_042742MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRIL TAREHE 17/4/2016
20160417_042755
20160417_042815
20160417_042832
20160417_042844
20160417_042857
20160417_042907
MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRIL 17 2016
20160417_042907
20160417_042921
20160417_042934
20160417_042948
20160417_042959
20160417_043012
20160417_043021
20160417_043036
20160417_043047MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRIL TAREHE 17-4-2016
20160417_043100
20160417_043108
20160417_043120
20160417_043133
20160417_043216
20160417_043228
Share:

Saturday, 16 April 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAISI::YAHUSU TAARIFA YA KUZIMWA KWA DATA KWENYE MAKAMPUNI YA SIMU

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 
Share:

Takukuru kukata rufaa hukumu ya Mhando wa Tanesco

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Siku moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumwachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, William Mhando, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inaandaa utaratibu wa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo. 
Aprili 14, mwaka huu Mahakama hiyo ilimwachia huru Mhando na wenzake wanne akiwamo mkewe, Eva na maofisa watatu wa Tanesco; Francis Mchalange, Sophia Misida na Naftali Kisinga waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya fedha. 
Mashtaka mengine yaliyokuwa yakiwakabili ni kughushi  na kuwasilisha nyaraka za uongo kwa mamlaka za Serikali. 
Hata hivyo, washtakiwa hao waliibwaga Takukuru baada ya mahakama kuona kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha tuhuma hizo.
 Akisoma hukumu hiyo kwa niaba ya Hakimu Mkazi Mkuu, Kwey Rusema, Hakimu Hellen Riwa alisema kwa mujibu wa ushahidi, suala la msingi lilikuwa ni mkataba kati ya kampuni ya Santa Clara Supply Limited na Tanesco. 
Alisema katika mkataba, Mhando alikuwa mshtakiwa wa kwanza, akituhumiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kushindwa kutangaza masilahi yake kwa kampuni ya Santa Clara inayomilikiwa na Eva ambaye ni mkewe.
 “Suala la msingi ni kujiuliza ni vipi mshtakiwa huyo alihusika katika utoaji wa zabuni na nani aliyekuwa na uamuzi wa mwisho,” alisema. 
 Taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Tunu Mley ilisema imefikia uamuzi huo baada ya wadau wengi kuhitaji kujua hatua zitakazochukuliwa na chombo hicho baada ya hukumu hiyo. 
“Takukuru inawataka wadau na wananchi kwa ujumla kutambua kwamba ni utaratibu wa kisheria kwamba upande mmoja usioridhika na hukumu iliyotolewa kukata rufaa katika mahakama ya juu,” ilieleza taarifa hiyo.
Baada ya hukumu hiyo juzi, Wakili wa Takukuru, Leonard Swai aliomba Mahakama kuingilia kati.
Share:

Rais Magufuli Aweka jiwe la Msingi ujenzi wa Barabara ya Juu katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela jijini Dar leo

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale akitoa maelezo kwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi ujwenzi wa Barabara ya Juu (FlyOver) kwenye makutano ya Barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara, Jijini Dar es salaam leo.
Share:

MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA 2016 SHULE YA TUSIIME SECONDARI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


 WANAFUNZI 469 wa kidato cha Sita Sekondari ya Tusiime ya Tabata jijini Dar es Salaam leo wamehitimu kidato cha Sita katika mahafali yaliyo fanyika shuleni hapo. Pichani ni wahitimu mbali wa kidato cha sita wakiwa katika kusanyiko la mahafali.


 Meza kuu ya mgeni rasmi.
 Wazazi nao wapo wanafuatilia vitu mbalimbali 

Share:

MECHI ZA LEO JUMAMOSI LIGI KUU YA UINGEREZA-EPL APRIL 16 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Tangazo la Kazi Mohammed Enterprises Tanzania limited

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mohammed Enterprises Tanzania limited, agriculture division is now hiring for the below positions. The requirements and criteria for applications are as below:

Assistant Managers and Managers
Field Officers

Graduate in Agriculture with 5 to 8 years of experience working on the farms
Must have strong man management skills
Must be confident, positively aggressive and a hands on person
Must have good communication and interpersonal skills
Must have dealt with unions

Personnel officers :
Graduate in HR with 3-5 years of experience in operational HR role
Must have dealt with CMA and Unions and should be well aware of disciplinary procedures
Computer savvy with communication and translation skills (English)

APPLICATION INSTRUCTIONS:

We are looking for candidates who are ready to work and stay on our agriculture farms.
Interested candidates may send their CV only through recruitment@metl.net 
Female candidates are encouraged to apply.
Only shortlisted candidates will be contacted.
Share:

Manispaa ya Kinondoni Inayoongozwa na UKAWA Yasema Itawalipia Wananchi wake Wote Bima za Afya

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Manispaa  ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, inayoongozwa na Chama cha Demkrasia na Maendeleo (Chadema), chini ya Ukawa imeanza kazi kwa staili ya aina yake baada ya kutangaza neema ya bima ya afya kwa wananchi wa Manispaa hiyo.

Imeahidi kuanzisha mpango maalum ambao kila mwananchi wa Manispaa hiyo atachangia Sh. 40,000 kwa mwaka ili aunganishwe na mpango wa matibabu wa bima ya afya ambao utawawezesha kupata matibabu ya bure katika hospitali mbalimbali.

Mpango huo utaanza kutekelezwa mwezi Juni mwaka huu, huku bajeti ya Manispaa hiyo ikiongezeka kwa asilimia 59 kutokana na kukua kwa mapato ya ndani.

Wazee wa Manispaa hiyo nao wametangaziwa neema ya matibabu bure kwani watapewa kadi maalum zitakazowawezesha kutibiwa hospitali za umma.

Mapato hayo yametokana na ukusanyaji madhubuti katika kodi za majengo, mabango, leseni za biashara, huduma za kuegesha magari, hoteli na ruzuku ya serikali kuu.

Bajeti ya mwaka 2016/2017 katika Manispaa hiyo inafikia Sh. Bilioni 248.47 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana ambayo ilikuwa ya Sh. Bilioni 156.24.

Katika bajeti ya mwaka huu kuna ongezeko la Sh. zaidi ya bilioni 92.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob aliwasilisha bajeti hiyo jana jijini Dar es Salaam katika kikao cha Baraza la Madiwani.

Baada ya kuwasilisha bajeti hiyo, Madiwani wote wakiwamo wa upinzani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliipitisha kwa kauli moja ili ianze kuwahudumia wananchi.

Akisoma bajeti hiyo, Jacob alitaja ukusanyaji wa mapato ya ndani umeingiza Sh. bilioni 64.28 na kwamba imeongezeka kutoka Sh. bilioni 56.6 za mwaka jana.

Licha ya bajeti ya mwaka huu kulenga kugharamia huduma za matibabu, lakini imelenga kujenga shule ya bweni katika Kata ya Goba kwa gharama ya Sh. milioni 250, ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule, kujenga vyumba vya madarasa na ununuzi wa madawati 30,000.

Kazi nyingine zitakazofanyika ni pamoja na ujenzi wa Barabara kuelekea kituo cha daladala cha ya Simu 2000 na Barabara ya Akachube ambazo zimetengewa Sh. bilioni 50.

Kuhusu suala la usafi, Meya Jacob alisema kila Kata itakuwa na gari lake la kuzolea takataka na Manipaa imetenga Sh. 2.2b .
 
Manispaa hiyo ina jumla ya Kata 25 na Sh. bilioni 3.6 zimetengwa kwa ajili ya gharama za kusafirisha takataka.

Aidha, katika bajeti hiyo, Manispaa inatarajia kununua Trekta lenye kijiko kwa ajili ya kutengeneza barabara na zimetengwa Sh. bilioni 1 kwa ajili ya kazi hiyo.

Kazi nyingine za fedha hizo ni kuweka sakafu ngumu katika masoko yote ya manispaa, ili kuondoa adha ya uchafu na matope katika msimu wa mvua na zimetengwa Sh. bilioni 1.65.

Kuhusu vijana na wanawake Manispaa hiyo imetenga Sh. bilioni 4.7 kwa ajili ya kuwakopesha na kila Kata itapata Sh. milioni 200.
Share:

BIBI KIZEE ABAKWA MKOANI SINGIDA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Pichani ni Bibi kizee mwenye umri wa miaka 84 na mkazi wa Kijiji cha Chungu, tarafa ya Ihanja, wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida akiwa amebebwa na mmoja wa ndugu zake wakati akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mjini Singida kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili kijana mmoja mwenye umri wa miaka 32 (jina lake halikupatikana) anayetuhumiwa kumbaka bibi kizee huyo kwa mara ya tatu sasa ndipo walipofanikiwa kumkamata. (Picha Na Jumbe Ismailly)
Share:

BUNGE LATOA UFAFANUZI KUHUSU MKATABA WA LUGUMI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kupotosha umma na baadhi ya vyombo vya Habari kuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipokuwa ikitekeleza majukumu yake tarehe 5 Aprili, 2016 ililitaka Jeshi la Polisi kuwasilisha Mkataba ulioingiwa Kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System).

Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili kwamba, taarifa hizo si za kweli na zina lengo la kupotosha umma kutokana na kile kilicho amuliwa na kamati hiyo. 
Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba tarehe 5 Aprili, 2016, kamati hiyo ilikutana na kujadili Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi la Polisi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo mengine ilibaini dosari katika utekelezaji wa mkataba huo.

Kutokana na dosari hizo, kamati iliomba Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua. 
Kufuatia agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo tarehe 12 Aprili, 2016 ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Afisa Masuhuli.

Aidha, Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani tarehe 12 Aprili, 2016 kuwasilsha Taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha tarehe 5 Aprili 2016 kabla ya tarehe 18 Aprili, 2018 kama ilivyoshauriwa na kamati . 
Hivyo ni vyema Umma ukafahamu kuwa kilichoombwa na Kamati ni Maelezo ya utekelezaji wa Mkataba huo na sio Mkataba kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari ambapo Ofisi ya Bunge iliomba maelezo hayo yawasilishwe kabla ya tarehe 18 Aprili, 2016.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM 15 Aprili, 2016.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger