Tuesday, 16 February 2016
Monday, 15 February 2016
Ugonjwa sugu wa figo (Chronic Kidney Disease)-2
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
UGONJWA WA FIGO HUSABABISHA KISUKARI
Leo tunaendelea kuelezea ugonjwa sugu wa figo kwa kuanzia na jinsi unavyosababisha matatizo ya kisukari. Endelea.
Kisukari cha aina ya 1 na ya 2 husababisha hali iitwayo kisukari cha figo au kwa kimombo Diabetic Nephropathy. Shinikizo la damu kama lisipodhibitiwa vyema, baada ya muda fulani husababisha madhara katika figo.
Pia magonjwa ya kurithi ya figo kama vile Polycystic Kidney Disease (PKD). PKD huambatana na hali ya kuwa na vimbe ndogondogo zilizojaa maji katika figo.
Vimbe hizi hufanya figo ishindwe kufanya kazi zake sawasawa na hivyo kusababisha ugonjwa sugu wa figo.
Vilevile matumizi ya kila siku ya muda mrefu ya baadhi ya madawa ya kutuliza maumivu kama vile Ibuprofen au Acetaminophen yanaweza pia kusababisha ugonjwa sugu wa figo. Hali hii huitwa kitaalamu Analgesic Nephropathy.
Matumizi ya baadhi ya madawa kama Antibiotics za Aminoglycosides kama vile Gentamicin pia husababisha madhara katika figo na hatimaye ugonjwa sugu wa figo.
Kadhalika hali ya mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye figo kuzeeka, kuwa migumu kiasi cha kushindwa kutanuka na kusinyaa. Atherosclerosis husababisha upungufu mkubwa wa damu katika figo husika, kwa kitaalamu hali ambayo inaweza pia kusababisha madhara zaidi kwa figo na hatimaye ugonjwa sugu wa figo.
Magonjwa kama vijiwe katika figo, kuvimba tezi dume, kuziba kwa njia ya mkojo pamoja na saratani, vyote vinaweza pia kusababisha madhara katika figo na hatimaye kusababisha ugonjwa sugu wa figo.
Vyanzo vingine vya ugonjwa sugu wa figo ni pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi ambayo husababisha hali inayoitwa HIV Nephropathy, ugonjwa wa upungufu wa damu mara kwa mara yaani Sickle Cell, unaweza kusababisha kuziba kwa mirija inayosambaza damu kwenye figo au upungufu wa damu kwenye figo.
Pia matumizi ya madawa ya kulevya, maambukizi sugu katika figo na saratani za figo. Mtu aliye na mojawapo ya vitu au magonjwa haya ana hatari kubwa ya kupata ugonjwa sugu wa figo.
USHAURI
Wenye matatizo haya, hawana budi kuhakikisha kuwa figo zao zinafanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara ili kuangalia utendaji kazi wake.

Mungu aliyekupa, amemchukua na ndiye atakupa mwingine
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Asante Mungu Valentine’s Day imepita salama hapo jana (Jumapili) japokuwa najua wapo waliopata misukosuko ya hapa na pale. Natumia nafasi hii kuwatakia mfungo mwema (Kwaresma) kwa Wakristo wote duniani na mfungo huu uwe mwanga wa maisha yetu mema kwa siku zote.
Mada ya Jumatatu hii inalenga kuwafariji wale wote ambao wamefikwa na masaibu mbalimbali kwenye uhusiano wao, hasa wale ambao wenza wao wametangulia mbele ya haki (wameaga dunia) mara tu baada ya kuanzisha uhusiano wao. Poleni sana!
Msomaji ambaye pengine unahisi kama ni mtu mwenye mikosi katika uhusiano kwa kupata mchumba, mke au mume na ndani ya muda mfupi akafariki dunia akiwa mikononi mwa penzi lako, tafadhali usiwaze wala kusononeka moyoni, ndivyo dunia ilivyo.
Ni kweli ulimpenda, alikuheshimu na pengine alikuwa msaada na tegemeo katika maisha yako na watu wengine waliowazunguka. Pamoja na hayo yote, nakusihi usisononeke, ulimpenda ila Mungu amempenda zaidi.
Amini nakwambia, Mungu ndiye aliyekupa, ndiye aliyempenda zaidi yako na Mungu huyohuyo atafanya njia pasipo na njia, naamini atakupa mwenza mwingine atakayerejesha furaha ya maisha yako daima.
Najua ni namna gani unaumia, pengine uchumba au penzi lenu lilikuwa bado bichi, bado pevu kama mwezi angavu mara umpendaye akakutoka, inauma, inasikitisha kibinadamu, inakatisha tamaa, wakati mwingine unahisi hautapenda na wala hautapata tena mpenzi mwingine kama yule, la hasha! Utapata, mwamini Mungu hajawahi kushindwa na wala hatashindwa.
Usijione huna thamani ya kuwepo au kuishi katika dunia hii bila ya uliyempenda. Yawezeka ilikuwa ni siku chache tu tangu ajitambulishe au umtambulishe kwa wazazi wako au tangu akuvishe pete ya uchumba na pengine tangu mfunge ndoa au mlipotoka tu kwenye fungate (honeymoon) naye akatoweka duniani.
Ni vigumu kuvumilia kwa mtu uliyempenda, uliyemthamini akakuthamini, mliyependana na kuheshimiana, mliyefurahia penzi lenu, leo haupo naye kimwili, ingawa kiimani unaweza kuendelea kuwa naye.
Safu hii ya XXLove inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki, wapenzi, wachumba au wanandoa waliofiwa na wenza wao, tambua kuwa pamoja na yote hayo, maisha bado yapo na yanatakiwa yasonge kwani sote ni wasafiri.
Na hata dini zetu zinaamini katika uwepo wa kifo kama njia ya kurejea kwake muumba, hivyo jipe moyo, tumaini kuwa ipo siku utapata tena neema.
Kweli kuna pengo kubwa kuanzia moyoni hadi maishani mwako, kuna kitu cha kipekee unakimisi kutoka kwake, unamisi tabasamu, utani, ucheshi nk.
Unakumbuka mengi, rangi za nguo alizokuwa akizipenda, chakula alichokipenda, harufu ya manukato na unakumbuka ustadi wake mlipokuwa faragha.
Mpenzi msomaji pata japo muda mchache wa kumkumbuka ndugu, rafiki, mpenzi, mke au mume wako aliyetangulia mbele za haki, muombee bila kujali alikufa mkiwa katika hali gani, mathalan ya kutoelewana kisha sema Amen!
Tuma maoni yako kama ni mmoja wa walengwa na yatatoka wiki ijayo kwenye safu hii.Kwa habari, ushauri zaidi kuhusu mapenzi, tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook, tu-follow Insta:@mimi_na_uhusiano au kujiunga kwenye group letu la WhatsApp.

Hatimaye Jide apewa talaka rasmi kortini
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
DAR ES SALAAM: BAADA ya mvutano wa muda mrefu, hatimaye diva wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ amepewa talaka rasmi kwenye Mahakama ya Manzese, Sinza jijini Dar.
Jide alifungua kesi ya madai ya talaka katika mahakama hiyo baada ya kutofautiana na mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash ‘Captain’, aliyekuwa mumewe wa ndoa kabla ya kumwagana takriban miaka miwili iliyopita.
Baada ya taarifa hizo kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwanahabari wetu alimtafuta Jide ili aweze kuzungumzia hatua hiyo waliyoifikia lakini simu yake haikuwa hewani kama ilivyokuwa kwa Gardner lakini bahati nzuri mmoja wa ndugu wa mrembo huyo mkongwe wa Bongo Fleva aliyeomba hifadhi ya jina alipatikana na kufunguka:
“Ni kweli tulikuwa mahakamani. Jide ameshapewa talaka yake na kila kitu kimeenda vizuri. Gardner naye kapewa hati yake ya talaka hivyo kuanzia sasa kila mmoja yupo huru kufanya yake.”
Judith Wambura Mbibo ‘Jide
Stori: Erick Evarist, WikiendaDAR ES SALAAM: BAADA ya mvutano wa muda mrefu, hatimaye diva wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ amepewa talaka rasmi kwenye Mahakama ya Manzese, Sinza jijini Dar.
Jide alifungua kesi ya madai ya talaka katika mahakama hiyo baada ya kutofautiana na mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash ‘Captain’, aliyekuwa mumewe wa ndoa kabla ya kumwagana takriban miaka miwili iliyopita.
Gardner G. Habash ‘Captain’
Taarifa kutoka kwa chanzo cha kuaminika,
wawili hao waliooana mwaka 2005, walitinga katika viunga vya mahakama
hiyo Alhamisi iliyopita kisha hukumu ya kesi hiyo kusomwa na talaka
rasmi kutolewa kwa Jide na Gardner.
“Nimemuona Jide na Gardner hapa, wamekuja kusikiliza hukumu yao.
Taarifa za uhakika ni kwamba tayari mahakama imevunja rasmi ndoa na kila
mmoja kapewa hati yake ya talaka na sasa kila mtu yupo huru kuendelea
na maisha yake,” kilisema chanzo.Baada ya taarifa hizo kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwanahabari wetu alimtafuta Jide ili aweze kuzungumzia hatua hiyo waliyoifikia lakini simu yake haikuwa hewani kama ilivyokuwa kwa Gardner lakini bahati nzuri mmoja wa ndugu wa mrembo huyo mkongwe wa Bongo Fleva aliyeomba hifadhi ya jina alipatikana na kufunguka:
“Ni kweli tulikuwa mahakamani. Jide ameshapewa talaka yake na kila kitu kimeenda vizuri. Gardner naye kapewa hati yake ya talaka hivyo kuanzia sasa kila mmoja yupo huru kufanya yake.”
Kisa utajiri wenye maswali, Zari atajwa freemason
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Habari kutoka Kampala, Uganda zilizoripotiwa hivi karibuni zilieleza kwamba, mwanamama huyo ana ukaribu mkubwa na matajiri wa Nigeria ambao wanaaminika kuwa utajiri wao ulitokana na kuwa ‘memba’ wa mtandao huo mkubwa duniani.
Katika habari hiyo, wengine waliotajwa ni pamoja na aliyekuwa mumewe aliyezaa naye watoto watatu, Ivan Semwanga, wachungaji maarufu nchini humo na wanamuziki kama Joseph Mayanja ‘Jose Chameleone’ na Bebe Cool.
Zari anayemiliki hoteli ya kifahari iliyopo kwenye Mtaa wa Kagwa, Kampala nchini Uganda, anasemekana kumiliki vyuo vya urembo na maduka ya vipodozi nchini Afrika Kusini huku akijiingizia mkwanja kupitia shoo zake za Zari All White Party anazozifanya kwenye nchi za Afrika Mashariki za Uganda, Tanzania na Kenya.
Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Zari hakupatikana badala yake aliyezungumzia ishu hiyo ni mpenzi wake, Diamond ambaye alisema kuwa mama mtoto wake ana miradi mingi na siyo kama wanawake wa mjini ambao wanabweteka badala ya kutafuta mkwanja.
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’
Stori: Musa mateja, Wikienda
Dar es Salaam: Mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ameorodheshwa kwenye
listi ya watu maarufu nchini Uganda ambao ni wanachama wa jamii ya siri
ya Freemason kisa kikielezwa kuwa ni utajiri alionao wenye maswali
mengi.Habari kutoka Kampala, Uganda zilizoripotiwa hivi karibuni zilieleza kwamba, mwanamama huyo ana ukaribu mkubwa na matajiri wa Nigeria ambao wanaaminika kuwa utajiri wao ulitokana na kuwa ‘memba’ wa mtandao huo mkubwa duniani.
Gari la Zari.
Ilidaiwa kwamba, Zari amekuwa akifanya kufuru ya fedha
zinazowashangaza wengi, kuwa kwa muziki au biashara gani anazofanya
zinazomuingizia mkwanja mrefu kiasi cha kumiliki magari ya kifahari kama
Lamborghini na Hummer ambayo yote ameyaandika majina yake badala ya
namba za usajili.Katika habari hiyo, wengine waliotajwa ni pamoja na aliyekuwa mumewe aliyezaa naye watoto watatu, Ivan Semwanga, wachungaji maarufu nchini humo na wanamuziki kama Joseph Mayanja ‘Jose Chameleone’ na Bebe Cool.
Zari anayemiliki hoteli ya kifahari iliyopo kwenye Mtaa wa Kagwa, Kampala nchini Uganda, anasemekana kumiliki vyuo vya urembo na maduka ya vipodozi nchini Afrika Kusini huku akijiingizia mkwanja kupitia shoo zake za Zari All White Party anazozifanya kwenye nchi za Afrika Mashariki za Uganda, Tanzania na Kenya.
Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Zari hakupatikana badala yake aliyezungumzia ishu hiyo ni mpenzi wake, Diamond ambaye alisema kuwa mama mtoto wake ana miradi mingi na siyo kama wanawake wa mjini ambao wanabweteka badala ya kutafuta mkwanja.
Nay wa Mitego: nitauawa muda wowote
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
DAR ES SALAAM: Hali ni tete! Siku chache baada ya nyota wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuwasiliba wasanii wenzake kwenye wimbo wake mpya wa Shika Adabu Yako, ameibuka akidaiwa kujisalimisha polisi kufuatia kutishiwa kuuawa na watu asiowafahamu.
CHANZO CHAWEKA WAZI
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya kuachia wimbo huo, jioni yake tu, Nay alipigiwa simu na watu asiowafahamu wakimtaka aupotezee wimbo huo kabla haujamgharimu maisha kwa njia yoyote ile.
APUUZA, ATUMIWA MESEJI
Chanzo kilidai kuwa, Nay alipuuzia simu hizo lakini alishangaa ilipofika asubuhi siku iliyofuata, alikuta ujumbe wa maneno (SMS) kwenye simu yake ukiwa na maneno makali na ya kuendelea kumtishia kifo.
KWENDA POLISI
Imezidi kudaiwa kwamba, baadhi ya watu wake wa karibu na mama yake mzazi, walimshauri aende akaripoti Kituo cha Polisi Kimara (jirani na nyumbani kwake) kwa vile anaweza kupata matatizo makubwa.
MAMA YAKE ANALIA TU
“Mbaya zaidi, mama yake naye, amepaniki kiasi kwamba analia tu. Inabidi sisi ndiyo tumpe moyo maana anafikiria hatima ya mwanaye kwani kila anapokwenda akikutana na watu wanamlalamikia juu ya wimbo huo,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Nay kutaka kujiridhisha kuhusu madai hayo lakini hakuwa hewani. Ilibidi kumtafuta mtu wa karibu yake na ndipo alipopatikana.
Naye alikiri kutishiwa kuuawa. Alisema hatua ya awali alichukua uamuzi wa kwenda Kituo cha Polisi Kimara, Dar lakini hakufunguliwa faili la kesi kwa maelezo kuwa, usiku huo askari wasingeweza kufanya hivyo badala yake walimtaka arudi kesho yake.
HUYU HAPA NAY
“Hapa nilipo nimechanganyikiwa. Kwa hali ilivyo nimeona bora niende polisi maana najua nitauawa wakati wowote. Nilikwenda Polisi Kimara lakini sikufanikiwa, sasa najiongeza, nitakwenda Kituo cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (kwa Kamanda Simon Sirro).
Wikienda: “Nimesikia unakwenda Lindi kwenye shoo, sasa huko Polisi Kanda Maalum umeshakwenda au utakwenda ukirudi?”
Nay: “Kwanza nilikwenda polisi pale Kimara, wakashindwa kufungua faili. Waliniambia niende asubuhi lakini nimeshindwa kwa kuwa nimeondoka Dar na hapa nipo Lindi.
“Ila kuna ujumbe nimeukuta Insta (Instagram) ni mbaya sana. Nimepanga nikirudi nienda Kanda Maalum, lakini kuna wenzangu niliokuja nao hapa Lindi wamenishauri niende Kituo cha Polisi Kikuu cha hapahapa nikaripoti.”
TIMU WEMA WAMFANYA VIBAYA
Wakati huohuo, wadau wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu (Team Wema), wanadaiwa kuchukua picha ya mrembo huyo akiwa kwenye gari na kuipachika sura ya Nay ili aonekane ni demu.
Kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, picha hiyo imeenea huku wengi wakikitafsiri kitendo hicho kuwa ni cha kutaka kumdhalilisha Mbongo Fleva huyo aonekane ni shoga.
Katika wimbo huo ulioleta figisufigisu, kuna kipengele Nay alisema Wema hana mimba bali anatafuta kiki ya msimu hali iliyotibua hasira za Team Wema.
Nyota wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Stori: Musa Mateja, WIKIENDADAR ES SALAAM: Hali ni tete! Siku chache baada ya nyota wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuwasiliba wasanii wenzake kwenye wimbo wake mpya wa Shika Adabu Yako, ameibuka akidaiwa kujisalimisha polisi kufuatia kutishiwa kuuawa na watu asiowafahamu.
CHANZO CHAWEKA WAZI
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya kuachia wimbo huo, jioni yake tu, Nay alipigiwa simu na watu asiowafahamu wakimtaka aupotezee wimbo huo kabla haujamgharimu maisha kwa njia yoyote ile.
APUUZA, ATUMIWA MESEJI
Chanzo kilidai kuwa, Nay alipuuzia simu hizo lakini alishangaa ilipofika asubuhi siku iliyofuata, alikuta ujumbe wa maneno (SMS) kwenye simu yake ukiwa na maneno makali na ya kuendelea kumtishia kifo.
Picha iliyotengenezwa kumdhalilisha Ney wa Mitego.
INSTAGRAM NI ZAIDI
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, Nay, akiwa anafikiria namna ya kukabiliana na vitisho hivyo, aliingia kwenye akaunti yake ya Instagram ‘direct’ (moja kwa moja) na ‘hamadi’ akakutana na ujumbe ukiwa na vitisho vya kumuua.
“Jamaa hana raha hata kidogo, amekutana na meseji na simu
alizopigiwa. Ameamua kuzima simu zake zote. kilisema chanzo hicho.“Kwa
sasa anajiandaa kwenda mkoani Lindi kuna shoo hivyo tunapata hadi
wasiwasi kama jamaa ataweza kweli kufanya kazi inavyotakiwa,” Chanzo.Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, Nay, akiwa anafikiria namna ya kukabiliana na vitisho hivyo, aliingia kwenye akaunti yake ya Instagram ‘direct’ (moja kwa moja) na ‘hamadi’ akakutana na ujumbe ukiwa na vitisho vya kumuua.
KWENDA POLISI
Imezidi kudaiwa kwamba, baadhi ya watu wake wa karibu na mama yake mzazi, walimshauri aende akaripoti Kituo cha Polisi Kimara (jirani na nyumbani kwake) kwa vile anaweza kupata matatizo makubwa.
MAMA YAKE ANALIA TU
“Mbaya zaidi, mama yake naye, amepaniki kiasi kwamba analia tu. Inabidi sisi ndiyo tumpe moyo maana anafikiria hatima ya mwanaye kwani kila anapokwenda akikutana na watu wanamlalamikia juu ya wimbo huo,” kilisema chanzo hicho.
Kamanda Simon Sirro.
WIKIENDA LAMSAKABaada ya kupenyezewa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Nay kutaka kujiridhisha kuhusu madai hayo lakini hakuwa hewani. Ilibidi kumtafuta mtu wa karibu yake na ndipo alipopatikana.
Naye alikiri kutishiwa kuuawa. Alisema hatua ya awali alichukua uamuzi wa kwenda Kituo cha Polisi Kimara, Dar lakini hakufunguliwa faili la kesi kwa maelezo kuwa, usiku huo askari wasingeweza kufanya hivyo badala yake walimtaka arudi kesho yake.
HUYU HAPA NAY
“Hapa nilipo nimechanganyikiwa. Kwa hali ilivyo nimeona bora niende polisi maana najua nitauawa wakati wowote. Nilikwenda Polisi Kimara lakini sikufanikiwa, sasa najiongeza, nitakwenda Kituo cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (kwa Kamanda Simon Sirro).
Wikienda: “Nimesikia unakwenda Lindi kwenye shoo, sasa huko Polisi Kanda Maalum umeshakwenda au utakwenda ukirudi?”
Nay: “Kwanza nilikwenda polisi pale Kimara, wakashindwa kufungua faili. Waliniambia niende asubuhi lakini nimeshindwa kwa kuwa nimeondoka Dar na hapa nipo Lindi.
“Ila kuna ujumbe nimeukuta Insta (Instagram) ni mbaya sana. Nimepanga nikirudi nienda Kanda Maalum, lakini kuna wenzangu niliokuja nao hapa Lindi wamenishauri niende Kituo cha Polisi Kikuu cha hapahapa nikaripoti.”
TIMU WEMA WAMFANYA VIBAYA
Wakati huohuo, wadau wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu (Team Wema), wanadaiwa kuchukua picha ya mrembo huyo akiwa kwenye gari na kuipachika sura ya Nay ili aonekane ni demu.
Kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, picha hiyo imeenea huku wengi wakikitafsiri kitendo hicho kuwa ni cha kutaka kumdhalilisha Mbongo Fleva huyo aonekane ni shoga.
Katika wimbo huo ulioleta figisufigisu, kuna kipengele Nay alisema Wema hana mimba bali anatafuta kiki ya msimu hali iliyotibua hasira za Team Wema.
Mwanamke ammwagia mwanaume maji ya moto
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Abdallah Adamu akipata tabu ya kukaa kutokana na jeraha alilolipata baada ya kumwagiwa maji ya moto.
Stori: Mayasa Mariwata na Makongoro Oging’
Huu ni ukatili ulioje! Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Eva Mwakajinga (32), mkazi wa Buguruni jijini Dar, anadaiwa kummwagia maji ya moto na kumuunguza vibaya mgongoni kijana, Abdallah Adamu (21), naye mkazi wa Buguruni kisa kikiwa kinashangaza.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa tabu, Abdallah alisimulia kwamba, mwishoni mwa wiki iliyopita, akiwa nje ya nyumba anayoishi akifanya shughuli ndogondogo za nyumbani, alimuona Eva ambaye ni mpangaji mwenzake, akimwaga takataka kwenye eneo lake (Abdallah) baada ya kufanya usafi ndani kwake hivyo kumtaka aziondoe.
“Nilimuona Eva akimwaga uchafu pale nje, nikamwambia autoe kwa sababu ‘site’ (Mamlaka ya Jiji la Dar) siku si nyingi walipita wakawatoza faini watu wanaoharibu mazingira, lakini mwenzangu hakunisikiliza, akaanza kufoka na kudai atakachonifanyia sitasahau maisha yangu yote, wakati hatukuwahi kuwa na ugomvi.
“Sikujua kama anachoongea anamaanisha kwa kuwa sikuona kosa langu, nikamwambia asipoutoa ule uchafu, nitauchukua na kuurudisha ndani kwake ili kuepuka kulipishwa faini, nikaona mwenzangu anaingia ndani.
Baada ya kufanya tukio hilo, Eva alikimbilia ndani kisha akajifungia ndipo majirani wakafika na kufanya jitihada za kuvunja mlango kwa kuwa hakutaka kuufungua, wakamchukua na kumpeleka ofisi za kata kisha Kituo cha Polisi cha Buguruni.
Akizungumzia tukio hilo kwa majonzi, mama mzazi wa Abdallah, Ashura Fundi alisema kuwa kitendo alichofanyiwa mwanaye ni cha ukatili uliopitiliza kutoka kwa jirani yao huyo ambaye tangu apange maeneo hayo ana miezi mitatu tu, lakini anaamini sheria itafuata mkondo wake.
“Nilihisi naota, nikajikuta naangua kilio kama mtoto mdogo ila nilikaza moyo tukamkimbiza mwanetu Hospitali ya Kwa-Mnyamani na kuambiwa twende Hospitali ya Amana ambapo alipatiwa matibabu japokuwa hakulazwa kutokana na mazingira ya pale hospitalini.
“Kutokana na tukio hilo la aina yake lililogubikwa na roho ya ukatili na unyama uliokithiri, Eva bado anashikiliwa kituoni hapo kwa jalada la kesi namba BUG/RB/1218/2016 SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI.
Gazeti hili lilifika kituoni hapo na kukutana na polisi aliyekuwa zamu ambaye alithibitisha kushikiliwa kwa Eva na kwamba uchunguzi unaendelea.
Abdallah Adamu akipata tabu ya kukaa kutokana na jeraha alilolipata baada ya kumwagiwa maji ya moto.
Huu ni ukatili ulioje! Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Eva Mwakajinga (32), mkazi wa Buguruni jijini Dar, anadaiwa kummwagia maji ya moto na kumuunguza vibaya mgongoni kijana, Abdallah Adamu (21), naye mkazi wa Buguruni kisa kikiwa kinashangaza.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa tabu, Abdallah alisimulia kwamba, mwishoni mwa wiki iliyopita, akiwa nje ya nyumba anayoishi akifanya shughuli ndogondogo za nyumbani, alimuona Eva ambaye ni mpangaji mwenzake, akimwaga takataka kwenye eneo lake (Abdallah) baada ya kufanya usafi ndani kwake hivyo kumtaka aziondoe.
“Nilimuona Eva akimwaga uchafu pale nje, nikamwambia autoe kwa sababu ‘site’ (Mamlaka ya Jiji la Dar) siku si nyingi walipita wakawatoza faini watu wanaoharibu mazingira, lakini mwenzangu hakunisikiliza, akaanza kufoka na kudai atakachonifanyia sitasahau maisha yangu yote, wakati hatukuwahi kuwa na ugomvi.
“Sikujua kama anachoongea anamaanisha kwa kuwa sikuona kosa langu, nikamwambia asipoutoa ule uchafu, nitauchukua na kuurudisha ndani kwake ili kuepuka kulipishwa faini, nikaona mwenzangu anaingia ndani.
Muonekano wa jeraha hilo.
“Baada ya muda, nikiwa nimempa mgongo, nilishtuka ananimwagia maji ya
moto aliyokuwa akichemsha kunde,” alisema Abdallah akiwa katika hali
mbaya nyumbani hapo.Baada ya kufanya tukio hilo, Eva alikimbilia ndani kisha akajifungia ndipo majirani wakafika na kufanya jitihada za kuvunja mlango kwa kuwa hakutaka kuufungua, wakamchukua na kumpeleka ofisi za kata kisha Kituo cha Polisi cha Buguruni.
Akizungumzia tukio hilo kwa majonzi, mama mzazi wa Abdallah, Ashura Fundi alisema kuwa kitendo alichofanyiwa mwanaye ni cha ukatili uliopitiliza kutoka kwa jirani yao huyo ambaye tangu apange maeneo hayo ana miezi mitatu tu, lakini anaamini sheria itafuata mkondo wake.
“Nilihisi naota, nikajikuta naangua kilio kama mtoto mdogo ila nilikaza moyo tukamkimbiza mwanetu Hospitali ya Kwa-Mnyamani na kuambiwa twende Hospitali ya Amana ambapo alipatiwa matibabu japokuwa hakulazwa kutokana na mazingira ya pale hospitalini.
Akiandaliwa mahali pa kujipumzisha.
“Lakini tunampeleka hospitalini kusafisha kidonda,” alisema mzazi huyo na kuongeza:“Kutokana na tukio hilo la aina yake lililogubikwa na roho ya ukatili na unyama uliokithiri, Eva bado anashikiliwa kituoni hapo kwa jalada la kesi namba BUG/RB/1218/2016 SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI.
Gazeti hili lilifika kituoni hapo na kukutana na polisi aliyekuwa zamu ambaye alithibitisha kushikiliwa kwa Eva na kwamba uchunguzi unaendelea.
Baba mzazi wa Isha Mashauzi kuzikwa leo Dar
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Msiba uko nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Msuguri ambapo shughuli yote itafanyika ikiwa pamoja na kisomo, sadaka ya chakula na kumswalia marehemu kabla ya kwenda kumhifadhi kwenye nyumba yake ya milele.
Mtoto wa marehemu, Juma Ramadhan, amesema hiyo ndiyo taarifa rasmi na sahihi baada ya kuwepo vuguvugu la sintofahamu juu ya wapi baba yake angezikwa kati ya Dar es Salaam na Musoma. Ramadhan Makongo ambaye pia ni baba wa mwimbaji wa taarab Saida Ramadhan na mume wa mwimbaji Rukia Juma, alifariki katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua kwa siku kadhaa.
Picha ndogo ni baba yake Isha Mashauzi mwenye kipaza sauti.
BABA mzazi wa mwimbaji Isha Mashauzi, Ramadhan Makongo, aliyefariki
Jumamosi alfajiri wiki iliyopita, anazikwa leo (Jumatatu) saa 6 mchana
huko Mbezi kwa Musuguri, jijini Dar es Salaam kwenye makaburi ya
Msingwa.Msiba uko nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Msuguri ambapo shughuli yote itafanyika ikiwa pamoja na kisomo, sadaka ya chakula na kumswalia marehemu kabla ya kwenda kumhifadhi kwenye nyumba yake ya milele.
Mtoto wa marehemu, Juma Ramadhan, amesema hiyo ndiyo taarifa rasmi na sahihi baada ya kuwepo vuguvugu la sintofahamu juu ya wapi baba yake angezikwa kati ya Dar es Salaam na Musoma. Ramadhan Makongo ambaye pia ni baba wa mwimbaji wa taarab Saida Ramadhan na mume wa mwimbaji Rukia Juma, alifariki katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua kwa siku kadhaa.
Ziara ya waziri mkuu kila kukicha, bandarini kuna kitu
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Stori: Gabriel Ng’osha, Wikienda
Dar es Salaam: Kunani bandarini? Kufuatia ziara za kila kukicha za kushtukiza za bandarini za Waziri Mkuu, Cassim Majaliwa, baadhi ya Wabongo wamekiri kwamba, kwa vyovyote kuna kitu waziri mkuu amegundua au anakifahamu juu ya utendaji wa wahusika.

Mke Wa Kafulila ( Jesca Kishoa ) Ataka Dkt. Harrison Mwakyembe Naye Akamatwe Na Kufikishwa Mahakamani Kwa Kuhusika Na Sakata La Mabehewa Mabovu
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mbunge
wa Viti Maalumu, mkoani Singida Jesca Kishoa(CHADEMA), amesema
aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe na Katibu Mkuu
wake, wanapaswa kufikishwa mahakamani katika sakata la mabehewa mabovu.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Kishoa alisema viongozi hao, pia aliyekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha wakati huo, naye afikishwe mahakamani kwa
sababu ndiye alikuwa mlipaji Mkuu wa Serikali.
Alisema
ni aibu Kiti cha Spika kumfukuza mbunge bungeni akidaiwa kuzungumza
uongo kabla ya kudai ripoti ya mabehewa ili kujua ukweli wa jambo hilo
ni upi.
Aliongeza
kuwa, Katibu Mkuu huyo alilipa fedha asilimia 100 kinyume cha sheria
wakati Dkt. Mwakyembe ambaye kwa sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria,
aliruhusu mabehewa yanunuliwe.
"Aliyekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi naye awajibishwe kwa kosa hilo kama
Mtendaji Mkuu wa Wizara...mabehewa hayo yalipokewa kwa mbwembwe lakini
kasoro zake zinatokana na zabuni ya utengenezaji wake kutozingatia
viwango.
"Kampuni ya Hindustan Engineering haikufanyiwa uchunguzi kuhusu rekodi na uwezo wake, malipo yalifanyika kwa asilimia
100 kabla ya mabehewa hayajawasili nchini," alisema.
Alisema
umma unashuhudia baadhi ya vigogo wa TRL wanafikishwa mahakamani
kutokana na sakata la mabehewa hayo na kusisitiza sheria ichukue mkondo
wake kwa wote waliohusika si kuwashtaki wachache wakati Mawaziri
wanaachwa.
Kishoa
ambaye ni Mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila
(NCCR-Mageuzi), alisema hakuna mtu mwenye uhakika kwamba mabehewa mabovu
ni 25 kati ya 275.
"Nani
ana uhakika kwamba waliokamatwa ndio wanahusika peke yao, haiwezekani
Serikali ikajichunguza yenyewe, kujishughulikia yenyewe kwa kuamua nani
imtoe kafara, nani imlinde wote, wote washtakiwe kama ilivyo kwa
wengine," alisema Kishoa.
Kishoa
alihoji kwanini ripoti ya mabehewa inaendelea kufichwa na haifikishwi
bungeni ili Bunge liweze kuisimamia Serikali jambo ambalo halitoi picha
kwa Bunge la 11.
Sunday, 14 February 2016
Diamond Platnumz amfanya Mrisho Mpoto asitishe kuachilia video ya 'Sizonje
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Kauli ya staa wa muziki Diamond Platnumz ‘Kuna kushoot video na
kurekodiwa’ imemfanya msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto kuitia
kapuni kwanza video yake mpya ya wimbo ‘Sizonje’ ili aichunguze kwanza
kama inafaa.
Kupitia ukurasa wa instagram, Mpoto ameandika "Diamondplatnumz post yako ya leo imenifanya nisile Siku nzima. Nikiitafakari na sasa nimeamua kusitisha kutoa video yangu mpya ya #SIZONJE maana sina uhakika kama nime shoot au nimerecord. Ukimkimbiza sana mjusi anageuka kuwa nyoka"
Ijumaa hii Diamond aliachia video mpya ya wimbo ‘Make Me Sing’ akiwa na AKA wa Africa kusini na kutwitter.