Thursday, 11 February 2016
Wednesday, 10 February 2016
WAZIRI BASIL MRAMBA AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YA GEREZANI
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Aliyekuwa
Waziri wa Fedha katika Serikali ya awamu ya tatu, Basil Mramba,
ameishauri Serikali kuhakikisha inawatumia wafungwa kutumikia jamii
badala ya kuwarundika magerezani.
Amesema pamoja na hayo, maisha ya gerezani si salama na si njia pekee ya kumrekebisha mhalifu aliyehukumiwa na mahakama.
Kutokana
na hali hiyo, alisema kuna haja kwa Serikali kuanza kutumia sheria
namba 6 ya huduma kwa jamii kuwaangalia wafungwa wenye taaluma kutumika
adhabu zao katika fani au taasisi za umma ili kupunguza gharama
kuwahudumia watu ambao wanaweza kuisaidia jamii.
Mramba
alitoa kauli hiyo jana, wakati yeye na mwenzake aliyekuwa Waziri wa
Nishati na Madini, Daniel Yona, walipomaliza kufanya usafi katika
Hospitali ya Sinza Palestina, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya
kutumikia adhabu ya kifungo chao cha nje baada ya wiki iliyopita
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuridhia kuwa wanastahili kutumikia
jamii kwa kipindi cha miezi sita hadi Novemba 5.
Alisema
imekuwa ni kawaida jamii kuwa na mtazamo kwamba mtu yeyote anayekutwa
na hatia lazima atapelekwa jela ajirekebishe na kuacha tabia aliyonayo
jambo ambalo si sahihi.
“Jamii
inaamini jela ni sehemu salama na mtu akishikwa na hatia kwa kosa
lolote, mahala sahihi ni jela tu, kule anakutana na watu wa kila aina,
wenye makosa tofauti, hali ambayo inamfanya ajifunze mambo mengine
mapya.
“Unakuta
mtu amefanya uhalifu wa kuiba kitu, anafungwa na kupelekwa gerezani,
anakutana na majambazi sugu wanaompa mbinu zaidi, sasa akitoka jela
anakuja akiwa ameiva, anarudia kwenye matukio akiwa amekamilika,” alisema Mramba.
Alisema kuwapeleka wafungwa katika huduma za kijamii kutasaidia kupunguza gharama kwa Serikali na msongamano ndani ya magereza.
Akizungumzia
suala la kuwatumia wafungwa ambao ni wanataaluma, Mramba alisema sheria
hiyo ikitumika vizuri italisaidia taifa kwani wapo baadhi ya wafungwa
wana taaluma ya udaktari, ualimu, ufundi na uhasibu, ambao wanaweza
kutumika katika fani zao kwenye taasisi za umma.
“Kuna
maeneo mengine yana uhaba wa wataalamu ambao wengine wapo magerezani
wanahudumiwa na Serikali kuanzia chakula, malazi na hata afya zao, hivyo
wakiwatumia hao itakuwa faida kwa taifa kwa kuwa watafanya kazi bila
malipo,” alisema Mramba.
Alisema
suala la kuwatumia wafungwa katika huduma za kijamii si geni kwa nchi
zilizoendelea ambako kwa kiasi kikubwa wamesaidia kuinua uchumi wa nchi
zao.
Kwa
siku ya jana, Mramba na Yona walianza kufanya usafi saa 2 asubuhi kwa
kufagia nyuma ya jengo la wazazi katika hospitali hiyo.
Naye
Ofisa Huduma za Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Deogratius Shirima,
alisema gharama zinazotumika kuwahudumia wafungwa magerezani ni kubwa,
hivyo ni vyema wale wanaoguswa na sheria ya huduma za jamii namba 6 ya
mwaka 2002 kutumikia kifungo cha nje.
“Sheria
hii ni vyema ikatumika kwa wale inaowagusa kwani itapunguza gharama za
kuwahudumia magerezani, na pia adhabu wanayopata wafungwa wa nje ni wazi
jamii ambayo ndiyo iliyokosewa inaona utekelezaji wake kwa uwazi,” alisema Shirima.
Alisema
mataifa mengine ikiwamo nchi ya Kenya wanatumia sheria hiyo ambapo nusu
ya wafungwa nchini humo wapo katika huduma za jamii.
Februari
6, mwaka huu mawaziri hao walibadilishiwa adhabu ya jela na kupewa
adhabu ya kutumikia kifungo cha nje mwishoni mwa wiki iliyopita na
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukamilika kwa mchakato wa
kufikia hatua hiyo.
Hakimu
Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha, alisema sheria ya huduma kwa
jamii namba 6 kifungu namba 3(1) ya mwaka 2002 inasema mtu yeyote
anayetiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni miaka mitatu kushuka
chini mahakama inaweza kumpa adhabu ya kutumikia jamii.
Mramba
na Yona, ambao baada ya rufaa walibakiwa na adhabu ya miaka miwili,
walitiwa hatiani kwa kutumia madaraka vibaya ambapo walitakiwa kumaliza
kifungo Novemba mwaka huu.
Hata
hivyo, hakimu huyo alisema magereza walifikisha barua mahakamani hapo
Desemba 5, mwaka jana yenye kumbukumbu namba 151/DAR/3/11/223,
wakipendekeza kifungo cha nje kwa mawaziri hao.
Hakimu
Mkeha alisema baada ya kupokea barua hiyo, mahakama iliamuru watu wa
huduma za jamii kuchunguza kama wanastahili kupewa adhabu hiyo na kwamba
walifanya hivyo na kurudisha ripoti kwamba wanastahili.
Alivitaja vigezo vya kupewa adhabu hiyo kuwa ni umri ambapo Mramba na Yona wana miaka 75.
Tuesday, 9 February 2016
Jeshi La Polisi Lakamata Majangili 9 Waliotungua Helkopta na Bunduki 29.....Miongoni Mwa Waliokamatwa ni Mhifadhi wa hifadhi ya Ngorongoro
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Siku
chache baada ya kutokea tukio la majangili katika pori la akiba Maswa
wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, kuitungua ndege (helikopta) iliyokuwa
doria na kuaawa kwa rubani wake Rodgers Gower (37), watu 9 wamekamatwa
kuhusika na tukio hilo.
Katika watuhumiwa hao mmoja ni Mhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kitengo cha Interejensia, ambaye alitajwa kuwa mhusika Mkuu wa kufanikisha tukio hilo sambamba na kukamatwa mganga wa jadi.
Akitoa
taarifa mbele za waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa
polisi Mkoani Simiyu Lazaro Mambosasa alisema kuwa kukamatwa kwa
watuhumiwa hao kumetokana na jeshi hilo kufanya kazu usiku na mchana
kwa kushirikiana na wananchi, pamoja na uongozi wa TANAPA.
Kamanda
Mambosasa alisema watuhumiwa wote walikamatwa na kukiri kuhusika na
tukio hilo, huku akieleza kuwa msako mkubwa uliofanywa na jeshi hilo
mara baada ya tukio kutokea chini ya Mkuu wa upelelezi Mkoa Jonathan
Shana.
Alisema
katika msako huo baadhi ya watuhumiwa walibainika kuwa kiungo kikubwa
kufanikisha tukio hilo kwa kutoa mbinu za uharifu, huku wakijihusisha na
matukio ya ujangili kwa muda mrefu.
Aliongeza
kuwa baadhi yao walibainika kuwa waganga wa jadi, ambapo walikuwa
wakitoa dawa kwa majangili za kuosha silaha, ikiwa ni pamoja na kuosha
na kusafisha miili yao ili wasiweze kukamatwa.
Mambosasa
aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shija Mjika (38), Njile Gonga (28)
Mhazabe, Masasi Mandago (48) pamoja na Dotto Pangali (41) , ambao ndio
walihusika kutungua helkopta hiyo.
Wengine ni Iddi Mashaka (49) ambaye Kamanda Mambosasa alimtaja kuwa Mhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro Kitengo cha Intelijensia na ndiye alikuwa kiungo Mkuu wa tukio hilo.
Aliwataja
wengine kuwa ni Mapolu Njige (50) ambaye ni mganga wa jadi aiyekuwa
anatumika kutoa dawa za kutokamatwa kwa majangili hao, Mwigulu Kanga
(40) , Dotto Huya (45) , Pamoja na Mange Balumu.
Aidha
Mambosasa alisema kuwa Mtuhumiwa Dotto Pangali alikamatiwa katika
wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga mnamo tarehe 7/02/216 na kufanyiwa
upekuzi nyumbani kwake ambapo alikutwa na bunduki aina ya Riffle yenye
namba .7209460 CAR Na.63229.
Mkuu
huyo wa polisi alisema Mtuhumiwa huyo alikiri bunduki hiyo kutumika
katika tukio la kuuawa kwa rubani huyo, ambapo ilibainika kuwa bunduki
hiyo inamilikiwa na Mange Magima ambaye pia amekamatwa.
Alisema
msako uliendelea nyumbani kwa Pangali na kufanikiwa kukamatwa kwa
bunduki nyingine aina ya Riffle Na3478 CAR 458 ikiwa na risasi 6 ambayo
ilibainika kumilikiwa na Nghomango Jilala ambaye mpaka sasa hajakamatwa.
Alieleza
kuwa jeshi hilo liliendelea kupata taarifa ambapo mnamo tarehe
29/01/2016 walikamatwa Shija Mjika, Njile Gonga, pamoja na Masasi
Mandago wakiwa na meno ya tembo 2 yakiwa na uzito wa Kilo 31 yakiwa
yamefichwa chini ya daraja katika kijiji cha Itaba.
Aidha
Mambosasa alieleza kuwa baada ya kukamatwa kwa wahusika wote ilibainika
kuwa bunduki zilizotumika katika tukio hilo zinamilikiwa kihalali na
watu ambao waliomba kuzimiliki kwa ajili kujilinda.
“Mbali
na tukio hilo bunduki nyingi wamiliki wake wanawaazimisha majangili kwa
ajili ya kutumika kwa uhalifu pamoja na kuua wanyama ndani ya
hifadhi…lakini na hao wamiliki wanalipwa pesa baada ya uhalifu
kufanyika” ,alisema.
Alisema
baada ya kubaini hilo kulifanyika msako mwingine kwa wanaomiliki
silaha, ambapo alisema asilimia kubwa wanaishi karibu na hifadhi, na
jumla ya bunduki 27 zimekamatwa na mara baada ya uchunguzi wamiliki
watarudishiwa.
“Tunajiandaa
kupeleka zuio la silaha mahakamani ili kubaini kama wana sifa za
umiliki…lakini mbali na hilo sasa kutaanzishwa oparesheni kwa watu wote
wanaomiliki silaha hasa maeneo ya hifadhi kwa ajili ya kuwanyanganya”, alisema.
Mkuu
huyo wa polisi alisema kuwa upelelezi juu ya tukio hilo umekamilika na
watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani leo Jumanne ili kujibu tuhuma
zinazowakabili, ambapo alioomba mahakama kuharakisha hukumu kwa vile
uchunguzi umekamilika.
Kwa
upande wake Mhifadhi mkuu wa Serengeti William Mwakilema amelipongeza
jeshi la polisi ambapo amesema tukio hilo lilipotokea liliwasikitisha
sana kwani hasara ilipatikana kutokana na kutunguliwa kwa helkopta.
Mnamo
tarehe 29/01/2016 saa 11:30 jioni katika eneo la Gululu lililopo ndani
ya hifadhi ya Maswa kata ya Mwangudo wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu,
majangili waliipiga risasi ndege (helkopta) 88HFCG iliyokuwa doria na
kusababisha kifo cha rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza
huku Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika
kifo.
Hashim Rungwe Akosoa kauli za Rais Magufuli Kuhusu idara ya Mahakama, asema Zinaingilia Uhuru wa Mahakama.
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mwenyekiti
wa chama cha ukombozi wa umma CHAUMA Hashim Rungwe amesema kauli
iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt John Pombe
Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya Mahakama nchini iliingilia
uhuru wa mahakama.
Mwenyekiti
wa chama cha ukombozi wa umma CHAUMA Hashim Rungwe amesema kauli
iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt John Pombe
Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya Mahakama nchini iliingilia
uhuru wa mahakama.
Akielezea
utata uliojitokeza katika hotuba hiyo Rungwe amesema hotuba hiyo
ilionekana kama kuifundisha mahakama wajibu wake jambo ambalo lina utata
katika uongozi wa kisheria lakini hata hivyo Rungwe ameielezea hotuba
hiyo kuwa itaongeza uwajibikaji katika mahakama na haki kupatikana kwa
wakati.
Wakati
wa siku ya maadhimisho ya siku ya mahakama Alhamisi iliyopita, Rais
Magufuli aliahidi kuipatia idara ya mahakama fedha kwa ajili ya
kuendesha shuhguli za mahakama na kuitaka mahakama hiyo kuharakisha
kusikiliza kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kesi za watuhumiwa wa
kukwepa kulipa kodi.