WAZIRI wa Tamisemi, Hawa Ghasia, Julai 14, mwaka huu, amefungua
mkutano wa Viongozi wa Vyama vya Siasa vilivyokuwa na usajili wa kudumu
ngazi ya Taifa kujadili maoni ya wadau mbalimbali ya kuboresha kanuni
za uchanguzi wa viongozi wa mamlaka za serikali za mitaa unaotarajia
kufanyika Oktoba 2014.
Arafa MohammedMke wa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akimkabidhi zawadi ya vyombo vya ndani na Tende Mzee Ahmad Ramadhan mmoja wa wazee wa kijiji cha Changarikwa wakati alipotoa zawadi hizo kwa familia zenye mahitaji muhimu katika kata ya Mbwewe jana.
KOCHA wa timu ya Taifa Brazil, Luiz Felipe Scolari ametangaza rasmi
kuachia nafasi ya ukocha katika kikosi hicho baada ya matokeo mabaya
katika michuano ya Kombe la Dunia 2014.
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY WATU
zaidi ya wawili wanadhaniwa kupoteza maisha baada ya kufunikwa na
kifusi wakati wakiendelea na shughuli za uchimbaji wa miamba kwa ajili
ya uchongaji wa matofali.
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY GERMANY 1-0 ARGENTINA kwa mara ya kwanza timu ya taifa ujerumani imetwaa kombe la dunia ikiwa katika ardhi ya america ya kusini;Ujerumani imetwaa taji hilo ikiwa ni mara ya kwanza tangu 1990.
Pongezi za pekee ziende kwa mshambuliaji Mario Goetze ambae alitokea bench na kufunga goli na kuiwezesha ujerumani kuongoza kwa ushindi wa goili 1-0 katika dakika ya 113.
Serikaliinatarajia kutoa vibali vya kuajiriwafanyakazi
200 katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na zaidi ya asilimia 95 ya
wafanyakazi hao wataongeza nguvu katika kutayarisha na kusimamia
viwango vya ubora.
Zikiwa ni takribani wiki tatu tangu tasnia ya muziki wa injili nchini
kumpoteza mmoja wa waimbaji wake marehemu mchungaji Debora Saidi,
taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba mwimbaji mwingine wa muziki wa
injili Orida Njole amefariki dunia mchana wa leo katika hospitali ya
Temeke jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
1 KUONGEA NA KUKAA MUDA MWINGI NA WEWE kama
msichana anakupenda hatoichezea nafasi ya kukuona kukaa na kuongea na
wewe. Siku zote atatafuta nafasi ya kuongea au kukuona. Unapoongea naye
anakuwa makini kukusikiliza na hufurahi kila unachokiongea hata kama
hakifurahisha.
MAMBO MAKUU 4 UNAPOKUWA CHUMBANI NA MPENZI WAKO Mambo ya Chumbani hayoooo!! Fahamu mambo 4 muhimu unayopaswa kuyazingatia uwapo chumbani na mpenzi wako mnapotaka kufanya mapenzi 1. WEKEZA MAWAZO YAKO KWA MPENZI WAKO
Nicola
Rizzoli amechaguliwa na Fifa kuwa mwamuzi katika mchezo wa fainali -
Kombe la Dunia Brazil 2014 kati ya Ujerumani na Argentina. Howard Webb kutoka England, aliyechezesha fainali ya Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini, aliorodheshwa lakini hakuchaguliwa.
Ofisi ya Waziri Mkuu –
TAMISEMI inatangaza orodha ya Majina 3,733
ya watumishi wa Umma waliohamishwa katika Mamlaka za Serikali za mitaa
nchini,Aidha orodha ya watumishi 112
ambao hawakukidhi vigezo vya kuhama nayo imetangazwa.
KUBADILISHA SHULE NA TAHASUSI KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO 2014
Taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa
kuingia kidato cha Tano katika Shule za Serikali na Vyuo vya Ufundi kwa
mwaka 2014 ilitangazwa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI mwezi Juni,
2014. Wanafunzi waliochaguliwa awali walitakiwa kuripoti kuanzia tarehe
10 – 30/7/2014 .
Baada ya taarifa ya Uchaguzi wa wanafunzi
kutolewa, baadhi ya wanafunzi/wazazi/walezi wamewasilisha barua za
maombi ya kuwabadilishia wanafunzi waliochaguliwa shule na tahasusi au
mojawapo ya hivyo. Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI baada ya kupokea
imechambua maombi hayo na kubaini kuwa sababu zilizotolewa kwenye baadhi
ya maombi hayo zina tija na hivyo kulazimika kuridhia kuwabadilishia
shule, tahasusi au vyote kwa pamoja baadhi ya wanafunzi hao.
Wakati
jamii ikiwa bado haijasahau mateso aliyoyapata mtoto Nasra Mvungi na
kusababisha kifo chake, tukio lingine la aina hiyo limetokea katika
Kijiji cha Matongola, Tarafa ya Magole Wilaya ya Kilosa, baada ya
kubainika mtoto wa miaka sita akiwa amefichwa uvunguni mwa kitanda na
kufanyiwa vitendo vya kikatili na mama yake mzazi.