Tuesday, 20 May 2014

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE

1_2aead.jpg
2_a0005.jpg
3_35cc1.jpg
4_02117.jpg
5_15b42.jpg
6_df0e6.jpg
7_dc172.jpg
8_356a2.jpg
09_41dd0.jpg
11_d3397.jpg
12_68832.jpg
13_fc5ff.jpg
14_8d176.jpg
15_7df39.jpg
16_20384.jpg
17_39010.jpg
18_99a67.jpg
19_2a898.jpg
20_e97e5.jpg
22_201de.jpg
23_36a46.jpg
24_82757.jpg
25_d6b29.jpg
26_9476b.jpg
27_89a34.jpg
28_3e26d.jpg
29_f4629.jpg
30_466c5.jpg
31_b1617.jpg
33_5e913.jpg
34_83c5b.jpg
35_27f3e.jpg
36_ea790.jpg
37_d0f38.jpg
038_3a7e3.jpg
38_81dff.jpg
39i_4a9cd.jpg 
USIASAHAU KULIKE PAGE YETU FACEBOOK
Share:

MADUDU KATIKA ELIMU YAENDELEA


WABUNGE wamesema hali ya elimu nchini ni mbaya na kumshauri Rais Jakaya Kikwete, kuunda Tume ya Kudumu ya Elimu ili kuangalia ubora na kudhibiti sekta hiyo muhimu.
Katika michango yao kwenye mjadala wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, uliotarajiwa kuhitimishwa jana jioni, wabunge wamesema suala la elimu halina siasa, na nchi isipochukua hatua sasa, itakuwa hatari kwa vizazi vijavyo.
Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alieleza matatizo kadhaa katika mitihani ya Darasa la Saba pamoja na ule wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na kudai kuwa “kuna madudu makubwa.”(Martha Magessa)
Mbatia aliyekuwa ameshika nakala za mitihani hiyo na baadaye kuiwasilisha kwa Naibu Spika, Job Ndugai, alidai baadhi ya mitihani hiyo ni migumu na imewashinda maprofesa wa vyuo vikuu.
Profesa, dau “Mimi niliwapatia mitihani hii maprofesa wa vyuo vikuu, imewashinda. Niliwapa huu wa Hisabati, akanirudishia akisema mtihani wenyewe haufanyiki. “Sasa kama yupo mtu humu atamudu kuufanya na kupata alama mia moja, nampa milioni kumi,” alisema Mbatia, huku Naibu Spika akieleza kuwa Waziri Profesa Sospeter Muhongo yuko tayari kuufanya. “Profesa Muhongo ni profesa wa miamba, kama ataweza huu hapa aje achukue,” alitamba Mbatia.
Mbatia alisema elimu ya Tanzania ni dhaifu na nchi imeshindwa katika elimu na kuwa suala hilo si la chama cha siasa.
Akitoa majawabu ya hoja zake, Mbatia alimshauri Rais kuunda Tume ya Kudumu ya Elimu, ambayo pamoja na mambo mengine, alisema itaangalia ubora na kudhibiti elimu nchini.
Msomi huyo alitaka pia Tume hiyo ifanye kazi ya kuandaa mitaala, kuhariri vitabu akisema Tanzania haina wahariri wa vitabu kama ilivyo kwa vyombo vya habari vyenye wahariri wa aina mbalimbali.
Alizitaja kazi nyingine kuwa ni kufanya utafiti wa kisayansi, kuamua lugha ya kufundishia na kuangalia kwa ujumla tatizo la kushuka kwa elimu.
Alisema elimu siyo bidhaa ya kuuzwa sokoni, bali iwe huduma na kukerwa na kodi nyingi katika elimu na gharama za ada kwa shule binafsi.
“Ni lazima tuukubali ukweli na kukabiliana nao. Elimu yetu imeshuka. Watoto wa walalahoi watapata tabu, kama hatukuisimamia hili, tutapata tabu katika miaka 20 au mia ijayo hasa wakati huu wa sayansi na teknolojia,” alisema Mbatia.
Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM), aliyesema kuwa elimu iko katika chumba cha wagonjwa wenye uangalizi maalumu (ICU). Kama Mbatia, Serukamba alishauri kuanzishwa kwa Tume ya kujichunguza kuhusu kuporomoka kwa elimu nchini, akisema “tukubali waseme, tujisahihishe.”
Alisema suala hilo si la mtu mmoja, na kuacha siasa na kuongeza kuwa kama kuna jambo “tunacheza nalo, basi ni elimu, tunaua kizazi kijacho.”
Alisema si vyema kutatua tatizo la elimu kwa kuangalia leo tu, bali uwepo mkakati wa dhati wa muda mrefu, na kutolea mfano Marekani ilivyopitia mfumo wake wa elimu mwaka 1981.
Ada kubwa Kwa upande wake, Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza (CCM), ambaye anamiliki shule kadhaa nchini, alisema kuna tatizo la shule binafsi kulundikiwa kodi nyingi, na ndio manaa zinatoza ada kubwa.
“Kuna sijui kodi ya mapato, PAYE, majengo, SDL, yaani ni michango, michango, kodi. Kwa staili hii, ada inapanda, baadaye shule inakufa,” alisema Rweikiza.
Aidha, kama walivyopendekeza wabunge wengine waliochangia jana, mbunge huyo alitaka ukaguzi utiliwe mkazo, akitoa mfano kuwa shule zake hazijakaguliwa tangu mwaka 2005.
Mbunge wa Ngara, Deogratius Ntukamazina (CCM), alisema kwa sasa hakuna Wizara ya Elimu baada ya kuondolewa kwa shule za msingi na sekondari.
Badala yake, akashauri wizara hiyo ibaki kuwa kitovu cha mawazo bora ya elimu kama ilivyo Tume ya Mipango kuhusu masuala ya mipango.
Said Arfi wa Mpanda Mjini (Chadema), licha ya kuzungumzia ukaguzi, alisema bajeti ya elimu imezidi kutegemea wahisani ambao hawatekelezi ahadi zao.
Nyambari Nyangwine wa Tarime (CCM), ambaye ni mtunzi wa vitabu, alipendekeza kuanzishwa kwa Shirika la Uchapaji, kwani vitabu ni moja ya maeneo yanayochangia mporomoko wa elimu nchini.
Mbunge wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya (CUF) alisema mazingira mabovu, ukaguzi kuachwa, shule kukosa maabara na kushuka kwa morali ya walimu, kumechangia kushuka kwa elimu nchini.
Muundo Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter Msolla (CCM), alitaka masuala ya shule za msingi na sekondari yabaki katika wizara hiyo na irejeshwe wizara ya kusimamia elimu ya juu, huku akisisitiza kuwa upangaji madaraja ni angamizo katika elimu nchini.
Naibu Spika Ndugai naye alipendekeza masuala ya elimu yaondolewe Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na kurejeshwa kwa wizara hiyo ili yasimamiwe vyema.
Kambi Rasmi ya Upinzani ilisema kuwa malengo na mikakati yote iliyoainishwa ni mizuri, lakini “tunadhani mikakati hiyo imekuwepo muda mrefu, kilichokosekana ni utekelezaji na ufuatiliaji wake.”
Msemaji wake, Susan Lyimo alishauri mikataba ya utendaji kazi katika kila ngazi ya elimu iwekwe wazi ili atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake ijulikane atawajibika vipi. LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPA
Share:

WAKUBWA TU!! NI ZAIDI YA LAANA WAFUMWA WAKINYONYANA 'SEHEMU ZA SIRI' HADHARANI KWEUPEE, JIONEE HAPA

 
Kwa jinsi dunia ilivyo sasa hivi hata hiki kitendo kitaonekana cha kawaida maana maovu uanayotendeka asa hivi ni zaidi ya laana. Hawa walikutwa wakifanya kitendo 
hicho hadharani bila kuona aibu hata kidogo!! Hebu tazama hapa ujionee vioja!!
Bofya hapo chini kuangalia picha na video  ila ni lazima uwe na miaka zaidi ya 21 maana ukizimia mie simo




VIDEO HAPA
LIKE PAGE YETU FACEBOOK HAPA::LIKE FACEBOOK HAPA
Share:

BALAA JINGINE GEITA!! KIJANA AJINYONGA HADI KUFA KWENYE CHOO CHA MAMA MKWE WAKE,ALITAKA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE AKAKIMBIWA NA MKEWE

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Daudi James(33) mkazi wa mtaa wa Shilabela mjini Geita mkoani Geita amekutwa amekufa kwa kujinyonga chooni kwa mama mkwe wake kwa kutumia kitenge.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo Daud James amekutwa amejinyonga chooni kwa mama mkwe wake eneo la General Tyre.

Akizungumzia tukio hilo mama mkwe wa marehemu Lucia Magulu(32) amesema marehemu alimuoa binti yake Dorothea Jacksoni(18) mwaka mmoja uliopita huku akiwa na ujauzito wa mwanamme mwingine na baada ya kujifungua wameendelea kuishi na mtoto wao ambaye ni Hellena mwenye umri wa miezi kumi.

Akiendelea kusimulia mkasa huo amesema binti yake Dorothea Jacksoni(18) walikuwa wamehitlafiana na mme wake na kurudi nyumbani takribani zaidi ya mwezi mmoja kwa sababu za marehemu mme wake kuwa anamutaka mkewe wafanye tendo la ndoa kinyume na maumbile ndicho kilichomfanya arudi nyumbani.

"Jana jioni alipofika hapa nyumbani alikaa hadi walipomaliza kula chakula cha jioni na alipoambiwa arudi nyumbani kwake Shilabela alikataa na kutaka aende na mke wake ",anaeleza mama mkwe.


"Baadae mke wake alipomkatalia kwenda marehemu alimuomba kitenge mke wake kwa maelezo ya kuwa anaenda kulala kwa rafiki zake na ndipo alipopewa,cha kushangaza na kusikitisha leo asubuhi tumemkuta kajinyonga kwa kitenge hicho chooni",ameongeza mama mkwe.


Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa

uchunguzi bado unaendelea ili kubaini sababu gani zilipelekea kifo chake.


Hata hivyo kamanda Konyo ameitaka jamii kuacha mambo ya kujichukulia maamuzi ya kujiua bila sababu za msingi huku akiwataka waandishi wa habari nao kuelimisha jamii iachane na tabia za kujinyonga kila mara wanapokuwa wamezozana na wake zao.


Hili ni tukio la pili kutokea ndani ya siku tatu ambapo juzi mkazi wa tambukareli mjini Geita alijinyonga na kijining’iniza kwenye mti wa mpera baada ya kuhitlafiana na mke wake.
Share:

LOUIS VAN GAAL KOCHA MPYA MANCHESTER UNITED


Kocha mpya wa Manchester United, Louis van Gaal.
KOCHA wa timu ya Taifa ya Uholanzi, Louis van Gaal ndiye kocha mpya wa Manchester United. Gaal ataiongoza timu hiyo kwa miaka mitatu baada ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Aliyekuwa kocha wa muda wa timu hiyo, Ryan Giggs ndiye atakuwa msaidizi wake.
Klabu ya Manchester United imethibitisha taarifa hizi kupitia ukurasa wake wa Facebook hivi 
Share:

Pombe yamponza Isabela Mpanda .....Avua nguo hadharani na kuacha CHUPI wazi



 
Miss Ruvuma 2006, Isabela Mpanda amedhihirisha jinsi asivyojiheshimu  baada ya kuvua nguo hadharani na kuacha nyeti nje bila kujali watu waliokuwa wakimshangaa.

Tukio hilo la kushangaza lilitokea Alhamisi iliyopita kwenye Ukumbi wa Mawela uliopo Sinza, Dar ambako kulikuwa na kitchen party ya mwigizaji, Vanita Omary ambapo Isabela aliwashangaza watu baada ya kuacha nyeti nje.
 
Bila chembe ya aibu, Isabela akivalia gauni fupi akiwa tilalila, alikuwa akicheza muziki huku akilinyanyua gauni juu na kuacha sehemu nyeti za makalio nje na kusababisha ‘kufuli’ yenye muundo wa bikini kuonekana.

Ishu hiyo ilizua minong’ono kwa baadhi ya wageni waalikwa na kubaki wakimshangaa kwa kitendo hicho....
 
Akiwa anafanya tukio hilo la kujifunua alisikika akisema amepania sherehe hiyo kwani yeye ndiye wifi wa Vanita na kama mwigizaji Jacqueline Wolper aliacha kufuli lake kubwa wazi na yeye aliamua kuonyesha lake aina ya bikini nje ili lionekane kwani ni la bei kubwa.

Share:

BIBI HARUSI ATOA YA MOYONI SOMA ALICHOSEMA NA KUWAPA ISHARA YA MBAYA WALIO UZURIA HARUSI YAKE



1. Ukiwa single watakuuliza...... kwanini huna GF au BF??
2. Ukiwa na mchumba..... watahoji mmekaa sana mwaoana lini??
3. Ukioa utasikia............. mbona hamzai nyie twataka wajomba na shangazi..!!

4. Mkizaa watakuja na hii..... mtoto kakua mtafutieni dada au kaka yake!
5. Ukimtafuta....... utasikia mbona mnazaa haraka haraka hamuogopi maisha.??
Share:

UCHAWI MCHANA KWEUPE!!..NJIWA MWENYE HIRIZI ATIKISA MUHIMBILI

 USHIRIKINA! Hofu kubwa ilitanda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jumatatu ya wiki iliyopita, baada ya Njiwa mweusi, mwenye miguu myekundu akiwa na hirizi iliyofungwa katika mojawapo ya mabawa yake, kutua katika miguu ya mgonjwa aliyekuwa amelazwa wodi namba tatu, jengo la Mwaisela.
Njiwa aliyetua kwenye kitanda cha mgonjwa na baada ya muda mgonjwa akafariki.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya wauguzi wa wodi hiyo ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema tukio hilo lilitokea saa 3.55 asubuhi ambapo njiwa huyo aliingia kupitia dirishani na kwenda kutua mguuni mwa Mwanahawa Ngunda (61) aliyekuwa amelala kitanda namba 7, ambaye anadaiwa kuwa mkazi wa Kimara.
Njiwa huyo aliingia dirishani muda mfupi baada ya mgonjwa aliyekuwa jirani na Mwanahawa, aitwaye Fatuma Musa (45) kurejea wodini hapo akitokea kupata vipimo ambapo alisaidiwa na ndugu zake kupanda kitandani kutokana na kuishiwa nguvu.
Inadaiwa kuwa baada ya kuingia wodini, njiwa huyo alianza kuzunguka na kuleta taharuki kubwa kwa wagonjwa, wauguzi na ndugu waliokuwemo, kiasi cha baadhi yao kukimbia huku wakipiga mayowe, kabla ndege huyo hajaenda kutua miguuni mwa mgonjwa huyo, huku akiwa ametuna na macho yake mekundu yakiwa yanalenga lenga machozi.
Inasemekena baada ya muda, ndege huyo aliruka na kutua dirisha lililokuwa usawa wa kitanda alicholala Fatuma na kuzidi kuwakoroga watu ambao waliamini kuwa ni mambo ya kishirikina. Ndugu wa mgonjwa aliyetuliwa na njiwa huyo, anayedaiwa kuwa ni mama yake mzazi, alikosa amani akiamini jambo baya lingemtokea.
Lakini katika hali ya kushangaza zaidi, mhudumu mmoja wa wodi hiyo alisema wakati watu wakitaka njiwa huyo aondolewe ili kuondoa usumbufu, dada wa Fatuma, aliyejulikana kwa jina la Mwanaisha Musa alimwambia mhudumu kuwa yeye amempenda ndege huyo na anaomba apewe kwani anahitaji kwenda kumfuga.
Kitanda kikiwa tupu baada ya mgonjwa kufariki.
Mhudumu huyo alimweleza dada huyo kuwa anaweza kumchukua kama anaweza, ndipo dada huyo alipomwambia kaka yake aliyetajwa kwa jina la Yasini amkamatie, ambaye alimfuata dirishani na kumkamata bila ndege huyo kuleta ubishi na kumkabidhi dada yake.
Baada ya dada huyo kukabidhiwa ndege huyo na yeye kumfunika na kanga yake kama kichanga, ndipo ndugu wa mgonjwa aliyetuliwa na njiwa huyo alipodaiwa kupandisha mashetani, akimfuata Mwanaisha ambaye alishaanza kutoka wodini hapo.
Ndugu huyo alimfuata akidai kulikuwa na jambo kwani haiwezekani watu wote wamuogope njiwa huyo, lakini yeye amchukue bila hofu.
Inadaiwa kwamba pamoja na mtoto wa marehemu kupiga mayowe lakini Mwanaisha hakuweza kumwachia njiwa huyo. Hata hivyo, mkusanyiko mkubwa wa watu na mayowe, yaliwafanya walinzi kuingilia kati kumtaka mama aliyemchukua njiwa huyo, kumkabidhi kwao mara moja.
Baada ya kukabidhi, Mwanaisha na kaka yake waliondoka na kumuacha ndugu wa mgonjwa akilalamika juu ya usalama wa mama yake, hivyo kuanza kuwapigia simu ndugu na jamaa zake akiwaeleza juu ya tukio hilo.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika wodi hiyo na kukuta kitanda alicholazwa mgonjwa aliyekanyagwa na njiwa akiwa hayupo na alipouliza, wauguzi walisema mgonjwa huyo alifariki siku iliyofuata (Jumanne wiki iliyopita) muda kama uleule wa saa 3.55 ambao njiwa huyo alifika.
Bi. Fatuma akiwa wodini.
Fatuma ambaye bado amelazwa wodini hapo alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikiri kutokea.
“Ni kweli njiwa mwenye hirizi alitokea hapa wodini na alipoingia akamkanyaga mgomjwa mwenzangu, hata hivyo dada yangu alimpenda,

alimuomba mhudumu amruhusu amchukue, alikubaliwa na alipomchukua ndipo mtoto wa marehemu alipandisha mashetani na dada aliamua kuwakabidhi askari,” alisema mgonjwa huyo aliyedai hali yake bado siyo nzuri na kwamba anasubiri vipimo.
Habari zaidi zinasema njiwa huyo alitoweka kiaina kutoka mikononi mwa askari wa Muhimbili wakati akishikiliwa katika ofisi kuu ya usalama wakisubiri agizo kutoka kwa viongozi wa juu.

Msemaji mkuu wa hospitali hiyo, Aminiel Akaesha alipohojiwa alikiri kutokea kwa tukio hilo huku baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo wakizungumzia kuhusu uwepo wa ishara ya mambo ya kishirikina wakati mwingine watu wasioonekana wakizungumza hasa katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti.
Share:

ZIJUE SIFA ZA MWANAMKE WA KUOA (WIFE MATERIAL)



Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.

Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.

Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.

Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtamkia kwamba anataka kumuoa.
  1. MWEYE MAPENZI YA KWELI
  2. MWENYE TABIA NZURI
  3. MWENYE UCHU NA MAENDELEO
  4. ASIYEPENDA MAKUU
  5. MVUMILIVU
Mwanamke ukiwa na sifa hizo tano hapo juu unauwakika wa 100% kuolewa.Nawasilisha!
Share:

BREAKING NEWZ:: AJALI MBAYA YATOKEA NCHINI MSUMBIJI, WATANZANIA 7 WAHOFIWA KUFA

Majira ya Saa 11 jioni imeripotiwa kutokea ajali mbaya iliyohusisha Gari ndogo aina ya Toyota Haice...Nchini Msumbiji katika Sehemu inayoitwa Namanyambili.

Chanzo cha ajali hiyo Chasemakana kuwa ni Kupasuka kwa Tairi la Mbele upande wa Kushoto wa Gari hilo na Kugonga Mti uliopembezoni mwa Bara Bara. Watu 7 wahufiwa kufa na Majeruhi 5 wako hoi katika Hospitali Nchini Msumbiji. Gari likitokea Montepuez/pemba.

Watu hao walikuwa wakitokea katika machimbo wakielekea Nyumbani kwa ajili ya Mapumziko.
Share:

Monday, 19 May 2014

HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI MHE. DKT. SHUKURU JUMANNE KAWAMBWA (MB)

Ministry of Education and Vocational Training
















HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI MHE. DKT. SHUKURU JUMANNE KAWAMBWA (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2014/2015
Read more...
 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger