Monday 29 July 2024

SERIKALI KUFADHILI MASOMO YA TEKNOLOJIA YA NYUKILIA

...


Na Dotto Kwilasa,Dodoma

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema Serikali imetenga bilioni 1.6 kuwekeza kwenye Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Hayo yameelezwa jijini hapa na Waziri wa Wizara hiyo Prof.Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ufadhili wa masomo ya Chuo Kikuu nje ya nchi kwa asilimia 100 kwa shahada za umahiri(MSc)katika fani za Sayansi na teknolojia ya nyukilia ambapo kiasi hicho cha fedha kimetengwa kwa jili ya ufadhili huo.

Prof.Mkenda amesema kuwa Wizara hiyo kupitia Tume ya nguvu za Atomu Tanzania (TAEC)imetangaza kutoa ufadhili kwa mwaka huu wa fedha 2024/25 wa Samia Scholarship Extended ambapo itasaidia kukidhi mahitaji makubwa ya huduma zitokanazo na Teknolojia ya nyukilia na upungufu wa wataalamu nchini.

"Wizara imebaini ongozeko kubwa la matumizi haya hasa kwenye miradi mikubwa ya madini kama vile Urani,Madini adimu na maeneo mengine ambayo yanahitaji nchi kuwa na wataalamu wa ndani na wabobezi kwelikweli,

"Tangu mwaka wa fedha 2022/23 serikali kupitia Wizaracya Elimu ilianza programu ya kutoa ufadhili kwa asilimia 100 kwa wanafunzi bora katika masomo ya sayansi kuanzia ngazi ya kidato cha sita,"amesema.

Amesema kuwa ufadhili unawalenga wanafunzi walichagua kusoma shahada ya kwanza katika masomo ya Sayansi,TEHAMA na Teknolojia, Uhandisi wa uhasibu,hisabati na elimu tiba.

"Mpaka sasa Tanzania inawataalamu sita tu wa Medical Physics pamoja na Nuclear Medical Doctors ambapo mtaalamu mmoja ni wa Radiochemistry na madaktari wawili tu wa Radio Pharmacist.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Prof.Najat Mohamed ametaja lengo la ufadhili huo kuwa unalenga eneo la Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia katika ,matibabu ya saratani,utafiti viwandani na mazao,nishati ya Nyuklia na utafiti wa vinu vya Nyuklia pamoja na uzalishaji wa dawa za mimea.

Ametaja sifa za waombaji wa ufadhili huo kuwa utatolewa kwa waombaji wenye sifa katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanazania(TCU)kwenye nchi za Australia,Austria,Ubelgiji,Canada,China,Jamhuri ya Czech,Sweden,Ufaransa,India,Korea ya Kusini,Uturuki,Urusi,Finland,Uingereza na Marekani.

Pamoja na hayo Prof.Najat alisema kuwa dirisha la maombi lipo wazi na waombaji wote wapitie tovuti ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger