Saturday 13 July 2024

KATAMBI AZINDUA UMOJA WA WAZEE WASTAAFU TARAFA YA OLDSHINYANGA,ALIA NA MMOMONYOKO WA MAADILI

...

 

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu amekutana na kufanya mazungumzo na Wazee kupitia Baraza la Ushauri la Ushauri la Wazee Manispaa ya Shinyanga na 

amezindua umoja wa wazee wastaafu tarafa ya Oldshinyanga,huku akiwaomba wazee kusimamia suala la Mmomonyoko wa maadili.

Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 12,2024 katika ya Oldshinyanga.

Katambi akizungumza wakati wa kuzindua umoja huo wa wazee wastaafu, amesema wazee hao wamefanya jambo jema la kizalendo kwa kuanzisha umoja wao ambao utasaidia kutoa ushauri kwa viongozi mbalimbali wakiwamo watumishi wa Serikali pamoja na kuzuia Mmomonyoko wa maadili.

Amesema wazee ni tunu ya taifa,hivyo wanategemewa katika mambo mbalimbali ya ushauri na ndiyo maana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anawathamini na hata kuweka mambo sawa katika masuala ya pensheni.
"Umoja huu wa wazee ambao nimeuzindua leo tunautengemea sana katika masuala ya ushauri,watu kuwa wazalendo na kupenda uraifa wao pamoja na kuzuia tatizo la Mmomonyoko wa maadili," amesema Katambi.

"Tatizo hili la mmonyoko wa maadili ni tishio kwa usalama wa nchi, sababu hata baadhi ya viongozi wa Serikali limewakumba na hata kutumia madaraka vibaya na kufanya ufujaji wa mali za umma na kunyanyasa wananchi,"ameongeza.
Aidha,amewaomba wazee kuchukua hatua za makusudi juu ya kudhibiti tatizo la Mmomonyoko wa maadili sababu kuna uwezekano taifa kuja kukosa viongozi imara kutokana na sasa wanaume kwa wanaume wanaoana na hata wanawake hivyo hivyo.

Naye Katibu wa umoja wa wazee wastaafu tarafa ya Oldshinyanga Stephano Tano,akisoma risala amesema wameanzisha umoja huo katika kusaidiana masuala mbalimbali yakiwamo ya shida na raha na kujikwamua kiuchumi.
Amesema kutokana na ongezeko la wazee wastaafu tarafa ya Oldshinyanga ndipo wakona waanzishe umoja wao mwezi juni mwaka huu na sasa wapo wazee 100.

"Umoja wetu ambao unazinduliwa leo una shabaha ya kuwaunganisha wastaafu wote,kusaidiana katika shida na raha,kujikwamua kiuchumi pamoja na kusimamia maadili mema kwa jamii,"amesema Tano.
Amesema pia wazee hao wanampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi zake na uongozo wenye dira nzuri kwa taifa.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger