Thursday 29 February 2024

KERO ZA ARDHI MOTO ZIARA YA RC MNDEME KAHAMA, VIONGOZI WANNE WASIMAMISHWA KAZI ...."POLISI KAMATENI WAUZAJI NA WATEJA BIASHARA YA NGONO"

...
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameshikilia hati wakati akisikiliza kero ya ardhi kutoka mmoja wa wananchi katika Manispaa ya Kahama.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameendelea na ziara ya kupokea, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambapo leo amekutana na wananchi wa Manispaa ya Kahama ambapo kero zilizotawala ni kuhusu migogoro ya ardhi lawama nyingi zikitolewa Ofisi ya ardhi Manispaa ya Kahama.

Akizungumza katika mkutano wake na wananchi uliofanyika katika viwanja vya Parking ya Malori katika kata ya Majengo Manispaa ya Kahama, Mhe. Mndeme amewasimamisha kazi viongozi wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Kahama.

"Malalamiko mengi Kahama ni ardhi, ardhi, ardhi, Rais samia anataka wananchi waishi bila migogoro, waishi kwa amani na usalama, hakuna aliye juu ya sheria. Viongozi wengi wamekuja hapa kero kubwa ni ardhi, huko ardhi kuna nini?, baada ya kuona ardhi ni changamoto kubwa hapa Kahama. Nimeamua kuwasimamisha kazi viongozi wanne Idara ya ardhi Manispaa ya Kahama. Naagiza wasimame kazi kuanzia leo, kuna sehemu zingine hati wanapewa watu wawili,Katibu Tawala simamia hili, unda tume ichunguze viongozi hawa kama watabainika hawana makosa watarudishwa kazini", amesema Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mbali na migogoro ya ardhi ikiwemo ya Maimuna Misana na  Caroline Dotto Magege iliyochukua muda mrefu kupatiwa ufumbuzi, kero zingine ni ubovu wa barabara, ukosefu wa huduma ya maji kwenye baadhi ya maeneo pamoja na uhalifu kwenye baadhi ya maeneo likiwemo eneo la Majengo linalodaiwa kuwa na vibaka huku wanawake wanaofanya biashara ya Ngono wakihusishwa na vitendo vya wizi.

Mhe. Mndeme ameliagiza jeshi la polisi kufanya doria za mara kwa mara ili kuwakamata wanawake wanaofanya biashara ya ngono pamoja na wateja wao kwani serikali hairuhusu biashara hiyo haramu.

“Naliekeza Jeshi la Polisi kufanya doria za mara kwa mara kwenye maeneo yote ambako panafanyika biashara ya ngono, kamateni anayefanya biashara ya ngono, mteja wake, mlinzi wake pamoja mmiliki wa nyumba inayohifadhi wanafanyabiashara ya ngono. Tunataka kila mmoja afanye kazi halali,wengine wanajificha kwenye biashara hii na kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi. Bidhaa na mnunuzi wa biashara ya ngono wote kamata, wanaowahifadhi nao kamateni”,amesema Mhe. Mndeme.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme anaendelea kusikiliza kero za wananchi muda huu

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameshikilia hati wakati akisikiliza kero ya ardhi kutoka mmoja wa wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameshikilia hati wakati akisikiliza kero ya ardhi kutoka mmoja wa wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiandika dondoo muhimu wakati akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiandika dondoo muhimu wakati akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameshikilia hati wakati akisikiliza kero ya ardhi ya Maimuna Misana (aliyesimama)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameshikilia hati wakati akisikiliza kero ya ardhi ya Maimuna Misana (aliyesimama)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameshikilia hati wakati akisikiliza kero ya ardhi ya Maimuna Misana (aliyesimama kushoto)
Caroline Dotto Magege akielezea kero ya mgogoro wa ardhi
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisikiliza kero ya ardhi ya Caroline Dotto Magege (aliyesimama kushoto)

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger