Friday 23 February 2024

BYABATO AKUTANA NA WANANCHI, WAFANYABIASHARA BAKOBA

...

Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Adv Stephen Byabato ambaye pia ni Naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki

Na Mariam Kagenda _ Bukoba

Mbunge wa Jimbo  la Bukoba Mjini  Adv Stephen Byabato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  leo Februali 23  2024 amefika  kata ya  Bakoba na kuzungumza na wananchi wa kata hiyo.

Licha ya kuzungumza na wananchi hao pia  amekagua shughuli za wafanyabiashara wadogo na kupitia eneo la mradi wa TACTIC katika  barabara ya Shabridin kuangalia maandalizi ya mapokezi ya mradi huo mkubwa. 
                         Mhe. Adv. Byabato alipata fursa ya kuzungumza na wananchi wanaopatikana katika maeneo hayo na kuwaeleza juu ya miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  ndani ya manispaa ya Bukoba pamoja na kuwaomba wananchi hao kuendelee kutoa ushirikiano kwa viongozi waliopo kuanzia kwa wenyeviti, madiwani na yeye mbunge ili mambo mazuri yaendelee kutekelezwa kama ilivyoahidiwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM  2020-2025.  

Kwa upande wake  diwani wa kata Bakoba Mhe Shabani Rashidi wakati akimkaribisha Mhe Mbunge baada ya kufika katika kata hiyo   amesema kuwa  wanabakoba wanajivunia  uongozi wa Mhe Rais   Samia Suluhu Hassan pamoja na  mbunge wa jimbo la Bukoba Mhe Stephen Byabato  kwani kila sehemu kuna mradi wa maendeleo  unaoendelea  hivyo wanaamini  miradi vipolo ikikamilika watakuwa hawana deni kwa wananchi.

Aidha Mhe. Shabani amesema kuwa wanaendelea kushirikiana  kushirikiana na wananchi katika maeneo tofauti tofauti katika kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za  serikali za kutatua kero za wananchi.

 Mhe.Adv Byabato  aliambatana na diwani kata Bakoba Mhe. Shabani Rashidi pamoja na viongozi wa mtaa.







Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini akiambatana na Mhe diwani wa kata ya Bakoba na wananchi wa kata hiyo wakati wa kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger