Na Frankius Cleophace Mara
SERIKALI imesisitiza utoaji wa elimu kwa jamii namna ya kuzingatia lishe bora ili kuweza kuepukana na udumavu kwa watoto na kuwa na afya bora.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu, Doroth Gwajima,kwenye ufunguzi wa mkutano wa 8 wa wadau wa lishe.
Amesema katika kutekeleza mpango jumuishi wa lishe Tanzania suala la elimu lina umuhimu wa pekee kwa kila mmoja ili kufikia malengo.
Amedai mpango huo wa miaka 5 utekelezaji wake wa hali ya lishe hauwezi kuwa na mafanikio kama hakutakuwa na elimu jumuishi ikiwa ni pamoja na kwa jamii husika.
Amesema kasi ya mapambano dhidi ya utapiamlo inaendelea kufanyika huku mbinu za kuboresha hali ya lishe hapa nchini zikifanyika.
" Yapo mambo 8 ambayo yakizingatiwa na kila mmoja ikiwemo wadau wa lishe kuhakikisha miradi inakuwa shirikishi marengo yetu yatakwenda kufanikiwa",amesema.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde, amesema wizara imeelekeza fedha nyingi kwenye masuala ya lishe na kuimalisha kilimo cha umwagiliaji kwa ajili ya chakula.
Amesema licha ya fedha hizo kwaajili ya masuala ya lishe kuasi cha shilingi bilioni 15 zimetengwa kwaajili ya kuwawezesha maafisa ugani ili waweze kuwahudumia wakulima.
Mwenyekiti wa wabunge vinara wa lishe na mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara, Ester Matiko, amesema wabunge wataendelea kuishauli serikali juu ya masuala mazima.
0 comments:
Post a Comment