Monday, 5 December 2022

BENKI YA CRDB, VISA WATAMBA KOMBE LA DUNIA

...

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiwa uwanjani kushuhudia mechi ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Poland ikiwa ni sehemu ya mwaliko kutoka Visa International, washirika rasmi wa malipo wa FIFA. Benki ya CRDB imekuwa na mahusiano ya muda mrefu na Visa kupitia mifumo yake ya malipo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulamajid Nsekela (katikati) akiwa na Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile (kushoto), na Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully Mwambapa wakati wa mkutano maalum uliondaliwa na kampuni ya Visa International nchini Qatar kujadili ushirikiano katika mifumo mipya ya malipo.
Mwakilishi wa Visa nchini Qatar akielezea juu ya mwenendo wa huduma za malipo na biashara kote duniani katika kipindi cha mwaka 2022




Kampuni ya Visa ambayo ndio mwezeshaji mkuu wa malipo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa), imeikaribisha Benki ya CRDB kushuhudia maboresho ya huduma zake kwenye michuano ya kombe la dunia yanayoendelea nchini Qatar.


Ili kurahisisha malipo kwa mashabiki na washiriki waliohudhuria michuano hiyo, Visa imefanya maboresho kadhaa kuondoa usumbufu kwa wateja wake.


Maboresho yaliyofanyika yanamruhusu mteja anaweza kuidhinisha malipo kwa kutumia sura yake bila kulazimika kutumia kadi au simu baada ya kukamilisha usajili, kutumia kadi za kidijitali pamoja na kulipia teksi kidijitali.


Katika kusherehekea mafanikio hayo, Visa imezialika benki kubwa inazoshirikiana nazo kutoka kila pembe ya dunia huku Tanzania ikiwakilishwa na Benki ya CRDB.


Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema mashabiki wa mpira nchini ambao wameenda kujionea michukuano hiyo wanaweza kulipia huduma na bidhaa wanazozitaka iwe hotelini, dukani au katika chombo cha usafiri.


“Michuano hii ya kombe la dunia ni fursa kwa Benki ya CRDB na Visa kuonyesha na kudhihirisha ubora wa huduma zetu za malipo.


Kadi zetu za TemboCard Visa zinatumiwa na Watanzania wengi wlaiokuja kushuhudia michuano inayoendelea hapa Qatar,” amesema Nsekela.


Ushirikiano wa Benki ya CRDB na Visa umekuwa na mchango mkubwa katika kuwawezesha Watanzania kupata huduma bora za benki hata kushiriki kwenye uchumi wa kidijitali.


Tangu mwaka 2014 ulipoanza kwa kuitambulisha Tembocard Visa, ushirikiano huo umewawezesha Watanzania kupata huduma za fedha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.


"Benki ya CRDB inajisikia fahari kuwa mbia wa Visa kuwawezesha mashabiki wa mpira wa miguu kufurahia mchezo huku wakilipa kwa namna rafiki kwa kutumia kadi zetu za TemboCard Classic, Gold, Platinum, na Infinite zenye huduma zinazokidhi mahitaji ya mteja,” amesema Abdulmajid Nsekela.


Wakati wote, Nsekela amesema benki imekuwa ikitumia juhudi kubwa, kwa kushirikiana na Visa, kuboresha na kuongeza ujumuishaji wa wananchi kwenye huduma za fedha.


Kutokana na uwezo wake, Nsekela amesema TemboCard Visa zinaweza kutumiwa kwenye mashine za kutolea fedha (ATM), vituo vya mauzo hata majukwaa ya mtandaoni yanayomruhusu mteja kufanikisha muamala akiwa mahali popote duniani.


"Mpaka sasa tuna zaidi ya wateja milioni 4 wanaotumia huduma kupitia kadi zetu, wengi wanamiliki TemboCard Visa. Malengo yetu ni kuhakikisha mteja anaweza kupata huduma aitakayo kutoka popote alipo na wakati wowote anaoihitaji.


Mwanzon wateja hawakuwa tayari kufungua akaunti kutokana na ulazima wa kwenda kwenye tawi la benki watakapohitaji kuzitumia fedha zao lakini ushirikiano wetu na Visa umeondoa ulazima huo,” amesema Nsekela akisistiza kuwapo kwa CRDB Wakala nako kumeongeza maeneo ambako wateja wa benki wanaweza kupata huduma.


Kwa sasa kuna zaidi ya CRDB Wakala 25,000 wanaosaidia kufikisha huduma hata maeneo yasiyona tawi huku mifumo ya kidijitali ya benki ikiongeza fursa za kulipia bili za Serikali kwani imezijumuisha zaidi ya taasisi 4,000 za umma.


Huduma za kidijitali ni kati ya vipaumbele vya Visa hata Benki ya CRDB kwani teknolojia hiyo siyo tu imerahisisha miamala ya wateja bali ukusanyaji mapato kwa mamlaka za serikali.


Katika kampeni iliyoizindua mapema mwaka huu kuhamasisha uchumi wa kidijiti, wateja wanne wa Benki ya CRDB wanaotumia TemboCard Visa walilipiwa nauli ya ndege na tiketi za kuingia uwanjani kushuhudia mechi za kombe la dunia, visa ya kuingia Qatar pamoja na malazi ili kuwapa nafasi ya kufurahia michuano hiyo inayoendelea kutokana na matumizi ya kadi zao.


Ujumbe wa Benki ya CRDB ulioenda Qatar ulipata fursa ya kutembelea vituo vya ubunifu kama sehemu ya mwaliko wa kuhudhuria michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022.


Vilevile, ulishuhudia mtanange wa makundi uliozihusisha Argentina na Poland, pamoja na ule wa Japan na Hispania.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger