Thursday 10 March 2022

MUHIMBILI YATOA UFAFANUZI VIDEO YA PROF. JAY INAYOSAMBAA MTANDAONI

...


Hospitali ya Taifa Muhimbili leo Machi 10, 2022 imetolea ufafanuzi taarifa inayosambaa kwenye mtandao wa kijamii kuhusu Joseph Haule maaruru Professor Jay na kusema “Kuna video inayosambazwa na Mtandao ikimuonesha Profesa Jay akipatiwa matibabu Muhimbili Hospitali Upanga”.

“Uongozi wa Hospitali unatoa taarifa kuwa video hii haijarekodiwa na kusambazwa na Hospitali, tumesikitishwa na tunalaani vikali kitendo hiki cha kumrekodi mgonjwa anayepigania uhai wake ICU na kuisambaza, hiki ni kiwango cha juu cha kukosa utu na maadili”.

“Tunafuatilia kwa ukaribu tukio hili ili kubaini chanzo cha video hiyo ili hatua stahiki zichukuliwe, Wananchi endeleeni kuwa na imani na Hospitali ta Muhimbili” imeeleza taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Muhimbili.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger