Wednesday, 4 August 2021

RC Tabora Atoa Angalizo Kwa Watoa Huduma Wa Chanjo

...


NA TIGANYA  VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Buriani amewataka wafanyakaziwa sekta ya afya waliopewa jukumu ya kuendesha zoezi la kutoa chanjo ya UVIKO 19 kuwa waadilifu na kufanyakazi kwa uzalendo.

Ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa utoaji wa chanjo ya UVIKO kwa makundi mbalimbali iliyofanyika Kimkoa mjini Tabora.

“Naelekeza pia kwa huu mgao wa COVAX FACILITY ni marufuku Hospitali yoyote (ya umma au binafsi) kulipisha Wananchi gharama yoyote katika zoezi hili la chanjo na lifanyike kwa uadilifu na kwa haki kwa walengwa wa sasa” amesisitiza

Balozi Dkt Batilda Buriani amesema kuwa chanjo hiyo kwa sasa zinatolewa kwa kufuata vipaumbele vya makundi yenye uhitaji mkubwa ambayo ni Watumishi wa sekta ya Afya, watu wazima wenye umri wa miaka 50 na kuendelea na  watu wenye magonjwa sugu.

Amesema uchanjaji kwa makundi yote nchini ni wa hiari au huru kwa kila mwananchi.

Balozi Dkt, Batilda amesema Tabora imepata kiasi cha chanjo 30,000 ambazo zitatoa  fursa kwa Wananch ambao wako tayari kuchanjwa kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 pamoja na kupunguza hatari ya kupata ugonjwa na madhara makubwa endapo mtu atapata maambukizi.

Amesema kwa Mkoa wa Tabora umeanza rasmi utoaji wa chanjo ya UVIKO-19  tarehe 03 Agosti 2021 katika vituo vilivyoainishwa katika Mkoa ambavyo ni vituo vitatu (3) kwa kila Halmashauri na kufanya Mkoa wa Tabora kuwa na jumla ya vituo 24.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora (RMO) Dkt. Honoratha Rutatinisibwa amewataka watu waliochanja kuendelea kuchukua hatua za kujikinga na UVIKO 19.

Amesema katika nchi ambazo wamechanjwa wamepunguza vifo na kulaza wagonjwa.

Kwa upande wa Askofu wa Kanisa la Anglikana Dkt. Elias Chakupewa ameitaka jamii kuacha upotoshaji kuhusu chanjo badala yake waendelee kuwatia moyo wataalamu.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger