Afisa Mabinti wa Shirika la Rafiki SDO, Maria Kamage (kushoto) na Mabinti wakionesha bidhaa wanazozalisha kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Rafiki SDO limeshiriki Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yaliyofungwa leo Jumapili Agosti 1,2021 na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko kwa kuonesha na kuuza bidhaa zinazotengenezwa na Mabinti wanaofadhiliwa na shirika hilo kwa lengo kuwainua kiuchumi.
Afisa Mabinti wa Shirika la Rafiki SDO, Maria Kamage amesema wanawasaidia mabinti kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa elimu za ujasiriamali, akiba na uchumi ambayo inawawezesha kupitia hizo akiba kupata mikopo katika vikundi vyao kuanzisha biashara zao binafsi na kuwafanya wasiwe wategemezi na kuwaepusha na vishawishi na kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Mabinti kutoka Rafiki SDO wakionesha bidhaa wanazozalisha kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga.
Afisa Mabinti wa Shirika la Rafiki SDO, Maria Kamage (kushoto) akiwa banda la Rafiki SDO kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment