Monday, 2 August 2021

IGP Sirro Aionya CHADEMA na Wanaokusudia Kufanya Vurugu

...


Jeshi la polisi nchini limetoa onyo kwa mtu au kikundi cha watu watakaojaribu kuhamasisha mikusanyiko isiyo rasmi au kuandamana kwa namna yoyote.

Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu Agost 2,2021 Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro amesema tuhuma dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA  Freeman Mbowe na wenzake ziko chini ya mamlaka ya mahakama.


Mbowe na wenzake watatu, wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo la kupanga njama za ugaidi na uhujumu uchumi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Sirro amewaonya wale wote wanaokusudia kufanya maandamano tarehe 5 Agosti 2021, siku ambayo kesi hiyo itatajwa tena kutokufanya hivyo kwani “kuvamia mahakama ni sawa na kuvamia kambi ya jeshi.”

"Jeshi la polisi halitegemei mtu au kikundi cha watu kwa namna yoyote kutoa shinikizo kwa mamlaka ya mahakama au kwa mtuhumiwa Freeman Mbowe aachiwe "amesema Sirro.

"Jeshi la polisi linatoa onyo kwa mtu au kikundi cha watu kitakachojaribu kuhamasisha mikusanyiko isiyo rasmi au kuandamana au namna yoyote ile kutoa shinikizo lolote,"amesema.

“Chadema wanasema mwenyekiti wao (Mbowe) ameonewa, wanavyoona wao hawezi kufanya hivyo, sasa kama Mbowe ni mkweli na amamuamini Mungu waende wakamuulize jambo hili unasemaje.”

“Lakini kabla ya uchaguzi nilisema kuna watu wamepanga kuhakikisha uchaguzi haufanyiki, nilisema kuna watu wamepanga kulipua visima vya mafuta na nilisema wamepanga kuua viongozi na nilisema tutawakamata,” amesema Sirro

“Habari ya yeye wajue ni binadamu, anaweza kufanya makosa, tumempeleka mahakamani tuiache mahakama itimize wajibu wake.” amesema Sirro
 

Sirro amewataka viongozi wa dini na taasisi nyingine ziache kusema Mbowe anaaonewa na badaala yake wasubiri mahakama iamue.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger