Sunday, 20 June 2021

RAIS SAMIA AMTEUA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA, KHERI JAMES KUWA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO DAR, JOKATE TEMEKE

...


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Jumamosi Juni 19,2021 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilayanchini ambapo amewabadilisha vituo vya kazi baadhi, ameingiza sura mpya na kuwarudisha waliowahi kushika nafasi hizo.

Katika uteuzi huo, Rais Samia amemteua Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Kheri James kuwa mkuu wa wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameteua wakuu wa wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam kama ifuatavyo;


1.Godwin Crydon Gondwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

2 Ng’wilabuza Ndatwa Ludigija kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala.

3. Jokate Urban Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

4. Fatma Almas Nyangasa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni.

5.Kherry Denis James kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.

Wakuu wa Wilaya wateule wataapishwa kuanzia tarehe 21 Juni, 2021 saa nne (4) asubuhi na Wakuu wa Mikoa yao.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger