WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akizungumza leo Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya siku moja kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa |
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillow akizungumza wakati wa ziata hiyo
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akichimba Mtaro wa Maji Mtaa wa Kiruku Kata ya Mabokweni Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya siku moja
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso leo amefanya ziara ya siku moja ya kukagua mradi wa Maji Mabokweni Jijini Tanga huku akiagiza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani Tanga kutoa kiasi cha fedha Sh 818 milioni ili kukamilisha mradi wa maji Mabokweni ambao utekelezaji wake umekwama tangu mwaka 2013.
Mradi huo kwa sasa unatekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) huku akiagiza pia Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji(EWURA) kuja jijiji Tanga kupitia gharama za ankara za maji.
Ambapo gharama yake ya utekelezaji ni Sh 918 milioni na unaohudumia kata mbili za Mabokweni na Chongoleani ulikwama kwa muda mrefu hivyo Wizara ya Maji imetoa kiasi cha Sh.100 milioni na kuitaka RUWASA kutoa kiasi kilichobaki.
Kuhusu EWURA kuja jijini Tanga baada ya mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu kumueleza Waziri Aweso kuwa baadhi ya malalamiko ya wananchi wa Tanga kukatiwa huduma kutokana na bei kuwa kubwa.
" Wananchi Tanga wameunganishwa na huduma ya maji lakini hawana maji kutokana na bili kubwa,"alisema Ummy Mwalimu.
Kuhusu gharama za usanifu wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miradi ya maji amesema kuwa wizara hiyo imeandaa mwongozo wa usanifu wa ujenzi ambao unaonesha gharama za ujenzi nchini
Amesema kuwa wamekuja na mfumo huo baada ya kubaini katika miradi ya ujenzi wa miundombinu ya maji ya aina moja katika maeneo tofauti ilikuwa inapishana kwa gharama,hivyo kwa kuliona hilo wizara imeaandaa mwongozo huo.
Kuhusu mradi wa Mabokweni ambao utekelezaji wake ulianza mwaka 2013 chini ya Mpango wa Mradi wa Maji Vijiji 10 awamu ya kwanza(WSDP I) ambao haujakamilika amesema kuwa miradi hiyo ya maji vijijini ilikuwa ya kihuni kutokana na kwamba ilikosa usanifu na mengine wataalamu walikuwa wananakili na kudurufu na haikuwa na uhalisia.
"Hii michakato isiyokuwa ya lazima katika wizara ya maji sitaki,nataka wataalam wa wizara ya maji mkae kama jopo miradi ikamilike kwa wakati,"alisema.
"Lakini pia hii miradi ya maji katika vijiji 10 ilikuwa ya kihuni ukitizama miradi hiyo ilianzishwa haikuwa na chanzo"Alisema Waziri Aweso
Katika hatua nyingine ameagiza bei za maji pembezoni mwa mji ziwe Sh 50 baada ya Sh 100.
Awali akizungumza Mbunge wa Jimbo la Tanga,Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) alisema kuwa mradi huo ambao unahudumia vijiji vya kata mbili za Mabokweni na Chongoleani umekuwa ni changamoto kwa vijiji vya Kibafuta, Chongoleani, Mabokweni,Mzizima,Mleni na Kiruku.
Naye kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mhandisi Geofrey Hilly amesema kuwa mradi huo awali ulikuwa unatekelezwa na mkandarasi Ms NCL-Abbeys Joint Venture kwa gharama ya Sh.2,412,997,490/- lakini mkandarasi alishindwa kutekeleza kwa wakati hivyo baada ya mabadiliko ya Sheria ya Maji ya 2019 mradi huo ulikabidhiwa Tanga UWASA Januari 2020 kuukamilisha.
Alisema kuwa usanifu wa mradi ulipitiwa upya na kuanzisha mahitaji ya vifaa na gharama za mradi kwa utekelezaji kupitia 'Force Account '
0 comments:
Post a Comment