Friday, 12 February 2021

AMUUA DADA YAKE UGOMVI WA HELA YA NYANYA ROMBO

...

Picha ya nyanya
**
Na Mwandishi wa Malunde 1 blog
Mkazi wa kijiji cha Urauri ,kata ya Reha wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro Magreth Mushi ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na kaka yake aitwaye Neoni Lazaro kwa madai ya kugombania fedha alizouza nyanya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona amesema tukio hilo limetokea Februari 9, 2021 saa tatu usiku katika kijiji cha Urauri kata ya Reha wilayani Rombo.

Amesema Magreth alifariki dunia usiku huo wa kuamkia Februari 10 alipopelekwa katika Hospitali ya Huruma kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger