Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Anjelina Lutambi akiwahutubia wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwenge nyuma yake in Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.
Mkurugenzi Mkuu wa TASAF Radislaus Mwamanga akiangalia bidhaa za sabuni zinazotengenzwa na mnufaika wa TASAF Halima Musa
Bweni la Shule ya Secondari ya Mwenge lililokarabatiwa na Serikali hivi karibuni
Na John Mapepele,Singida
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu , George Huruma Mkuchika amewataka wananchi wote nchini kushirikiana na Serikali kuwabaini wananchi wasio na sifa ya kujiandikisha kwenye Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya utekelezaji Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) ambapo umezinduliwa hivi karibuni na Rais John Pombe Magufuli ili kukamilisha asililima 30 za utekelezaji katika kipindi kifupi kijacho.
Mkuchika ameyasema hayo leo akiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Selikari za Mitaa wakati wakikagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na kamati hiyo kwenye ziara ya siku mbili katika Mkoa wa Singida.
Amesema zoezi hilo linaweza kukamilika kwa asilimia 100 endapo wananchi watatoa ushirikiano kubaini kaya masikini zenye sifa ya kusajiliwa kwa kuwa ndiyo wanaoishi nao na wajua ni kaya zipi zinasitahili
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamilia kuondoa umasikini na kwamba kinachotakiwa ni kuhakikisha fedha zinatolewa zinafanya kazi iliyokusudiwa ili kuleta tija.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Jasson Rweikiza amesema Kamati yake imeridhishwa na kazi ya TASAF iliyofanywa kwenye Mkoa wa Singida na kwamba Kamati yake imejipanga kufuatilia utekelezaji wake na kuona namna gani fedha hizo zinatumika kwa walengwa
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha hizo ambapo amesema zimekuwa chachu ya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii.
Akitolea mfano amesema kutokana na fedha hizo watoto wa kike wameweza kununua taulo za kike na hivyo kuwawezesha kuhudhuria masoma katika kipindi chote cha mwaka na kuengeza ufaulu wao katika masomo.
Kwa upande wake,Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Anjelina Lutambi amewataka wanafunzi katika Mkoa wa Singida kuwa na nidhamu, kufanya bidii kwenye masomo, na kujitambua ili waweze kufaulu katika masomo yao ambapo amesisitiza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa pia wamewaheshimu wazazi wao ambao wamekuwa wakiwahangaikia ili wapate elimu bora itakayowakomboa katika maisha yao.
0 comments:
Post a Comment