Wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee na Ester Bulaya, Meya wa Ubungo Boniface Jacob, Katibu wa chama hicho Mkoa wa Dar, Henry Kileo na wanachama wengine wamekamatwa na polisi baada ya kutokea vurugu wakati wakifuatilia Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kutolewa katika gereza la Segerea.
Mdee na Bulaya walitoka jela jana baada ya kulipa faini, leo walikwenda kumpokea Mbowe ambaye amekamilisha taratibu za kutoka jela.
Viongozi hao wamekamatwa saa 7:30 mchana baada ya kufika katika gereza hilo na kuanza kuzuiwa na askari wa Jeshi la Magereza waliotumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.
Wakati mabomu hayo yakipigwa, viongozi hao wa Chadema waliwekwa chini ya ulinzi kwa madai ya kukiuka amri halali ya kuwataka kuondoka katika eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment