Rais Magufuli ameingia Uwanjani wa CCM Kirumba Mwanza jijini Mwanza huku akipokewa kwa shangwe na vigeregere kutoka kila kona ya uwanja huo uliofurika.
Rais Magufuli aliingia uwanjani hapo saa 3: 14 asubuhi leo Jumatatu Desemba 9, 2019 akiwa kwenye gari la wazi akiongozwa na pikipiki nane gari moja mbele na nyingine nyuma.
Ameingilia mkono wa kushoto mwa uwanja na kuuzunguka akiwapungia wananchi mikono huku akishangiliwa kila alipopita wakati ukiimbwa wimbo wa taifa.
0 comments:
Post a Comment