Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda yaKati, Lazaro Nyalandu wamewasili katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza, kuhudhuria maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru.
Hata hivyo, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu hawakuvaa sare maalum za chama wala kombati ambazo zinatumiwa kama vazi maalum chama chao lakini wamepigilia suti nyeusi, mashati meupe na tai.
Taarifa ya kushiriki kwenye maadhimisho kwa Mwenyekiti wa CHADEMA ilitolewa juzi na Kamati Kuu ya chama hicho kwa kumuagiza Mwenyekiti wake kwenda kukiwakilisha chama hicho kwenye Sherehe hizo za Uhuru.
Hii ni mara ya kwanza kwa CHADEMA kushirii kwenye maadhimisho ya Uhuru tangu mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment