Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameitaka Kamati ya Usalama Mkoa wa Tabora kuwachukulia hatua wanasiasa na watu ambao wamekuwa wakiwachochea wafugaji kuingia katika maeneo ambayo yamezuiliwa na kuwavamia na kuwashambulia Askari ya Wanyama pori wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.
Alisema hatua imesababisha kuwawa kwa Asakari wawili katika eneo la misitu ya Isawima wakati walipokuwa wakijaribu kuwaondoa katika misti hiyo hivi karibuni.
Kanyasu alitoa kauli hiyo leo Mkoani Tabora wakati akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi zilizoko chini ya Wizara ya wa Maliasili na Utalii na uongozi wa Mkoa wa Tabora.
Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mgogoro wa Mistu ya Hifadhi wa Isawima umekuwa ukichochewa na Kiongozi wa Wafugaji ambaye pia ni Kiongozi wa Kisiasa katika eneo la hilo wilayani Kaliua, jambo linasababisha Askari kuvamiwa na kuwawa.
Kanyasu alisema ni vema hatua dhidi ya Kiongozi huyo zikachukuliwa kwa ajili ya kuwafanya watumishi wa Wizara ya Maliasi na Utalii na wengine ambao wanashughulika kulinda maeneo ambayo yamehifadhiwa kufanya kazi katika mazingira salama.
Aidha alisema watu wanaoendesha uvamizi na mauaji ya watumishi wanalinda maeneo yaliyozuiliwa wanajulikana kwa kuwa wanamiliki ng’ombe , hivyo ni vema wakatafutwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili maamuzi yajulikane kwa watu hao.
Kanyasu alisema vitendo hivyo visipochukuliwa hatua kali wavamilizi wataendelea kutekeleza mauaji na kuona kuwa wao wako sahihi kuendelea kuharibu maliasili na kuhatarisha maisha ya wanyamapori na wananchi wanaotegemea mistu hiyo kupata maji.
“Anapowawa mtumishi analinda maeneo yaliyozuiliwa hakuna mtu anayepiga kelele ..lakini wavamizi wanapoondolewa na vibanda vyao kuchomwa moto wanajitokeza watu kuwatetea na kupiga kelele…inasikitisha sana” alisema.
Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema tatizo hilo limeshaundiwa Kamati ya Uchunguzi na wanatarajia kutoa majibu ya kilichobainika na hatua za kuwachukulia wahusika hivi karibuni.
Katika hatua Naibu Waziri huyo aliwaonya watu ambao wametafisiri vibaya tamko la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania la kuruhusu vijiji 900 vilivyo kwenye hifadhi kuwapati hati na wao kuanza kuvamia maeneo mengine mapya kuwa watachukuliwa hatua kali.
Alisema tamko la Rais Magufuli halikusema kuwa watu waanze upya kuingia katika maeneo mapya kwa mtanzamo kuwa ipo siku nao wataruhusiwa kuendelea na shughuli zao.
Kanyasu alisema watakaokutwa katika maeneo ambayo yamezuiliwa watachukuliwa hatua kama wavamizi.
0 comments:
Post a Comment