Saturday, 9 November 2019

DC Chongolo Atekeleza Agizo La Rais Jpm La Kusimamia Kurudishwa Kwa Nyumba Ya Bibi Mwenye Miaka Zaidi Ya 80.

...
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo ametekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la kusimamia kurudishwa kwa nyumba ya Bi Amina Muhenga mwenye miaka zaidi ya 80 aliyozurumiwa kwa kipindi cha miaka zaidi ya 30 iliyopita.

Rais Dk. Magufuli alitoa agizo hilo zaidi ya miezi miwili iliyopita alipokuwa kwenye ibada ya jumapili katika kanisa la mtakatifu Petro ambapo Bi Amina alimfuata na kumueleza malalamiko yake kuhusiana na nyumba yake kuchukuliwa na mtu mwingine kinyume cha taratibu na hivyo kumsababishia kukosa makazi maalumu ya kuishi.

Mhe. Chongolo alieleza kuwa baada ya Rais kutoa maagizo hayo, kwakuwa ni waisaidizi wake ,walilifanyia kazi na hivyo kufanikisha kumrudishia Bi Amina nyumba yake pamoja na hati huku utaratibu mwingine ukiendelea kufanyika.

“Baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Bibi, Mhe rais  kwakuwa sisi ni wasaidizi wake, alituagiza kulifanyia kazi na leo hii tumehitimisha kwa kumkabidhi hati za umiliki wa nyumba yake, na mambo mengine tunaendelea kuyakamilisha, kuanzia sasa bibi anarudi kwenye nyumba yake.” Amessema Mhe. Chongolo.

Aidha Mhe. Chongolo ameonyesha masikitiko yake ya baadhi ya wananchi wanaoishi katika Wilaya ya Kinondoni kuishi kwa ujanja ujanja na kusema kuwa kunaidadi kubwa ya watu wanaoishi kwenye mfumo huo na hivyo kutoa onyo la kuwataka kuacha mara moja tabia hiyo.

Amesema imekuwa ni jambo la kawaida kwa wananchi hao kwani kila siku ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko yanayohusiana na kuzurumiwa kwa nyumba zao kwakutumia kigezo cha hukumu ya Mahakama na hivyo kuacha watu wakiteseka.

Ameongeza kuwa,wakitoka Mahakamani wanakuja kuwatoa watu wenye haki, sijui niseme nini ila ukiangalia kunahali ya rushwa, ambayo imekuwa ikiwatesa sana baadhi ya wananchi, kazi yetu sisi ni kusimamia haki,nitahakikisha haki inasimamiwa na inatolewa kwa mwenye haki” amesema Mhe. Chongolo.

Kwa upande wake Bi Amina amemshukuru rais Magufuli kwa kumsaidia kupata nyumba yake, na hivyo kusema kuwa anamuombea kwa mungu aendelee kuwatumikia wanyonge.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger