Saturday, 9 November 2019

DAKTARI AIBUKA NA BIBLIA YA SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAMKE...ZIJUE SIRI 5 ZA SEHEMU ZA SIRI

...
Kuna imani potofu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu sehemu za siri za wanawake, mwanamke mmoja ameamua kujitoa kuelezea masuala hayo.

Dr Jen Gunter amekua daktari wa kina mama huko Marekani na Canada kwa miaka 25. Ametoa kitabu hivi karibu kinachoitwa biblia ya sehemu za siri za wanawake.

Kutokana na mijadala mbalimbali kuhusu sehemu za siri za wanawake, kuna mambo makuu matano ambayo mwanamke anapaswa kujua.

1- Sehemu za siri zinajisafisha zenyewe

Idadi kubwa ya wanawake, wana imani kuwa wakitumia bidhaa mbalimbali za urembo, kama sabuni basi ndio watajisafisha vizuri sehemu za siri. lakini Dr Gunter anasema kuwa hakuna haja ya kutumia chochote kusafisha sehemu ya siri, kwa sababu kunajisafisha yenyewe

''Ni sehemu inayojisafisha yenyewe'' anasema Dr Gunter

Pia anaonya juu ya kutumia manukato sehemu za siri, anasema kuwa ni kama sigara ilivyo hatari kwa mapafu ya binadamu.

''Hata maji wakati mwingine huweza kuharibu jinsi ya ufanyaji kazi wa sehemu za siri, pia inaweza kusababisha kuambukizwa kwa haraka kwa magonjwa ya ngono, kujifusha pia kuna madhara yake kwani unaweza kujichoma na mvuke.

''Sehemu ya nje inaweza kusafishwa na maji kwa utaratibu'' anasema Dr Gunter

Sabuni huweza kusababisha asidi kwenye sehemu za siri, na ikifika umri wa kukoma kwa hedhi basi inashauriwa kutumia mafuta kama ya mzaituni ama ya nazi.

Seli za kwenye sehemu za siri hujitengeneza kila baada ya saa 96, tofauti na eneo lolote la ngozi, sehemu za siri hujirekebisha haraka zaidi.

2 -Ni muhimu kujua sehemu za siri kuanzia sehemu ya nje (Vulva)

Sehemu ya siri imegawanyika sehemu ya ndani na nje, sehemu ya nje ndio sehemu ambayo itakugusa kwenye nguo yako ya ndani, Dr. Gunter anasema kuwa ni muhimu sana kujua kutofautisha maeneo hayo.

''Huwezi kutaja maneno haya ya sehemu za siri kwa uwazi kwasababu tu ni jambo la aibu, hii si sahihi''

Anasisitiza kuwa kutumia maneno ya sehemu za siri si suala la aibu, na inaweza kuleta madhara kwa mwanamke pale ambapo atashindwa kueleza kwa usahihi ni sehemu gani za sehemu za siri anaumwa.

3 - Sehemu za siri za mwanamke ni kama bustani

Sehemu za siri zina jeshi kubwa la bakteria wazuri ambao wanasaidia kufanya kuwe na afya.

Bakteria wazuri wanatengeneza ute ambao una asidi kidogo ambazo zinaondoa bakteria wabaya, na hufanya kuweka unyevunyevu wakati wote.

Sababu hii inatakiwa kusiwekwe wala kupanguswa kwa kitu chochote ndani ya sehemu za siri ili kuhakikisha bakteria wazuri wabaki na kuwazuia bakteria wabaya kutokuchukua nafasi.

Dr Gunter anasema baadhi ya wanawake wamekua wakikausha sehemu za siri kwa kutumia kifaa cha kukaushia nywele, hawatakiwi kufanya hivyo, eneo hilo linatakiwa linabaki na unyevunyevu wakati wote.

4 - Nywele za sehemu za siri zipo hapo kwasababu.

Gunter anasema kuwa imekua ni utamaduni kwa wanawake kunyoa sehemu za siri na kubakiza upara kabisa, hii inaweza kusababisha kushambuliwa kwa urahisi na bakteria.

''Unavyonyoa sehemu za siri, unasababisha usumbufu kwenye ngozi, anasema Dr Gunter, tumeona watu wanajikata, na maambukizi pia''

Kama unataka kunyoa, unapaswa kutumia wembe safi, mpya, na unyoe namna ambayo nywele zimeota, ili kuepusha nywele kuota vibaya.

Lakini pia nywele zinatakiwa zibaki kwa sababu kwa namna moja ama nyingine husababisha athari kwa masuala ya ngono.

''Nywele zina maana yake, na ni sehemu muhimu kati ya ngozi na sehemu za siri'' anasema Dr Gunter.

5 - Umri unavyoenda unaathiri na sehemu za siri.

Baada ya miaka kadhaa ya kupata hedhi, wakati mwingine watoto, mayai ya uzazi huacha kuzalishwa na hedhi pia inakoma. Idadi ya homoni inayofanya mwili wa mwanamke uzalishe zinapungua sana, hii inaleta athari kwa sehemu za siri.

Tishu ambazo zinaleta unyevunyevu kwenye sehemu za siri zinapungua na kusababisha kubaki kukavu, na husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa,

Hii inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa baadhi ya wanawake, lakini Dr Gunter anasema kuwa wanaweza kupata msaada kwa kutumia vilainishi ambavyo huuzwa kwenye maduka ya dawa.

''Sio lazima upate shida unaweza kutumia vilainishi'' anasema Gunter.
Chanzo - BBC
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger