Sunday, 22 September 2019

Rais Magufuli Ashauri Wanaotuhumiwa kwa Uhujumu Uchumi na utakatishaji fedha Wakiri Makosa Yao na Waachiwe Huru

...
Rais Magufuli ameshauri mahabusu wa makosa mbalimbali hasa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ambao wapo tayari kuomba msamaha na kurudisha fedha walizotakatisha, wasikilizwe ndani ya siku saba kuanzia kesho Jumatatu Septemba 23 hadi Jumamosi ya Septemba 28, 2019.

Magufuli ameyasema hayo leo Jumapili Septemba 22, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua Ijumaa iliyopita ya Septemba 20, 2019.

“Mimi naumia kuona watu wapo mahabusu au watu wamefungwa. Ni bahati mbaya kwa sababu sheria zipo. Lakini mtu anapowekwa mahabusu inaumiza sana,” amesema Magufuli.

Kutokana na hilo, Magufuli amemwagiza Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), Biswalo Mganga na wote wanaohusika na sheria kuwasikiliza mahabusu wenye kesi za uhujumu uchumi ambazo hazitawafanya kutoka mapema kwa mujibu wa sheria na kama itaruhusu watoke.

Amewataka kutengeneza mazingira watu hao warudishe fedha zote walizochukua kwa sababu wanateseka kukaa mahabusu miaka hadi mitatu na wengine wamekonda.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger