Wednesday, 11 September 2019

Mwili wa Robert Mugabe kuwasili Zimbabwe leo

...
Mwili wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe aliyefariki dunia Ijumaa unasafirishwa leo kurejeshwa nyumbani kutoka Singapore kwa ajili ya mazishi.

Mugabe ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 , alikuwa hospitalini kwa matibabu nchini Singapore.

Taratibu za kitaifa za kuuaga mwili wake zitafanyika siku ya Jumamosi , kabla ya kuzikwa kijijini kwao Jumapili.

Robert Mugabe, ambaye alikuwa kiongozi wa vita vya msituni ambaye aliiongoza Zimbabwe baada ya Uhuru mwaka 1980, aling'olewa madarakani  mwaka 2017.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger