Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku vitu vitatu kutoonekana katika mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye kongamano la Dini lililofanyika katika uwanja wa Taifa alisema..’Kwanza
kwa watumiaji wa biashara ya Sheesha katika maeneo ya Bar, Clubs na
sehemu zingine kuanzia leo ni marufuku katika maeneo hayo’- Paul Makonda
‘Pili
ni marufuku kwa wavutaji wa Sigara kwenye sehemu za wazi kwani
wataalamu wanasema ule moshi unamuathiri yule asiyetumia hiyo Sigara
kuliko yule anayetumia Sigara’– Paul Makonda
‘Tatu
ni marufuku kwa ushoga kwenye mkoa wangu wa Dar es Salaam na mashoga
wote walio kwenye instagram na Facebook watakamatwa na wale wote wanao
wa follow mashoga kwenye mitandao ya kijamii basi watakuwa na hatia ile
kama ya mashoga‘- Paul Makonda
VIDEO
VIDEO
0 comments:
Post a Comment