Good news kwa watanzania wote kwa mwaka 2016 ilikuwa ni headlines za nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji, lakini leo July 5 2016 jina la Samatta limerudi tena kwenye headlines za usajili.
Kuanzia usiku wa July 4 hadi leo July 5 habari zilizokuwa zimesambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu Samatta ni kuwa yupo njiani kujiunga na klabu ya AS Roma ya Italia, hii ni taarifa ambayo imeenea kwa kiasi kikubwa hata kufikia baadhi ya wanasoka Tanzania kutumia social network zao kumpongeza.
Baada ya habari hii kuenea kwa kiasi kikubwa, MASWAYETU BLOG ilifatiliwa ambapo meneja wa staa huyo Jamal Kisongo amesema kwamba
“Huo ni uzushi tu hata sijui umetoka wapi na mimi nimesikia mitandaoni,
lakini nimewasiliana na Samatta hakuna habari kama hizo wala mawakala
wake hawana taarifa hizo”
0 comments:
Post a Comment