Mtoto wa kike, Rahila
Salim Ali (4) amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa umening’inizwa
kisimani na vidole vya mikono vikiwa vimekatwa na mashavu kuchubuliwa.
Tukio hilo limetokea jana asubuhi, katika eneo Njiapanda, Mbagala, Temeke baada ya mtoto huyo kutoweka nyumbani siku nne zilizopita.
Tukio hilo limetokea jana asubuhi, katika eneo Njiapanda, Mbagala, Temeke baada ya mtoto huyo kutoweka nyumbani siku nne zilizopita.
Akizungumzia tukio hilo, mama mzazi wa mtoto huyo, Raziah Ramadhani
alisema binti yake alitoweka nyumbani saa tano asubuhi, wakati wakiwa
pamoja wakitazama televisheni.
“Alitoka nje kama anaenda kucheza na wote
hatukuwa na wasiwasi. Baada ya saa moja tulishtuka baada ya kutomuona,
hivyo ikabidi tuanze kumtafuta,” alisema.
Alisema walitoa taarifa polisi
na kwenye baadhi ya vyombo vya habari bila mafanikio hadi jana mwili
wake ulipokutwa umening’inizwa kwenye kisima cha nyumba ya jirani yao.
“Nilipofika nilishangaa kuona nguo zake ni kavu na ana majeraha,”
alisema.
Alisema kisima hicho kina tundu dogo ambalo huenda wauaji
walijitahidi kuusukumiza mwili huo ili ionekane kama amefia humo
ikashindikana.
Alisema mpaka juzi mchana, kilikuwa kikitumika na kuwa
huenda mwili huo ulining’inizwa usiku wa kuamkia jana.
Baadhi ya
majirani waliliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina na
kuwachukulia hatua watu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya
ukatili dhidi ya watoto.
Kamanda wa Polisi Temeke, Andrew Satta alisema
wanaendelea na uchunguzi: “Taarifa zilizopo ni kwamba amekufa maji
lakini kwa hayo mazingira mengine tunaendelea kufanya uchunguzi zaidi.”
0 comments:
Post a Comment