BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

TAARIFA KWA UMMA
KUKANUSHA TAARIFA KWAMBA BODI HAINA FEDHA
Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa za upotoshaji zinazoenezwa
kwa sasa kwamba haina fedha.
Si kweli kwamba
Bodihaina fedha, ila ni kweli kwamba kumekuwa na ucheleweshaji wa kufikisha
fedha za wanafunzi vyuoni kutokana na zoezi la kuhakiki wanafunzi wanaonufaika
na mikopo linaloendelea vyuoni hivi sasa.
Hata hivyo,
maandalizi ya malipo hayo yameshafanyika na ‘pay sheets’ zimeshapelekwa vyuoni
tayari kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kusaini.
Bodi inatarajia
wakati wowote wiki ijayo baada ya zoezi la uhakiki kukamilika; itapeleka fedha
hizo vyuoni.
IMETOLEWA
NA:
KITENGO
CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
BODI
YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAREHE
2 JULAI 2016
0 comments:
Post a Comment