MTU
mmoja aliyejulikana kwa jina la David Makali maarufu kama Peter Mabula
amekamatwa na jeshi la polisi na kufikishwa mahakamani kwa kuwatapeli
wastaafu nchini.
Kamanda
wa polisi mkoani Dodoma, David Misime aliwaambia waandishi wa habari
kuwa, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatapeli wastaafu kwa kujifanya yeye ni
mtumishi wa Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
“Mtuhumiwa
pia amekuwa akijifanya ni mtumishi wa Mfuko wa pensheni wa Serikali za
Mitaa (LAPF), Mfuko wa Pensheni wa PSPF na Mtumishi wa ofisi ya Katibu
Mkuu wizara ya Afya na kufanikiwa kuwaibia fedha kwa njia ya mtandao
wastaafu kutoka katika mikoa mbalimbali.
“Wanachofanya
watu hawa hupiga simu Idara mbalimbali na kujifanya wapo TAMISEMI au
wizara nyingine na kuwataka wawatumie orodha ya wastaafu wa mwaka fulani
pamoja na namba za akaunti zao za simu,” amesema Kamanda Misime.
Amesema
kwa njia hiyo matapeli hao wamefanikiwa kupata orodha ya wastaafu
kutoka katika mikoa takriban 15 hususan kutoka kwenye idara ya afya.
“Wakishapata
orodha ya majina ya wastaafu na namba zao za simu, humpigia mstaafu na
kujitambulisha anatokea wizarani na kwamba anashughulikia wastaafu ambao
inaonekana walipunjwa kwenye mafao yao na inaonesha naye amepunjwa
milioni fulani,” amesema Kamanda Misime.
Amesema
watuhumiwa hao hutumia mwanya huo kuwatapeli fedha wastaafu kwamba
watume fedha ili wawasaidie waweze kupata fedha zao walizopunjwa na
baada ya mstaafu husika kutuma hizo fedha, mtu huyo anakuwa hapatikani
tena katika simu.
Kamanda
Misime amewatahadharisha wastaafu kutokubaliana na watu wa aina hiyo na
idara mbalimbali zichukue tahadhari na kila mara wahakikishe
kinachohitajika kinatoka katika idara husika na kwa mtu sahihi.
0 comments:
Post a Comment