Sunday, 3 May 2015

NEWS:"VIGOGO WATATU TANESCO WASIMAMISHWA KAZI"

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Waziri wa nishati na madini Mh.George simbachawene ameagiza
kusimamishwa kazi mara moja kwa wahandisi watatu wa shirika la umeme nchini TANESCO kutoka maeneo matatu jijini dar es salaam baada ya wahandisi hao kushindwa kuwajibika ipasavyo ikiwa ni pamoja na  kutochukua hatua wanapopewa taarifa za kero za wananchi  kwenye maeneo wanayosimamia .
Mh simbachawene amesema ameamua kuchukua umauzi huo baada ya yeye kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Tazara,Tabata Magengeni, na Temeke kuwapigia simu waandisi hao juu ya kero ya kuanguka kwa nguzo ambazo zinatishia uhai wa wananchi na kuambulia majibu ya kebehi na dharau kana kambwa watumishi hao sio serikali na sio wajibu wao wa kazi jambo ambalo amedai limesikitisha sana hivyo akiwa na wajumbe wa bidi ya Tanesco ameamua kuchukua aumuzi wa kuwasimimisha kazi na kufanya operesheni yeye mwenyewe ya kukagua magari ya imeegency ambayo yanaegeshwa Bar.
Wakati huo huo waziri huyo wa nishati na madini ametoa ufafanuzi juu ya Tanesco kuvunja mkataba na Kampuni ya SELCOM na kukiri kuwa kitendo hicho kimesababisha adha ya upatikanaji wa huduma ya umeme Kwa wananchi na tatizo hilo kwa sasa limeshatatuliwa baada ya TANESCO kuweka mambo sawa na makampuni mbalimbali ambayo yamekuwa yakitoa huduma ya mauzo ya umeme kwa njia ya mitandao ya simu na kudai huduma ya kununua umeme kwa sasa imesharejea kama kawaida katika mitandao ya simu.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger