Chelsea
ndio mabingwa wapya wa ligi kuu nchini Uingereza mara baada ya
kuwachinja Crystal Palace bao 1-0, mchezo uliopigwa katika uwanja wa
Stamford bridge jijini London.
Bao
la Chelsea lilifungwa na Eden Hazard katika dakika ya 45, kupitia
mkwaju wa penati mara baada ya hapo awali kipa kupangua penati hiyo na
kisha baadae kuunganisha kwa mara nyingine tena.
Ushindi huo umeipeleka Chelsea pointi 16 zaidi ya Arsenal ambao hata hivyo wana michezo mitano kibindoni.
Lakini hata Arsenal na Man City wakishinda michezo yao yote iliyosalia bado hawataweza kuwafikia Chelsea.
Hii
ni mara ya tatu sasa kwa Mourinho kushinda kombe hilo akiwa na Chelsea
na ni mara ya kwanza kwake tangu arudi tena klabuni hapo mwaka 2013.
Chelsea sasa watakuwa wamechukua kombe hilo kwa mara ya tano tangu klabu hiyo kuanzishwa.Chelsea (4-2-3-1): Courtois, 6.5, Ivanovic, 7, Cahill, 7, Terry, 7.5, Azpilicueta, 7.5, Matic, 7.5, Fabregas, 6.5, Cuadrado, 5 (Mikel 46, 6), Willian, 8 (Zouma 84, 6), Hazard, 6.5 (Filipe Luis 90, 6), Drogba, 6.5
Subs: Cech, Ake, Remy, Loftus-Cheek.
Scorer: Hazard: 45
Booked: Ivanovic, Terry
Jose Mourinho - 8
Crystal Palaxce (4-4-1-1): Speroni, 6, Mariappa, 6.5 (Kelly 60, 6) Dann, 7, Delaney, 7, Ward 7, Puncheon 6.5 (Sanogo 71, 6), McArthur, 7, Ledley 7, Zaha 6.5, Mutch 6.5 (Murray 61, 6.5), Bolasie 6.5
Subs: Hangeland, Hennessey, Jedinak, Lee.
Booked: Mariappa, Dann.
Alan Pardew - 7
MOM: Willian
Referee: Kevin Friend (Leicestershire)
Attendance: 41, 566
0 comments:
Post a Comment