Nyumba
kadhaa zimeboka na nyingine 80 kujaa maji kufuatia
mvua kubwa iliyonyesha kwa masaa mawili katika vijiji vya kitete na kadudu wilaya ya kilosa mkoani morogoro na kusababisha uharibifu wa mazao na baadhi ya familia kukosa makazi.
mvua kubwa iliyonyesha kwa masaa mawili katika vijiji vya kitete na kadudu wilaya ya kilosa mkoani morogoro na kusababisha uharibifu wa mazao na baadhi ya familia kukosa makazi.
Wakizungumza kwa huzuni wananachi wa vijiji vya kitete na kadudu
wameeleza mvua zimesababisha madhara makubwa ikiwemo nyumba kuanguka
na kusababisha baadhi ya kaya kukosa makazi ambapo kwa sasa wananchi
hawana chakula kutokana na vyakula kuharibika baada ya kujaa maji
huku mazao yaliopandwa mashambani yakiwemo mahindi yameseombwa na mvua
na kuomba serikali kuwasaidia chakula wanachi waliokubwa na
mafuriko.
Akitoa tarifa za tathmini ya awali ya mafuriko hayo afisa tarafa wa
tarafa ya dumila MOSES NCHIMBI amesema nyumba zilizo anguka kabisa ni
nane na nyingine 80 zimeharibika vibaya na kujaa maji ambapo
ameeleza chanzo cha athari hizo hayo ni kuziba kwa mto DYONGOYA
kutokana na baadhi ya wananchi kulima kando ya mto huo.
Mkuu wa wilaya ya kilosa BWANA JOHN NJEWELE amewapa pole wananchi
wa vijiji hivyo kwa athari walizozipata ambapo ameagiza watendaji wa
vijiji kata na vitongoji kuanza zoezi la kukagua na kubaini wananchi
waliolima na kujenga kando kando ya mito na kusabaisha mito kuziba na
maji kupoteza uelekeo na kujaa katika makazi ya wananchi.
0 comments:
Post a Comment