Baadhi ya madereva wa mabasi katika stendi kuu ya Mabasi
yaendayo Mkoani na nchi jirani Ubungo,wakishangilia wakiwa na mabango yao yenye jumbe : “Mabomu tumeyazoea! Tanzania bila madereva haiwezekani! muda huu wakiwa wamejikusanya wakimsubiria Waziri Mkuu Mizengo Pinda afike kuongea nao kufikia suluhu
Mgomo
wa madereva umeibuka tena leo Mei 4 baada ya mabasi na magari ya mizigo
kugoma tena kwa mara ya pili kwa lengo la kushinikiza kutatuliwa madai
yao ambayo awali baadhi ya viongozi wakuu wa Serikali walijaribu kutatua
mgogoro wao ambapo hata hivyo hawakufikia suluhu.
Kwa
hali ya leo Mei 4, Madereva hao wanashinikiza kuonana na Waziri Mkuu
Mizengo Pinda ndipo wafikie muafaka wao. Hata hivyo, Modewji blog
imeweza kushuhudia misululi ya wananchai wakitembea kwa miguu kuelekea
makazini na sehemu mbalimbali za miangaiko yao ambapo wengi wa wananchi
hao baadhi yao walikuwa wakipanda usafiri wa bajaji, Pikipiki na hata
baiskeli ilimradi kufika waendapo.
Maeneo
mengi ya vituo vya mabasi kumekuwa na misululu mengi ya abiria ambao
wamekosa tumaini licha ya wengine kupanda Pikipiki na wengine kutembea
kwa miguu.
Ubungo: Madereva waamuliwa kurudisha nauli za abiria
Katika
kile kinachoelezwa kuondoa usumbufu, jeshi la Polisi limeamua
kuwatangazia wenye mabasi kuakikisha wanarudisha nauli za abiria
waliokwisha wakatisha tiketi. Modewji blog imeshuhudia tangazo hilo
lililokuwa likitolewa na jeshi la Polisi waliokuwa ndani ya gari laa
POLISI. Hata hivyo licha ya tangazo hilo abiria na wenye mabasi
hawajachukua hatua yoyote ya kufanya hivyo zaidi ya kuangaliana!.
Moja ya basi lililokuwa limeegeshwa karibu na mlango wa kutokea baada ya awali kutaka kuondoka na kuishia mlaangoni..!
Hali ilivyo muda huu nje ya Mabasi Ubungo!
BONYEZA HAPO CHINI KUANGALIA PICHA ZAIDI
0 comments:
Post a Comment