SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
KUITWA KAZINI
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya
usaili kuanzia tarehe 04 hadi 30 Machi, 2014 kuwa walioorodheshwa
katika tangazo hili wamefaulu usaili na wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri
kama ilivyoonyeshwa katika tangazo hili. Aidha, wanatakiwa kuripoti
katika vituo vyao vipya vya kazi katika muda ambao umeainishwa katika
barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals
Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili
vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.
Barua za kuwapangia vituo vya kazi
zimetumwa kupitia
anuani zao. Aidha, wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo
hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite
kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
Kufungua majina yote BOFYA HAPA