Sunday 30 August 2020

UHURU NA WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI KURIPOTI UCHAGUZI MKUU TANZANIA


Waandishi wa habari wakiendelea na majukumu yao kwenye moja ya mikutano.

Na Kadama Malunde 
Tanzania ni mojawapo ya nchi za bara la Afrika zenye idadi kubwa ya vyombo vya habari.

 Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kuna zaidi ya vituo 190 vya redio zikiwemo vituo vya redio vya mtandaoni,vituo vingi vya runinga, zaidi ya vituo 350 vya runinga za mtandaoni, zaidi ya blogu 100 na magazeti zaidi ya 100 yaliyosajiliwa kuripoti taarifa na habari mbalimbali nchini. 

Nyongeza ya vyombo hivyo, kukua kwa matumizi ya mtandao wa intaneti nchini kumeongeza idadi kubwa ya njia za kupashana habari na taarifa kupitia mitandao ya kijamii. 

Hata hivyo wingi wa vyombo vingi vya habari utakuwa na manufaa tu endapo utahamasisha ushiriki wa wananchi katika kufanya maamuzi na kuchangia mawazo yao kuhusu kujiletea maendeleo.

 Aidha, vyombo vingi vya habari vitakuwa na msaada endapo vitafanya kazi katika mazingira wezeshi yanayochochea mawazo kinzani na ushindani wa hoja mbalimbali pasipo kuathiri ulinzi na usalama wa nchi na ustawi wa raia wake. 

Ripoti za tafiti za miaka ya hivi karibuni zinatoa taswira ya changamoto ya uwepo wa mazingira wezeshi nchini ambazo, kwa namna fulani zinaathiri uhuru wa vyombo vya habari kuhabarisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo uchumi na siasa.

 Kwa mujibu wa ripoti hizo, utungaji na utekelezaji wa sheria mbalimbali za vyombo vya habari na kanuni zake imekuwa mojawapo ya changamoto kubwa inayoathiri wajibu wa vyombo vya habari na wanahabari kuwajibika ipasavyo katika misingi ya kiuweledi. 

Taifa limeingia kwenye Kampeni za uchaguzi mkuu ambapo wananchi watachagua Rais, wabunge na madiwani, bado kuna sintofahamu ya namna vyombo vya habari vitatimiza wajibu wake kikamilifu kwa kutoa habari za uchaguzi kwa usawa linganifu kwa vyama na wagombea wote kama inavyoelekezwa na sheria za uchaguzi. 

Sintofahamu hii inachangiwa na kukosekana kwa maoni kinzani na uchambuzi yakinifu wa taarifa zinazotangazwa na vyombo hivi. Kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari na wanahabari wamekuwa waangalifu katika kuchagua na kuripoti aina fulani za taarifa kwa hofu ya kuingia kwenye mgogoro na mamlaka husika. 

Pamoja na changamoto zilizopo, bado vyombo vya habari na wanahabari wanao wajibu wa kuripoti taarifa mbalimbali za uchaguzi kwa kuzingatia weledi.

 Ni wajibu wa vyombo hivyo kuhakikisha wapiga kura na wananchi wanahabarishwa kikamilifu kwa taarifa zilizofanyiwa uchambuzi wa kina ili kuwawezesha wapiga kura kuchagua kiongozi anayewafaa. 

Vyombo vya habari vitoe habari na taarifa zisizoegemea wala kupendelea chama chochote cha siasa na/au mgombea yoyote. 

Ni matarajio ya kila Mtanzania kuona kwamba vyombo vya habari na wanahabari wakijielekeza zaidi katika kufanya uchambuzi wa sera na ahadi za vyama na wagombea badala ya kusifia au kushambulia wagombea na kuchochea chuki na mifarakano katika jamii.

 Aidha, mamlaka husika zihakikishe uwepo wa mazingira wezeshi na huru yatakayowawezesha wanahabari kutimiza wajibu wao bila hofu, au kuingiliwa na mtu au taasisi yeyote. 

Vyombo vya habari vihamasishe ushiriki wa wananchi katika mchakato wa uchaguzi ikiwemo kupaza sauti zao, na kuhoji utekelezaji wa sera na ahadi zinazotolewa na vyama vinavyoshiriki uchaguzi. 

Mwezi Oktoba mwaka huu Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu ambapo wananchi watashiriki kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wabunge na madiwani. 

Kupitia vyombo vya habari wananchi watapata fursa ya kuwafahamu wagombea na sera za vyama vinavyoshiriki uchaguzi na kuwapima kabla ya kufanya maamuzi kupitia sanduku la kura.
Share:

Maalim Seif achukua fomu ya kuwania Urais Zanzibar

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo  Maalim Seif Sharif Hamad amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar leo August 30, 2020 katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Akitoa fomu hizo na kueleza masharti yanayopaswa kuzingatiwa na wagombea hao, Mwenyekiti wa ZEC Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud amesema wagombea hao wanatakiwa  kusaka wadhamini na kurejesha fomu hizo baadaye kwa uhakiki.



Share:

TUNDU LISSU KUTUA SHINYANGA MJINI JUMATANO KUZINDUA RASMI KAMPENI ZA UCHAGUZI CHADEMA KANDA YA SERENGETI

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami (kulia).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti kimetangaza kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia CHADEMA Mhe.Tundu Anthipas Lissu pamoja na Mgombea Mwenza,ndugu Salum Mwalimu watazindua rasmi Kampeni za CHADEMA Uchaguzi Mkuu 2020. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari leo Jumapili Agosti 30,2020 Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi amesema Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA utafanyika siku ya Jumatano Septemba 2,2020 katika viwanja vya Joshoni Lubaga Mjini Shinyanga kuanzia saa nane mchana. 

“Ndugu Watanzania, watu wa Kanda ya Serengeti inayojumuisha Mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu napenda kuwajulisha kuwa Mgombea Urais Mhe.Tundu Anthipas Lissu pamoja Mgombea Mwenza,ndugu Salum Mwalimu watafika kwenye mkoa wa Shinyanga Septemba 2,2020 kuja kufanya uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu katika Kanda ya Serengeti”,amesema Ntobi. 

Kwa upande wake, Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami amesema ufunguzi wa kampeni za CHADEMA kwa Kanda ya Serengeti utawakaribisha wananchi na wanachama wa CHADEMA kutoka kwenye mikoa mitatu inayounda Kanda ya Serengeti ambayo ni Shinyanga, Simiyu na Mara ambapo pia tutakuwa na mapokezi maalumu ya mgombea Urais ambaye atatua katika uwanja wa Ndege Kahama kisha kuelekea Shinyanga Mjini.

“Tunawaomba wananchi kutoka vyama vyote wahudhurie kwa wingi kuja kumsikiliza Mgombea wetu wa Urais ana nini cha kuwafanyia baada miaka 58 ya utawala wa CCM ambapo wananchi pia watatumia fursa hiyo kuwasikiliza wagombea kupitia CHADEMA”,amesema Mnyawami. 

Katika hatua nyingine Mnyawami amesema CHADEMA imekata rufaa kwenye kata na majimbo ambako wagombea wake hawajateuliwa kugombea ubunge na udiwani.

Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu leo Jumapili Agosti 30,2020 katika Ofisi za CHADEMA Kanda ya Serengeti Mjini Shinyanga. Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi. 
Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu leo Jumapili Agosti 30,2020.
 Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari leo Jumapili Agosti 30,2020 kuhusu Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu CHADEMA Kanda ya Serengeti ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia CHADEMA Mhe.Tundu Anthipas Lissu pamoja na Mgombea Mwenza,ndugu Salum Mwalimuza watakuwa katika Jimbo la Shinyanga Mjini siku ya Jumatano Septemba 2,2020 katika viwanja vya Joshoni Lubaga Mjini Shinyanga kuanzia saa nane mchana. 


Share:

KANGOYE ATAKA WENYEVITI WA MITAA, MABALOZI NA VIJANA KUENDELEZA MSHIKAMANO WAGOMBEA CCM WASHINDE KWA KISHINDO


Picha ya Jackson Kangoye akiongea na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM nyumbani kwake


Na Mwandishi wetu - Tarime

Wenyeviti wa mitaa, mabalozi vijana pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi jimbo la Tarime mjini wameaswa kuendeleza ushirikiano na kuvunja makundi ili mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki aweze kushinda kwa lengo la  kuleta maendeleo.

 Kauli hiyo imetolewa na Jackson Kangoye ambaye alishinda kwenye kura za maoni Jimbo la Tarime mjini katika hafla fupi aliyoandaa kwa ajili ya kutoa shukrani zake kwa wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi.

Jackson alisema kuwa ameamua kuandaa hafla hiyo ya pamoja kwa ajili ya kushukuru wajumbe wa Halmashauri kuu kwa kumchagua kwa kura nyingi licha ya jina lake kutorudi lakini bado ataendelea kupigania Chama Cha Mapinduzi mpaka kinashika dola katika majimbo yote mawili ya Tarime mjini na vijijini.

“Najua hapa kuna wenyeviti wa mitaa hawapigi kura katika mkutano wa Halmashauri kuu lakini walishawishi wajumbe kwamba tunaomba mkapigie flani kuna vijana, wanachama wote nimeamua kuwaita kujumuika na nyie kuwambia mimi niko pamoja na mgombea aliyeteuliwa na chama naheshimu maamuzi ya cha kuanzia ngazi za kata, Wilaya, Mkoa hadi Taifa”,alisema Jackson.

Pia Jackson aliongeza kuwa hayupo tayari kuhamia chama chochote kwa sababu amelelewa ndani ya Chama Cha Mapinduzi kwani amekuwa akipokea simu mbalimbali kutoka vyama tofauti wakimshawishi kugombea kupitia vyama hivyo.

“Nimepigiwa simu sana kwenda vyama vingine lakini nimeheshimu wanachama wa jimbo la Tarime mjini kwa kuwa walinihamini hivyo siwezi kuangusha wazee wangu nimelelewa na chama hiki sitaweza kuwa msaliti”,alisema Jackson.

Aidha Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiwemo wazee maarufu wamedai kuwa Ushirikiano Umoja na Upendo utachangia kwa kiasi kikubwa Ushindi.

Pia Wanachama hao wamempongeza Jackson kwa kitendo cha kuwaita wanachama wote ili kushiriki chakula cha pamoja jambo ambalo limewashangaza na kuzidi kusema kuwa kijana huyo ni mkomavu wa siasa kwani baadhi ya wagombea wamekuwa wakishindwa kurejea baada ya kutoteuliwa na chama.

Chama cha Mapinduzi Jimbo la Tarime Mjini wanatarajia kufungua rasmi kampeni za mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki hii leo  Agosti 30 katika viwanja vya soko la zamani mjini Tarime ambapo Kangoye amehaidi kushiriki kikamilifu kumtafutia kura mgombea huyo.
Share:

INTERNSHIP Opportunities at Envision Africa – Tanzania, TEACHERs

Teacher – Internship  Job Description Envision Africa is a social enterprise dealing with innovative and effective ways in empowering youths to learn, thrive and succeed in personal and professional life.Envision Africa provides necessary tools, resources and opportunities for students and mid careers professionals to identify and communicate career interests and transferable skills for personal and […]

The post INTERNSHIP Opportunities at Envision Africa – Tanzania, TEACHERs appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Accountant at Afroil Investment Limited

Overview We, Afroil Investment Limited an oil marketing company based in Dar Es Salaam, Tanzania fully licensed and incorporated on 23rd October 2008 is currently looking for dynamic result oriented individual to fill the following position ( Women are highly preferred).  Job Title: Accountant Reports to: Finance Manager Department: Finance. JOB PURPOSE  To facilitate accurate and timely entry […]

The post Accountant at Afroil Investment Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AGOSTI 30,2020











  
Share:

NYOTA WA FILAMU YA BLACK PANTHER CHADWICK BOSEMAN AFARIKI DUNIA

Mwigizaji nyota wa Marekani Chadwick Boseman enzi za uhai wake
Boseman hakuwahi kusema hadharani kuhusu maradhi yake

Mwigizaji nyota wa Marekani Chadwick Boseman, aliyefahamika sana kwa filamu ya Black Panther amefariki dunia kwa ugonjwa saratani akiwa na umri wa miaka 43.

Boseman amekufa nyumbani huko Los Angeles akiwa na mke wake na familia, kulingana na taarifa iliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii.


Boseman alipatikana na saratani ya utumbo mpana miaka minne iliyopita lakini hakuwahi kusema hilo hadharani.

Taarifa za kifo chake zimeacha mashabiki wake kote ulimwenguni na mshutuko mkubwa.

Mwongozaji wa filamu ya 'Get Out' Jordan Peele, amesema kwamba hilo "ni pigo kubwa".

"Mpiganaji haswa, Chadwick alivumilia yote na kuwaletea filamu nyingi tu ambazo mumetokea kuzipenda," familia yake imesema kwenye taarifa.


"Kuanzia filamu ya Marshall to Da 5 Bloods, Ma Rainey's Black Bottom ilioandikwa na August Wilson na nyingine nyingi - filamu zote hizo zilitengenezwa wakati anapitia upasuaji na kupokea matibabu ya kemikali yaani kemotherapi. Ilikuwa fahari katika taaluma yake kushiriki kwenye filamu ya Black Panther."

Boseman alikuwa maarufu katika filamu ya michezo ya '42' ya mwaka 2013 kuhusu ubaguzi aliofanyiwa mchezaji wa kulipwa wa besiboli Jackie Robinson na ile ya 'Get on Up' mwaka 2014 kuhusu maisha ya mwimbaji wa nyimbo aina ya soul James Brown.

Hata hivyo, kama mhusika wa filamu ya Black Panther ndio atakayokumbukwa nayo zaidi.

Nyota huyo, Boseman, aliigiza kama mtawala wa Wakanda, filamu iliyoangazia Afrika ya kufikirika yenye teknolojia zilizoendelea sana za kisasa.

Pamoja na sifa alizopokea na kupata zaidi ya dola bilioni 1.3 za Marekani kupitia sinema kote ulimwengini, filamu hiyo ilichukuliwa sana kama hatua iliyopigwa kitamaduni kwa misingi ya filamu inayofanya vizuri mno ambayo waigizaji na mwelekezi, Ryan Coogler, wote ni watu weusi.

Mwaka jana, Boseman alisema filamu hiyo imebadilisha mtazamo wa kuwa "kijana, mwenye kipaji na mweusi".

Uzinduzi wa Filamu ya Black Panther, Kisumu Kenya

Black Panther ilikuwa filamu ya kwanza yenye maudhui ya ushujaa kuchaguliwa kama yenye picha bora katika tuzo la Oscar.

Pia aliigiza kama mhusika wa aina hiyo hiyo katika filamu nyingine nyingi mfano: Civil War, Avengers: Infinity War na Avengers: Endgame.

Filamu ya 'A sequel' ilikuwa inaendelea kufanyiwa kazi na ilitarajiwa kutoka mwaka 2022 huku Boseman akitarajiwa kurejea tena.


Taarifa za kifo chake zimeshutua wengi wakati ambapo hajawahi kuzungumzia ugonjwa wake hadharani.

Hata hivyo mashabiki walikuwa na wasiwasi kuhusu afya yake mwaka mmoja uliopita kwasababu ya kupunguza uzito kupita kiasi.

Tayari watu wameanza kutuma risala za rambirambi akiwemo mwigizaji na nyota mwenzake katika filamu ya Marvel Mark Ruffalo.

Mwigizaji Dwayne Johnson ameandika kwenye mtandao wa Twitter: "Asante kwa kungara kwenye na tasnia yako na kushirikisha dunia kipaji chako. Upendo wangu na maombi ni kwa familia yako."

Wanasiasa pia wameanza kutuma risala zao ikiwemo aliyeteuliwa kuwa makamu rais wa mgombea urais wa chama cha Democratic Kamala Harris.


Mwaka 2018, Boseman alirejea kwenye chuo kikuu alichosomea na kuzungumza katika sherehe ya kuhitimu kwa mahafali.

"Wengi wenu hapa wanapitia wakati mgumu dhidi ya chuo chenyewe," alisema hivyo katika hadhara ambayo wengi wao walikuwa ni kutoka kundi la walio wachache.

"Wengi mutamaliza Howard na kujiunga na mifumo na taasisi ambazo zina historia ya ubaguzi wa rangi na kutengwa.

"Lakini ukweli wa kwamba mumepambana katika chuo hiki ambacho munakipenda ni ishara tosha kuwa munaweza kutumia elimu yenu kuboresha dunia mutakayojiunga nayo."

CHANZO BBC SWAHILI
Share:

DC TANO MWERA: "SERIKALI IMEPIGA HATUA KWENYE HUDUMA ZA AFYA BUSEGA"

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera

Na Mwandishi wetu - Busega

MKUU wa Wilaya ya Busega, Bi. Tano Mwera amewataka Wananchi wa Busega kutembea kifua mbele na kuendelea kuiamini Serikali yao iliyo madarakani kwani imeweza kufanya maendeleo mbalimbali na makubwa kwenye Wilaya hiyo.

Amesema hayo wakati wa kutoa ripoti maalumu ya miradi iliyotekelezwa na Serikali kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020 ndani ya Wilaya ya Busega iliyopo Mkoa wa Simiyu
ambapo Bi. Tano Mwera aliwashukuru viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine wakiwemo Makamo wa Rais, Mhe. Samia Luhuu Hassani  na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kwa uimala wao na nchi kupiga hatua.

"Viongozi wetu wameweza kuwa chachu ya kukuwa  Kitaifa na  Kimataifa kiuchumi, ulinzi na usalama, masuala ya kodi na huduma mbalimbali na tumekuwa wa mfano Afrika  na sasa tunajifunia kuwa Taifa lenye uchumi wa kati.

Chachu yao imetufanya sisi wasaidizi huku chini kusimamia vyema maagizo na miradi mbalimbali kiutekelezaji kwa mafanikio makubwa ikiwemo ya huduma za jamii, miundombinu, elimu, afya, ulinzi na usalama na mikakati ya kiuchumi kwa Wananchi na nchi kwa ujumla".Alisema.

Katika suala la Afya, Bi. Tano Mwera amesema Serikali imetoa kiasi cha Tsh. Bilioni 1.5, kwa ajili ya ujenzi wa majengo saba (7) Hospitali ya Wilaya hiyo na majengo yote yamekamilika.

"Tsh. 1.5 Bilioni fedha za Serikali imeweza kusaidia majengo muhim ya hospitali na kwa sasa yanatumika. 

Pia Serikali iliongeza kiasi cha Tsh. Milioni 300 kwa ajiri ya kukamilisha ujenzi wa jengo la wazazi (Theatre and Lanour Ward) pamoja na njia za wagonjwa  ambapo ujenzi unaendelea hivyo jumla ya fedha yote kufikia Bilioni 1.8 " Alisema.

Bi. Tano Mwera ameongeza kuwa, Upanuzi wa Vituo vya Afya vya Nassa na Igalukilo vimeweza kugharimu Tsh. 850,000,000 ambapo sasa vituo hivyo vinafanya huduma ya upasuaji kwa wananchi.

Aidha, amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendelea katika sekta ya Afya imeweza kuboresha miundombinu kwenye vituo vya afya na zahanati kwa gharama ya Tshs 606.5 Millioni.

"Serikali kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo, tumeweza kufanyia maboresho katika Zahanati za Nyamikoma, Mwasamba, Mwanhale, Ijiha, Nyaluhande, Mwamagigisi, Badugu, Ngasamo, Kalemela na vituo vya afya vya Kiloleli na Lukungu." Alisema.

Akizungumzia hali ya upatikanaji wa Dawa, Ambapo umeongezeka kwa sasa  na kufikia asilimia 95.8 2019.

Pia alisema Vifo vya kina mama wajawazito na Watoto chini ya miaka mitano vimepungua huku idadi ya kina mama waliojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya imeongezeka.

"Kwa sasa Busega huduma bora za afya zilizosimamiwa imara na serikali ya awamu ya tano zimekuwa chachu kwa Wananchi. Vifo vya uzazi vimepungua na hata idadi ya akina mama wanaenda jifungulia vituo vya afya ikiongezeka maradufu.

Haya yote ni matunda ya awamu hii ya tano lakini pia hii imefanya wananchi kupata huduma bora na hata idadi ya wananchi waliojuinga CHF iliyoboreshwa kuongezeka na imefikia 3684" aliongeza Bi. Tano Mwera.
Share:

ALAT YAZITAKA HALMASHAURI KUHESHIMU FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ALAT), Elirehema Kaaya akizungumza  katika ziara hiyo


Na Mwandishi wetu
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za  Mitaa (ALAT) Elirehema Kaaya  amezitaka halmashauri nchini  kuhakikisha  fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo zinatumika kikamilifu ikiwa ni pamona na kubana mianya yote ya ubadhirifu inayoweza kujitokeza.

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kutembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa katika halmashauri mbalimbali nchini ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuona Tanzania nzima inakuwa yenye maendeleo.

Akizungumza mara baada ya  kutembelea miradi shule, zahanati pamoja na vituo vya afya vilivyopo katika manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ,alisema ni vyema halmashauri zinazotekeleza miradi mbalimbali chini, kuhakikisha zinazingatia suala la matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa hatua ambayo mbali na mambo mengine itawezesha miradi mingine kuendelea kujengwa.

"Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kwa sasa ipo kazini kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inakuwa yenye tija, ili kufanikisha hilo inatakiwa kuwe na nidhamu nzuri katika matumizi ya fedha za ujenzi wa miradi ili malengo yote yaliyokusudiwa yaweze  kufikiwa" alisema Kaaya.

Alisema halmashauri hizo hususani zilizopo katika miji, zina kila sababu ya kuhakikisha zinafanya matumizi bora ya adhi kwa kujenga majengo hayo ya ghorofa kwa kuwa kutazifanya halmashauri hizo kuwa na majengo bora na mengi katika eneo dogo.

Katibu Mkuu huyo wa ALAT pia alisema  halmashauri zote zinazotekeleza ujenzi wa miradi yake kwa kuzingatia utaratibu huo wa matumizi bora ya ardhi sambamba na thamani ya fedha katika miradi yake mbalimbali, zinaunga kwa vitendo harakati za Rais John Magufuli kulieletea Taifa maendeleo.

Aliipongeza Manispaa ya Ilala kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa shule uliozingatia matumizi bora ya ardhi sambamba na fedha  iliyoendana na miradi hiyo jambo lililoiwezesha kupata hati safi.

"Huu ni mfano mzuri wa matumizi ya fedha hizi za Serikali, lakini pamoja na hili imekuwa moja ya manispa bora nchini ambazo zimekuwa zikipata hati safi, hili ni jambo linaloonyesha kuwa ina nidhamu nzuri katika matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya miradi hiyo" alisema Kaaya.

Alizitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha inatumia mashine za kielektroniki (POS) katika utoaji huduma ili kurahisisha kazi ya ukusanyaji wa mapato mbalimbali ya Serikali.
Share:

WATEJA WA TIGO KUNUNUA TIKETI ZA ZANFAST FERRIESS KWA TIGO PESA

Share:

Saturday 29 August 2020

Serikali yaahidi milioni 200 kujenga madarasa DIT Myunga

Na Mwandishi Wetu, Momba (Songwe)
SERIKALI kupitia Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo imeahidi kutoa sh milioni 200 kwaajili ya ujenzi wa madarasa matano katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Kampasi ya Myunga ikiyoko Wilaya ya mkoani Songwe.

Ahadi hiyo ilitolewa jana na Dk Akwilapo alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa bwalo la chakula lililojengwa kwa fedha zilizotolewa na serikali kupitia wizara hiyo.

"Nilikua naongea na mkuu wa Taasisi hapa kwamba nikiwapa milioni 200 so mtajenga madarasa matano ili Hawa wanafunzi wasirundikane kwenye darasa moja," alisema Dk Akwilapo.

Ahadi hiyo ilikuja kufuatia ombi la wanafunzi la kuomba serikali kuboresha niundombinu ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na madarasa, uwanja wa michezo na vifaa vya michezo pamoja na gari la kwaajili ya kwenda kwenye mafunzo viwandani.

Dk Akwilapo alisema anaamini kwa fedha hizo DIT itajenga madarasa mazuri yenye ubora unaofaa kwa kutumia wataalamu wa ndani wa Taasisi hiyo.

Aidha katika tukio hilo, Dk Akwilapo aliahidi pia kumlipia ada mwanafunzi wa pili TEHAMA, Nozen Mkubwa ambaye alikuwa na changamoto ya ulipaji ada Jambo ambalo lilikuwa likimkwamisha katika masomo yake.

Akizungumzia ujenzi wa bwalo hilo, aliipongeza Taasisi hiyo kwa usimamizi mzuri wa rasilimali fedha uliofanikisha kukamilika ujenzi huo kwa asilimia 100.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Profesa Preksedis Ndomba alishukuru serikali na Katibu Mkuu huyo kwa msaada ambao umekuwa ukitolewa na serikali kupitia wizara hiyo na kuahidi kuendelea kusimamia vema miradi inawekezwa na serikali katika Taasisi.

Mkurugenzi wa Kampasi ya DIT Myunga, Dk Frank Lujaji alishukuru kwa msaada wa kijana Nozen kulipiwa ada ambapo alitoa wito pia kwa Taasisi nyingine kusaidia vijana wenye changamoto za kupata ada kwani wengi Wana uwezo wa kimasomo pamoja na nia ya kusoma.


Share:

TIC yasema Milango ipo wazi kwa Wawekezaji Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Mtwara.
Katika kuhakikisha azma ya Serikali ya kuendeleza na kukuza uchumi wa Viwanda, Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC kimesema ipo haja kwa Wawekezaji kukitumia kituo hicho katika kufanikisha shughuli zao ambazo ndio chachu ya ukuaji wa uchumi huo.

Kituo hicho ambacho kinaratibu, kuhamasisha na kusimamia Uwekezaji nchini sasa kinafanya jitihada za kuwatembelea Wawekezaji kwenye maeneo ya uwekezaji wao ili kukagua na kutatua changamoto zinazowakabili.

Mkurugenzi wa Kituo hicho Dkt Maduhu Kazi aliwatembelea Wawekezaji Mkoani Mtwara ambapo akiwa katika Kiwanda cha Saruji cha Dangote,alisema lengo ni kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana na Wawekezaji pamoja na Wadau wa Sekta mbalimbali za Serikali na Binafsi zinazohusika na uwekezaji katika kufanikisha shughuli hizo nchini.

“Nawapongeza sana Wawekezaji wa Kiwanda hiki cha Dangote, mnafanya kazi nzuri katika uwekezaji wenu, sisi TIC tupo kwa ajili yenu, kitumieni kituo hiki kwa maendeleo ya Uwekezaji katika nchi yetu na sisi tupo tayari kuwahudumia wawekezaji wote ili kukidhi matarajio ya nchi katika ukuaji wa uchumi” alisema Dkt Kazi.

Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Bw. Aboyomi Awofodu amesema kwa sasa kiwanda hicho kinafunga mitambo ya kisasa itakayowezesha kutumia umeme wa gesi, makaa ya mawe na maji ili kuwa na umeme wa uhakika wakati wote.

Kiwanda cha Saruji cha Dangote chenye eneo la ekari 1,700 kilichopo katika eneo la Msijute katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ni moja ya Uwekezaji Mkubwa Nchini Tanzania, Kiwanda hiki ni kikubwa katika eneo la Kusini mwa  Jangwa la Sahara na kina uwezo wa kuzalisha tani za saruji milioni tatu kwa mwaka.

Kiwanda hiki kilianza kazi Desemba 2015 na hadi sasa kiwanda hicho kinazalisha saruji ya kiwango cha daraja la 32.5 na 42.5 ambayo inatumika nchini na nyingine kusafirishwa nje ya nchi, hivi karibuni Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani alizindua mradi wa kwanza wa kuunganisha miundombinu ua gesi asilia katika kiwanda hicho kwa ajili ya kuzalisha umeme wa megawati 45, Mmiliki wa kiwanda hicho ni Raia wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote.

Mwisho.


Share:

KISHINDO DODOMA DK.MAGUFULI ATAJA ATAYAKAYOANZA NAYO

*Ni iwapo watapata ridhaa CCM kuongoza tena kwa miaka mitano ijayo
 *Kununua ndege nyingine mpya tano kuimarisha usafiri wa anga nchini



Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimezindua rasmi kampeni zake katika uchaguzi mkuu mwaka huu huku mgombea wake wa urais Dk.John Magufuli akitumia nafasi hiyo kuelezea mambo kadhaa yenye tija kwa Taifa hili iwapo watapata ridhaa tena ya kipindi cha miaka mitano ijayo.

Dk.Magufuli ambaye ametumia nafasi huyo kuzungumzia Ilani ya Uchaguzi Mkuu yaCCM ya mwaka 2020-2025 amewaomba Watanzania wa vyama vyote, dini zote na makabilia yote kuhakikisha wanakipa ushindi Chama chake ili kuendeleza yale ambayo wameyaanza katika miaka mitano ya kwanza.

Katika ufunguzi huo wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Jiji hilo na mikoa jirani ,Dk.Magufuli ametoa hotuba iliyojitosheleza kwa kuelezea hatua kwa hatua mambo ambayo Serikali yake imefanya na yale wanayotarajia kuyafanya iwapo watapewa ridhaa ya kushika dola.

Mgombea huyo wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema katika miaka mitano ya kwanza wamefanya mambo makubwa yakiwemo ya kurudisha nidhamu katika utumishi wa umma.

Pia kukomesha rushwa, kudhibiti rasilimali za nchi ili ziwanufaishe Watanzania pamoja na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo sekta ya afya,elimu, maji, barabara, usafiri wa anga na sekta nyingine muhimu.

“Katika miaka mitano ya kwanza ya uongozi wetu tumejitahidi kwa kadri ya uwezo wetu na sasa tunakuja kwenu tena watanzania kuomba ridhaa yenu mtupe tena miaka mitano mingine.

“Ili tuendelee na kazi ya kuwatumikia maana hatuna hakika kama mkiwapa wengine wataweza kuifanya kazi hii nzuri ambayo tumeianza na tunataka kuimalizia,”amesema Dk.Magufuli

Hata hivyo ameeleza alivyofurahishwa na na wananchi wa Dodoma kwa kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo wa kampeni, hivyo amewaahidi atakapochaguliwa kazi ya kwanza akiwa madarakani itakuwa ni kuendelea kulijenga Jiji la Dodoma.

“Wananchi wa Jiji la Dodoma ambako ndiko makao makuu ya Serikali niwahakikishie tutaendelea kuijenga Dodoma, tutajenga uwanja mkubwa wa michezo ambao utawezesha wananchi wengi kuingia na kutosha tofauti na uliopo sasa,”amesema.

Pia amesema katika Jiji la Dodoma utajengwa uwanja mkubwa wa ndege wa kilometa tatu na hivyo ndege zote kubwa zitatokea Dodoma kwenda  nchi za Ulaya kwani fedha zipo na Tanzania ni tajiri.

Hata hivyo amesema mwaka2015 Watanzania walitaka mabadiliko na hivyo baada ya kuingia madarakani walianza kufanya mabadiliko makubwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya kusimamia uwajibikaji , kudhibiti mianya ya upotevu wa makusanyo ya fedha yatokanayo na kodi.

Ameongeza katika mabadiliko hayo Serikali anayoingoza ilisimama imara kuhakikisha sekta za ajira zinaimarishwa ili kuotoa ajira kwa Watanzania.” Tutahakikisha zinapatikana ajira milioni 8 ili kukuza uchumi kupitia ajira hizo.”

Pamoja na kuwepo kwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo ambayo watafanya baada ya kuchaguliwa kwa mara nyingine tena, Dk.Magufuli amesema wataendelea kuimarisha usafiri wa anga kwa kununua ndege nyingine mpya tano.

Kati ya ndege hizo mbili zitakuwa za masafa marefu,mbili za masafa ya kati na ndege moja itakuwa ya mizigo.Kwa sasa tayari kuna ndege mpya nane na hivyo itafanya kuwa na jumla ya ndege 11.



Share:

DK.JOHN MAGUFULI AAHIDI KUENDELEA KUIMARISHA SEKTA YA NISHATI YA UMEME

Na Said Mwishehe,Michuzi Tv-Dodoma

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28,2020 Dk.John Magufuli amesema katika miaka mitano ijayo iwapo Chama Cha Mapinduzi(CCM) kitapata ridhaa ya kushika dola wataendelea kuimarisha sekta ya nishati.

Akizungumza leo Agosti 28, mwaka2020 katika Uwanja wa Jamhuri wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM ,Dk.Magufuli amesema wataingiza megawati 5000 za nishati ya umeme katika gridi ya Taifa ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha kunakuwa na umeme wa uhakika.

Dk.Magufuli amesema kumekuwepo na mkakati kabambe wa kuimarisha sekta ya nishati ya umeme na licha ya uwepo wa miradi mikubwa ya umeme iliyotekelezwa, kazi inayoendelea sasa ni ujenzi wa bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere.

Kwa upande wa sekta ya afya,Dk.Magufuli amesema kwa kipindi cha miaka mitano wamefanikiwa kujenga zahanati 1,198, Hospitali za Wilaya tisa, vituo vya afya 487, Hospitali za Mikoa 10, Hospitali za Rufaa katika kanda tatu huku pia watumishi wa sekta hiyo 14,479 wakiongezwa.

Amefafanua kwamba bajeti ya imeongezeka kutoka Sh.bilioni 31 hadi Sh.bilioni 270 na tumenunua magari mapya ya wagonjwa 117.Pia amesema wamepunguza safari za rufaa nje ya nchi kwa wagonjwa wa moyo, figo, ubongo na saratani.

“Katika kuimarisha sekta ya afya nchini tuliamua kusomesha madaktari bingwa katika fani mbalimbali ndani na nje ya nchi.Hivyo tunayo sababu ya kuomba miaka mitano mingine ili tuendelee na kazi ambayo tulianza miaka mitano iliyopita,” amesisitiza.

Kuhusu sekta ya madini, Dk.Magufuli amefafanua usimamizi mzuri uliopo umeiwezesha  sekta hiyo kukua kwa asilimia 17.7.”Mapato yatokanayo na madini yameongezeka kwa kiwango kikubwa kwani hapo awali yalikuwa Sh.bilioni 168 katika mwaka 2014 hadi mwaka 2015 na sasa yamefikia Sh.bilioni 528.

“Tumeendelea kuboresha sheria kwani sheria mpya ya madini inaeleza kwa kila mgodi ambao utaanzishwa nchini kwetu serikali itakuwa na hisa ya 16,”amesema Dk.Magufuli na kufafanua kutokana na usimamizi mzuri Watanzania wamekuwa wakinufaika na madini yaliyoko katika nchi yao.

Ametumia nafasi hiyo kuzungumzia sekta ya elimu ambapo amegusia elimu bure ambayo inatolewa na Serikali na kufafanua kuwa Sh. Trilioni 1.09 zimetumika kusomesha watoto.

 Pia amesema katika kipindi cha miaka wamejenga shule mpya za msingi 905,  sekondari 228,wamekarabati shule kongwe 73, mabweni 253 na wameongeza madawati na  walimu sambamba na kuangalia maslahi yao.

Ametumia nafasi hiyo kuwaambia Watanzania kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu, wagombea wengi watapita kwa wananchi kunadi sera zao , kikubwa ni kuwasikilisa na kisha kufanya uamuzi sahihi Oktoba 28 mwaka huu ambayo ndio siku ya kupiga kura.

“Niwaombe tu wasikilizeni wagombea wote wataokuja kwenu na baada ya hapo mfanye uamuzi sahihi kwa kuchagua viongozi ambao wataleta maendeleo ya nchi yetu.CCM tunayo sababu ya kupewa dhamana ya kuongoza nchi kwasababu nia yetu ni kuendelea kuleta maendeleo.”


Share:

DK.HUSSEIN MWINYI AAHIDI KUENDELEZA PALE ALIPOISHIA RAIS MOHAMED SHEIN ZANZIBAR


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MGOMBEA Urais wa Serikali ya Mapinduzi Sanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Dk.Hussein Mwinyi amesema akichaguliwa kuwa Rais wa Serikali hiyo atahakikisha anafanya kazi kwa kasi kubwa  ya kuendeleza pale ambapo ameishia Dk.Mohamed Ali Shein.

Dk.Hussein Mwinyi ameyasema hayo leo Agosti 29 ,2020 wakati akitoa salamu za wananchi wa Zanzibar katika uzinduzi wa kampeni za mgombea Urais wa Chama hicho Dk.John Magufuli ambapo amesema hakika Dk.Shein amefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo,hivyo akipata nafasi ataendeleza kuanzia pale ambapo Rais Shein ameishia.

"Zanzibar wanasema wako tayari kuwachagua viongozi wa ngazi zote katika uchaguzi mkuu mwaka huu kuanzia Rais , Wabunge, Wawakilishi,Madiwani na Viti maalum.Ilani ya CCM imetekelezwa vizuri kwa pande zote na inatoa nafasi CCM kushinda.

"Nitafanya kazi ya kuendeleza pale alipoishia Rais Dk.Shein ambaye amefanya mambo nengi na nitafanya kazi kwa kubwa sana,"amesema Dk.Hussein Mwinyi na kusisitiza kwamba atasimama imara kuleta maendeleo.

Hata hivyo amesema kwamba hakuna sababu ya kubweteka na badala yake wanachama wa CCM na mashabiki wa Chama hicho kufanya kampeni ya nguvu na hatimaye kushinda kwa kishindo na ni matumaini yake ushindi utakuwa mkubwa kuliko wakati wowote.

Wakati huo huo Dk.Hussein Mwinyi ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kujiepusha na vurugu ambazo zinaweza kusababisha uvunjifu wa amani huku akifafanua tayari kuna baadhi ya watu wameanza kutoa kauli ambazo zinaonekana kuhatarisha amani ya nchi.

*Hivyo niwaombe wananchi wote tujiepushe na  vurugu.Kuna wanasiasa wameanza kutoa kauli ambazo zinaashiria uvunjifu wa amani, tujiepushe na watu hao wasikuwa na nia njema na Taifa letu,"amesema Dk.Hussein Mwinyi.

Awali wakati anazungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi huo wa kampeni za mgombea urais wa CCM, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Mohamed Ali Shein amesema kabla ya kutambulisha Dk.Hussein Mwinyi amesema Watanzania tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwani nchi yetu imepiga hatua ya maendeleo.

"Ndugu wananchi leo tunazindua kampeni yetu na mimi nimetakiwa kumtambulisha mgombea urais Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi ambaye jina lake ni maarufu.Ni mzalendo mkubwa kwa nchi yake,ni daktari bingwa na tunaamini ataendelea kuimarisha Muungano, Umoja na mshikamano,"amesema Dk.Shein wakati anamuelezea Mgombea huyo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


Share:

UWANJA WA JAMHURI DODOM KUMEANZA KUNOGA MAPEMA...CCM WANA JAMBO LAO


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KUMEANZA  kunoga mapema Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma!Ndivyo unavyoweza kuelezea jinsi ambavyo idadi kubwa ya wananchi wakiwemo wana CCM ambavyo wamejitokeza uwanjani hapo kushuhudia uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi Dk.John Magufuli.

Ratiba inaonyesha wananchi walianza kuingia uwanjani saa 12 asubuh. Lakini hadi saa tatu uwanja ulishaanza kufurika kuanzia majukwaa yote na katikati ya uwanja vikundi mbalimbali vilionekana wakipiga jaramba huku wengine wakiendelea kuingia uwanjani hapo.

Hali  hiyo pengine haikufikiriwa kwa kuwa wasanii walipoanza kutumbuiza saa mbili asubuh tayari mashabiki wao(wananchi)walikuwa tayari kuwashangilia kinyume na matarajio pengine uwanja ungefurika nyakati za mchana.

Aidha, ni dhahiri wanaCCM pamoja na wananchi wengine wasio makada wa chama hicho hawakutaka kuwa sehemu ya wale watakaohadithiwa au kuangalia kwenye runinga na mitandao ya kijamii kile kitakachotokea Uwanja wa Jamahuri.

Michuzi TV na Michuzi Blog imeshuhudia msusuru wa umati mkubwa wa wananchi ukiendelea kuingia uwanjani hapo huku wale ambao wameshafika uwanjani wakiendelea kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya,wanamuziki wa dansi, waigizaji na kila aina ya wasanii kuhakikisha kila aina ya burudani inapatikana.

Hata hivyo wakati wananchi hao wa Jiji la Dodoma pamoja na Wana CCM hao wakiendelea kupata buradani za nguvu ambazo kwa lugha ya mjini wanaita burudani Konki wapo wananchi wengine ambao wameonekana kuwa makini wakisoma majarida,vipeperushi pamoja na gazeti la Uhuru ambalo ni gazeti la Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambayo yanaelezea maendeleo na mafanikio makubwa ambayo Serikali ya Awanu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli imeyapata katika miaka mitano ya kwanza.

Aidha, uelewa mpana wa wananchi kuhusu  mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli kipenzi cha Watanzani imekuwa karata ya turufu kwa CCM wakati wakianza kampei zao leo jijini Dodoma ambako pia ndio makao makuu ya nchi na chama hicho.

Ukweli kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Serikali itamsaidia kwa kiasi kikubwa mgombea wa CCM kunadi Ilani ya Chama chao kwa urahisi na kuongeza mawili matatu bila ya kutumia nguvu nyingi kuongeza ahadi.





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger