Friday 7 August 2020

PICHA: Mgombea Urais wa Chama cha ACT -Wazalendo, Benard Membe Achukua Fomu Ya Urais NEC

Mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo Bernard Membe amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Agosti 07, 2020 katika Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi (NEC) Dodoma.

Membe amesindikizwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad na Katibu Mkuu,  Ado Shaibu


 


Share:

PICHA: Mgombea Urais kwa tiketi ya Allance for democratic change ADC Queen sendiga Achukua Fomu ya Urais NEC

Mgombea Urais kwa tiketi ya Allance for democratic change ADC Queen sendiga akiwa na mgombea mwenza Shoka Juma akionyesha fomu baada ya kuchukua katika ofisi za tume ya uchaguzi NEC iliyopo Njedengwa jijini Dodoma



Share:

Vyama viwili vya upinzani nchini Uganda Vyagombania Rangi Nyekundu

Vyama viwili vya upinzani nchini Uganda vimeingia katika mzozo juu ya haki ya kutumia rangi nyekundu huku kila chama kikidai kuwa kina haki ya kuitumia rangi hiyo kama utambulisho wake.

Chama kikongwe cha UPC kinadai kuwa chama kipya cha NUP kinachoongozwa na msanii maarufu kama Bobi Wine kilikosea kuanza kutumia rangi ambayo imekuwa yao kwa miaka mingi.

Lakini NUP imekanusha madai hayo ikisema imetumia rangi hiyo ikiwa vuguvugu la 'People Power' na hakuna aliyejitokeza kupinga hadi pale waliposajiliwa kama chama.

Rais wa chama cha UPC Jime Akena ambaye ni mtoto wa mwasisi wa chama hicho Milton Obote anasema rangi nyekundu ni ya UPC tangu miaka 60.

Hata hivyo, Tume ya uchaguzi ndiyo itatoa maamuzi ya mwisho kati ya vyama hivyo viwili ni kipi kina haki ya kutumia rangi nyekundu katika nembo yao kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2021.


Share:

Aliyeua mtoto wake kwa kumtenganisha na panga ahukumiwa kunyongwa hadi Kufa

Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba imemuhukumu kunyongwa hadi kufa  Melchedes Burchard (30) mkazi wa Kiluluma mkoani Kagera  kwa kukutwa na hatia ya kumuua kikatili mtoto wake mwenye umri wa miaka 2 na nusu witness melchedes kwa kumkata mapanga kisha kutenganisha kichwa chake na kiwiliwili kwa madai kuwa mke wake alimzaa nje ya ndoa.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Lucia Kairo ambapo amesema vitendo vya mauaji vinavyoendelea kushika kasi mkoni Kagera hususani kati ya wanandoa na watoto ambao hawana hatia  kuwa vinahatarisha usalama na amani hivyo mahakama itaendelea kutoa adhabu kali kwa wanaojihusisha na vitendo hivyo .

 Melchedes alifanya mauaji hayo ya kikatili ya mtoto huyo Julai 27, 2015, katika tukio hilo baada ya kukata mapanga mtoto huyo alimficha kwenye kichaka kilichoko karibu na nyumba yake na alipomaliza kufanya hivyo alirudi ndani ya nyumba yake na kuendelea na shughuli zake.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo wakili wa serikali Haruna Shomari amesema kuwa ameridhishwa na hukumu iliyotolewa na mahakama kwa kuwa itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia ambazo sio za kibinadamu.


Share:

HII HAPA RATIBA YA ROBO FAINALI EUROPA


Viungo matata wa Klabu ya Manchester United, Paul Pogba (Kulia) na Bruno Fernandes wakipongezaka kwa kazi nzuri.

Klabu ya Wolves imetinga hatua ya robo fainali ya mashindano ya Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya takribani miaka 48 baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya bao 2-1 dhidi ya Olimpiacos ya Ugiriki.

Bao pekee lililoivusha Wolves liliwekwa kimiani na mshambuliaji Raul Jimenez aliyefunga kwa penati dakika ya 8 ya mchezo, kufuatia jitihada za Daniel Podence kuzaa matunda baada ya kuangushwa kwenye eneo la hatari na mlinda mlango wa Olimpiacos, Bobby Allain.

Jimenez ambaye ni raia wa Mexico, alifunga bao hilo na kumfanya awe mchezaji pekee wa ligi kuu ya England aliyehusika moja kwa moja katika mabao mengi msimu wa 2019/20 wa mashindano yote, ambaye katika michezo 37,alifunga mabao 27 na pasi zilizozaa mabao 10.



Kwa ushindi huo, Wolves ilisonga mbele kwa jumla ya ushindi wa bao 2-1 na sasa watachuana na itaumana na Sevilla ambayo iliiondosha AS Roma kwa jumla ya mabao 2-0.

Matokeo mengine, Bayer 04 Leverkusen iliifunga Rangers kwa bao 1-0 na kusonga kwa jumla ya bao 4-1na sasa Wajerumani hao watakipiga dhidi ya Inter Milan ya Italia ambayo iliifunga Getafe bao 2-0.

Manchester United ambayo iliifunga bao 2-1 klabu ya LASK katika mchezo wa mwisho, sasa wataumana na FC Copenhagen hatua vilabu vya Shaktar Donetsk watakipiga dhidi ya FC Basel na michezo hiyo itapigwa kuanzia August 10 na 11.
Share:

Country Director at Farm Africa Limited

Country Director  Job Overview Country Director, Tanzania Location: Dar es Salaam with significant national travel and some international travel Full-time, fixed term (3 years) Salary: Competitive Effective agriculture has the power to change lives. It underpins prosperity, food security and stability the world over. Farm Africa focuses on transforming agriculture and managing natural resources sustainably. […]

The post Country Director at Farm Africa Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wajasiliamali watumie Cliniki za biashara kutatua changamoto zao

Na Samirah Yusuph, Simiyu.
Wajasiriamali wadogo wameshauriwa kutumia cliniki za kibiashara ili waweze kukabiliana na changamoto zinazopelekea kukwama na kuangusha biashara zao.

 Ushauri huo umetolewa na mratibu wa Cliniki hiyo Gilbert Waigama, amesema lengo la vituo hivyo ni kutibu matatizo ya biashara yanayozikabiri biashara zao.

Alisema licha ya kutatua kero mbalimbali zilizopo, pia wanajenga biashara kwa kuwapa wakulima elimu sitahiki ambayo itawaongezea uwezo na umahili katika kuendesha biashara.

"Tatizo kubwa ambalo wafanyabiashara katika Kanda nyingi ni namna ya kurasimisha wa biashara, hivyo mteja akifika hapa changamoto hizo zinapata ufumbuzi," alisema.

Cliniki ya biashara inaundwa na taasisi mabali mbali za kifedha, (za kiserikali na sekta binafsi) Kama SIDO, TANTRADE, TBS, na nyingine ambazo zinatoa huduma hizo.

Ambapo tangu wameanza kuhudumia wafanyabiashara 2018 Hadi 2020 wamewafikia wafanyabiashara 1200 kote nchini.


Share:

Wananchi Kagera Watakiwa Kuwa Na Utamaduni Wa Kunywa Kahawa Wanayozalisha Ili Kuimarisha Afya zao.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Bukoba Kagera.
Wamiliki wa  viwanda vya kahawa Mkoani Kagera wametakiwa kutafuta soko  la ndani la zao hilo ili kuwajengea wananchi kutumia kahawa wanayozalisha wao.

Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa mkoa huo Profesa Faustine Kamuzora mnamo Agosti 5 mwaka huu wakati alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho cha AMIRAMZA kIlichopo katika halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na kuongeza kuwa wamiliki wa viwanda vya kahawa wakitafuta soko la ndani itakuwa vizuri kwa kuwa itakuwa chanzo cha kuongeza watumiaji wa kahawa mkoani hapa kutokana na watu walio wengi kutokuwa na utamaduni huo.

Profesa Kamuzora amesema kuwa kwa kipindi hiki cha COVID 19 soko la kahawa lilitakiwa kuwa kubwa zaidi kwa upande wa soko la ndani kwa kuwa soko la Tanzania alijafungwa kama zilivyo nchi za nje na kuongeza kuwa kahawa inayozalishwa hapa nchini ni bora na ina vionjo ambavyo wakati mwingine haipatikani kokote duniani.
 
Amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho bwana Amir Hamza kutumia utaalamu wake alionao kutengeneza soko la ndani ambalo litaongeza idadi kubwa ya watu kutumia zao hilo kwa upande wa mkoa huo.
 
“Watanzania walio wengi hasa wana Kagera hawana utamaduni wa kunywa kahawa mara kwa mara wakati sisi wenyewe ni wazalishaji wazuri wa kahawa na itakuwa vizuri ukianzisha migahawa ya kahawa ili wananchi wa mkoa huu wapate elimu ya kutosha juu ya matumizi ya kahawa”. Alisema Prof Kamuzola.
 
 Ili kuakikisha kwamba kahawa inayolimwa mkoani hapa inamunufaisha mkulima Prof Kamuzola amesema kuwa serikali imefungua milango kwa wanunuzi binafsi wa kahawa kwa kufuata vigezo na masharti yaliyowekwa ilimradi wasiharibu utaratibu uliopo.
 
Kwa upande wake Amir Hamza mmiliki wa kiwanda hicho amesema kuwa kiwanda hicho kwa sasa kinakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Uelewa mdogo wa mradi kwa  taasisi za kifedha hapa nchini uku akisema kwamba nchi za nje zinaitaji vitu kama dhamana ya serikalini,Tatizo la umeme wa uhakika, miundombinu ya barabara ya kuingilia kiwandani bado ni changamoto, Athari za COVID 19 kutokana na masoko ya nje kuwa yamefungwa, gharama kubwa za uzalishaji utafutaji masoko pamoja na usambazaji nk.
 
Pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo bwana Hamza amesema kuwa kiwanda hicho kimeweza kushiriki katika  maonesho mbalimbali ya  kibiashara ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni kutangaza vyema Mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla katika mataifa mbalimbali kama Italia, Ujerumani, Dubai, Uingereza, Misri, Marekani, Afrika kusini nk.
 
Aidha bwana Hamza ameiomba serikali kuwapatia mkopo wa muda mrefu ili waweze kutimiza kikamilifu mradi wa kiwanda hicho pamoja na upanuzi kuendana na kasi ya dunia.



Share:

Mtindo Bora wa maisha ni Kinga dhidi saratani

Mhudumu kutoka hospital ocean road akimhudumia mteja katika maonyesho ya nane nane Nyakabindi mkoani Simiyu.
 ***
Na Samirah Yusuph, Simiyu.
Taasisi ya saratani ya ocean road, imejikita katika kutoa elimu kwa wananchi dhidi ya mtindo Bora wa maisha ambao utawakinga dhidi ya saratani.

Mfumo wa maisha umetajwa kuwa ni sababu kubwa ya watu wengi kuungua sarati, kwa sababu ya kutokufuata misingi ya lishe bora Hali inayopelekea uzito uliopitiliza.

Akihimiza wananchi kufanya mazoezi pamoja na kutoa elimu juu ya saratani Dr. Maguha Stephano, alisema kuwa kufanya mazoezi pamoja na lishe bora ni moja ya Kinga ambayo inasaidia kulinda mwili.

"Inabidi wanachi waelewe namna ya kuweza kukabiliana na saratani lakini vilevile waweze kuelewa namna ya kuishi na saratani," alisema

Alisema kuwa kufika kwao Kwenye maonyesho ya nane nane ni pamoja na kuona wagonjwa wa kanda ya ziwa Ili waweze kuwahudumia, pamoja na kutoe elimu kuhusu saratani.

"Tunahimiza wananchi ili wapime Mara kwa Mara waweze elewe hatua za saratani na pia tunatoa chanjo za homa ya ini pamoja na saratani ya homa ya ini," aliongeza.

Hali ya maambuki ugonjwa wa saratani
Kwa takwimu za mwaka 2019 taasisi ya saratani ya ocean imebainisha kuwa Kati ya wagonjwa wote wanawake wa saratani ni 47%, saratani ya matiti 16% ,saratani ya utumbo mkubwa na mdogo ni 5.8%, saratani ya Koo 5.3% na saratani ya kichwa na shingo ni 4.2%.

Kwa upande wa wanamme saratani ya tezi dume ni 23%, saratani ya Koo 16%, saratani ya kichwa 12%, saratani ya utumbo ni 11.4%, na saratani ya matezi 9%.



Share:

Wizara Ya Maji Yatekeleza Ahadi Ya Rais Magufuli Mbalizi

Na Mohamed Saif, Mbeya
KATIBU Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (Mbeya UWASA) kwa kutekeleza kwa haraka agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuwafikishia huduma ya majisafi wananchi wa mji mdogo wa Mbalizi Wilayani Mbeya.

Ametoa pongezi hizo Agosti 6, 2020 alipotembelea mradi wa Maji wa Shongo-Mbalizi ikiwa ni ufuatiliaji wa utekelezaji wa maelekezo ya Rais Magufuli ya kuwaondolea kero ya ukosefu wa majisafi wananchi wa mji mdogo wa Mbalizi aliyotoa Aprili 27, 2019 kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa.

Mhandisi Sanga alisema amefurahishwa kuona ahadi ya Rais Magufuli kwa wananchi wa Mbalizi imetekelezwa na tayari mradi unafanya kazi na wananchi wameanza kunufaika.

“Mtakumbuka maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli aliyoyatoa alipopita hapa Mbalizi, alituagiza sisi Wizara kupitia Mbeya UWASA kuhakikisha tunawafikishia wananchi wake hapa huduma ya majisafi na alisisitiza mradi utekelezwe haraka nami ninafarijika kuona tayari wameanza kunufaika,” alisema Mhandisi Sanga.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo wa bilioni 3.3, Mkurugenzi Mtendaji wa Mbeya UWASA, Mhandisi Ndele Mengo alisema ulianza kujengwa Julai 1, 2019 na hadi hivi sasa umefikia asilimia 98 na huku idadi ya wananchi waliounganishwa na huduma ikiwa ni 108 na vituo 10 vya kuchotea maji.

Mhandisi Ndele alisema uwezo wa mradi ni kuzalisha kiasi cha lita milioni 8.5 hadi 10 kwa siku na kwamba maji yanayotumika kwa sasa ni chini ya lita milioni nne kwa siku kutokana na maunganisho yaliyokwishafanyika.

Kufuatia taarifa hiyo ya Mhandisi Mengo, Katibu Mkuu Sanga aliielekeza Mbeya UWASA kuhakikisha inaunganisha wateja wengi zaidi huku akisema kiasi cha wananchi waliounganishwa hakiridhishi ikilinganishwa na ukubwa wa mradi na hivyo alisisitiza kasi iongezeke ya kuwaunganisha wananchi.

“Dhamira ya Rais Magufuli ni kuona wananchi wake wanafikishiwa huduma ya majisafi; sasa kwa idadi mliyonieleza hawa mliyowaunganisha ni wachache sana, hakikisheni mnatanua wigo ili kuwafikia wananchi wengi zaidi kama anavyoelekeza Mheshimiwa Rais,” alielekeza Mhandisi Sanga.

Aidha, wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi wa Mbalizi walieleza kufurahishwa kwao na jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaondolea kero mbalimbali zilizokuwa zikiwasumbua kwa muda mrefu ikiwemo ya ukosefu wa huduma ya majisafi.

Akizungumza mbele ya Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Usahandeshi katika Mji Mdogo wa Mbalizi, Joster Mwalingo alimshukuru Rais Magufuli kwa maelekezo yake kwa Wizara ya Maji ya kuhakikisha wananchi wa Mbalizi wanapata maji na pia aliipongeza Wizara ya Maji kwa utekelezaji wa haraka wa maelekezo hayo.

Mwalingo alisema tangu kitongoji hicho kianzishwe hakikuwahi kuwa na huduma ya majisafi na kwamba wakuwahi kufikiria itafika siku nao watapata huduma kwa haraka kama ilivyotokea lakini kwa maelekezo ya Rais Magufuli na jitihada za Wizara kupitia Mbeya UWASA ndoto yao imetimia.

“Tunamshukuru sana Rais wetu, hakika anasema na kutenda na pia tunawapongeza nyinyi watendaji wa Wizara mkiongozwa na Waziri Mbarawa kwa kuyapokea maelekezo na kuyafanyia kazi kwa kasi na sasa hivi maji tunapata,” alipongeza

Mhandisi Sanga yupo Mkoani Mbeya kwa ziara ya siku tatu ya kukagua ujenzi wa miradi ya maji ambapo mbali na mradi huo wa Shongo Wilayani Mbeya, atatembelea miradi ya maji ya Busokelo na Bulongwe ya Wilayani Rungwe pamoja na Chitete na Ndalambo ya Wilayani Momba Mkoani Songwe.


Share:

Halmashauri zinavyo badirisha maisha ya wajasiliamali kupitia mikopo.

Na Samirah Yusuph
Kufuatia agizo la serikali kwa halmashauri zote nchini la kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwaajili ya kukopesha vikundi vya vijana, wanawake, na walemavu umewanufaisha walengwa na kuwainua kiuchumi.

Wanufaika hao walio katika vikundi mbali mbali vya wanawake na vijana, wameweza kuanzisha biashara mbalimbali na kujikita katika ujasiliamali hivyo kubadirisha maisha yao.

Baadhi  wanawake walio katika vikundi wameleta bidhaa zao katika maonyesho ya nane nane kitaifa mkoani Simiyu  na wameonyesha namna ambavyo mikopo hiyo imewanufaisha.

Akiongea katika maonyesho hayo katibu wa kikundi Cha Shida na Raha kutoka Wilayani Maswa Grace Kalunde, alisema wao walipata mkopo uliowasaidia kununua mashine  ya kuchakata Katani inayowasaidia kutengeneza bidhaa zitokanazo na zao Hilo.

"Tunatengeneza mikoba na mifagio ya Katani ambayo tunaiuza lakini sisi Kama sisi hatukuwa na uwezo was kununua hi mashine hivyo serikali ilitupatia mkopo wa milioni tatu," alisema kalunde.

Kalunde alisema tangu wamepata mkopo huo, wanaweza kutengeneza bidhaa na kuziuza wenyewe hivyo wanajipatia kipato ambacho kimebadirisha maisha yao.

Baadhi ya vijana waliopo katika maonyesho hayo walisema kwamba mikopo imewawezesha wao kujiinua na kujiajiri wenyewe hivyo wanaendelea kunufaika na mikopo hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi wa Tumaini la vijana kutoka kata ya Jija wilaya ya Maswa Sayayi Leonard alisema, mikopo hiyo imepanua wigo was kuendesha shughuri zao.

"Tunafanya shughuri za ushonaji wa nguo na vitambaa kabla ya mkopo tulikuwa hatujiwezi kiuchumi lakini Sasa tunafanya kazi vizuri kea sbabu tuna fedha zinazopelekea tuwezesha," alisema Sayayi.

Saba Kashilimu ni afisa kilimo wa wilaya ya maswa, alisema wao wanahamasisha wafugaji wa kisasa ili wapate faida kutoka kutoka kwa mifugo wao.

"Tunawashauri kuwa na mifugo michache ili wawafuge kisasa pamoja na kuachana na ufugaji wa mazoea ambao hauna faida," alisema Kashilimu.

Alisema wamewaelekeza wafugaji hao kuwapa lishe bora mifugo hatua iliyo Leta manufaa kwa sababu faida inaonekana.

Mratibu wa maonyesho ya nane nane wilaya ya maswa Mabula Yohana alisema, ni wakati wa watu wengi zaidi kujifunza kupitia vikundi vilivyofanikiwa ili na wao wanufaike na mikopo hiyo.

"Hapa hawaonyeshi namna wanavyo fanyakazi na bidhaa zao lakini pia wanaonyesha namna ambavyo mikopo inamanufaa," alisema Mabula.

Akiainisha namna ambavyo serikali imewawezesha wajasiriamali hao Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya  maswa  Rodgers Lyimo, alisema wametoa mafunzo ya kuwawezesha kumiliki  biashara.

"Tumewafundisha kuandaa mpango biashara, usimamizi wa fedha, kuandaa mchanganuo wa mapato na matumizi, na uendeshaji wa Vikundi pamoja na namna ya kutafuta masoko ya bidhaa wanazozalisha" Alisema

Aidha aliongeza kuwa, Kufanya wamekuwa wakifanya usimamizi na ufuatiliaji na tathimini ya kazi zinazofanywa na vikundi vyote.

Mwisho.


Share:

Wauguzi Nchi Watakiwa Kujifunza Vitu Vipya Ili Kuongeza Viwango Vyao Kutekeleza Majukumu

Na. Catherine Sungura-WAMJW-Dodoma
Wauguzi nchini wametakiwa kujiendeleza ikiwemo kujifunza vitu vipya ili kuweza kwenda na wakati katika kuongeza viwango vyao vya utekelezaji wa majukumu ya kila siku kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Prof. Mabula Mchembe wakati akifunga kikao kazi cha kuwajengea uwezo wa kusimamia maadili na utendaji kazi Wauguzi Wakuu wa Wilaya wapatao 89 kutoka wilaya 89 nchini.

Prof. Mchembe alisema kuwa hivi sasa nchi imeingia kwenye uchumi wa kati hivyo kwenye sekta ya afya inapaswa kuboresha huduma zenyewe ,vifaa na vifaa tiba pamoja na kuwa na stadi za kutosha kwa watumishi ili huduma zitolewazo ziwe na ubora wake.

“Mnapokua pamoja mnachangiana na kusaidiana mawazo ili muweze kuboresha huduma kwenye vituo vyenu lakini mtakaporudi ni vyema mkawahusisha wenzenu kwani kila mmoja ana mawazo yake na yakichukuliwa yataeleweka,sio ukiwa Muuguzi Mkuu wa wilaya au mkoa basi unajua kila kitu ni vyema mkayaheshimu mawazo ya wengine”Alisisitiza.

Aidha, Prof. Mchembe amesema kuwa wauguzi waliopo halmashauri na hospitali za rufaa wote ni sawa na wanafanya kazi za aina moja hivyo wanatakiwa kufanya kazi kwa kufuata maadili kwa kutenda kufuatana na taaluma yao.“Kutofufanya kinyume na fani yako ni muelekeo mzuri hivyo kukutana hapa mmeweza kukumbushana maadili yenu kwahiyo mnapaswa mkaendeleze mliyojifunza hapa mtakaporudi mkawafundishe wenzenu kwenye sehemu zenu za kazi”.

Akijibu azimio la upande wa mafunzo Katibu Mkuu huyo alisema amekubaliana na uwepo wa utaratibu wa kufuatilia vyuo vya mafunzo kwa idara ya mafunzo inapaswa kuwa na dawati la uwakilishi ili watakaochaguliwa wawe wanawakilisha kulingana na mahitaji na kushirikiana na wauguzi ili kuona ni upande gani wanapaswa kupatiwa mafunzo yapi kulingana na muundo pia.

Hatahivyo amewataka wanapomaliza vikao wawe wameweka vipaumbele na muda wa tekelezaji ili kurugenzi ya uuguzi na ukunga waweze kuifanyia kazi ikiwemo changamoto wanazokabiliana nazo sehemu zao za kazi.

Kikao kazi cha kuwajengea uwezo wa kusimamia maadili na utendaji kazi wauguzi wakuu wa wilaya kimefanyika kwa siku tatu jijini hapa kwenye ukumbi wa Cathedral ambapo imewakutanisha wauguzi wakuu wa wilaya 89 kutoka mikoa kumi na mbili ambapo yaliandaliwa na Baraza wa Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC).


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa Augudt 7





















Share:

Thursday 6 August 2020

WAZIRI BASHUNGWA ASEMA MFUMO WA CRDB WAKALA UNACHOCHEA UKUAJI SEKTA YA FEDHA NCHINI


IMG-20200806-WA0025
Waziri wa Viwanda Innocent Bushungwa ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jitihada za Serikali katika kuhakikisha Watanzania wengi wanapata fursa ya kujiunga na mfumo rasmi wa kibenki hususani maeneo ya vijijini. Bashungwa alisema hayo wakati wa ufunguzi wa Semina ya CRDB Wakala iliyofanyika Wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu.

Sekta ya fedha ni kichocheo muhimu cha maendeleo ya taifa letu. Lakini ili sekta ya fedha iweze kutoa mchango unaokusudiwa, inapaswa iwe imara, na iwe na uwezo mkubwa wa kufikia wateja wengi mijini na vijijini” alisema Bashungwa.

Akiipongeza Benki ya CRDB kwa kupanua wigo wake wa utoaji huduma kupitia mfumo wa mawakala ujulikanao kama CRDB Wakala, Bashungwa alisema ili kuendana na kasi ya maendeleo nchini Benki zinapaswa kuwekeza katika mifumo ya kidijitali inayotoa fursa ya kubuni njia mbadala za utoaji huduma kwa wateja.

“Nimefurahi kusikia sasa hivi mna zaidi ya CRDB Wakala 20,000 waliosambaa nchi nzima hususani vijijini. Hii itasaidia sana kuchochea shughuli za kibiashara katika maeneo ambayo mwanzo ilikuwa ni ngumu kufika kwa uwekezaji wa matawi,” aliongezea Bashungwa.

Bashungwa alisema pamoja na kuongezeka kwa huduma za benki kupitia uwakala, benki zinapaswa kutoa mafunzo kwa mawakala ili kuongeza weledi na kuboresha huduma kwa wateja. “Niwapongeze Benki ya CRDB kwa kuendesha semina hii ya kuwajengea uwezo mawakala. Niwasihi CRDB Wakala wote mliohudhuria hapa msikilize kwa umakini na kutoa huduma kama mafunzo yanavyoelekeza, weledi wenu katika kutoa huduma ni muhimu sana katika kuwahudumia Watanzania na kuboresha sekta ya fedha nchini,” alisema Bashungwa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliipongeza Benki ya CRDB kwa kufikisha huduma za CRDB Wakala kwa wakulima kupitia vyama vya ushirika (AMCOS) na mawakala binafsi huku akibainisha kuwa jitihada hizo zimesaidia wakulima wengi nchini kufungua akaunti za Benki. 

“CRDB Wakala imesaidia kuwawezesha wakaulima kupokea malipo yao moja kwa moja kupitia akaunti zao za Benki, jambo ambalo limeondoa udanganyifu na dhuluma kwa wakulima,” alisema Bashe.


IMG-20200806-WA0023
Lusinga Sita Meneja wa Kanda ya Ziwa akitoa maelezo kwa Waziri Innocent Bushungwa alie ambatana na Naibu waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwenye ufunguzi wa mafunzo ya CRDB Wakala yaliyotolewa na CRDB Benki Mkoani Simiyu.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Ziwa Benki ya CRDB, Lusing Sitta alimwambia Waziri wa Viwanda kuwa semina hizo zilizoandaliwa kwa ajili ya CRDB Wakala nchi nzima zinalenga katika kuboresha utoaji huduma kwa wateja na kuwajengea uwezo mawakala hao.

Sitta alisema CRDB Wakala wamekuwa na mchango mkubwa katika kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja kutokana na kusogeza hudma za benki karibu. “CRDB Wakala wanatoa huduma zote kuanzia kufungua akaunti, kuweka na kutoa pesa, malipo ya Ankara na malipo ya tozo na kodi za serikali,” alisema Sitta huku akibainisha kuwa mwaka jana pekee CRDB Wakala ilisaidia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 300.

Sitta alimwambia Waziri Bashungwa kuwa Benki ya CRDB katika mkakati wake wa biashara wa miaka mitano imedhamiria kuongeza matumizi ya mifumo ya kidijitali kama CRDB Wakala, SimBanking, SimAccount na Internet Banking ili kusaidia kufikisha huduma za kifedha kwa watanzania wengi zaidi.

“Mwaka jana asilimia 86 ya miamala ya wateja wetu ilifanyika kupitia njia hizi za kidijitali,” alimalizia Sitta huku akisema mwaka huu Benki ya CRDB imejipanga kufanya semina hizo za CRDB Wakala katika wilaya 50 Tanzania.

IMG-20200806-WA0022
Baadhi ya CRDB Wakala wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayo tolewa na Benki ya CRDB Wilayani Bariadi-Simiyu.

IMG-20200806-WA0027
Mkuu wa Wilaya ya Busega Bi. Tano Mwela akimkabidhi zawadi mmoja wa CRDB Wakala ambaye anafanya vizuri kwa kufungua akaunti nyingi zaidi kwa wastani wa akaunti 90 kwa siku.
IMG-20200806-WA0021 

Share:

Serikali Yahimiza Mabenki kutoa Mikopo Miradi Mikubwa ya Madini

Na Jonas Kamaleki
Serikali imezitaka benki na taasisi nyingine za fedha kukopesha miradi mikubwa ya uchimbaji wa madini nchini ili kukuza sekta hiyo ambayo imeanza kutoa mchango mkubwa kwenye pato la taifa.

Akifungua mafunzo haya leo jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema imekuwa ndoto yake ya muda mrefu ya Tume ya Madini kukutana na mabenki kwa ajili ya mustakhabali wa wachimbaji wa madini.

“Sekta ya madini kufungamanishwa na mabenki ni hatua kubwa katika kukuza sekta hiyo ambayo ina mchango mkubwa kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla”, amesema Nyongo.

Waziri Nyongo amebainisha ukuaji wa haraka wa sekta ya madini nchini na kusema kuwa miaka michache iliyopita sekta ya madini ilikuwa ikichangia aslimia 3.8 kwenye pato la Taifa lakini kwa sasa inachangia zaidi ya asilimia 5.2, ameongeza kuwa sekta hiyo inakuwa kwa asilimia 17.7.

Amesisitiza elimu ya biashara ya madini kuendelea kutolewa kwa mabenki ili kuwajengea uwezo wakopeshaji ili kutambua fursa zilizopo kwenye sekta ya madini na kuwataka kuajiri wataalaam wa madini ambao wanaweza kuchambua michanganuo ya mikopo ya uchimbaji wa madini.

“Natoa wito kwa mabenki mengine kupitishwa kwenye mafunzo haya ili waweze kuwakopesha wachimbaji hasa wadogo na kwa kufanya hivyo kipato chao kitaongezeka, ajira zitaongezeka na mabenki yatafanya biashara kutokana na riba”, alisema Nyongo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Katibu Mtendaji Tume ya Madini, Prof. Shukrani Manya amesema kuwa sekta ya madini ni sekta muhimu katika uchumi ambayo inahitaji mitaji mikubwa katika uwekezaji wake hivyo watoa mikopo ni muhimu kuwa na uelewa wa sheria na kanuni za madini.

“Sekta ya madini ni biashara kama biashara nyingine inahitaji mitaji mikubwa hivyo ninyi watu wa benki inabidi mjue vizuri leseni za madini, uhai wa leseni hizo na sheria na kanuni za madini”, alisema Prof. Manya.

Aidha, Prof. Manya amesema mafunzo hayo yataondoa kusitasita kutoa mikopo kwa wachimbaji hasa wadogo baada ya kuwa na uelewa mpana kuhusu mnyororo wa madini unaohusu wachimbaji, wauuzaji, vifaa vya uchimbaji na uchakataji wa madini na watoa huduma wengine katika sekta hiyo.

Prof. Manya ameyaomba mabenki mengine kujengewa uwezo na kutoa mikopo kwa wachimbaji wa madini kwa kuzingatia vigezo vilivyopo ikiwemo uhai wa leseni ya mchimbaji.

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo, Meneja wa Dawati Maalum la Wateja wakubwa Fredrick Mwamyalla amesema benki ya CRDB kwa kushirikiana na Tume ya Madini imeandaa mafunzo hayo kutokana na mageuzi yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ikiwemo kuanzisha masoko ya madini, kurekebisha Sheria ya Madini na kudhibiti mianya ya utoroshaji madini.

“Kupitia mafunzo haya tutakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kubuni bidhaa nzuri zinazohusu utoaji mikopo kwa sekta ya madini, hasa kwa wachimbaji wadogo, wakubwa na wa kati”, alisisitiza Mwamyalla.

Mwamyalla ametoa wito kwa wachimbaji, wanunuzi na wauzaji wa madini kufika CRDB Benki ili kupata mikopo ya kuwawezesha kuwekeza katika sekta hiyo.

Maafisa Waandamizi wa Benki ya CRDB wamepewa mafunzo kuhusu sekta ya madini ili kujengewa uwezo katika sekta hiyo ili kurahisiha utoaji mikopo kwa wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa ikiwemo watoa huduma.

Mafunzo hayo ambayo yameanza leo (Agosti 6, 2020) jijini Dodoma yanatolewa na wataalaam toka Tume ya Madini.

Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kwa. Baadhi ya mada ni Sheria na Kanuni za Madini, Jiolojia na Madini yanayopatikana nchini na Leseni za Madini. Mafunzo hayo ni mwendelezo wa kuyajengea uwezo mabenki kwani yalianza kutolewa kwa benki ya NMB.


Share:

Tanzania Yasaini Mkataba Wa Mapitio Wa Georgetown Wa Jumuiya Ya Nchi Za Afrika, Caribbean Na Pacific

Tanzania imesaini Mkataba wa mapitio wa Georgetown unaosimamia  mahusiano na uendeshaji wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribiani na Pasifiki ambayo zamani ilikuwa ikiitwa  ACP na sasa Organisation of African, Carribean and Pacific States (OACPS) iliyo na nchi wanachama 79.

Mkataba huo ulisainiwa na balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,  Mhe. Jestas Abuok Nyamanga kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Brussels, Ubelgiji tarehe 31 Julai 2020. Hivyo Tanzania inakuwa nchi ya 42 kati ya nchi 79 kusaini Mkataba wa mapitio wa Georgetown.

Mkataba wa Georgetown umefanyiwa mapitio ili uweze kuendana na wakati kwa kuzingatia mabadiliko makubwa yanayoendelea kutokea duniani katika nyanja za  kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimazingira tangu kuanzishwa kwa ACP mwaka 1975. Mchakato wa kufanya mapitio ya mkataba huu ulianza mwezi Machi 2013 kupitia timu maalum iliyoanzishwa kukusanya maoni na kuleta mapendekezo chini ya Uenyekiti wa Rais Mstaafu wa Nigeria, Mhe. Olusegun Obasanjo.

Aidha, Mwaka 2019 mchakato wa mapitio hayo ulihitimishwa kwa  kuridhiwa na Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za OACPS katika mkutano wao uliofanyika mwezi Desemba 2019 jijini Nairobi, Kenya.

Mkataba wa Georgetown ndiyo ulianzisha ACP mwaka 1975 katika mji wa Georgetown nchini Guyana.  Tanzania ilisaini Mkataba huo wa awali tarehe 11 Desemba 1975 na imedumu ikiwa mwanachama wa ACP tangu wakati huo.

Pamoja na kuwa mwanachama Tanzania imekuwa ikinufaika katika masuala ya kiuchumi, kijamii, biashara, na uwekezaji kupitia ushirikiano maalum baina ya nchi za ACP na Umoja wa Ulaya unaosimamiwa na mikataba ya Lome na Cotonou. Vilevile miradi ya ubia wa maendeleo na ile ya mtangamano wa nchi za ACP chini ya ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya. Pia ushirikiano katika masuala ya kubadilishana ujuzi na uzoefu na nchi za ACP, mshikamano wa kisiasa na kidiplomasia katika kutetea maslahi ya Tanzania kimataifa kupitia jukwaa la ACP.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali


Share:

Tanzania Yachaguliwa Kuwa Rais Wa Baraza La Mawaziri Wa Jumuiya Ya Nchi Za Afrika, Carribean Na Pacific

Serikali ya Tanzania imechaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Carribean na Pacific (Organisation of African, Carribean and Pacific States-OACPS)  kwa kipindi cha miezi sita kuanzia tarehe 1 Agosti 2020 hadi tarehe 31 Januari 2021.

Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alikabidhiwa rasmi nafasi hiyo iliyopokelewa kwa niaba yake na Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro,  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 28 Julai 2020.

Tanzania inakuwa Rais wa Baraza hilo kutokana na Balozi  wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga kuchaguliwa kwa kauli moja kuwa Mwenyekiti wa Mabalozi wa Nchi za OACPS waliopo Brussels. Kwa mujibu wa Jumuiya ya OACPS,  nchi inayotoa Mwenyekiti wa Mabalozi wa Jumuiya hiyo, Waziri wake anayesimamia masuala ya OACPS ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje moja kwa moja anakuwa Rais wa Baraza la Mawaziri. Uamuzi wa kuichagua Tanzania ulifanywa na Mabalozi kutoka nchi 15 za Ukanda wa Mashariki mwa Afrika kwenye kikao kilichofanyika tarehe 2 Julai 2020 na kuthibitishwa kwa kauli moja na mabalozi wote wa nchi 79 wa OACPS kupitia kikao chao kilichofanyika Brussels tarehe 14 Julai 2020.

Tanzania ambayo inachukua nafasi hiyo kutoka kwa Gambia, imejipanga kutekeleza masuala mbalimbali yenye maslahi kwa Nchi za OACPS ikiwa ni pamoja na kusimamia ukamilishwaji wa majadiliano kuhusu Mkataba mpya wa ushirikiano wa Nchi za OACPS na Umoja wa Ulaya (EU) unaotarajiwa kuanza kutumika mwezi Januari 2021 baada ya mkataba wa sasa wa Cotonou (Cotonou Partnership Agreement)


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger