Friday 5 June 2020

Rais Magufuli: Tutafungua Shule za Msingi, Sekondari na Chekekea Hivi Karibuni, Corona Imepungua Sana

Rais wa Tanzania, Dr John Magufuli amesema atafungua shule za msingi na sekondari hivi karibuni, kama ataridhishwa na kasi ya upunguaji wa maambukizi ya ugonjwa wa Corona

Rais Magufuli amesema hayo leo Ijumaa tarehe 5 Juni 2020, wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), jijini Dodoma.

Amesema, maambukizi ya corona yamekuwa yakipungua siku hadi siku huku akiendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari  ya ugonjwa huo.

Huku akishangiliwa na umati wa mkutano huo,  Rais Magufuli amefurahishwa na washiriki wa mkutano huo walioujaza uwanja wa Jamhuri, Dodoma kutokuvaa barakoa huku akionyesha kushangazwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuvaa barakoa akiwa ndani ya Bunge. 

“Corona imekwisha ndiyo maana hata mabarakoa hakuna, hata leo tunaonana tu hapa kawaida, ndiyo maana nilikuwa namshangaa Spika Ndugai akiwa Bungeni yupo kiti chake peke yake lakini amelivaa hilo libarakoa mdomoni, Watanzania tumtangulize Mungu."-Amesema


Share:

Rais Magufuli: Hatukuwa na Ebola wala Mjukuu Wake Ebola....Walidhani Watalii Hawatakuja

Rais Magufuli amewataka Watanzania kutotilia maanani baadhi ya maneno ya uongo kutoka kwa watu wa nje, kuhusu milipuko ya magonjwa mbalimbali huku akisimulia namna   alivyomfuta kazi kiongozi mmoja wa taasisi ya umma baada ya kutangaza  taarifa za uongo kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Zika nchini Tanzania.

Akizungumza leo Ijumaa, Juni 5, 2020, katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania unaofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma,  Rais Magufuli amesema Watanzania wasitishwe wala wasiwe na hofu kuhusu Ugonjwa wa Corona kwani unaelekea kuisha kabisa.

“Wakati tunaingia madarakani tuliambiwa Tanzania kuna ugonjwa unaitwa Zika, aliyetangaza na aliyetumiwa kutangaza nikamfukuza kazi, bahati mbaya ni Mgogo

“Baada ya kumfukuza yule Mgogo aliyesema Tanzania kuna Zika na waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi, mpaka leo miaka karibu mitano hapajawahi kuwa na kesi ya Zika hapa Tanzania.

“Baada ya uzushi wa Zika kupita na nilipomfukuza kazi aliyesema kuna Zika,tukakaa baadaye tukaambiwa kuna Ebola, walijua wakisema tuna Ebola watalii hawatokuja, tukasema sisi hatuna Ebola, wala mjukuu au hawara yake Ebola, na kweli hatujaona mgonjwa amekufa kwa Ebola Tanzania.


“Umekuja ugonjwa wa Corona walikuwa wanazungumza kwamba maiti zitazagaa kwenye barabara hasa Afrika, wao walikuwa watabiri walishindwa kuelewa Mungu analipenda taifa la Tanzania pamoja na Afrika,” amesema


Share:

Rais Magufuli Awamwagia Sifa Walimu, Aahidi Kutowaangusha

Rais Magufuli amesema Serikali yake itaendelea kushirikiana na walimu kuhakikisha sekta ya elimu inasonga mbele na kwamba madai yao anaendelea kuyashughulikia na kuyatatua moja baada ya jingine, hivyo hawezi kuwatupa kwani hata yeye alikuwa mwalimu kabla ya kuingia kwenye siasa.

Magufuli amesema hayo leo Ijumaa, Juni 5, 2020, wakati akihutubia kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT), jijini Dodoma.

==>>Haya ni baadhi ya maneno aliyoyasema
“Ninamshukuru Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu, ametaja mambo ambayo tumeyafanya kwa miaka mitano iliyopita, moja ya mambo makubwa tuliyoyafanya kwenye elimu ni kutoa elimu bila malipo kuanzia shule za msingi hadi sekondari.

“Ndugu wajumbe wa mkutano huu, ninafahamu mkutano huu ni muhimu kwa ajili kuwapata viongozi wa walimu, nisingependa kuonekana nampigia chapuo mtu yeyote lakini uongozi huu unaomaliza muda wake umejenga uhusiano mzuri kati ya walimu na Serikali.

“Siwezi kuwatupa walimu, tunajenga nyumba moja, mimi nilikuwa mwalimu, kuwakana walimu ni kuikana nafsi yangu siwezi kuwatupa, naamini hata kama uongozi huu hautochaguliwa, huo uongozi ujao pia utajenga uhusiano mzuri na Serikali.

”Niwahakikishie walimu kuwa serikali hii imejaa walimu, hata mimi nikisahau nakumbushwa na Mama Janeth naye ni mwalimu, hata Majaliwa akisahau anakumbushwa na Mary Majaliwa tena mahala pazuri pa kukumbushwa, Waziri wa Madini ni mwalimu, hata Waitara ni mwalimu.

“Nilipotangaza kufunga vyuo na shule kupisha corona, kesho yake nikapigiwa simu na Rais wa CWT, akaniambia usifanye kama nchi nyingine ukakata mishahara ya walimu, nikatafakari, nikasema corona hata ikikaa miaka kumi sitakosa mshahara wa kuwalipa walimu.

“Napenda niwahakikishie walimu wote nchini, kuwa hata kama shule zingefungwa mwaka mzima au hata miaka kumi, tutaendelea kuwalipa mishahara yenu kama kawaida,kwa sababu Corona haikuletwa na walimu.

”Ili kuepuka udanganyifu, Serikali kwa sasa inaandaa mfumo wa kielektroniki wa kuhakiki madai ya watumishi wakiwemo walimu, ambao utaanza kutumiwa kwa majaribio mwezi huu hapa Dodoma na endapo utaonesha mafanikio utatumika kwa nchi nzima.”

“Kuhusu malimbikizo ya madeni, tangu Novemba 2015 Serikali imelipa shilingi bilioni 115, tutaendelea kulipa madeni hayo kadiri tutakavyokuwa tunayahakiki.

“Tumesogeza bajeti ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu ya kutoka Sh.341 bilioni, mwaka 2014/2015, hadi kufikia Sh.450 bilioni,mwaka 2019/2020. Ufaulu wa kidato cha nne umeongezeka kutoka asilimi 69.8 mwaka 2015 hadi 89 mwaka 2019.

“Ualimu ndio sekta mama, na tunawathamini sana, hata kama corona itakaa miaka mitano tutawalipa mishahara yenu kama kawaida kwa kuwa walimu wao hawajaileta hiyo corona.

“Kwenye huu uchaguzi chagueni viongozi wenye uchungu na walimu, epukeni kuchaguana kwa kujuana au kwa rushwa, mtakaochaguliwa muwatumikie walimu sio kwa maslahi yenu binafsi” amesema.


Share:

Rais Magufuli aagiza wanaogawa barakoa zisizothibitishwa Washughulikiwe

Rais wa Tanzania, Dkt.  John Magufuli amewaagiza viongozi katika maeneo mbalimbali nchini kuwakamata na kuwahoji wale wote wanaogawa barakoa kwa wananchi ili waeleze zimethibitishwa wapi kuwa zinafaa kutumika.

“Ukimuona mtu anagawa barakoa kwa wananchi, ashikwe akaulizwe zimethibitishwa wapi,” amesema Rais Magufuli wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Aidha, amewataka wananchi kuwa makini kwa kutokupokea barakoa ambazo hawajui mgawaji amezitoa wapi kwani vifaa hivyo vinaweza kutumiwa kusambaza virusi vya corona.

“Tusidanganywe kwa kuletewa mabarakoa ambayo hatujui yametoka wapi, tutaeneza corona bila sisi kujua. Anapokuletea mtu barakoa hujui hata ameitoa wapi kataa, mwambie kavae wewe na mke wako na watoto wako nyumbani.”

Amewasihi wananchi wanaotaka kuvaa barakoa washone wenyewe kwani watakuwa na uhakika wa usalama wake.


Share:

Uvutaji Wa Tumbaku Una Athari Kiuchumi Wa Mtu Mmoja Mmoja Anayetumia

 Na WAMJW-Dodoma
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema Tanzania kama nchi nyingine za Kiafrika wavutaji wa tumbaku wako hatarini kuyumba kiuchumi na kupata magonjwa yasiyoambukizwa kama tahadhari hazitachukuliwa mapema.

Waziri Ummy amesema hayo  wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa matumizi ya tumbaku kwa watu wazima wa mwaka 2018 nchini uliofanyika mapema leo katika Ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema utafiti huo umeonesha kuwa kwa wastani matumizi ya tumbaku kwa mtu mmoja kwa mwezi inagharimu Shilingi za Kitanzania 28,840/= fedha ambayo ingetosha kupunguza kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi kwa mtu mmoja mmoja kwa mwezi kwa asilimia 58 na umaskini wa kupindukia (mahitaji ya chakula) kwa mtu mmoja mmoja kwa mwezi kwa asilimia 85.

“Kwa kutumia taarifa za Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya binafsi kwa Tanzania Bara wa Mwaka 2017-18, fedha za kujikimu kwa ajili ya mahitaji ya msingi kwa mwezi kwa mtu mmoja ni Shilingi za Kitanzania 49,320/= na mahitaji ya chakula kwa mwezi kwa mtu mmoja ni Shilingi za Kitanzania 33,748/=”. Amesema Waziri Ummy.

Kwa mujibu wa utafiti huo, Matokeo yameonesha kuwa mtu mmoja kati ya 10 (8.7%), wenye umri wa miaka 15 au zaidi nchini Tanzania wanatumia tumbaku ya aina yeyote na hivyo kuwa na watu milioni 2.6 kati ya watu zaidi ya milioni 55. Wanaume ni asilimia 14.6 na wanawake ni asilimia 3.2.

Aidha, Waziri Ummy amesema watu 4 kati ya 10 (40.3%) nchini wamewahi kuona onyo la matumizi ya tumbaku kupitia redio au runinga. Pia matokeo ya utafiti yameonesha kuwa, watu 9 kati ya 10 (92.3%) wenye umri wa miaka 15 au zaidi wanaamini uvutaji wa sigara husababisha magonjwa, wakati watu 8 kati ya 10 (84.4%) wanaamini kuvuta hewa ya mtu anaevuta sigara kunaweza kuwasababishia magonjwa hata kama wao hawavuti sigara.

katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. Taarifa inaonesha kuwa watu 4 kati ya 10 (32.9%) wameathiriwa na moshi wa tumbaku sehemu za kazi ikiongozwa na sehemu za mabaa na kumbi za starehe kwa asilimia 77 (watu milioni 3), maeneo ya huduma za biashara za vyakula asilimia 31.1(watu milioni 3.5) na majumbani asilimia 13.8 (watu milioni 4.1).

Waziri Ummy amesema utafiti huo una umuhimu wa kipekee katika Wizara, kwani matokeo yake yatasaidia katika kutathmini hatua zilizofikiwa katika kupambana na magonjwa makuu manne yasiyoambukiza ambayo ni Saratani, magonjwa ya moyo, magonjwa ya mfumo wa hewa na kisukari.

katika kuhakikisha elimu dhidi ya athari ya tumbaku inaifikia jamii ipasavyo. Waziri Ummy ametoa maelekezo kwa Watendaji wa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na wadau wengine, kutengeneza au kupitia upya Sheria ya kudhibiti matumizi ya Tumbaku ili iendane na Mkataba wa Kimataifa wa kudhibiti matumizi ya Tumbaku na kuendelea kutoa Elimu kwa jamii kuhusu madhara yake;

Wizara ya Elimu kuendelea kuimarisha juhudi za kuwakinga wanafunzi dhidi ya tumbaku na bidhaa zake; Wizara ya mambo ya ndani kuhakikisha wale wanaokiuka miongozo kama vile kuendelea kuvuta sigara kwenye maeneo ya wazi wanachukuliwa hatua stahiki; Watengenezaji na wauzaji wa sigara, kufuata miongozo iliyowekwa na Serikali ikiwemo kutokuweka mabango au kutangaza na kuhamasisha matumizi ya sigara, kupitia bidhaa kama miamvuli, T-Shirts, kofia, na kutowauzia watoto wenye umri chini ya miaka 18; jamii kuacha kutumia tumbaku na bidhaa zake na Taasisi za Utafiti kufanya Tafiti za kuangalia vifo vitokanavyo na matumizi ya tumbaku ilikuwe na takwimu za nchi na siyo kutegemea za kutoka nje.


Share:

Sales Executive at CityPlan Consultants

Job Summary Builds business by identifying and selling prospects; maintaining relationships with clients Minimum Qualification: Diploma Experience Level: Executive level Experience Length: 2 years Job Description JOB VACANCY: CITYPLAN is constituted of two major significant operating companies engaged in services related to Lands, Environment, Human Settlement and Infrastructure systems. The two companies under CITYPLAN group (parent company) include CityPlan Consultants (T)… Read More »

The post Sales Executive at CityPlan Consultants appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

FIELD ELECTRICIAN at Capital Drill

Job Summary We have an immediate requirement for experienced, motivated and professional Electrician’s for the African market. You will have had an extensive background in the mining or contracting fields. Minimum Qualification: Diploma Experience Level: Senior level Experience Length: 5 years Job Description Capital Drilling is an international & highly respected mineral exploration drilling company with operations spanning over 3 continents, an… Read More »

The post FIELD ELECTRICIAN at Capital Drill appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya 12 na 13

Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0657072588(whatsapp) au 0768516188


ILIPOISHIA   
RPC akaifunua maiti moja na akamuonyesha Tomas maiti ya Selemani D iliyo chakaa kwa kupigwa risasi.
“Hawa jana tu walikuwa hai, wakisherekea pesa nyingi walizo zivuna kwa kumteka nabii Sanga. Ila sasa hivi wapo hapa hawajitambui. Wewe upo hai ila hii bastola yangu ina weza kukulaza na wewe hapa na ukajumuika na hawa wezako. Niambie ni wapi wezako walipo mpeleka nabii Sanga la sivyo, utaungana nao na wewe utaingizwa kwenye jokofu lile pale ukiwa maiti”


RPC alizungumza huku akimuwekea Tomas bastola ya kichwani na kumfanya Tomas kuanza kutetemeka mwili mzima huku akiona mwisho wa maisha yake sasa umefika, tena ana fia ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti.
   
ENDELEA
Kwa woga ulio mtawala Tomas akashindwa kuizuia haja ndogo na kujikuta akijikojolea. RPC hakulijali hizo zaidi ya kuendelea kuzungumza kwa ukali huku akiwa ameishikilia bastola hiyo.
“Kwa nini ulimteka nabii Sanga, nini alikufanyia ikiwa wewe ni mtu wake wa karibu?”
“Ehee…..!!”
“Nini alikufanyia?”
RPC alizungumza kwa ukali na kumfanya Tomas kuanza kukumbuka jinsi alivyo anza mahusiano na mke wa nabii Sanga. Kukolea kwa mapenzi yao kuliwafanya washiriki katika dhambi ya kumteka nabii Sanga ili wazuie mpango wake wa kumfungulia mgahawa na kumnunulia nyumba Magreth.
“Oya andaa hilo jokofu la hapo kwa ajili ya huyu mjinga, nina muua na siri itabaki kati yako mimi na wewe?”
RPC alizungumza huku akimtazama muhudumu wa Mochwari. RPC akaikoki bastola hiyo na kumfanya Tomas kuzidi kuweweseka. Japo ame fanya makosa, ila hatamani kabisa kufa.
“Nitasema ukweli”
Tomas alijikuta akiropoka na kumfanya RPC atoe simu yake mfukoni. Akaweka upande wa kurekodi sauti na kusubiria ukweli ambao Tomas ata ukiri.
“Zungumza nina subiria.”
“Ahaa miezi kadhaa iliyo pita nabii Sanga na mke wake walinipa jukumu la kuwatafutia eneo kubwa la kujenga mji, kule kigamboni. Jukumu la kusimamia mpango huo, alimkabidhi mke wake. Hivyo nilipata muda mwingi sana wa kuongozana na mke wake kwenda kutembelea maeneo mbali mbali ambayo nilikuwa nimeyapata.”
Tomas alizungumza huku akiendelea kutetemeka. RPC hakuishusha bastola yake, hii ni kuhakikisha kwamba Tomas ana zungumza kila kitu.
“Tulijikuta tukianza mahusiano ya kimapenzi na mwana mama huyo”
RPC akastuka sana ila hakuhitaji kuonyesha mstuko huo kwani ana hitaji kufahamu mambo mengi sana kutoka kwa Tomas.
“Tulifanya kwa siri sana. Kadri siku zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi penzi letu lilivyo zidi kuchanua. Kuna siku nabii Sanga alinipigia simu na kuniambia kwamba ana hitaji nimtafutie sehemu ya kufungua Mgahawa na nyumba ya kupanga maeneo ya Mikocheni. Alikuwa na mpango wa kumpangishia binti mmoja ambaye ni muumini pale kanisani kwake”
“Binti huyo ana itwa nani?”
“Magreth. Swala hilo nabii Sanga aliniomba nisimuambie mke wake kabisa. Ila kwa upande mmoja roho iliniuma kuona binti mdogo ana nunuliwa nyumba ya milioni mia tano. Nilimueleza mke wake na mkewe aka toa wazo la kumteka mume wake, hadi wiki ijayo ndio aachiliwe na watekaji ili aende nchini Nigeria kwenye kikao cha wachungaji na manabii”
RPC akajikuta akishusha pumzi taratibu. Katika miaka yote ya kuifahamu familia ya nabii Sanga, hakutarajia kwamba mke wa nabii huyo ipo siku ata fanya kosa kubwa kama hilo.
“Niliwatafuta vijana na nikawapa kazi hiyo na waliweza kuikamilisha kikamilifu”
Tomas alizungumza huku akiendelea kutetemeka kwa woga.
“Kwa hiyo mzizi wa tukio zima ni mke wa nabii SANGA?”
“Ndio”
Taratibu nabii RPC akashusha bastola yake na kuirudisha kiunoni mwake. Aka yahifadhi mazungumzo hayo ya Tomas kwenye simu yake na kuiweka mfukoni.
“Zirudishe hizo maiti”   
Nabii Sanga alimueleza mtu huyo anaye hudumia Mochwari kisha wakatoka katika chumba hicho. Akamuingiza Tomas kwenye gari lake, kabla ya yeye kuingia, akatafuta namba ya kijana wake mmoja na kumpigia.
“Ndio mkuu”
“Upo wapi?”
“Bado nipo nyumbani kwa nabii Sanga.”
“Hakikisha huyo mke wake hatoki kwenda eneo lolote”
“Kwa nini mkuu?”
“Hupaswi kunihoji kwa nini, fwata amri yangu”
“Samahani sana mkuu.”
RPC akakata simu na kuingia ndani ya gari.
“Huyo Magreth ana ishi wapi?”
“Ahaa sifahamu, ila wale vijana mulio waua ndio walimfwatilia msichana huyo na kufahamu ni wapi ana fikishwa na nabii Sanga. Ila kwa mimi sijui”
RPC akamtazama Tomas machoni mwake kwa sekunde kadhaa na kuamini kwamba anacho kizungumza ni kitu cha ukweli. Nabii Sanga akawasha gari hilo na kurudi makao makuu ya polisi. Akakabidhi Tomas kwa vijana wake na akarudishwa mahabusu. RPC moja kwa moja akapitiliza hadi ofisini kwake, akajifungia na kuisikiliza sauti ya Tomas jinsi inavyo toa maelezo hayo.
“Haki ya Mungu hawa wanawake hawaaminiki”
RPC alifikiria huku akitafakari ni jinsi gani anavyo weza kuvumbua mbele ya jamii kesi hiyo ambayo kwa namna moja ama nyingine ina weza kwenda kuligawanya kanisa la nabii Sanga huku naye akiwa ni miongoni mwa waumini wa kanisa hilo.
                                ***
    Magreth akabaki kama alivyo zaliwa huku akimtazama nabii Sanga anaye malizia kuivua suruali yake. Akatembea taratibu hadi kitandani. Akamlaza nabii Sanga chali,huku taratibu akimtazama.. Aibu aliyo kuwa nayo awali, yote ime muondoka. 


Magreth kwa jinsi alivyo pagawishwa na kiasi cha pesa alicho pewa na nabii Sanga, hakuona haja kumbania mzee huyo, huku moyoni mwake akiamini kwamba swala zima la kumpenda Evans litakuja hapo baade akiwa amesha weka kila kitu sawa. Mtanange wa wakati huu hakuwa wa kinyonge,  Nabii Sanga alizidi kuchanganyikiwa na kupagawa na penzi bichi kabisa la Magreth.
“Nitakupa kila utakacho kitaka Mage”
Nabii Sanga
“Kweli?”
“Haki ya Mungu vile, sijawahi kupata penzi tamu kama lako.”
“Uta nilinda dhidi ya mke wako?”
“Ndio baby, hawezi kukugusa”
“Niahidi”
“Nakuahidi, haki ya Mungu vile”
Magreth alifanya mahojiano hayo huku akijituma vzr. Kuokoka kwake hakukumfanya ashindwe kumpagawisha nabii Sanga. Hadi mzunguko una kwisha kila mmoja akajikuta akiwa ameridhika

“Niambie nini una hitaji nikufanyie?”
“Aahaa…kuna yule mgonjwa wangu kule hospitalini. Nilikuwa nina ombi moja”
“Ombi gani baby”
“Nimezungumza naye na amenieleza shida alizo pitia. Siku ile aliyo niokoa aliweza kuibiwa vyeti vyake vya kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu na siku ile aliondoka kwa rafiki yake na hakuwa na pakuishi. Nina omba nitakaopo hamia kwenye ile nyumba kigamboni, niweze kuishi naye”
Magreth alizungumza huku akiwa amejilaza kifuani mwa nabii Sanga
“Ahaha. Una muamini?”
“Kama aliweza kuyatoa maisha yake kwa ajili yangu. Nina muamini kwa maana wale Panya road siku zile wange nibaka na sijui ningekuwa kwenye maisha gani. Inawezekana ningekuwa nimesha kufa sasa”
“Nimekuelewa mke wangu. Basi akitoka hospitalini, utaishi naye. Ila hakikisha kwamba huni saliti”
“Kwa nini nikusaliti mpenzi wangu, ikiwa usichana wangu wewe ndio ume bahatika kuutoa. Au huniamini?
“Nakuamini tena sana kwa maana nime jionea jinsi gani ulivyo ”
“Nashukuru mume wangu”
“Leo usiku nitarudi kwangu, ila hakikisha kesho una kwenda kununua asset zote za ndani kisha zinapelekwa kwenye hiyo nyumba mpya.”
“Sawa mpenzi”
“Kuna rafiki yangu mmoja ana kampuni ya magari. Nitamuambia kesho akutafutie gari zuri na lenye hadthi na wewe”
“Asante sana mpenzi wangu, ila mimi siwezi kuendesha gari?”
“Ohoo usijali katika siku hizi ambazo nita kuwa hapa Tanzania, nitakufundisha gari, hadi nina ondoka nina imani utakuwa umesha mudu kuendesha”
“Sawa sawa mume wangu”


                                **********
‘Kama porini hakuweza kuonekana na majambazi tumewakuta wao wenyewe, je watakuwa wamemuaa? Hapana hajauwawa au wamemuachia?’
RPC aliwaza kichwani mwake huku akijaribu kujiongeza kutokana na mazungumzo ya Tomas.
‘Kama wamemuachia ata kuwa amekwenda wapi? Au ame fahamu kwamba mke wake ndio msaliti?’
‘Ila kama aliamua kumnunulia mwanamke nyumba ya milioni mia tano na kuhitaji kumfungulia mgahawa, nina imani kwamba atakuwa ana muamini sana huyo mwanamke na kumpenda’
‘Magreth…..Yaa Magreth anaweza kufahamu ni wapi alipo nabii Sanga. Ni lazima tumpate huyu msichna’
RPC baada ya kupata mwanga katika swala la kuto kumpata nabii Sanga, akanyanyuka kwa haraka na kuelekea mahabusu alipo fungiwa Tomas.
“Nileteeni mtu wa kuchora”
RPC alimuagiza bodyguard wake huku akimtazama Tomas ambaye amejikunyata kwenye kona ya chumba hicho.
“Nahitaji utuelezee sifa za Magreth. Si una mkumbuka kwa sura?”
“Ndio nina mkumbuka”
Polisi mwenye taaluma ya kuchora akafika eneo hilo. Tomas akaanza kuelezea muonekano wa Magreth.
“Ana sura nyembaba kiasi iliyo chongoka kwenye kidevu chake. Ana macho yaliyo kaa muundo kama wa yai, ila si makubwa. Ana pua ndogo ndogo kiasi na lipsi zake pia ni ndogo kiasi. Ni mrefu kama futi sita kasoro kidogo. Ana rangi ya chocolate fulani hivi.”
Kila alicho kieleza Tomas ndicho anacho kifanya mchoraji. Baada ya muda mfupi sura halisi ya Magreth ikapatikana kwenye karatasi ya mchoraji.
“Imekamilika?”
“Ndio mkuu”
RPC akaitazama picha hiyo ya Magreth, kweli ni mwanamke mzuri sana na anaye vutia. RPC akamgeuzia Tomas picha hiyo.
“Ndio huyu?”
“Ndio ndio huyo huyo wala hujakosea”
Tomas alizungumza wa kubabaika.
“Vijana wako hawakukuambia ni wapi walipeleleza hadi wakatambua anapo ishi?”
“Hapana hawakunijulisha kwani lengo lao kubwa ilikuwa ni nabii Sanga na waliweza kumfwatilia nabii Sanga alipo kuwa ana rudi kwake ndio waka mvamia na kumteka.”
RPC akaikunja vizuri karatasi hiyo yenye picha ya Magreth. Akaeleka kwenye kitengo cha askari wanao dili namitandano.
“Scan hii picha na unitafutie huyu binti”
“Sawa mkuu”
Kijana huyo aka iscan picha hiyo na kuiingiza kwenye computer yake na kuanza kutafuta picha hiyo ya Magreth kwenye mtandao. Haikuchukua muda maelezo yote kuhusiana na Magreth yakatokea katika computer hiyo. Imekuwa ni rahisi sana kwa askari hao kuipata kwani Magreth ni miongoni mwa  walio jisajili kwenye kitambulisho cha taifa hivyo taarifa zote zinazo muhusu yeye zipo hapo.
“Magreth Jonas Asinga”
RPC alisoma maelezo yanayo onekana kuhusiana na Magreth.
“Hembu tuma maelezo hayo kwenye mitando ya simu watupatie information za binti huyo. Nina imani mtandoa mmoja wapo utakuwa na information zake za mawasiliano.”
“Sawa mkuu”
Kijana huyo akaandika email kwa mitandoa mikubwa mmine ya mawasiliano , huku email hiyo ikwia huku ikiwa na wito wa kuomba data za mteja Magreth Jonas Asnga, ikiwemo namba yake ya simu. Baada ya dakika tano kijana hiyo akajibiwa email yake na mtandao wa simu ambao Magreth ana utumia.
“Waombe simu zote zilizo pigwa jana na leo watutumie”
Maombi hayo hayakuweza kukataliwa kwa maana yana tokea makao makuu ya polisi. Wakaanza kuorozesha audio za mazungumzo yote aliyo yafanya Magreth kwa siku ya jana na leo. Wakaanza kusikiliza mazungumzo hayo ambayo yanamuhusisha Magreth na nabii Sanga ambaye alimpa maelekezo ya kwenda kuchukua pesa ofisini kwake. Wakazidi kuendelea kusikiliza mazungumzo hayo hadi jinsi MagreLth aivyo wasiliana na majambazi hao na kuwajulisha amefika Mkinga.
    Mazungumzo ya siku ya leo kati ya nabii Sanga na muhasibu wake akimuomba amfwate sehemu alipo, ikampa picha RPC ya kuweza kufahamu kwamba nabii Sanga yupo sehemu gani na yupo sehemu salama. Ila kutokana ni ahadi ambayo alitoa kwa wananchi kwamba jeshi la polisi lita hakikisha kwamba lina mrudisha nabii Sanga salama salmini mikononi mwa familia yake. Ikamlazimu RPC kuandaa kikosi cha vijana wake wanne na kuianza safari ya kuelekea nyumbani kwa Magreth, huku zoezi hilo likifanyika kwa siri sana pasipo askari wengine kuweza kufahamu ni kipi RPC wao ame kigundua.


 ==>>SIN -Sehemu ya 13  
“Huu ndio mtaa anao ishia huyo binti?”
RPC aliwaambia vijana wake huku wakitazama mtaa huu wa uswahilini wenye mchanaganyiko wa watu wa kila aina.
“Msichana mwenyewe anafanania hivi?”
RPC alizungumza huku akiwaonyesha picha ya Magreth iliyo chorwa kwenye karatasi hiyo.
“Huyu ame fanya kosa gani mkuu?”
“Ina sadikika huyu ndio yupo na babii Sanga?”
“Mkuu unataka kuniambia kwamba huyu binti ndio alite mteka nabii Sanga?”
“Hapana, hapa inaonekana nabii Sanga alisha achiwa na watekaji, ila akaamua kuelekea kwa kimada wake kujificha”
“Mmm!! Sasa kwa nini asiende kwake au kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi?”
“Hilo ni swali ambalo tutalipata mara baada ya kuwapata wote wawili. Hembu waulize hao watoto juu ya picha hiyo”
“Sawa”
Askari mmoja aliye valia nguo za kirai. Akashuka kwenye gari hilo na kuwasogelea watoto wanao cheza pembezoni mwa barabara hiyo ya vumbi.
“Mambo”
“Poa shikamoo”
“Marahaba. Nina swali nahitaji kuwaliza”
“Uliza tu?
“Muma mfahamu dada huyu?”
Askari huyo aliwaonyesha watoto hao picha ya Magreth, wenye miaka kati ya sita hadi kumi.
“Ndio tuna mfahamu ana itwa dada Mage”
“Ana ishi wapi?”
Watoto hawa wakatazamana, kisha mmoja wao akaonyesha ishara ya kuhitaji kupewa pesa. Askari huyu akatoa noti ya shilingi elfu tano mfukoni mwake na kuwakabidhi. Mtoto huyo mwenye kimo kirefu kuliko wezake wote, akaipokea pesa hiyo.
“Ana kaa pale kwa bi Ngedere. Ile nyumba yenye kibaraza mbele na ngazi?”
“Ile nyumba yenye matairi mbele na wale wamama walio kaa??”
“Ndio”
“Sawa asanteni”
Askari huyo akarudi kwenye gari.
“Daa kweli kazi ipo bosi, yaani hadi watoto wameanichomoa pesa ya kuelekezwa tu”
“Hahaahaa, ni wapi alipo sema?”
Askari huyo akawaonyesha wezake nyumba hiyo. Taratibu wakaegesha gari hilo kwenye hiyo nyumba na wakashuka askari wawili ambao wote wamevalia nguo za kiraia. Gari hilo iana ya Toyota VX V8 likawastua sana wapangaji wa nyumba hiyo walio kuwa wamekaa kibarazani.
“Habari zenu?”
“Salama”
“Tume mkuta Magreth?”
Wapangaji hawa wkatazamana, katika siku mbili tatu hizi Magreth amekuwa akiletwa na magari ya kifahari jambo ambalo lime zua maswali mengi kwa wamama hao wanne.
“Ndio yupo”
“Ahaa muna weza kutusaidia kutuonyesha chumba chake?”
“Mmm shosti yetu amekuja kufumaniwa nini?”
Mama Boka aliwanong’oneza kwa sauti ndogo wezake hao kwa maana wana sikia sauti ya mwanaume katika chumba cha Magreth ila hawajamuona mwanaume ambaye yupo ndani humo.
“Ahaa ingieni humo ndani, chumba cha pili, mkono wa kulia ndio chumba chake”
“Tuna shukuru”
“Ila nyinyi ni kina nani?”
“Ni watu wema kabisa musiwe na mashaka”
“Mmmm haya”
Askari hao wakaingia ndani humo, wakasimama kwenye mlango wa Magreth na kusikilizia miguno ya kimahaba inayo tokea ndani humo.
“Gonga mbona una shangaa?”
“Wapo kwenye starehe zao bwana”
“Sisi tupo kazini. Ngoja nigonge”
Askari huyo akaanza kugonga kwa nguvu hadi Magreth na nabii Sanga ambao wapo katikati ya mapenzi mazito wakastuka.
“Nani huyo?”
Nabii Sanga aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka.
“Atakuwa ni mama mwenye nyumba. Kwani sauti yangu ina sikika hadi huko nje?”
“Sijajua, ila mbona naona ina sikika hapa hapa”
“Ngoja”
Magreth akajichomoa ,. Akashuka kitandani, akajifunga tenge na kufungua mlango huo huku akiwa na jazba kubwa, na amepania kama ni mama mwenye nyumba basi ata mpatia jibu litakalo mtingisha mwana mama huyo mwenye maneno mengi. Magreth akastuka sana mara baada ya kukutana na sura za wanaume ambao haja wahi kuwaona hata siku moja.
“Wewe ndio Magreth?”
“Ndio ni mimi. Ny….i….nyi ni kina nani?”
Magreth aliuliza huku woga ukiwa umemtawala. Mahojiano hayo yakamfanya nabii Sanga kutafuta suruali yake nakuivaa kwa haraka huku kichwani mwake akihisi kwamba watu hao ni majambazi.
“Tume mkuta nabii Sanga?”
Swali hilo lika wachanganya kabisa, nabii Sanga na Magreth kwani watu hao hawajajitambulisha hadi sasa hivi.
“Ahaa nyingi ni kina nani?”
Ikamlazimu Magreth kuuliza swali hilo kabla ya kujibu swali alilo ulizwa.
“Sisi ni maofisa wa polisi kutoka kituo cha kati”
“Waache waingie”
Nabii Sanga alimuambia Magreth na kumfanya ageuke na wakatazamaana huku Magreth akiwa na mshangao mkubwa sana.
“Waache wapite”
“Karibuni”
Askari hao wakaingia na kumkuta nabii Sanga akiwa ana vaa shati lake
“Habari yako mzee”
“Salama. Tumekuja kukuchukua na kukuweka mikono salama”
“Hapa pia ni mikono salama. Ila nina elewa nini munataka kufanya. Sasa hivi ni saa kumi na mbili, acheni kigiza kiweze kuingia nami nitatoka ndani humu”
“Ila muheshimiwa, tupo hapa na mkuu wetu na ametoa agizo la sisi kukuchukua na kukupeleka kwenye gari lake lipo hapo nje”
“Nendeni mukamuite mkuu wenu”
“Ahaa kwa nini?”
“Nyinyi nendeni mukamuite yeye, ndio nahitaji kuzungumza naye”
Askari mmoja akatoka ndani humo na kurudi kwenye gari. Akamueleza RPC nini anacho hitaji nabii Sanga.
“Waondoeni hao wamama hapo barazani, sihitaji wafahamu juu ya uwepo wangu mtaani hapa?”
“Sasa tuta fanya nini mkuu”
“Fanyeni chochote.  Nyinyi ni askari hakikisheni kwamba wana ondoka eneo hilo”
Askari hao watatu wakajishauri na kushuka kwenye gari hilo. Wakawasogelea wana mama hao wanao endelea kutazama kila kinacho endelea na kila mmoja ana hamu ya kufahamu ni nini kinacho endelea kwa mpangaji mwenzao.
“Sisi ni maofisa polisi. Muna ishi humu ndani?”
Wamama hao wakastuka kidogo huku wakiwatazama askari hao.
“Ndio”
“Basi kila mmoja aingie chumbani kwake na asidhubutu mtu kuchungulia”
“Kwani kuna nini?”
“Mama hatuna muda wa kutangaza au kukueleza kuna nini. Ingieni ndani”
Askari mmojaa alizungumza kwa ukali sana na kuwafanya mama Boka na wezake wanyanyuke huku wakikunja mkeka walio kuwa wameukalia. Wakaingia ndani huku wakiwa na hofu kubwa. Askari walipo hakikisha kwamba hali imekuwa shwari, bodyguard wake akamfungulia mlango na akashuka kwenye gari hilo na kuingia ndani. Nabii Sanga aka simama na kuepeana mkono na RPC kwani ni watu wanao fahamiana kwa muda mrefu na pia wana heshimiana.
“Naomba mutupishe”
RPC alizungumza na vijana wake wakatoka na kusimama kwenye kordo hiyo kuimarisha ulinzi.
“Huyu ni Mage, binti ambaye aliweza kujitolea kunipa msaada wa kipesa kipindi nilipo kuwa nimewekwa kizuizini na majambazi”
“Ahaa sawa mzee. Nina litambua hilo kwa maana tume fwatilia mazungumzo ya simu ya binti. Hayo mazungumzo ndio yameweza kutusaidia sisi kuweza kufika hapa”
“Sawa sawa”
“Tumekuja kwa jambo moja tu. Tunahitaji tukupeleke nyumbani kwako kwa maana sehemu hii sio salama kabisa.”
“Sawa hilo halina shaka. Ila nahitaji huyu msichana asi sumbuliwe kwa chochote na wala asiweze kuitwa kituoni kwa mahojiano”
“Sawa sawa”
“Mage kuwa na amani na kesho hakikisha kwamba una fanya ule utaratibu nilio kuagiza uweze kuufanya”
“Sawa baba”
“Kwa heri”
Nabii Sanga na RPC pamoja na vijana wake wakatoka ndani hapo na moja kwa moja wakaeleka katika gari na kuondoka. Magreth akashusha pumzi na kujitupa kitandani, kwani uwepo wa maaskari hao umemfanya awe katika wakati wa mashaka. Ila alipo kumbuka kwamba ana kiasi kikubwa cha pesa benki, basi mawazo na matatizo hayo ya polisi yakamuondoka kabisa kichwani mwake.
“Sasa mimi ni tajiri”
Magreth alizungumza kwa furaha. Mlango wake ukagongwa na akasikia sauti ya mama Boka ikimuita.
“Nakuja”
Magreth alizungumza huku akishuka kitandani. Akajifunga tenge lake vizuri na kufungua mlango.
“Ehee upo salama wewe?”
“Ndio kwa nini?”
“Hawa polisi wamekuja kufanya nini hapa?”
“Hahaa mbona muna mashaka hivyo au mume hisi nime tekwa na watu ?”
“Weee!! Mwanzo tulihisi kwamba ume kuja kufumaniwa. Ila walipo tuambia tuingia ndani na kujifungia, hapo ndipo matumbo yalipo tupata moto”
“Kweli shosti yetu tulijawa na wasiwasi mwingi sana. Haya tuambie ni nini kinacho endelea?”
Mama Amina naye aliuliza.
“Ngoja kwanza niwashukuru majirani zangu kwa kuishi nami kwa amani japo tulikwaruzana katika maswala ya zamu za usafi na ununuzi wa luku, ila yote katika yote. Mungu yeye pekee ndio anaye fahamu nini tunacho pitia kwenye haya maisha”
“Mbona una ongea hivyo?”
Mama mwenye nyumba aliuliza huku akitokea mlango wa uwani na kuwafanya wapangaji hao walio simama kwenye mlango wa Magreth kumshangaa.
“Kesho nina hamia Kigamboni. Kuna nyumba yangu nimenunua kule”
Magreth aliwadanganya wezake hao katika swala zimala kununua nyumba.
“Mage ume nunua nyumba!!?”
“Ndio mbona muna shangaa au sina hadhi ya kununua nyumba?”
“Mmmm kwa kazi gani ulio kuwa nayo? Hembu acha kuwaongopea wezako na wewe”
Mama mwenye nyumba alizungumza kwa kejeli.
“Hahaa, wewe baki hapo hapo kwenye hili banda lako la kuku”
“Hahaaa!! Banda la kuku, ulitumwa kujakukaa hapa kupanga?”
Bi Ngedere alizungumza kwa hasira kwani hakupenda nyumba yake iweze kudharauliwa namna hiyo.
“Mage hembu achana naye. Tupe siri ya mafanikio yako kwa maana siku mbili hizi tumekuona una shushwa kwenye magari ya kifahari na wala hatukuoni jikoni ukijumuika nasi katika swala zima la kuchoma maandazi”
“Ni kweli jamani, kesho mimi nina hama. Haya yaliyo tokea humu ndani kwangu sinto weza kuwaambia. Leo mumesha pika?”
Magreth alibadili mada kwa kuwaliza maswali.
“Mimi nimepika toka mchana”
“Mimi nasubiri saa mbili mbili nisonge ugali nile na wanangu”
“Mimi nita nunua maandazi tu ninywe na chai.”
“Mimi bado sijapika”
“Bi Ngedere na wewe?”
“Na mimi nini, una pesa ya kunipa nikanunue chakula?”
“Ahaa…maneno yote ya nini mama angu. Hivi wewe mama una shindwa kuwa na kinywa kizuri cha kuzungumza?”
“Babuu weweee nikiwa na kinywa kizuri nita faidika na nini?”
“Haya nisamehe mimi. Jamani nisubirini”
Magreth akaingia ndani na kuchukua laki moja na nusu na kutoka nayo nje. Akawapa wapangaji wezake wanne kila mmoja elfu thelethini.
“Jamani hizo mutanunua mukipendacho usiku huu”
Wapangaji hao wakajawa na furaha sana, huku wengine wakimuona Magreth ndio mkombozi wao kwani baadhi yao tayari wamesha anaza kuwakimbia vijumbe wa michezo yao wanayo cheza kila siku kwa kukosa pesa za kutoa.
“Wewe mama utakula jeuri yako. Hata mia sikupi na kesho nitakagwa vitu vyangu vyote vya ndani na hata kijiko sikupi. Muangalie ndio maana Mungu alikunyima kimo kirefu ndio maana akili zako zipo kama kimo chako”
Maneno ya Magreth yakawafanya wapangaji wezake hao kucheka kwa dharau huku wakigongeana mikono na kumfanya mama mwenye nyumba ajisikie vibaya sana.
                                ***
“Kile mulicho kiona pale nyumbani kwa yule binti musi mueleze mtu yoyote”
Nabii Sanga alizungumza huku gari hilo la RPC likizidi kuchanja bunga kueleka nyumbani kwake.
“Hatuto mueleza mtu”
RPC alijibu huku akiwa amekaa siti ya mbele, pembeni kabisa ya dereva.
“Nashukuru kusikia hivyo.”
“Upo salama lakini?”
“Ndio nipo salama”
Wakafika nyumbani kwa nabii Sanga. Wakaelekea moja kwa moja sebleni na kumfanya mtoto wa nabii Sanga kumkimbilia baba yake na kumkumbatia kwa nguvu. Mfanyakazi wake wa ndani naye akafanya hivyo alivyo fanya binti huyo. Kelele za furaha zinazo sikika sebleni zikamfaya mrs Sanga kukurupuka ndani kwake na kukimbilia sebeeni. Mapigo ya moyo yakamstuka mara baada ya kukutanisha macho yake uso kwa uso na mume wake ambaye hajaonyesha sura yoyote ya kumchangamkia. RCP akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa pingu huku akimtazama mrs Sanga anaye shuka kwenye ngazi huku akilazimisha tabasamu la kinafki kwani shida zote zilizo tokea katika siku mbili hizi yeye ndio chanzo.
                                                                                                ITAENDELEA
Haya sasa, Nabii Sanga amesha rudi nyumbani kwake, moyoni mwake ana ufahamu ukweli kwamba mke wake ndio adui namba moja. RPC ana toa pingua mfukoni je ata mfunga mrs Sanga na kuondoka naye kama mtuhumiwa? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 14.

 


Share:

Relationship Manager (Chinese Portfolio)

Relationship Manager (Chinese Portfolio) Job Purpose To evaluate Chinese portfolio credit risks associated with lending at the client interface, with the primary objective to contain credit risk within acceptable parameters. Main Responsibilities Provision of direct credit evaluation services at the customer interface. Identify credit and risk management requirements at the source of the deal negotiation/ business proposal. Conduct credit… Read More »

The post Relationship Manager (Chinese Portfolio) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Opportunities at DUCE – Various Posts

Overview The Dar es Salaam University College of Education (DUCE) is a Constituent College of the University of Dar es Salaam established in 2005.The main functions of the College as stipulated in the Dar es Salaam University College of Education Charter and the Rules of 2010, are to provide integrated teaching, research and public service. The College invites… Read More »

The post Job Opportunities at DUCE – Various Posts appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WAZIRI WA MADINI AIMWAGIA SIFA GGML KUWEKEZA KIMKAKATI GEITA



Waziri wa Madini, Dotto Biteko akielekea kukagua soko kuu la Geita huku akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Josephat Maganga (kulia) pamoja na maofisa wengine wa mji wa Geita.
Waziri wa Madini, Dotto Biteko akitoa pongezi za serikali kwa GGML baada ya kutembelea miradi hiyo. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Josephat Maganga wakati kushoto ni baadhi ya maofisa wa mji wa Geita. 
Waziri wa Madini, Dotto Biteko akitoa pongezi za serikali kwa GGML baada ya kutembelea miradi hiyo.



Makamu wa Rais anayeshughulikia Maendeleo Endelevu katika Kampuni ya GGML, Simon Shayo akizungumza katika ziara ya Waziri wa Madini, Dotto Biteko aliyetembelea miradi ya kampuni hiyo inayotekelezwa chini ya mpango wa kusaidia jamii (CSR) mkoani Geita.


****
Na Mwandishi wetu - Geita

Waziri wa Madini, Dotto Biteko ameipongeza Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya dhahabu - Geita (GGML) kwa kuwa mdau wa mfano katika kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Geita.

Biteko ametoa kauli hiyo jana katika ziara fupi aliyoifanya mkoani Geita na kukagua miradi inayotekelezwa na Kampuni ya GGML chini ya mpango wake wa kusaidia jamii (Corporate Social Responsibility) katika Mji wa Geita.

Aidha, alisema lengo la Serikali ni kuona maisha ya watu katika maeneo yote yenye rasilimali madini, ikiwemo Geita yanabadilika kiuchumi.

“Nimefurahishwa na namna ambavyo Serikali katika Mkoa wa Geita inavyosimamia ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye sekta ya madini. Tayari tumeshafikia lengo la kukusanya zaidi ya Sh bilioni 400 kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 2020 kutoka kwenye sekta hii, na sehemu kubwa ya makusanyo haya imetoka Geita, hususan GGML. 

“Inatia moyo sana kuona kwamba sekta hii sasa inachangia zaidi ya asilimia 5 ya uchumi wa nchi yetu. Lengo ni kuhakikisha kwamba sekta ya madini inachangia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025,’’ alisema Biteko.

Mojawapo ya miradi ambayo ilikaguliwa na waziri huyo katika ziara yake ni ujenzi wa Kanda maalumu ya uwekezaji 'Special Economic Investment Zone' ambao utasimamiwa na Mamlaka ya ukanda maalumu wa Uwekezaji (EPZA) na Halmashauri ya Mji wa Geita.

Pia alitembelea miradi mingine ya kimkakati inayofadhiliwa na GGML, ikiwemo ujenzi wa Soko Kuu la Geita Mjini na soko la Katundu. 

Aidha, Makamu wa Rais anayeshughulikia Maendeleo Endelevu katika Kampuni ya GGML, Simon Shayo alisema utekelezaji wa miradi ambayo imetembelewa na waziri Biteko ni sehemu ya mpango wa mwaka 2018/19 unaoenda sambamba na mojawapo ya tunu za kampuni hiyo inayoelekeza kwamba jamii inayozunguka shughuli zake sharti ifaidike kwa uwepo wake.

Alisema GGML ambayo ni sawa na kampuni-raia inawajibika ipasavyo kwa jamii kwani hutumia Sh bilioni 9.2 kila mwaka kugharimia miradi ya jamii katika mkoa wa Geita na kuifanya kampuni hiyo kuwa ya kipekee kutokana na mchango mkubwa inayotoa kusaidia jamii.

“Kama Kampuni-raia ndani ya Tanzania, GGML iliyoko chini ya AngloGold Ashanti itaendelea kuunga mkono na kusaidia jamii zinazotuzunguka. Utekelezaji wa miradi ya CSR na shughuli zingine kama hizo ni ushahidi wa wazi kwamba kampuni, serikali na jamii zikifanya kazi pamoja zinaweza kuboresha maisha ya watu kupitia uwekezaji endelevu katika miundomuni ya biashara na huduma.

“Tunataka kuona maisha ya mtu wa kawaida katika jamii yetu yakiwa bora zaidi kupitia uwekezaji endelevu wa Kampuni yetu”, alisema.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2018, GGML iliwezesha utekelezwaji wa miradi kadhaa kupitia mpango wake wa kuwekeza katika jamii. 

“Miradi hii inajumuisha; uwekaji wa taa za barabarani katika mji wa Geita, ujenzi wa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti, ujenzi wa soko la kisasa Geita mjini, umaliziaji wa majengo zaidi ya 600 ya afya na elimu na ujenzi kamili wa shule tatu mpya na vituo vya afya vinne.

“Pia GGML imetenga kiasi cha Sh bilioni 18 kwa ajili ya miradi mingine kama hiyo katika kipindi cha kati ya mwaka 2019/20 na 2020/21.
Share:

Jobs at AMREF Health Africa Tanzania – Various Posts MBEYA and DSM

Overview Amref Health Africa is an independent, non-profit, non-governmental organization (NGO) whose mission is “to improve the health of people by partnering with and empowering communities and strengthening health systems”. Amref Health Africa has over 1000 employees throughout Africa with its headquarters in Nairobi, Kenya. Amref Health Africa has offices in Tanzania, Ethiopia, Kenya, Uganda, and South Africa,… Read More »

The post Jobs at AMREF Health Africa Tanzania – Various Posts MBEYA and DSM appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

BODI YA MAZIWA NA WADAU KUWEKA MIKAKATI YA KUZALISHA MAZIWA YA KUTOSHA NCHINI


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Mpina akizungumza na wandishi wa habari na wadau wa maziwa wakati wa kilele cha wiki ya maziwa jijini Dodoma.
Sehemu ya Wadau wa maziwa wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Mpina wakati wa kujadili mambo mbalimbali ya sekta ya maziwa katika wiki ya maziwa ambayo kitaifa imefanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe Patrobas Katambi,aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akizungumza na wadau wa maziwa wakati wa kilele cha wiki ya maziwa jijini Dodoma.
Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dk Sophia Mrote akizungumza na wadau wa bodi ya maziwa wakati wa ufungaji wa kilele cha siku wiki ya maziwa.
Mwenyekiti wa Baraza la wadau ni Bi.Catherine Dangat,akizungumza na wadau wa maziwa wakati wa kilele cha wiki ya maziwa jijini Dodoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (wa pili kushoto) akinywa maziwa kuashiria kufunga wiki ya maziwa nchini sambamba na Viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi (wa tatu kutoka kushoto) na Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dk Sophia Mrote (katikati).
..............................................................................................
Na. Mwandishi wetu, Dodoma
SERIKALI imeitaka Bodi ya Maziwa na Wadau wote wa maziwa kuweka mkakati wa pamoja wa kuhakikisha ndani ya miaka miwili ijayo Tanzania inazalisha maziwa ya kutosha ili kusiwe na haja ya kuagiza maziwa nje Nchi.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina leo jijini Dodoma wakati akihitimisha wiki ya Maziwa duniani ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka wenye viwanda vya kusindika maziwa kuongeza uzalishaji zaidi.

Mhe. Mpina amesema kiwango cha kunywa maziwa kwa watanzania kinapaswa kuwa Tani 200 lakini hadi sasa kiwango kinachonyweka ni tani 54 hivyo kuwataka watanzania kuongeza unywaji wa maziwa kwani husaidia kuboresha kinga za mwili na kukuza ubongo.

Mhe. Mpina amesema kuwa ili kuhakikisha uzalishaji wa maziwa unaongeza serikali imewaunganisha wawekezaji wa maziwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ili waweze kupatiwa mifugo sambamba pia na kutoa msamaha wa kodi kwenye sekta hiyo.

" Ndugu zangu ni muda sasa wa kuhamasisha unywaji wa maziwa nchini kwani Maziwa ni mlo kamili hasa katika kuimarisha mifupa na kuweka ubongo sawa, na yana viini lishe vya kuimarisha pia kinga za mwili”, amesisitiza Mhe. Mpina.

Aidha Mhe. Mpina ameweka wazi kuwa Tanzania ni Nchi ya pili kwa kuwa na Ng'ombe wengi nyuma ya Ethiopia kuwa Tanzania ina Ng'ombe Milioni 33 lakini Ng'ombe wanaozalisha maziwa ni Milioni 1.9 na kiwango cha maziwa kinachozalishwa ni Bilioni tatu ambacho ni kidogo kulinga na mifugo tuliyinayo.

Mhe. Mpina amesema kwa sasa kuna programu ya kuhamasisha unywaji wa maziwa mashuleni kwa baadhi ya mikoa na kusisitiza sasa ni wakati wa kila mkoa kuweka mkakati wa kuhimiza unywaji wa maziwa kwenye kila shule ndani ya mikoa yao.

Pia Mhe. Mpina ametoa wito kwa wawekezaji nchini kutumia fursa ya kuwekeza kwenye usindikaji wa maziwa kwani viwanda vilivyopo kwa sasa vinazalisha asilimia 23 tu ya maziwa na vipo 99.

Mhe. Mpina amehitimisha kwa kuelekeza Halmashauri zote nchini kuzingatia bei elekezi ya chanjo ya mifugo na atakayekaidi hatua kali za kisheria na kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake

Naye Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dk Sophia Mrote amesema wiki ya Maziwa imekua ya manufaa sana kwani wiki hii waligawa Lita 1650 kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma.

Dkt. Mrote amesema kuwa ndani ya wiki hiyo ya maziwa walikutana wadau wote wa maziwa na kujadili mambo mbalimbali yatakayoweza kuivusha sekta hiyo ili kufikia hatua ya kuzalisha maziwa mengi na kukuza soko hilo hadi nje ya mipaka ya Nchi.


Share:

NCCR Mageuzi kutoa ratiba ya uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Madiwani Wiki Ijayo

Baada ya CHADEMA kuwataka watangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais ndani ya chama hicho wajitokeze, NCCR Mageuzi nao wamesema kuwa wanatarajia kutoa ratiba ya uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Madiwani wiki ijayo, na kuiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutenda haki katika uchaguzi ujao.

Pia, chama hicho kimefungua milango kwa chama chochote cha siasa nchini, ambacho kipo tayari kushirikiana ili kuiondoa Serikali ya Chama cha Mapinduzi madarakani.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alibainisha hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma.

Mbatia alisema, tayari ameshamwagiza Katibu Mkuu wa chama hicho kutoa ratiba ya uteuzi wa wagombea ndani ya chama mapema wiki ijayo.

“Nitoe wito kwa vijana na wale wote wenye sifa, kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali, katika uchaguzi huu, nafasi za urais Tanzania bara na Zanzibar, ubunge, wawakilishi pamoja na zile za udiwani,” alifafanua Mbatia.

Alisema, katika uchaguzi mkuu mwaka huu, chama hicho kipo tayari kushirikiana na vyama vingine vya siasa kwa maslahi ya taifa.
 
“Sisi tupo tayari kushirikiana na chama chochote kile cha siasa kwa maslahi ya mama Tanzania, kwani hata salamu yetu inasema kwa pamoja tutashinda,” alisema Mbatia.


Share:

Kinana amuomba radhi Rais Magufuli kutokana na kauli zake

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahaman Kinana, amemwomba msamaha hadharani Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Dk. John Magufuli.

Kiongozi huyo ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa CCM wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne, alitangaza hadharani kuomba msamaha huo kwa makosa aliyoyatenda kipindi chake cha uongozi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha jana, Kinana alisema akiwa kiongozi anaamini kuwa yapo mambo aliyoyafanya ambayo yaliwakwaza viongozi wengine akiwamo Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuli, ambaye ni Rais wa Tanzania na anaamini atamsamehe.

“Naamini ilifika wakati nikakereka na kusema maneno ambayo yanaweza kuwa siyo mazuri, nimekaa na kutafakari sasa, namuomba radhi Mwenyekiti wa CCM, Magufuli,” alisema Kinana na kuongeza:

“Kama kiongozi ni kweli naamini ilifikia hatua nikatofautiana na wenzangu ama niliwakera wenzangu na pia, hata kiongozi wangu, Mwenyekiti wa Chama, kiukweli ninamwomba radhi.”

Akiwa Arusha, Kinana pia alikutana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Zelote Steven na Katibu wa Mkoa wa huo, Mussa Matoroka na kuwaeleza kuwa pamoja na kustaafu, ataendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali ndani na nje ya chama chake.

“Mimi kwa sasa nimestaafu uongozi, ninamshukuru Mungu na ninaendelea kujifunza, kusoma vitabu na kufanya mazoezi na niko tayari kuendelea kutoa mchango wangu wa hali na mali ndani na nje ya chama,” alisema.

Desemba 13, mwaka jana, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), iliagiza makada watatu wa chama hicho akiwamo Kinana, waitwe na wahojiwe na Kamati ya Maadili na Usalama, baada ya kutuhumiwa kwa makosa ya kufanya mambo kinyume na taratibu za chama.

Kamati Kuu, iliwaadhibu viongozi hao na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Memba, kufukuzwa uanachama kwa kukiuka maadili ya chama hicho.

Kadhalika, Makamba alisamehewa huku Kinana akipewa barua ya onyo ikiwamo kuwa chini ya uangalizi kwa miezi 18 na kuzuiliwa kujihusisha kugombea nafasi yoyote ndani ya chama hicho.


Share:

LIVE: Rais Magufuli Mgeni Rasmi Katika Mkutano Mkuu Wa Uchaguzi Wa Chama Cha Walimu Tanzania

LIVE:  Rais Magufuli Mgeni Rasmi Katika Mkutano Mkuu Wa Uchaguzi Wa Chama Cha Walimu Tanzania


Share:

Trump ashtakiwa kuhusiana na mashambulizi ya polisi dhidi ya waandamanaji

Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Marekani yamewasilisha kesi dhidi ya rais Donald Trump baada ya vikosi vya usalama kuwarushia mabomu ya moshi waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa amani nje ya Ikulu ya White House. 

Umoja wa Uhuru wa Raia wa Marekani, ACLU pamoja na makundi mengine, yalimshtumu rais huyo na maafisa wakuu serikalini kwa kukiuka haki za waandamanaji hao waliokuwa wakiendesha kampeni inayojulikana kama maisha ya watu weusi ni muhimu pamoja na waandamanaji wengine wa kibinafsi.

 Mkurugenzi wa masuala ya kisheria katika umoja huo wa ACLU Scott Michelman amesema kuwa matamshi ya ''kiuhalifu'' ya Trump dhidi ya waandamanaji hao kwasababu anatofautiana na maoni yao yanatikisa msingi wa mpangilio wa kikatiba nchini humo. 

Waandamanaji hao wamekuwa wakifanya maandamano nchini humo katika siku za hivi karibuni kuelezea kughadhabishwa kwao na kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd mikononi mwa polisi katika jimbo la Minnesota.

-DW


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger