Monday 30 March 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu March 30





















Share:

Sunday 29 March 2020

Ngoma Mpyaa : MWANASELEWA Ft NTEMI 'Ng'wana Kang'wa' - MILEMO

Nakualika kutazama video mpya kutoka kwa Mwana Selewa amemshirikisha Ntemi 'Ng'wana Kang'wa' kutoka Kahama Mkoani Shinyanga inaitwa Milimo...Tazama Video hapa chini
Share:

SUMAYE AKABIDHIWA RASMI KADI YA UANACHAMA CCM


Na .Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Dkt BASHIRU ALLY leo  Machi 29,2020 amemkabidhi rasmi kadi ya uanachama wa chama hicho Waziri mkuu mstaafu FREDRICK SUMAYE huku akiahidi kufanya sherehe ya kumpokea mwanachama huyo mara baada ya tishio la Virusi vya Corona litakapoisha.

Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dodoma ambapo amesema siku zote chama kinapopokea mwanachama mpya kinafanya sherehe lakini kutokana na uwepo wa virusi hivyo wamesitisha sherehe hiyo kwa sasa.

 Amesema SUMAYE amekabidhiwa kadi Dodoma kwa sababu Chama hicho ni chama cha kitaifa nasio chama cha watu.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi SUMAYE amesema amefurahi amerudi rasmi kwenye chama chake na sasa ni mwanachama kamili.

Amesema wakati anaondoka CCM alisema anaondoka akiwa hana chuki na chama,hana chuki na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wakati huo dokta JAKAYA KIKWETE na hana chuki na mgombea aliyeteuliwa wakati huo dokta JOHN MAGUFULI 

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM MIZENGO PINDA amesema amefurahi kwa kuwa wakati wanaondoka CCM alipata shida sana.


Share:

Mfanyabiasha Afariki Dunia Kwa Mshtuko Wa Kuunguliwa Maduka Samunge Jijini Arusha

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mtu mmoja amefariki dunia Mara baada ya moto mkubwa kuzuka na kuunguza soko la Samunge jijini Arusha baada ya kufika na kushuhudia maduka yake yote yakiwa yameketea na moto.


Akiongea na waandishi wa habari Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo 

Aidha wakati zoezi la kuzima moto likiendelea mtu  mmoja aliyefahamika kwa majina ya James Peter Temba, 57 Mfanyabiashara na mkazi wa Moshono ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa vibanda vilivyoungua ndani ya Soko hilo, alifika eneo hilo na kukuta vibanda vyake vimeungua.

Kaimu kamanda Koka  alieleza kuwa majira ya saa 23:30hrs, katika soko la Samunge, lililopo Mtaa wa NMC, kata ya Kati, Tarafa ya Themi, katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, moto ambao bado chanzo chake hakijajulikana uliwaka na kuteketeza vibanda vya Soko hilo ambavyo idadi na thamani yake bado haijajulikana. 

Ameeleza kuwa vibanda hivyo vilikuwa vinamilikiwa na wafanyabiashara wa Soko hilo ambavyo vilijengwa kwa Mabati, Mbao na Mabanzi. Mara baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Wananchi walifanikiwa kuzima moto huo ambao haukuleta madhara kwa binadamu. 

Mtu huyo alipata mshtuko na kuanguka chini na kuzimia ambapo alichukuliwa na kupelekwa katika Hospital ya Mkoa ya Mount Meru na alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu. 

Hata hivyo Uchunguzi unaendelea ili kubaini thamani halisi ya mali zilizoungua pamoja na chanzo cha moto huo. 

Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi wa Daktari. 

Natoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapoona majanga kama haya ya moto kwa Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kudhibiti matukio kwa haraka kabla ya kuleta madhara makubwa. 

 Alitoa wito kwa wananchi na kuwaomba  pamoja na wafanyabiashara kuwa watulivu wakati vyombo vya Ulinzi na Usalama vikifanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo halisi cha tukio hilo


Share:

Mbunge wa Moshi Vijijini, Antony Komu Atangaza Kujiondoa CHADEMA

Mbunge wa Moshi Vijijini, Antony Komu leo Machi 29, 2020 ametangaza kujiondoa kwenye Chama cha Demokrasia na Maendeleo mara baada ya kipindi chake cha ubunge kuisha na kusema atahamia chama cha NCCR Mageuzi.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika Hotel ya Nepherland Magomeni Jijini Dar es salaam, Komu amedai kuwa anaamini Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kitatumia busara kumuacha amalizie majukumu yake ya kibunge kwa muda uliobakia kwani bado anahitaji kuwatumikia wananchi wake.


Share:

MFANYABIASHARA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHUHUDIA LIVE VIBANDA VYAKE VIKITEKETEA KWA MOTO SOKO LA SAMUNGE

Na Ahmed Mahmoud - Arusha
Mfanyabiashara aitwaye James Peter Temba, 57 Mfanyabiashara na mkazi wa Moshono  amefariki dunia baada ya kufika na kushuhudia vibanda/maduka yake yote yakiwa yameteketea na moto kutokana na moto mkubwa kuzuka na kuunguza soko la Samunge jijini Arusha.

Akiongea na waandishi wa habari Sokoni hapo Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Koka Moita amesema tukio hilo limetokea jana usiku majira ya saa 23:30  katika soko la Samunge, lililopo Mtaa wa NMC, kata ya Kati, Tarafa ya Themi, katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Amesema chanzo cha moto huo uliowaka na kuteketeza vibanda vya Soko hilo hakijajulikana na idadi na mpaka sasa thamani ya mali zilizoteketea haijajulikana.

"Wakati zoezi la kuzima moto likiendelea mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya James Peter Temba, 57 Mfanyabiashara na mkazi wa Moshono ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa vibanda vilivyoungua ndani ya Soko hilo, alifika eneo hilo na kukuta vibanda vyake vimeteketea kwa moto alipata mshtuko na kuanguka chini na kuzimia ambapo alichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu",ameeleza Kamanda.. 

Ameeleza kuwa vibanda hivyo vilikuwa vinamilikiwa na wafanyabiashara wa Soko hilo ambavyo vilijengwa kwa Mabati, Mbao na Mabanzi. Mara baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Wananchi walifanikiwa kuzima moto huo ambao haukuleta madhara kwa binadamu vimeungua.

Hata hivyo Uchunguzi unaendelea ili kubaini thamani halisi ya mali zilizoungua pamoja na chanzo cha moto huo. 

Soko la Samunge likiteketea kwa Moto kama lilivyokutwa na kamare ya matukio jijini Arusha usiku wa kuamkia leo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Soko la Samunge likiteketea na Moto usiku wa kuamkia leo jijini Arusha ambapo imeelezwa kuwa thamani ya Mali iliyoteketea bado haijajulikana huku mfanyabiashara Mmoja akifariki kwa mshtuko Mara baada ya kukuta maduka yake matatu yameungua.

Share:

JIKO LA MKAA LAUA WATU WANNE WA FAMILIA WAKIJIKINGA NA BARIDI YA MVUA SHINYANGA



Nyumba ambayo marehemu walikuwa wamelala

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia baada ya kuvuta ya hewa yenye sumu ya Carbon monoxide iliyotokana na mkaa waliowasha kwenye jiko la mkaa kisha kulala ndani ya nyumba yao wakijikinga na baridi katika kitongoji cha Ngilimba ‘B’ kijiji cha Ngilimba kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga. 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Machi 28,2020 ambapo ndugu hao wa familia moja waligundulika kuwa wamefariki dunia wakiwa nyumbani kwao wamelala baada ya kuvuta hewa yenye sumu ya Carbon Monoxide. 

“Chanzo cha tukio hilo ni kwamba siku hiyo mvua kubwa ilinyesha kijijini hapo na kupelekea uwepo wa baridi nyumbani kwa marehemu hao na ndipo wakati wakijiandaa kulala waliacha jiko la mkaa likiwa limewashwa ndani ya nyumba na kufunga mlango na dirisha hali iliyo pelekea mgandamizo wa hewa kuwa mdogo ndani ya nyumba yao na kuvuta hewa hiyo iliyokuwa na sumu ya carbon monoxide”,amesema Kamanda Magiligimba. 

“Waliofariki dunia ni Masanja Emmanuel (35), Mngole Masanja (25), Holo Masanja,(05) na Matama Masanja wote wakazi waNgilimba wote wa familia moja”,ameeleza Kamanda Magiligimba 

Amesema miili ya marehemu imekabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari.
Share:

PRISCA KIBASA MWANAMKE ASIYEOGOPA KUZUNGUKA USIKU KUIMARISHA ULINZI SHIRIKISHI


Mwenyekiti wa mtaa wa Kibasa kata ya Sabasaba wilaya yaTarime mkoani Mara ,Prisca Kibasa (CCM).
Na Dinna Maningo - Tarime


Ni saa tisa alasiri nawasili nyumbani kwa Prisca Kibasa mwenye umri wa miaka (56) ambaye ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kibasa kata ya Sabasaba wilaya yaTarime mkoani Mara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).



Ananikaribisha huku usoni kwake akionekana mtu mwenye furaha.Lengo la kufika kwake nikutaka kufahamu ni kwa namna gani anawatumikia wananchi ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa mtaa.



Licha ya kwamba baadhi ya wanawake hawajitokezi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa uoga waliojijengea kutokana na dhana zilizopo ndani ya jamii kuwa mwanamke hana haki kuzungumza mbele ya watu au kuwaongoza wanaume lakini hali hiyo ni tofauti kwa mama Kibasa.



Mama Kibasa ambaye amekuwa kiongozi ngazi ya kitongoji na Mtaa tangu mwaka 2004 hadi sasa  ni kiongozi akihakikisha anaimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi na mali zao na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.



Je Kwanini Mwenyekiti huyo anaitwa Prisca Kibasa na mtaa nao unaitwa Kibasa?



"Wakati tunagawa mitaa nilikuwa ni Mwenyekiti nikasema kwanini niite majina mengine nikaita jina langu hata nije kukumbukwa kwa hilo na nilipoita na wengine nao wakajiitia majina yao kama mtaa wa Nyangai,Chomete,na mtaa wa Nyarusai kwa hiyo ndiyo ujue kuwa mwanamke akiamua kufanya jambo inawezekana na wengine wakaiga kutoka kwako",anasema Kibasa.



Kibasa anaeleza historia yake ya uongozi ambapo anasema kuwa amekuwa mwenyekiti wa Kitongoji cha Serengeti kwa awamu mbili mfululizo tangu mwaka 2004 hadi 2014.



"Wakati huo ilikuwa ni halmashauri moja ya wilaya mimi nilikuwa ndiyo mwanamke peke yangu niliyechaguliwa hadi nilikuwa najishangaa nikisimama kuzungumza mbele ya wanaume nilikuwa naona aibu, lakini baadae nilizoea nikajiamini kwanini nijishushe nawakati nimegombea sawa na wanaume" anasema Kibasa.



Kibasa anaeleza kuwa licha ya kuwa kiongozi mwanamke pekee wananchi walimpa ushirikiano kutokana na ujasiri wake na kujituma uliofanikisha kuleta maendeleo kutokana na ushawishi baina yake na wananchi. 



"Mimi si Mkurya kabila langu ni mrangi wa Kondoa niliolewa na mkurya pamoja nakwamba mimi ni mkabila tena musagane mwanamke ambaye sikukeketwa bado wananchi waliniona nafaa wakanichagua. Kitongoji chetu kilikuwa na wananchi 490 walinichagua kwa sababu mimi sipendi rushwa na sina ubaguzi huduma yangu wanahifurahia",anasema.



Anaongeza"Nilipokuwa mwenyekiti wa kitongoji tulifanikiwa kujenga madarasa shule ya msingi Sabasaba,darasa moja shule za Sekondari Nyamisangura,Rebu na Nkende, kuimarisha ulinzi shirikishi na shughuli zingine za kimaendeleo".



Akizungumzia suala la ulinzi shirikishi anasema kuwa pamoja na yeye kuwa kiongozi mwanamke hakusita kutembea usiku akiwa ameambatana na wanaume kuhakikisha wanazunguka maeneo yote ya kitongoji kuimarisha ulinzi.



Anasema kuwa wakati wa zamu ya ulinzi aliwaandaa wananchi na kuwapanga kwa makundi kisha kupita kwenye maeneo ya giza na vichochoro vyote jambo ambalo lilifanikisha baadhi ya wahalifu kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.



"Tulikuwa tunaanza ulinzi saa sita usiku nachagua watu kwa zamu nilivaa  mavazi yangu Suruali,kofia na jaketi kisha tunaenda kulinda,lazima na mimi Mwenyekiti niende maana ukiacha waende wenyewe wapo baadhi ya wananchi si wazuri watatumia muda huo kufanya uhalifu kama kuwaibia simu wapita njia,kabla ya kuanza ulinzi tunakutana nyumbani kwangu nawapanga makundi matatu yenye watu sita tunaondoka kila kundi linaenda sehemu yake kufanya ulinzi.



"Tulikuwa tunalinda hadi saa kumi kisha tunakutana mahali ambapo tumepanga kukutana ili kuona kama tuko wote, kwakweli tulifanikiwa sana maana tulikuwa tunawapata wezi, maeneo mengine tulikuta vitu vilivyoibwa vimetunzwa ,wakati wa ulinzi tuliwapa Polisi Taarifa na walifika kubeba na kuwakamata wezi, kabla ya kuwakabidhi Polisi tulikuwa tunawapa kwanza kichapo",anasema Kibasa.



Mbali na kuwa Mwenyekiti wa Kitongoji mwaka 2019 katika uchaguzi wa Serikali za mitaa Mama Kibasa aliibuka tena na kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa mtaa wa Kibasa na alifanikiwa kupita katika kura za maoni kupitia chama cha CCM dhidi ya wapinzani wake.



"Nilishindana na wanaume wawili mwanamke nilikuwa mimi peke yangu na nikawashinda na sasa mimi ni mwenyekiti wa mtaa japo napata changamoto kuwa hatukuchaguliwa na wananchi lakini hainikatishi tamaa mimi ndiyo mwenyekiti wao bahati nzuri wengi wananikubali". 



"Kuna mwananchi mmoja waligombana nikamwita kwa barua alikataa kuja akasema hanitambui kwakuwa ninajiamini nikamwambia sasa utanitambua kuwa mimi ni mwenyekiti na kufikisha ngazi za juu alivyoona nimekuwa mkali alikuja kuomba radhi kwa kuwa alikiri kosa nikamsamehe nilitaka nimwonyeshe kuwa hata mwanamke ana uwezo wa kujisimamia",anasema Kibasa.



Mahende Kangoye mkazi wa mtaa wa Kibasa anasema Mwenyekiti huyo anafaa kuongoza kwa kuwa ni mtu anayejali watu na kwamba hakuna changamoto inayotokea akashindwa kuitatua,anasisitiza kuwa kadri siku zinavyokwenda mila kandamizi zinapungua.



Kangoye anasema kuwa baadhi ya wanawake ni waoga kusimama mbele za watu hali inayosababisha wasigombee,anasema usipokuwa jasiri huwezi kuongea au kushauri jambo kwenye mikutano.



Anaongeza kwamba mila ya Kabila la Wakurya  mwanamke hawezi kufanya jambo bila ruhusa ya mme wake na wengine ukataliwa na ukijichukulia maamuzi yao hufukuzwa nyumbani hali inayosababisha wengine kuacha kugombea.



"Wapo baadhi ya wanaume wakiona mwanamke anaongea jukwaani wanasema huyu mwanamke ni shida nyumbani mara atakuwa ana sauti nyumbani, ukienda kwenye vikao ukachelewa anadhani ulikuwa kwa wanaume",anasema.



Anaongeza" ni vyema wanaume waelimishwe watambue kuwa hata mwanamke anaweza kuongoza na kuna wanawake wana uwezo lakini niwaoga anajiuliza kuwa nikipata uongozi je nitahimili mikikimikiki ya vijana, nitaweza kweli anaamua kuacha" anasema Kangoye.


Katibu wa Umoja wa Wanawake Chama cha Mapinduzi (UWT) wilaya ya Tarime Sauda Kashombo anasema kuwa kuna haja ya elimu kuendelea kutolewa ili kuwapa fursa kugombea na kwamba wasiwe na hofu kwani uongozi si nguvu bali ni akili.


Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Tarime Mkaruka kura anasema kuwa baadhi ya wanawake hawajiamini kuwa wana uwezo wa kugombea na wanaume na kwamba Chama cha Mapinduzi hutoa kipaumbele kwa wanawake lakini baadhi yao wanashindwa baada ya kutopigiwa kura wakati wa kura za maoni na kwenye uchaguzi.



Lilian Liund ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) anasema kuwa ushindi wa wanawake kwenye chaguzi hutegemea uamuzi wa wapiga kura,wanawake kwa wanaume, na kwamba wanawake ndiyo ujitokeza kwa wingi kupiga kura ikilinganishwa na wanaume.



Liund anatoa rai kwa wanawake na wanaume kuwapigia kura wanawake wenye uwezo na wenye kubeba ajenda ya ukombozi wa mwanamke,kuhakikisha wanahamasisha wanawake wenye uwezo wanajitokeza kugombea,Kushawishi vyama kuteua wanawake,kuwapa moyo wanawake waliojitokeza kuwania viti vya uchaguzi na kuwapigia kura. 


Share:

FULL POWER , ZATI 50 SULUHISHO LA KUDUMU NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO



Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi
⇒Msongo wa mawazo 

⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.

FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

MATUKIO YA ZIARA YA KIMASOMO YA WASHINDI WA SHINDANO LA CMSA KWA VYUO VIKUU NA TAASISI ZA ELIMU YA JUU





Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA)
Nicodemus Mkama akizungumza na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa
ziara ya mafunzo ya washindi wa shindano la vyuo vikuu na Taasisi za
Elimu ya Juu kwa mwaka 2019 linaloendeshwa na CMSA.


Baadhi ya washindi wa Shindano linaloendeshwa na CMSA kwa vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu kwa mwaka 2019.

Watendaji wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)
wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa mamlaka hiyo (hayupo pichani)wakati
wa ufunguzi wa ziara ya kimasomo kwa washindi.

Ofisa wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) akiwafundisha wanafunzi
vinara wa shindano la vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu kwa mwaka
2019.
Ofisa wa Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE)wakiongea na wanafunzi.

Mkurugenzi wa Utafiti,Sera na Mipango CMSA, Alfred Mkombo (wa kwanza
kulia) na Mkurugenzi wa Usimamizi na Maendeleo ya Masoko CMSA,Exaut
Julius.

Mkurugenzi wa Utafiti,Sera na Mipango CMSA, Alfred Mkombo
akiwasilisha mada katika ziara ya wanafunzi washindi wa shindano la
CMSA kwa vyuo vikuu.
Mmoja wa watendaji akizungumza na wanafunzi. 

Mkurugenzi wa masuala ya kisheria, Fatma Simba, akizungumza na wanafunzi (hawapo pichani) 




Picha ya Pamoja ya wanafunzi vinara wa shindano la CMSA kwa vyuo
vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu. Wa Kwanza kushoto ni Ofisa wa
Mawasiliano CMSA, Charles Shirima.
Picha ya pamoja ya wanafunzi na watendaji wa CMSA.
Wanafunzi vinara wa shindano la CMSA kwa mwaka 2019
Share:

Waziri Mkuu Majaliwa Aridhishwa na Maandalizi ya Kituo Cha Kuhudia Wagonjwa wa Corona

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea eneo lililotengwa kwa ajili kuwahudumia watu watakaobainika kuwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) na amesema ameridhishwa na maandalizi.

Aliyasema hayo jana (Jumamosi, Machi 28, 2020) wakati akizungumza na wananchi wilayani Kibaha, Pwani baada ya kukagua hospitali ya wilaya ya Kibaha ambayo imetengwa kwa ajili ya kuwahudumia watu watakaogundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Alisema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kukabilia na COVID-19, ambapo kwa sasa watu wote wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege, vituo vya mabasi na bandari lazima wapimwe na wakigundulika wanamaambukizi wanawekwa kwenye maeneo maalumu kwa muda wa siku 14.

“Tunazingatia sana wale wanaotoka kwenye nchi ambazo zimeathirika sana wakiingia hapa Tanzania tunawazuia kwanza, tunawapima na tunafuatilia historia yake anatoka wapi na tunaangalia katika siku 14 amepita kwenye nchi zipi.”

Waziri Mkuu alisema wawaweka kwenye maeneo maalumu ili kuweza kuwapima kila siku na kujirishika kama hawana maambukizi kwani mtu anaweza kupimwa leo akaonekana yuko vizuri lakini ana maambukizi ambayo bado hayaonekani kwenye vipimo. Kama katika kipindi cha siku 14 mtu atabainika hana maambukizi anaruhusiwa kwenda kujiunga na familia.

Pia, alisisitiza wananchi waendelee kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuzuia mikusanyiko na kwa wale wanaosafiri kwenye usafiri wa umma wasibanane kila mtu akae kwenye kiti.

Waziri Mkuu alisema wananchi wanapokwenda kufuata huduma kwenye masoko wahakikishe wanapeana nafasi baina ya mtu mmoja na mwingine na kabla hawajaingia katika maduka wanawe mikono kwa sabuni na maji tiririka ili kujikinga na maambukizi ya corona.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kuwachukulia hatua watu wote wanaopotosha kuhusu taarifa za ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). “Aliyetangaza kuwa shule zinafunguliwa tumeshamkamata na atachukuliwa hatua.”

Hivyo aliwataka wananchi wajihadhari na taarifa zinazotolewa na watu ambao si wasemaji rasmi. Alisema taarifa kuhusu virusi vya corona itatolewa na Waziri Mkuu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Msemaji wa Serikali.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Korea Kaskazini yafyatua baharini Makombora Mawili

Korea Kaskazini imefyatua leo kile kilichoonekana kuwa ni makombora mawili ya masafa mafupi katika pwani yake ya mashariki, ikiwa ni jaribio la nne la aina hiyo katika mwezi huu wakati ulimwengu ukipambana na janga la virusi vya corona. 

Taarifa ya pamoja ya Wakuu wa Jeshi la Korea Kusini imesema makombora mawili yalifyatuliwa kuelekea mashariki kutokea mji wa bandari wa Wonsan na kuanguka katika Bahari ya Japan, inayofahamika pia kama Bahari ya Mashariki. 

Wizara ya Ulinzi ya Japan imesema makombora hayo hayakuvuka mipaka yake ya baharini au kufika katika kanda ya kipekee ya kiuchumi ya nchi hiyo. 

Korea Kaskazini wiki moja iliyopita ilifyatua makombora mawili ya masafa mafupi. 

Siku moja baadaye, chombo cha habari cha nchi hiyo yenye silaha za nyuklia kikatangaza kuwa Rais wa Marekani Donald Trump alimtumia barua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ikielezea kwa kina mpango wa kukuza mahusiano. 

Credit: DW


Share:

Alliance One Yatoa Vifaa Vya Ujenzi Vya Milioni 23.9 Kwa Wilaya Mbili Za Mkoa Wa Tabora

NA TIGANYA VINCENT
KAMPUNI ya Tumbaku ya Alliance One Tanzania (AOTTL)  imeukabidhi uongozi wa Mkoa wa Tabora vifaa mbalimbali vikiwemo vifaa ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 23.9.

Msaada huo umekabidhiwa jana na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kampuni hiyo David Mayunga kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri katika halfa iliyofanyika Ofisini kwake.

Mayunga alivitaja vifaa vilivyotolewa ni Bati 270, Saruji mifuko 300  na nondo 320.

Alisema msaada huo kwa ajili ya ujenzi wa mabweni na vyoo  katika Wilaya ya Tabora na Wilaya ya Uyui kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kike.

Mayunga alisema Wilaya ya Tabora imepewa mifuko 200 ya saruji na nondo 240 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 8.6.

Alisema msaada huo ni kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika Shule ya Sekondari ya Itojanda na Ndevelwa zote za Manispaa ya Tabora.

Mayunga alisema kwa upande wa Wilaya ya Uyui wamekabidhi mabati 250 , mifuko 100 ya saruji na nondo 80 kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa Mabweni ya watoto wa kike katika Sekondari ya Idete na kumalizia majengo ya shule mpya ya Nsimbo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mwanri aliwataka Idara Wakuu wa Wilaya zote zilizopata msaada huo  kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa malengo ya kutoa mazingira mazuri ya watoto wa kike kupata elimu.

Alionya kuwa hatasitakuchua hatua kwa watendaji wote waliopewa vifaa ambao watavitumia kwa maslahi binafsi.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala aliishukuru Kampuni ya Alliance One kwa msaada huo ambao utawasaidia kuongeza kampeni yake ya kujenga mabweni kwenye shule mbalimbali ili kuwa kinga watoto wa kike na mimba.

Alisema hatua hiyo ni muhimu katika kukabiliana na watoto kutembea umbali mrefu kwenda shuleni na huku njiani wakikutana na vishwawishi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya alisema msaada waliopata utasaidia kumalizia mbweni ya wasichana  katika Shule ya Idete ambayo walikuwa washaanza kujenga chini ya Kampeni ya Nishike mkono kuwasaidia watoto wa kike wapate elimu.


Share:

Maafisa Ustawi Na Maendeleo Ya Jamii Watakiwa Kutoa Elimu Kwa Ya Kujikinga Na Corona

Na Mwandishi wetu, Arusha
Wizara ya Afya kupitia Idara kuu ya maendeleo ya Jamii imeanza kutoa mafunzo kwa Wataalamu wa Ustawi wa Jamii pamoja na Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuelimisha Jamii kuhusu ugonjwa unaoenezwa na Virusi vya Corona.

Akifungua mafunzo hayo kwa maafisa wa Wilaya na kata zote za Mkoa wa Arusha jana tarehe 28/03/2020 jijini Arusha, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw. Hargeney Chitukuro amewataka kutumia fursa hiyo kuwaelimisha wananchi kwa usahihi kuhusu maambukizi na namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona bila hofu.

Bw. Chitukuro amesema kuwa, tangu ugonjwa huo ulipoingia Mkoani Arusha, mafunzo mbalimbali yameshatolewa kwa wataalamu na kuwaelekeza namna ya kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga.

“Katika kipindi cha takribani wiki mbili tangu ugonjwa huu uingie tayari tumeshatoa mafunzo kwa wataalamu wa Afya 240 kwenye Wilaya zetu na Halmashauri zote. Kwa mafunzo ya leo tunatarajia kuwafikia wataalamu wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii zaidi ya 185” amesema.

Amewaomba pia wadau wote kuelekeza nguvu zao kushirikiana na Serikali katika kufanikisha ukarabati wa kituo cha dharura Mkoani Arusha pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kujikinga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Patrick Golwike ametoa wito kwa Maafisa hao ili kuepusha msongamano watumie Redio za Jamii zilizopo kwenye maeneo yao kuelimisha jamii.

“Baadhi ya Halmashauri zina Televisheni zao pamoja na Redio za kijamii. Vyombo hivi vikitumika vizuri kwenye kusambaza elimu ya kujikinga na virusi vya Corona ili kuepuka msongamano, zitakuwa ni sehemu mojawapo ya kusaidia kufikisha ujumbe” amesema.

Akitoa mada kwa washiriki hao, Dkt. Meshack Chinyuli kutoka Wizara ya Afya, kitengo cha Elimu kwa Umma amewasisitiza kutumia takwimu sahihi zinazotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na hapa nchini ni Wizara ya Afya.

Awali akitoa lengo la mafunzo hayo kwa washiriki, Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Maendeleo ya Jamii Zakia Mohamed amesema kuwa mafunzo hayo yatawajengea uelewa wa kufahamu njia za maambukizi, dalili zake na inapotokea mtu amepata dalili ni wajibu wa maafisa hao kuelekeza wapi pa kwenda kupata huduma.

Akishukuru kwa niaba ya washiriki, Afisa maendeleo ya Jamii Mkoa Bi. Blandina Mkini amewahimiza Maafisa hao kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kuwa Mkoa wa kwanza kuundoa ugonjwa huo hapa nchini.

“Sasa tutakuwa kifua mbele kwa sababu tuna tuna uwezo wa kumueleza mwananchi kuhusu ugonjwa huu na kukanusha upotoshaji” amesema.

Mgonjwa wa kwanza kuripotiwa nchini alitokea Mkoa wa Arusha hapo tarehe 16 Machi, 2020 ambaye amepona na hadi sasa wagonjwa waliothibitishwa ni 13.

MWISHO


Share:

NHC Yatakiwa Kukamilisha Ujenzi Jengo La Kitega Uchumi Mutukula

Na Munir Shemweta, WANMM MISENYI
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi DkT Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kukamilisha haraka mradi wake wa ujenzi wa Jengo la Kitega Uchumi lililopo mpaka wa Tanzania na Uganda eneo la Mutukula wilaya ya Misenyi mkoani Kagera ili kuliwezesha shirika kupata faida kupitia jengo hilo.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo juzi wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo akiwa katika ziara yake mkoani Kagera kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo sambamba na kufuatilia utekelezaji maagizo aliyoyatoa kuhusiana na wa sekta ya ardhi.

Alisema, mradi wa jengo la kitega uchumi unaoendelea eneo la Mutukula uko sehemu nzuri ya mpakani mwa Tanzania na Uganda na kuna muingiliano mkubwa wa kibiashara hivyo ni vizuri Shirika la Nyumba likaona haja ya kuharakisha ujenzi wake ili kutoa fursa kwa taasisi na wawekezaji kupanga kwenye jengo hilo.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, mji wa Mutukula umechangamka na una mzunguko mzuri wa biashara hatua inayosababisha kuwepo mvuto kwa wafanyabiashara na wawekezaji katika eneo hilo na kukamilika kwake kutaiwezesha NHC   kupata wapangaji na kujipatia mapato.

‘’Naagiza Miradi yote ya Shirika la Nyumba la Taifa inayoweza kuliingizia Shirika mapato likiwemo hili la kimkakati lazima iishe ili NHC iingize mapato na kujiendesha kibiashara’’ alisema Dkt Mabula

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mikoa ya Kagera na Geita Benit Masika alisema shirika lake liko katika jitihada kubwa za kuhakikisha mradi huo wa jengo la kitega uchumi Mtukula unakamilika mapema na kubainisha kuwa kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 88 na utakapokamilika litapangishwa kwa taasisi zilizoonesha nia ya kupanga zikiwemo za kifedha kama vile mabenki.

Aidha, Nabu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliitaka halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoani Kagera kutumia vizuri fursa ya kuwa eneo la mpakani kwa kuhakikisha inakamilisha zoezi la kupanga, kupima na kumilikisha viwanja ili wananchi waweze kujenga nyumba nzuri na zenye sura ya nchi ya Tanzania.

Alisema, halmashauri ya Misenyi wakati wa kupanga mji huo ihakikishe inakuwa na soko la mazao zikiwemo ndizi ili kuwawezesha watanzania kuuza bidhaa zao nchini Uganda tofauti na sasa ambapo tegemeo kubwa lipo upande wa Uganda na kuwataka watanzania kubadilika kwa kuitumia fursa ya kuwa eneo la mpakani kuchangamkia kuwekeza katika ardhi.


Share:

Waziri Mkuu Majaliwa Atembelea Hospitali Ya Wilaya Ya Kibaha Iliyotengwa Kuwahudumia Wagonjwa Wa Corona

Waziri Mkuu, Kaasim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (wa tatu kulia) wakati alipokagua hospitali ya wilaya ya kibaha iliyopo eneo la Lulanzi  ambayo imetengwa kwa ajili ya kuwahuduma kwa wagonjwa wa Coroma, Machi 28, 2020.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo  na wa pili kushoto ni  Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Bakari.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger