Thursday 31 January 2019

MKURUGENZI MPYA BENKI YA CRDB ATAMBULISHWA RASMI MWANZA


Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya Ushirika na Maendeleo Vijijini (CRDB), Abdulmajid Nsekela (aliyesimama) ametambulishwa rasmi kwa wafanyakazi na wateja wa benki hiyo Kanda ya Ziwa Mwanza na Shinyanga.

Hafla ya kumtambulisha Mkurugenzi huyo aliyechukua nafasi ya Dkt. Charles Kimei imefanyika Januari 29, 2019), katika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay alibeba jukumu la kufanya utambulisho huo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wageni mbalimbali wakiwemo wateja na viongozi wa CRDB pamoja na viongozi wa serikali.
Wateja na wafanyakazi wa CRDB wakiwa kwenye hafla hiyo.

Tazama Video hapa chini





Share:

CHANGAMOTO ZAAINISHWA UTEKELEZAJI SERIKALI MTANDAO


Kaimu katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Micky Kiliba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Serikali mtandao kilichofanyika leo jijini Dodoma
Kaimu katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Micky Kiliba walio kaa (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Serikali mtandao

Picha na Alex Sonna-Dodoma

Serikali imesema kuwa bado kuna changamoto zinazokabili utekelezaji wa serikali mtandao ambapo baadhi ya mifumo ya Tehama kuendelea kutowasiliana na kutobadilishana taarifa ndani ya taasisi na kati ya taasisi na taasisi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dk, Laurean Ndumbaro kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na kaimu katibu mkuu Micky Kiliba wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha serikali mtandao kilichofanyika hapa jijini Dodoma.

Dk, Ndumbaro amesema kuwa kuna mafanikio mengi yaliyopatikana kupitia wakala wa serikali mtandao ikiwemo kufanyika kwa uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ya Tehama kama vile mkongo wa Taifa, vituo vya kitaifa vya data na kutenga masafa ya intaneti ya Serikali.

Aidha amesema kuwa pamoja na mafanikio hayo lakini bado kuna changamoto ya urudufu wa mifumo ambapo kila taasisi inakuwa na juhudi za kipekee katika kusimika na kutumia mifumo na miundombinu ya Tehama ambayo ingeweza kutumiwa na taasisi zaidi ya moja.

“Baadhi ya sababu zilizochangia uwepo wa changamoto hizi ni pamoja na kutozingatia miongozo na kanuni za usimamizi wa serikali mtandao zilizopo, upungufu wa wataalamu wa Tehama wenye uwezo na ujuzi wa kutosha, misukumo kutoka kwa wafanyabiashara na wafadhili na uratibu
hafifu wa shughuli za Tehama ndani na kati ya taasisi za serikali,”amesema Dk.Ndumbaro

Hata hivyo Dk.Ndumbaro amebainisha kuwa lengo kuu la utekelezaji wa serikali mtandao ni kuboresha utoaji wa huduma kwa umma, kuimarisha utawala bora na kuongeza tija na ufanisi katika uendeshaji wa taasisi za umma kwa kuhakikisha uwepo wa mawasiliano ya haraka yenye uhakika na salama ndani na taasisi mbalimbali za serikali.

Kwa upande wake Kaimu katibu Mkuu, Micky Kiliba amewataka Watumishi wa umma kuutambulisha mfumo huo kwa serikali mtandao kwa wananchi ili kuwapunguzia gharama za kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma.

Kiliba amesema kuwa wananchi wakielimishwa kuhusiana na serikali mtandao watakuwa wanapata huduma mbalimbali za kiserikali kwa kupitia simu zao za mkononi kwa kuwa lengo la kuanzishwa kwa wakala wa serikali mtandao ni kusogeza huduma karibu na wananchi.

“Hata katika masuala ya uwekezaji hakutakuwa na haja ya wawekezaji kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kupata taarifa za uwekezaji watakuwa wanaingia kwenye mfumo wetu na kujua kila kituwanachokihitaji bila hata ya kuja huku,” amesema Kiliba.

Share:

WADAIWA KUNYWA DAWA ZA ARV BILA KUPIMA VIRUSI VYA UKIMWI

Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Kupambana na Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk Leonard Maboko amesema Watanzania wengi wana mwamko wa kutumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARV) kuliko kujua hali zao.

Dk Maboko alibainisha hayo jana wakati akizindua mpango mkakati wa miaka mitano wa taasisi ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi ya Agpahi.

“Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya wajawazito wanajua hali zao kati yao, asilimia 98 wanatumia dawa za ARV. Hata hivyo, utafiti uliofanyika ilibainika kuna watu hawajui hali zao lakini walipopimwa damu zilionyesha tayari wanatumia ARV,” alisema.

Awali, mkurugenzi mtendaji wa Agpahi, Dk Sekela Mwakyusa alisema kupitia mpango huo wanatarajia kupanua wigo wa huduma ili kufika maeneo mengi zaidi na kuhakikisha maambukizi kwa watoto wanaozaliwa yanakoma.

Na Ephrahim Bahemu, Mwananchi 

Share:

Wednesday 30 January 2019

SOT, PRALENA KUCHANGISHA MILIONI 45

Taasisi ya Michezo ya watu wenye Ulemavu wa Akili Tanzania, Special Olympics inahitaji shilingi milioni 45 kwa ajili ya kuisaidia timu ya Taifa inayotarajia kushiriki michezo ya Dunia itakayofanyika mwezi Machi mwaka huu, Abu Dhabi Falme za Kiarabu (UAE).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays alisema fedha hizo ni kwa ajili ya tiketi za kwenda na kurudi sambamba na kambi ya maandalizi kuelekea katika michezo hiyo.

Rays alisema kambi ya maandalizi kwa siku 14 inahitaji shilingi milioni 10.5 huku tiketi kwa ajili ya kwenda na kurudi Abu Dhabi ni sh.milioni 34.5.

Aidha Rays alisema ili kufanikisha kushiriki katika michezo hiyo wameomba ridhaa ya Taasisi ya PRALENA Network Ltd ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa fedha hizo kupitia mfumo wa simu za mkononi.

Naye mwakilishi wa PRALENA, Thabit Said alisema ili kufanikisha upatikaji wa fedha hizo wametengeneza mifumo mbalimbali ambayo wadau watachangia fedha.

Said alisema mfumo huo utatumika kwa kila anayeguswa katika mitandao ya simu ya Tigopesa, M-Pesa na Airtel Money.

“Tunawaomba wadau katika jamii, kusaidia kupatikana kwa fedha hizo kupitia Tigopesa, M-Pesa na Airtel Money kupitia namba ya kampuni 123123 na kumbukumbu namba ni 60024833555,” alisema Said.

Said aliweka bayana kauli mbiu ya ufanikishwaji wa fedha hizo ni ‘Ushindi wao ni ushindi wetu’.

Na Andrew Chale

Mwakilishi wa PRALENA, Thabit Said akizungumza namna ya mifumo mbalimbali ambayo wadau watachangia fedha ili kukusanya kiasi hicho cha Sh. Milioni 45.

Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kuchangisha fedha za tiketi. Kulia ni Mwakilishi wa taasisi ya PRALENA, Bi. Irine Victor na kushoto ni Mjumbe wa bodi ya SOT, Makuburi Ally.

Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kuchangisha fedha za tiketi.
Share:

POLISI ALIYEUA MKE NA MTOTO AMEJIUA KWA KIPANDE CHA CHUPA

Afisa mmoja wa polisi aliyeshtakiwa kwa madai ya kumuua mkewe pamoja na mtoto mwenye umri wa miaka 5 katika kambi ya maafisa wa kupambana na wezi wa mifugo eneo la Suswa Machi 2018, amejiua. 

Cosmas Kipchumba Biwott, 27, ambaye alikuwa amesimamishwa kazi kwa muda, alijiua Jumanne, Januari 29 katika kituo cha polisi cha Nandi Hills alikozuiliwa kwa mashtaka ya wizi wa kimabavu.

Kulingana na habari zilituzofika katika meza yetu hapa TUKO.co.ke, Kipchumba alimwomba mlinzi wa selo alimokuwa kumsindikiza chooni majira ya saa sita na dakika 10 mchana mita 20 kutoka kwenye selo hiyo. 

Wakiwa njiani, alikiokota kipande cha glasi/chupa na kukitumia kujirarua shingo. 

Alivuja damu nyingi huku akilepelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Kapsabet alikothibitishwa kufariki.

 ‘Njiani, mfungwa huyo aliokota kipande cha glasi na kujirarua shingo upande wa kushoto na kuanza kuvuja damu,’’ polisi walisema.

Wakiwa njiani, alikiokota kipande cha glasi na kukitumia kujirarua shingo.

Ilibainika kuwa Kipchumba alizuiliwa kituoni Jumatatu, Januari 28 kusubiri uchunguzi kuhusu kesi nyingine.

 Alikuwa amefikishwa kortini awali lakini hakimu wa mahakama ya Kapsabet akatoa agizo la kuzuiliwa kwa muda. 

Katika kisa kingine, inadaiwa kuwa Kipchumba alimuua mkewe Jane Njoki na mwanawe Shantel Nyambura. 
 Kulingana na ripoti ya polisi, Kipchumba alimpiga mkewe risasi 20 kabla kumgeukia mwanawe na kumuua vile vile. 

Alifikishwa kortini lakini akaachiliwa kwa dhamana kabla kukamatwa tena kwa wizi wa kimabavu.

Share:

SAKATA LA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE LATUA BUNGENI…LUGOLA ASEMA NI USHIRIKINA.

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema imebainika kuwa mauaji ya watoto mkoani Njombe ni ya imani za kishirikina. Lugola ametoa kauli hiyo leo Jumatano Januari 30, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa Mufindi Kusini (CCM), Mendrad Kigola. Mbunge huyo amehoji ni mkakati gani umewekwa na Serikali katika kukomesha mauaji ya watoto katika mkoa wa Njombe ili kurudisha amani mkoani humo. Akijibu swali hilo, Waziri Lugola amesema tangu juzi Januari 28, 2019 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni…

Source

Share:

IGP SIRRO AAGIZWA KUTUMA TIMU YA WATAALAMU NJOMBE KUSAIDIA UPELEZI MAUAJI YA WATOTO

Na.Amiri kilagalila Naibu waziri wa mambo ya Ndani ya nchi HAMAD MASAUNI amemuelekeza Inspecta genarali wa polisi SIMON SIRRO kutuma timu ya wataalamu mbali mbali mkoani Njombe ili kusaidiana na jeshi la polisi mkoani humo kupambana na vitendo vya utekaji na mauji ya watoto wadogo. Agizo hilo limetolewa mkoani Njombe wakati waziri wa mambo ya Ndani akizungumza na waandishi wa habari na kutoa tathmini ya ziara yake ya siku tatu mkoani mkoani humo yenye lengo la kupambana na mauaji dhidi ya watoto wadogo yanayoendelea mkoani Njombe. “Namuelekeza IGP kwanza kutuma…

Source

Share:

Tanzia : ALIYEZAWADIWA MILIONI 100 NA JPM KWA KUGUNDUA MADINI YA TANZANITE AFARIKI DUNIA


 
Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, Jummane Ngoma amefariki dunia leo Jumatano Januari 30, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mtoto wa marehemu, Hassan Ngoma amesema, “Ni kweli Mzee amefariki leo jioni hii hapa Muhimbili,” amesema Ngoma

Hassan amesema kinachofanyika kwa sasa ni kuuhifadhi mwili wa baba yake kisha baadaye watatoa taarifa rasmi ikiwamo utaratibu wa msiba utakuwa wapi na mazishi yatafanyika wapi baada ya kikao cha familia.

Aprili 6 mwaka jana, Rais John Magufuli akizindua ukuta wa mgodi wa Tanzanite, Mirerani mkoani Manyara alimzawadia Sh100 milioni kama shukrani kwa mchango wake kwa kugundua madini hayo.

Chanzo- Mwananchi
Share:

FACEBOOK KUUNGANISHA WHATSAPP, INSTAGRAM NA MESSENGER

Facebook ina mipango ya kuunganisha huduma zake za kutuma ujumbe katika Instagram, WhatsApp na Facebook Messenger.

Licha ya kwamba huduma zote tatu zitasalia kuwa programu huru zitashirikiana kupitia ujumbe utakaotumwa kutoka huduma moja hadi nyingine.

Facebook imeambia BBC kwamba ndiyo mwanzo wa mchakato mrefu.

Mpango huo kwanza uliripotiwa mjini New York na unaaminika kuwa mradi wa kibinafsi wa mwanzilishi wa facebook Mark Zuckerberg.

Utakapokamilika , ushirikiano huo utamaanisha kwamba mtumiaji wa facebook anaweza kuwasiliana moja kwa moja na mtu ambaye anamiliki akaunti ya WhatsApp.

Hili haliwezekani kwa sasa kwa kuwa programu zilizopo hazina uhusiano.

Hatua ya kuunganisha huduma hizo tatu umeanza , kulingana na gazeti la The new York Times na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2019 ama mapema mwaka ujao.
Je facebook ina mpango gani?

Facebook haikupendelea kuzungumzia kuhusu swala hili katikati mwa kashfa ilioikumba, lakini ililazimishwa na watu waliokuwa wakiwasiliana na New York Times.

Hadi kufikia sasa , WhatsApp, Instagram na Messenger zimekuwa zikifanya kazi kivyake na kushindana kibiashara.

Kuunganisha huduma hizo kwaa kutuma ujumbe kutarahisisha kazi ya facebook.

Haitalazimika kuunda programu mpya kama vile stories ambapo huduma zote tatu zimeongeza katika programu yake bila mafanikio ya kufurahisha.WhatsApp, Messenger na Instagram ni bidhaa huru zinazoshindana

Mawasiliano ya ujumbe kupitia huduma moja hadi nyengine yanaweza kuimarisha biashara katika huduma moja kwa kutuma ujumbe kwa huduma nyengine.

Pia yatairahisishia facebook kugawana data katika huduma zote tatu ili kusaidia juhudi za matangazo yake.

Hatua hiyo pia itaimarisha uwepo wa facebook na kuwa vigumu kuanguka iwapo serikali husika zitajaribu kuivunja kwa manufaa yao ya kibinafsi.
Usambazaji wa data.

Bwana Zuckerberg ameripotiwa kushinikiza ushirikiano huo ili kuimarisha huduma za kampuni yake kuwa muhimu na kuongeza muda wa wakati unaotumika na wateja wake katika huduma hizo.

Kupitia kuunganisha wateja wake katika kundi moja kubwa, facebook itaweza kushindani vizuri na kampuni ya Google na Apple iMessage kulingana na Makena Kelly wa mtandoa wa habari wa The Verge.

"Tunataka kuunda huduma bora zadi ya kutuma ujumbe ilio na ulinzi wa hali ya juu na kufanya kuwa rahisi kuwafikia marafiki na familia kupitia huduma tofauti'', aliongezea.

Taarifa hiyo ilisema kuwa kulikuwa na majadiliano na mjadala kuhusu vile mfumo huo utakavyofanya kazi.

Kuunganishwa kwa huduma hizo tatu kuteleta mabadiliko muhimu katika kampuni ya facebook kwa kuwa imeruhusu Instagram na WhatsApp kufanya kazi kama kampuni tofauti zilizo huru.

Gazeti la the New York Times linasema kuwa hatua ya Bwana Zuckerberg kupigania mpango huo wa kuunganisha huduma hizo umesababisha mgogoro wa ndani.

Inadaiwa ndio sababu ya waanzilishi wenza wa Instagram na WhatsApp kuondoka mwaka uliopita.

Hatua jhiyo inajiri huku facebook ikikabiliwa na uchunguzi na kukosolewa kuhusu vile inavyotunza data za wateja wake.
Chanzo - BBC
Share:

POLISI YAMSHIKILIA MWANAUME NA MCHEPUKO KWA KUMUUA MKE WAKE

Mary Wambui  anadaiwa kuuawa na mume wake Joseph Kori kwa ushirikiano na mwanamke(mchepuko) Judy Wangui.

 Wangui alikuwa mfanyakazi wa zamani wa Kamangara na kulingana na ripoti zilizosambaa ni kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wa bosi wake.

 Inadaiwa kulitokea ugomvi uliosababisha kifo cha Kamangara na mwili wake kutupwa katika bwawa la maji Jumamosi, Januari 26.

  Dada wa marehemu Esther Kamangara alisema, dada yake alitaka kufahamu ni nani aliyetaka kuondoka na mtoto wake, Kamangara alitoka nje na kukutana ana kwa ana na Wangui aliyekuwa mfanyakazi wake wa zamani na alikuwa akishuku kuwapo uhusiano kati yake na mume wake.

  Kori alikamatwa eneo la tukio na awali alikuwa ameripoti polisi kuhusu kutoweka kwa mke wake na hata kuwapeleka polisi katika nyumba ya Wangui ambapo matone ya damu yalipatikana. 

 Joseph Kori na  Judy Wangui  wanazuiliwa kwa madai ya kuhusika na mauaji ya mke wake Mary Wambui Kamangara.

Chanzo:Tuko
Share:

TAARIFA ZA SIRI ZA WATU 140,000 WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI ZAIBIWA NA KUVUJISHWA MTANDAONI

Taarifa za siri za watu zaidi ya 14000 waliyo na virusi vya HIV wakiwemo raia wa wageni zimeibiwa nchini Singapore na kuvujishwa mitandaoni.

Udukuzi huo unakuja miezi kadhaa baada ya rekodi za watu milioni 1.5 wa Singapore akiwemo waziri mkuu Lee Hsein Loong kuibiwa mwaka jana.

Taarifa za kibinafsi za wasingapore 5,400 na raia wa kigeni 8,800 zilizokuwa zimeorodheshwa kutoka Januari 2013 huenda zimevujishwa.

Hadi mwaka 2015, raia wa kigeni waliyo na virusi vya HIV hawakuruhusiwi kuzuru nchi hiyo japo kama watalii.

Kwa sasa, mtu yeyote anayetaka kuwa nchini humo zaidi ya siku 90 kwa ajili ya kazi, lazima afanyiwe uchunguzi wa kimatibabu kuhakikisha hana virusi vya Ukimwi.

Nani ilihusika na udukuzi huo?
Singapore ilitoa picha ya Mikhy Farrera-Brochez, raia wa Marekani anayehusishwa na kuvujisha wa taarifa za matibabu za watu binafsi

Mamlaka za nchi hiyo zinaamini aliyehusika na udukuzi huo huenda ni Mmarekani mmoja aliye na virusi vya ukimwi ambaye mpezi wake alikuwa daktari wa ngazi ya juu nchini Singapore

Mikhy Farrera-Brochez alishtakiwa na kufungwa baada ya kupatikana na kosa la ubadhirifu wa fedha na makosa mengine yanayohusiana na dawa za kulevya mwaka 2016.

Alifurushwa kutoka nchini humo mwaka uliyopita. Mpenzi wake Ler Teck Siang raia wa Singapore alishtakiwa kwa kumsaidia Farrera-Brochez kuweka taarifa za uongo katika rekodi zake za matibabu kuficha ukweli kuhusu hali yake ya HIV.

Maafisa wanasema Ler alijitolea kutoa damu yake na kuweka alam katika kitika kibandiko kuwa ni ya Farrera-Brochez ili kumwezesha kuingia nchini.

Katika taarifa, wizara ya afya ilimlaumu Ler kwa kutozingatia sera inayoongoza taarifa za watu binafsi.Singapore imeripotiwa kutafuta usaidizi wa kimataifa katika kesi

Maafisa wanasema kuwa walifahamishwa tarehe 22 mwezi huu wa Januari kuwa Farrera-Brochez huenda bado anashikilia taarifa ya sajili ya HIV.

"Sahamahani mmoja wa mfanyikazi wetu wa zamani ambaye alikua na idhini ya kufikia sajili ya taarifa binafsi za watu wenye virusi vya HIV huenda hakuzingatia mwongozo wa usalama uliyowekwa wa kushughulikia taarifa hizo"alisema waziri wa afya wa Singapore Gan Kim Yong.

Siku ya Jumatatu, maafisa wa afya walisema kuwa wamejaribu kuwasiliana na watu wote walio kwenye orodha hiyo ambao ni raia wa nchi hiyo lakini walifanikiwa kuzungumza na karibu watu 900 pekee kati ya 5,400.

Nambari ya dharura imetolewa kwa wale ambao huenda wameathiriwa na tukio hilo kupewa huduma ya ushauri nasaha.

Katibu wa wizara ya afya Chan Heng Kee amethibitisha hilo na kuongeza kuwa maafisa wanaamini Bw. Farrera-Brochez yuko ughaibuni lakini hawajui ni wapi hasa alipo.

"Kuna hofu huenda akaendelea kuvujisha taarifa hizo za siri mitandaoni," alionya Bw. Chan.
Chanzo - BBC
Share:

KIUNGO WA KATI WA MANCHESTER UNITED KUTIMKIA UCHINA

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini ameridhia makubaliano binafsi mkataba wa kibinasi na klabu ya Shandong Luneng kwa lengo la kuhamia klabu hiyo ya China.

United wamekataa kutoa tamko lolote ikiwa malipo yoyote yamefikiwa kumnunua mchezaji huyo raia wa Ubelgiji ambaye alitia saini nao mwaka 2018.

Fellaini, 31, alikuwa mchezaji mkubwa wa kwanza aliyesainiwa baada ya enzi ya Sir Alex Ferguson, akijiunga na Manchester Utd kwa kima cha pauni milioni 27.5 mwaka 2013 akitokea Everton.


Fellaini alitia saini kandarasi mpya ya miaka miwili Old Trafford mwezi Juni mwaka jana lakini hajawahi kukubalika na mashabiki wa United licha ya kukonga nyoyo za mameneja David Moyes, Louis van Gaal na Jose Mourinho.

Chanzo:Bbc
Share:

GUMZO LA BUNDI KUTUA BUNGENI LASHIKA KASI..WANANCHI WADAI KUNA KIFO

Wananchi mbalimbali wametoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuonekana kwa Bundi ndani ya ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, wengi wao wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

Leo Jumatano Januai 30, 2019 Mwananchi limeuliza swali katika mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp na Twitter linalosema, je Bundi anapoonekana inaashiria nini?

Kufutia swali hilo wananchi mbalimbali wametoa maoni yao.

Bundi huyo alionekana bungeni jana asubuhi na Spika, Job Ndugai aliwatoa hofu wabunge kuwa ndege huyo kuonekana ni jambo la kawaida lakini jana jioni ndege huyo alionekana tena ndani ya jengo la Bunge.

Katika mtandao wa Facebook, Abdul Mngwale amesema “Ina maana walichoazimia kukifanya hakikuwa sahihi, matokeo yataonekana ndani ya siku 21 baada ya kuidhinishwa. Kwa wale ambao hawajawahi kumuona bundi, ni ndege mwenye kichwa cha paka.”

Charles Shayo amesema “kule kwetu Moshi Bundi ni ishara mbaya, akija kulilia nyumbani kwako, inaashiria habari za kifo, huenda kikatokea maeneo hayo kwa wanaoamini hivyo.”

Christian Saleh ameandika “Inaashiria kiongozi mkuu wa wote wa mahali hapo anapotua bundi atakufa akiwa amesimama bila kuumwa, kwa hiyo kana yupo ajikabidhi mikononi mwa Mungu ili aelekee peponi, akishupaza shingo anaenda jehanam.”

Kennedy Manengo ameandika “Tanzania tumepeleka imani zetu kwenye imani za kishirikina, ila kwa nchi zilizoendelea wao wangeamini kwenye tekinologia ya ujasusi, hapo ndio tunapotofautiana na wazungu.”

Katika mtandao wa Instagram, wananchi pia wametoa mawazo yao: Yahaya Abrahman ameandika “Atakufa mtu mkubwa hapo.”

Deogratius Luhulula ameandika “Mara nyingi huwa ni huzuni na muda siyo mrefu basi hutokea huzuni yaani msiba.”

“Bundi ni ndege ambaye huwa anasikia harufu ya mzoga wa mtu kabla hata hajafa, maana mwanadamu mpaka siku anakufa huwa anaanza kuumwa taratibu na hatimaye kifo, hivyo hapo bungeni kuna mzoga, tusubiri,” ameandika Mbeti Mbeti.

Katika mtandao wa Twitter, Steven Kyando ameandika “Kwa kawaida Bundi ni ndege ambaye anafanya mawindo yake muda wa giza usiku. Kwa ishara ya Bundi kuonekana ndani ya Bunge watafakari moja ya ishara mbaya.”

Na Peter Elias, Mwananchi 
Share:

MAREKANI NA CHINA WAANZA MAZUNGUMZO YA KIBIASHARA

Marekani na China wanaanza duru tete ya mazungumzo kuhusu biashara huku kukiwa na matumaini finyu ya kufanikiwa kutokana na masharti ya viongozi wa mjini Washington kulazimisha mageuzi katika mfumo wa kiuchumi wa China.

Pande hizo mbili zitakutana si mbali na ikulu ya Marekani kwa mazungumzo ya ngazi ya juu kabisa kuitishwa tangu rais Donald Trump na rais wa China Xi Jinping walipokubaliana Desemba iliyopita, kipindi cha siku 90 cha utulivu katika vita vyao vya biashara.

Kwa miezi kadhaa sasa mvutano wa kibiashara umekuwa ukiendekea huku kukiwa na maoni tofauti yanayotolewa na rais Trump kupitia mtandao wa Twitter, mara yakiwa ya kutia moyo na mara nyengine ya vitisho. 

Wiki iliyopita tu Rais Trump alisema ameridhika na jinsi mazungumzo yalivyoendelea hadi sasa. Amesema ana hakika "China inapendelea sana kufikia maridhiano.

Matamshi kinyume na hayo lakini yalitolewa na waziri wake wa biashara Wilbur Ross ambae hatarajii makubaliano yoyote kufikiwa katika mvutano wa biashara pamoja na China.

 Chanzo:Dw
Share:

UTEUZI ULIOFANYWA NA RAIS MAGUFULI LEO JANUARI 30,2019




Share:

MASHABIKI 10,000 TU KUISHUHUDIA SIMBA IKIMENYANA NA AL AHLY

Kitengo cha usalama nchini Misri, kimetoa maagizo kwamba, mashabiki wanaotakiwa kuingia uwanjani kushuhudia mchezo kati ya Al Ahly dhidi ya Simba wasizidi 10,000.

Al Ahly itacheza na Simba Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Borg El Arab uliopo Alexandria nchini humo ambapo uwanja huo una uwezo wa kubeba watazamaji 860,000.

Agizo hilo limekuja ikiwa ni kwa ajili ya kiusalama zaidi ambapo tahadhari imechukuliwa ili kusiwe na aina yoyote ya kukosekana kwa amani.

Kama uwanja huo ungeruhusiwa kuingiza mashabiki kama ilivyo uwezo wake, ingekuwa shida kubwa kwa Simba, lakini kwa sasa inaweza kupunguza presha kwa wawakilishi hao wa Tanzania na kucheza kwa kujiamini sana.

Mchezo huo wa Kundi D katika michuano hiyo, ni wa tatu kwa timu hizo ambapo Al Ahly inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne, inafuatiwa na AS Vita Club yenye tatu sawa na Simba, huku JS Saoura inaburuza mkia na pointi moja.
Share:

WANACHAMA WA THRDC KANDA YA ZIWA WALAANI MAUAJI YA WATOTO NJOMBE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI   KULAANI MAUAJI YA WATOTO WASIOKUWA NA HATIA MKOANI NJOMBE 


 1.0 Utangulizi 

Sisi waanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu  (THRDC) Kanda  ya  Ziwa tumesikitishwa sana na  mauaji  ya  watoto kumi (10) yaliyotokea  Mkoani  Njombe (Nyanda  za juu  Kusini) na  kuacha  simanzi kubwa  kwa Taifa, familia, ndugu jamaa na marafiki.  Hivyo  basi  tunaungana  na wapenda  amani wote nchini  kwenye kuomboleza  msiba   huu  wa kitaifa. 

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi na waandishi mbali mbali ambao wamekuwa wakifwatilia suala la mauaji ya watoto hao, chanzo kikubwa cha mauaji hayo ni imani za kishirikina. Watu (waganga) ambao wamekuwa wakihusishwa na imani za kishirikina wamekuwa ni chanzo cha mauaji yaliyotokea mjini Njombe. Waganga hao wamekuwa wakiua wakiteka watoto na kuwaua huku wakichukua sehemu mbali mbali za miili yao. Aidha, jeshi la polisi linaendelea na upelelezi kuhakikisha wauaji hao wanatiwa nguvuni na kujibu mashtaka yatakayowakabili.

Ndugu  Waandishi wa habari  ifahamike  kuwa haki  ya  kuishi ni haki ya msingi  na ya Kikatiba kwa  kila  binadamu. Nchini Tanzania  haki  hiyo inalindwa  na Katiba  yetu  ya  Jamhuri  ya  Muungano wa Tanzania) kupitia  Ibara  ya 14. HIvyo basi kuvunja haki hii ni kukiuka Katiba pamoja na mikataba mbali mbali ya Kimataifa ambayo Tanzania ni nchi mwanachama.

Ndugu  waandishi,  mauaji  yaliyotokea  Mkoani Njombe  siyo  ya  kufumbiwa  macho   kwani kitendo  hicho  ni uhalifu   mkubwa   unaokiuka msingi  wa  haki ya  kuishi  na  utu wa  binadamu. Katika taifa  letu  hakuna  mwenye  mamlaka  ya  kuiondoa  roho  ya  binadamu  mwingine isipokuwa kwa mujibu wa sheria za nchi. Hata hivyo, historia yetu kama taifa la Tanzania japo bado tuna sheria inayomruhusu Rais kusaini adhabu ya kifo, ni mara chache sana tumeshuhudia marais wetu wastaafu na rais aliyepo madarakani wakisaini adhabu hii ya kifo. Ni dhahiri kwamba, suala la kutoa uhai wa mtu ni jambo baya kutokea katika taifa letu.

 2.0 Ulinzi wa Mtoto Kisheria 

Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 kifungu cha 9 inasema; mtoto ana haki ya KUISHI kujaliwa utu wake, kuheshimiwa, kupumzika (kucheza), kuwa huru, kuwa na afya bora, kupata elimu pamoja na makazi kutoka kwa wazazi wake.

 Hata hivyo, jukumu hili la ulinzi wa maisha ya mtoto lipo pia Kikatiba na katika Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kila mtu ana wajibu wa kulinda na kuteteta Katiba na sheria za nchi. 

Ipo pia mikataba ya Kimataifa ambayo Tanzania ni mwanachama ambayo imeweka haki mbali mbali za mtoto ikiwemo haki ya kuishi. Baadhi ya Mikataba hiyo ni pamoja na Mkataba wa Kimataifa kuhusu watoto wa mwaka 1989, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kisiasa na Haki za Kiraia wa mwaka 1966, Nyongeza ya Mkataba wa Maputo wa Mwaka 2003. 

Mikataba yote hii na mingine inaelekeza juu ya haki za watoto na ulinzi wa utu wao.

Ndugu waandishi  mauaji ya  watoto  kumi  ni  ukatili  mkubwa, kwani uhai  wa watoto hawa  umekatisha  ghafla maisha na ndoto zao  na kuleta  simanzi kubwa  kwa  ndugu  jamaa , marafiki  na taifa  kwa  ujumla. Taifa limepoteza kizazi ambacho kingeweza kulitumikia kwa maslahi mapana ya nchi.

Ndugu waandishi wa habari, Ikumbukwe kuwa watoto ni kundi ambalo kwa namna moja ama nyingine hawawezi kupata haki zao bila ya msaada wa watu wengine. Hivyo basi, inapotokea kundi hili la watoto linaathirika na matendo ya kinyama kama haya ya mauaji, ni jukumu letu sote kukemea vikali na kupaza sauti zetu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wauaji wa watoto hawa.

 Hivyo basi, nyinyi kama waandishi wa habari na sisi watetezi wa haki za binadamu naomba tushikamane katika kipindi hiki kuwasemea watoto na kuhakikisha haki na utu wao unalindwa wakati wote.

3.0 Wito Wetu
Jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa kina na kuwabaini wote waliohusika na mauaji tajwa na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi ya wote waliohusika na mauaji hayo.

Vyombo  vya  ulinzi  na usalama  viwe macho  na  waganga  wanaohusisha   utajiri/mafanikio  na  vitendo  vya  kishirikina na kuwachukulia hatua stahiki pindi wanapokiuka sheria na Katiba ya nchi.

Waandishi wa habari watumie  kalamu  zao  kwenye  kutoa  elimu kwa  jamii  juu  ya  athari  za ushirikina ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa kero kwa jamii na kusababisha hasara na simanzi kwa ndugu, jamaa, marafiki na taifa kwa ujumla.

Jamii  ishiriki  kikamilifu  kwenye  kuripoti  viashiria  vya ushirikina na uvunjifu wa haki za binadamu katika jamii.
Tamko   hili limetolewa na wanachama wa Mtandao wa  Watetezi wa Haki za Binadamu  kanda  ya  Ziwa.

 Mashirika  Wanachama 
OJADACT
ADLG
WOTE SAWA
SAUTI YA WANAWAKE  UKEREWE
UVUUMA 

Na Edwin Soko
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger